Sunday, 24 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 24,2022

Magazetini leo Jumapili April 24,2022














Share:

Saturday, 23 April 2022

MZEE WA MIAKA 95 AUAWA AKITUHUMIWA KUFANYA USHIRIKINA



Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 95 wa Kijiji cha Lwanzali kilichopo Lupembe Halmashauri ya Wilaya ya Njombe amekutwa ameuawa ndani ya nyumba yake huku upelelezi wa awali ukionesha kuwa chanzo ni kutokana na Mzee huyo kutuhumiwa kufanya ushirikina katika Familia yake.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema "Tumejaribu kwenda katika eneo lile na imebainika huyu Mzee walikuwa walikuwa wanamtuhumu kuwa anafaya mambo kishirikina katika Familia yake”

Kamanda Issah amesema Polisi wanaendelea kuchunguza ili kubaini ni nani aliyehusika na mauaji hayo ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Share:

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS AMBAYE PIA NI AFISA MTENDAJI MKUU WA WOODROW WILSON


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Woodrow Wilson International Center Balozi Mark Green mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Woodrow Wilson International Center Balozi Mark Green katika Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Woodrow Wilson International Center Balozi Mark Green katika Mdahalo uliofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mdahalo katika Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Woodrow Wilson International Center Balozi Mark Green katika Mkutano uliofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022.

Share:

RAIS SAMIA AZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA WAFANYABIASHARA WA MAREKANI USAFBC-WASHINGTON NCHINI MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Marekani Suzanne Clark mara baada ya mazungumzo yao katika Ofisi za Chemba hiyo Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Marekani Suzanne Clark wakati akiwasili katika Ofisi za Chemba hiyo Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa Wafanyabiashara wa Marekani uliofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi za Chemba ya Biashara ya Marekani Jijini Washington nchini Marekani tarehe 22 Aprili, 2022. PICHA NA IKULU

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 23,2022

Magazetini leo Jumamosi April 23 2022

Share:

WAZIRI MKUU AWATAKA WAKUU WA MIKOA, WILAYA KUTEMBELEA MASOKO NA MADUKA WACHUKUE HATUA KWA WANAOPANDISHA BEI



*Awataka pia wahamasishe wananchi kuhusu Sensa ya Makazi na Watu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wafanye ziara kwenye masoko na maduka ili kupata hali halisi ya bei za bidhaa na wachukue hatua kudhibiti upandaji holela wa bei hizo.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Ijