Tuesday, 13 September 2022

WAFANYAKAZI WANAWAKE GGML WAWAFUNDA KITAALUMA WANAFUNZI WA KIKE GEITA

Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya bweni ya wasichana ya Nyankumbu wakiwasikiliza viongozi na wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya GGML ambao waliwapatia mafunzo ya siku mbili kuhusiana na malezi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao wa kike mkoani Geita.
 **
Na Mwandishi wetu

Katika jitihada za kuhakikisha jamii inanufaika kutokana na shughuli za uchimbaji dhahabu nchini, wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Geita Gold Mine Limited (GGML) wameendesha semina ya siku mbili kwa ajili ya kutoa malezi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kike mkoani Geita.


Semina hiyo iliyofanyika juzi Mjini Geita katika Shule ya Sekondari ya bweni ya wasichana ya Nyankumbu iliyojengwa na GGML, imeasisiwa na kampuni hiyo kupitia Umoja wa Watumishi Wanawake wanaofanya kazi mgodini unaojulikana kwa jina la GGM ladies.


Akizungumza kwa niaba ya menejimenti ya GGML, Meneja Mwandamizi – Mawasiliano na Mahusiano, Manace Ndoroma amesema wanawake wanaofanya kazi mgodini, wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha umuhimu wa nafasi ya mwanamke katika jamii hususani.


Pia wametoa hamasa kwa mwanamke anayefanya shughuli zinazotokana na uchimbaji madini au biashara inayotokana na mnyororo wa thamani katika sekta ya uchimbaji.


Amesema GGML kupitia umoja huo imekuwa ikitoa misaada ya hali na mali ikiwemo fedha na vifaa mbalimbali kwa makundi maalumu ndani ya jamii yetu ili kuhakikisha jamii inayozungukwa na shughuli za uchimbaji wa dhahabu inafaidika kutokana na uwepo kampuni hiyo.


“Tumekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali kuhamasisha masuala ya usawa wa kijinsia. Mtakumbuka tarehe 26 Agosti mwaka huu ilikuwa siku ya usawa wa wanawake duniani. GGML tulitoa elimu kubwa kwenye mitandao yetu ya kijamii na vyombo vya habari juu ya nafasi muhimu ya mwanamke katika jamii.


“Tumekuwa tukifanya hivyo pia hata katika matukio ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kila tarehe 8 Machi,” alisema Ndoroma na kuongeza kuwa semina hiyo ni mwarobaini wa changamoto za wanafunzi wa kike kufahamu taaluma sahihi za kuchagua katika maisha baada ya kuhitimu elimu ya sekondari.


Amesema kumekuwepo changamoto ya wasichana wengi hususanI katika mwaka wao wa mwisho wa masomo au baada ya kumaliza elimu ya sekondari kushindwa kufahamu hatima ya masomo wanayoyasomea na uhalisia wa watakachokutana nacho katika elimu ya juu au baadae kwenye soko la ajira.


“Sisi menejimenti ya GGML tuliona ni vyema tuandae semina hii ili hata watakaopenda kuchagua nyanja mbalimbali za taaluma na hata kuwa wachimbaji au viongozi waandamizi katika kampuni za uchimbaji dhahabu ikiwemo GGML, wafikie ndoto zao kwa kuwaona akina mama wanaofanya vizuri katika taaluma hiyo tuliokuja nao kutoka GGML,” alisema Ndoroma.


Akihutubia kwa niaba ya serikali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara amewataka wadau mbalimbali nchini kuchangia maendeleo ya elimu nchini hususani kwa mtoto wa kike badala ya kuiachia serikali jukumu hilo pekee yake.


“Nawapongeza sana GGM kwa kuonyesha mfano mzuri wa wadau wanaochangia maendeleo ya elimu. Bahati nzuri nchi yetu imeendelea kuwa na mfumo mzuri wa elimu bora ukilinganisha na nchi zingine. GGM wanao mchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu kutokana na kodi wanayolipa.


“Jitihada kubwa wanayoionyesha katika jamii imeleta matokeo chanya ikiwemo kujenga miundombinu ya elimu na mafunzo kama haya yanayoleta tija kubwa katika jamii. Bahati nzuri mafunzo haya yanatolewa kwa wasichana wenye umri mdogo jambo ambalo sio rahisi kulisahau,” alisema Prof Kahyarara.


Akihamasisha wanafunzi kufikia ndoto zao katika Shule ya Wasichana Nyankumbu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita, Zahara Michuzi ameipongeza GGML na wafanyakazi wanawake wanaofanya kazi katika kampuni hiyo kwa kuandaa mafunzo hayo yanayotoa mwangaza kwa wanafunzi wengi wa kike kujitambua na kufikia malengo sawa na viongozi wa kike waliofanikiwa katika nafasi mbalimbali.


“Binafsi hata mimi sijafika hapa kwa nguvu zangu mwenyewe. Nilijitambua, nikamtanguliza Mungu lakini pia nikaomba watu mbalimbali akiwemo Profesa Peter Msofe wakati anafundisha Chuo Kikuu cha Dodoma kunipatia malezi ya kitaaluma ambayo yamenisaidia hadi kufikia hatua hii ya kuongoza Halmashauri ya Mji Geita kwa mafanikio,” alisema Zahara Michuzi.


GGML imekuwa kinara wa uwekezaji kwenye jamii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 ambapo vipaumbele vikuu vimekuwa ni miradi ya afya, elimu, maji, barabara, miradi ya kukuza kipato na miradi mingine mingi ya kijamii ili kuhakikisha jamii mwenyeji inapata maisha bora.


Kampuni imejenga zaidi ya shule saba za Msingi na tano za Sekondari ndani ya Mkoa wa Geita kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.


Mapema mwaka huu, GGML iliibuka mshindi wa jumla katika kampuni zinazofanya vizuri kwenye sekta ya madini nchini Tanzania kwa mwaka 2020/2021 baada ya kunyakua tuzo katika vipengele vya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, mazingira, usalama, mlipaji bora wa kodi na uendelezaji wazawa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita, Zahara Michuzi (kushoto) akizungumza katika mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya GGML kwa lengo la kuwapatia malezi ya kitaaluma wanafunzi wa kike mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya bweni ya wasichana ya Nyankumbu, Georgia Mugashe na kulia ni Meneja Mwandamizi – Mawasiliano na Mahusiano kutoka GGML, Manace Ndoroma.
Meneja Mwandamizi – Mawasiliano na Mahusiano kutoka GGML, Manace Ndoroma akizungumza katika semina hiyo.
Share:

AJIKATA KOROMEO BAADA YA KUMCHINJA MPENZI WAKE..."AMEISHI NAYE KAMA MKE"

Picha haihusiani na habari hapa chini
***
MKULIMA wa Kijiji cha Mshikamano, Wilaya ya Nachingwea, Albert Mkuwele (49), amemuua kwa kumchinja kwa panga mpenzi wake, Rejina Sotti (46) kisha naye kujiua kwa kujikata koromeo.

 Diwani wa Kata ya Mitumbati, Saimon Njende na Ofisa Mtendaji, Emmanuel Ndunguru, walisema wapenzi hao waliishi pamoja kama mke na mume kwa miaka 28 na kubahatika kupata watoto wanne na wajukuu wawili.

Alisema kabla ya mauaji hayo, wapenzi hao walionekana kutokuwa na maelewano mazuri kwa muda mrefu hali iliyomsukuma Mkuwele kuondoka na kwenda kuishi kijiji kingine.

“Wapenzi hawa hadi wanauana hawakuwahi kufunga ndoa na wameishi pamoja kwa miaka 28, wamebahatika kupata watoto wanne na wajukuu wawili,” alisema Diwani Njende.

Alisema siku ya tukio, mwanaume alirejea nyumbani na kuwakuta watoto alipowauliza alipo mama yao na kujibiwa kuwa yupo shambani akivuna mbaazi, alionekana akichukua panga huku akilinoa na kuelekea alipo mpenzi wake ambako alitekeleza mauaji hayo.

Taarifa zinasema kuwa alimkata shingo na kutenganisha kichwa na kiwiliwili, baadaye kugeuza panga alilolitumia kumjichinjia mzazi mwenzake, kujikata koromeo na kufariki papo hapo.

Chanzo - Nipashe


Share:

WALIMU WAPIGWA MARUFUKU KUKIMBILIA MJINI


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka ametoa zuio kwa walimu wa ajira mpya kuhama kutoka maeneo ya vijijini waliopangiwa kazi na serikali kwani kwa kufanya hivyo kumekuwa kikiathiri kiwango cha ukuaji wa elimu hususani maeneo ya vijijini.

Mkuu wa Mkoa amesema hayo wakati akikabidhi vitabu vya mwongozo wa namna ya ufundishaji ambapo mkuu wa mkoa amesema kuwa kumekuwa na tabia ya walimu kupewa ajira na serikali na baadaye kuanza kuomba kuhamia mijini kwa sababu ambazo hazina mashiko

Katika Kikao hicho pia mkuu wa mkoa amesikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuahidi kuzifanyia ufumbuzi.

Afisa elimu mkoa wa Njombe mwalimu Neras Aron Mulungu amesema kuwa wananchi mkoani Njombe wamefanya kazi kubwa kujenga nyumba za walimu huku akisema tabia ya walimu kukimbilia mijini inatokana na hulka ya mtu binafsi huku akisema kwa sasa huduma zote zilizopo mjini kama umeme zimefikishwa mpaka vijijini.

CHANZO-EATV




Share:

Monday, 12 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 13,2022

MAGA














Share:

SERIKALI YATAKA SHULE ZINGINE KUIGA KWA ST ANNE MARIE ACADEMY

Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdul Maulid, akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa darasa la saba, Fatma Mohamed wakati wa mahafali ya 19 ya shule ya St Anne Marie Academy yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara mwishoni mwa wiki. Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdul Maulid, akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa darasa la saba, Fatma Mohamed wakati wa mahafali ya 19 ya shule ya St Anne Marie Academy yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara mwishoni mwa wiki. Wanafunzi wa St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri wakisrebuka wakati wa mahafali yao ya darasa la saba mwishoni mwa wiki Mkurugenzi wa shule ya St Anne Marie Academy, Dk. Jasson Rweikiza akizungumza wakati wa mahafali ya 19 shuleni hapo mwishoni mwa wiki.

**************************

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imepongeza ubora wa elimu wa shule ya St Anne Marie Academy huku ikizitaka shule zingine kwenda kujifunza mafanikio yake.

Shule hiyo iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam inamilikiwa na Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Dk. Jasson Rweikiza.

Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Abdul Maulid, wakati wa mahafali ya darasa la saba ya shule ya St Anne Marie Academy ambapo jumla ya wahitimu 230 walitunukiwa vyeti.

Maulid alisema amefurahishwa na ubora wa elimu unaotolewa na shule hiyo ambayo imekuwa ikiongoza Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Ubungo na kuingia kwenye kumi bora kitaifa mara kwa mara.

“Kuna usemi kwamba usione vyaelea vimeumbwa maana umahiri wa wanafunzi niliouona hapa leo ni jitihada za walimu na menejimenti ya shule nawapongeza sana, shule ziko nyingi sana ila nimeamua kuja hapa St Anne Marie kwasababu hakuna longo longo hapa” alisema

“Mimi ni Ofisa Elimu wa Mkoa mkuu wangu wa mkoa anajua leo St Anne Marie kunanini ameniambia nije hapa na pia kuna Mkurugenzi wa Halmashauri kuna Ofisa Elimu wa Wilaya hapa, mheshimiwa diwani naye yupo hapa, kwanini, wazazi mmechagua shule bora na hamjakosea kuwaleta watoto wenu hapa,” alisema

Aliwataka wazazi kuwalinda watoto dhidi ya ukatili na wasimwamini mtu kuhusu ulinzi wa watoto wao kwani vitendo vya ukatili dhidi yao umekuwa mkubwa sana.

“Watoto hawa ndiyo tunawategemea wapatikane akina Rweikiza, akina Maulid mama Samia, hivyo tusiwachezee watoto hawa, mwanajamii ukiiona mtoto anafanyiwa ukatili toeni taarifa, shule zifanye kama St Anne Marie ziajiri wasimamizi wenye weledi wa hali ya juu,” alisema.

Pia aliwataka wamiliki wa shule wahakikishe mabasi yanayobeba wanafunzi yanakuwa salama kwa wanafunzi na aliwataka wapeleke mabasi hayo yakakaguliwe.

Aliwataka wamiliki wa shule kuacha kuwarundika wanafunzi kwenye basi moja na badala yake wanunue mabasi mengi ili wanafunzi wasibanane kupita kiasi.

“Hata wadhibiti ubora uliowaajiri ndio wamesababisha matokeo mazuri hapa shuleni kwenu ndiyo maana nawataka wengine waje wajifunze St Anne Marie maana haya matokeo hayajaja kutoka hewani tu,” alisema

Alitoa wito kwa shule kuacha kuwachuja wanafunzi kwa kisingizio kwamba wamefanya vibaya kwenye masomo hali ambayo inawapa msongo wa mawazo wazazi.

Aliwataka wamiliki wa shule zote kuhakikisha hawawazuii kufanya mitihani ya mwisho kwa kisingizio kwamba hawajalipa ada kwani sheria na sera ya elimu hairuhusu.

Aliwapongeza wazazi kwa kuendelea kuwasomesha watoto wao akisema kuwa hakuna urithi mzuri kama elimu kwani ni hazina anayoishi nayo miaka yote.

Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura, alisema matarajio yao ni kuendelea kuwa kwenye 10 bora kitaifa na kuendelea kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Ubungo katika matokeo ya kitaifa.

Share:

JAMAA AZUA GUMZO AKIRUDISHA DIGRII CHUONI APEWE ADA YAKE........"HAIJAMSAIDIA KITU"



Katika video inayosambaa, jamaa huyo anaonyeshwa akizua kioja chuoni akirejesha cheti chake akitaka arudishiwe karo zote alizolipa kwa sababu ya kukosa kazi Anadai kuwa licha ya kuwa na shahada, anahangaika na cheti hicho ambacho hakijamletea manufaa yoyote ya kifedha tangu alipohitimu Alisema ana kipawa cha kutumbuiza hivyo ana uhakika kwamba iwapo atarejeshewa karo yake atawekeza kwenye kazi yake ya burudani MAKINIKA: Tusaidie kubadilisha maisha ya wengi, jiunge na programu ya Patreon kutoka.


Alaba anaonyeshwa kwenye video hiyo akizua kioja kwenye mapokezi ya chuo hicho akirejesha cheti chake na kutaka arudishiwe karo zote alizolipa kwa sababu ya kukosa kazi. Mhitimu huyo alisema cheti hicho hakimsaidi chochote hivyo anataka karo zake.
Share:

Video mpya :NYANDA MATAMASHA - NITONGOZE YUPI

Hii hapa ngoma mpya ya Msanii Nyanda Matamasha inaitwa" Nitongoze yupi"
Share:

MAMA ALIYETELEKEZEWA MTOTO MLEMAVU NA MUME WAKE ZAIDI YA MIAKA 20 AELEZEA MACHUNGU ANAYOYAPITIA

Share:

MAJALIWA AZINDUA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU WA RUANGWA


\Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua uwanja wa Majaliwa katika halmashuri ya Ruangwa mkoa wa Lindi, Septemba 11, 2022. Kushoto kwake ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dkt. Theobald Sabi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua uwanja wa Majaliwa katika halmashuri ya Ruangwa mkoa wa Lindi, Septemba 11, 2022. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Share:

UGANDA YAPITISHA SHERIA YA MTANDAO


Bunge la Uganda limepitisha sheria ya mtandao ikilenga watumiaji wa computer nchini humo.


Sheria hiyo tata ambayo baadhi ya wabunge wamesikika wakisema kwamba watakwenda kuipinga mahakamani itawahusu watu wanaochapisha taarifa za uongo mitandaoni,taarifa ambazo hazijathibitishwa na wahusika, pia kuchapisha taarifa za watoto bila idhini ya wazazi au walezi wao.

Wakati wabunge wa nchi hiyo wakisema ndio ili kupitisha sheria hiyo, baadhi yao walisikika wakiguna , ndipo spika wa bunge Anita Among alipowaambia watafute namna na kwenda mahakamani.



Moja ya kifungu kilichopingwa , kinahusu adhabu kwa mtu atakayerekodi sauti ama video ya mtu mwingine bila ridhaa yake ambapo atakabiliwa na faini ya shilingi za Uganda Milioni 15 (zaidi ya Tsh. Milioni 9 ) au kifungo kisichozidi miaka 10 gerezani au vyote kwa pamoja
Share:

Sunday, 11 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 12,2022



















Share:

WAZIRI AWESO AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA RUWASA KARAGWE KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA MIRADI



Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amemsimamisha Kazi Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wilaya Karagwe, Mhandisi Magai Kakuru kwa kushindwa kusimamia miradi ya Maji inayoendelea kutekelezwa Wilayani Karagwe.


Ametoa agizo hilo leo Septemba 11, 2022 wakati alipoambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kukagua mradi wa maji wa Chanika/Omululama ulipo wilayani humo na kutoridhishwa na hali ya utekelezaji wa mradi huo.




“Mhandisi huyu anajitahidi kufanya kazi lakini haiendani na kasi inayohitajika kwahiyo ataenda kusaidia kwenye kazi nyingi, hapa karagwe nitaleta Meneja Mwingine anayeendana na kasi tunayoitaka” ,amesema Aweso




Waziri Aweso amesema alipokuja wilaya karagwe alitoa maelekezo mahususi kuhusu miradi ya maji, lakini leo baada ya kuona na kupata taarifa amegundua wakandarasi wanachezea fedha za miradi.




Aidha, Aweso ameagiza Mkandarasi ayetekeleza mradi wa maji wa vijijini nane wilayani Karagwe nae aondolewe na mchakato wa kupata Mkandarasi Mwenye Uwezo na atakayetekeleza miradi ya maji ndani ya muda wa mkataba.




Waziri Aweso amesema Serikali hatamvumilia wala kumbembeleza Mhandisi yeyote atakayeshindwa kusimamia miradi ya maji na akawasisitiza kusimamia na kukwamua miradi ya maji, “faraja ya Mhandisi wa Maji ni kuona Wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama”.



Pia, amesisitiza hawezi kukubali kuona Meneja wa Maji wa Mkoa ana zaidi ya shilingi Bilioni 9 kwenye akaunti lakini wananchi wanaendelea kuhangaika na kero ya Maji wakati Rais Samia ameshatoa fedha.




Nae, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema Kiu ya Wananchi wa wilaya ya karagwe ni kuona miradi ya maji inakamilika na wanapata maji safi na salama.
Share:

WAZIRI NAPE:IPO SIKU TUTAWAZOA WASAMBAZAJI WA MAUDHUI MITANDAONI YASIOFAA KWA JAMII.


***************************

*Waendeshaji wa Makundi ya Whatsapp watadharishwa kupokea maudhui na kuyaacha.


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa onyo kali kwa wanaosambaza maudhui yanayohamasisha Mapenzi ya jinsia moja (ushoga na usagaji) kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuacha mara moja la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Nape ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari, amesema kuwa baadhi ya watumiaji wa maudhui ya kulipia mtandaoni wamekuwa wakichukua maudhui yenye viashiria vya mahusiano ya jinsia moja kisha kuyasambaza kwenye mitandao kwa madai ya kutoa elimu ya madhara yake huku wakisambaza na maudhui hayo.

"Tutawazoa watu kwa kutafuta mnyororo wote waliohusika katika usambazaji pamoja na Maadmin wa makundi hii itakuwa mfano na kujua serikali ipo" amesema Nape

“Ili kukomesha jambo hili Serikali imeonya kuwa yeyote atakaebainika kusambaza maudhui ya aina hiyo kwenye mitandao hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na viongozi wa makundi ya Makundi (Whatsaap Admin) na yeyote atakayetumiwa maudhui hayo usalama wake ni kuifuta na sio kuisambaza”Amesema Waziri Nape.

Aidha amesema kwa lengo la kuilinda jamii dhidi ya maudhui yasiyofaa Serikali imetoa angalizo na tahadhari na kutoa onyo kwamba wanaosambaza maudhui yanayochochea mahusiano ya jinsia moja watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Waziri Nape amesisitiza kuwa siku za karibuni, kumekuwa na matukio mengi ya taarifa zinazosambazwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya Kijamii ikionyesha video fupi zenye viashiria vya ushoga na kuleta taharuki kubwa miongoni mwa jamii kibaya zaidi wanatumia mgongo wa kuelimisha jamii.

Ameongeza kuwa, si kweli kwamba vyombo vya utangazaji nchini vimekuwa vikirusha maudhui ya mapenzi ya jinsia moja al’maarufu “ushoga” na kwamba baadhi ya watumiaji wa maudhui ya utangazaji wamekuwa wakinunua maudhui hayo kwa hiari yao kisha kukata vipande vifupi na kuvituma kwenye mitandao wakidai kuwa vituo vya utangazaji vinarusha aina hiyo ya maudhui.

“Napenda kusisitiza kuwa TCRA wamekuwa wakifuatilia na wamebaini kuwa hakuna kituo cha utangazaji kinachorusha maudhui yenye viashiria vya mapenzi ya jinsia moja,” alionya Nape.

Ameonya kuwa hata kama nia ya anaesambaza maudhui ya aina hiyo ni kutoa tahadhari, bado hatua zitachukuliwa kwa kuwa lengo la Serikali ni kukomesha kabisa usambazaji wa maudhui ya aina hiyo kwa kuwa yanachochea vitendo vya ushoga.

“Baadhi ya clips hizo zinatuhumu kwamba maudhui hayo yanarushwa na baadhi ya vyombo vya Utangazaji hapa Tanzania baada ya ufuatiliaji wa karibu kuhusu clips hizo zilizokuwa zinasambazwa, tumejidhihirisha kuwa kwa kupitia utandawazi wa maudhui duniani, baadhi ya watazamaji wa maudhui ya kulipia mtandaoni wamekuwa wakitazama aina ya maudhui hayo na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii” amesisitiza Nnauye.

Waziri alionya kuwa Serikali haitamuonea muhali mtu yeyote atakaehusika na kusambaza maudhui yenye viashiria vya ushoga.

“Nichukue nafasi hii kutoa onyo kwa yeyote atakayesambaza maudhui ya aina hiyo kwa jamii. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayehusika,” alisisitiza Waziri na kuongeza.

“Niendelee kusisitiza kuwa wajibu wa kuwalinda Watoto kutokana na maudhui yasiyofaa hasa kwenye mitandao ya kijamii ni wa kwetu sote ikianzia kwa Wazazi, Walezi na Mashuleni ambapo Watoto wetu hutumia muda mwingi huko wakiwa masomoni,” ameonya Waziri Nape.

Hata hivyo ameipongeza Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kazi nzuri ya kusimamia maudhui nchini; na kuongeza kuwa ni wakati sahihi kwa wananchi wote kulinda maadili ya nchi.

“Serikali kwa kutumia vyombo vyake, itaendelea kufuatilia kwa karibu wasambazaji wa maudhui yasiyozingatia maadili ya mtanzania ikiwa ni pamoja na yale yenye viashiria vya ushoga,” ameongeza.

Sambamba na hayo Waziri Nape ametoa wito kwa wazazi, walezi na walimu kuhakikisha kuwa wanawalinda watoto wao na utandawazi ambao ukitumiwa vibaya madhara yake ni mabaya kwa jamii na Taifa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger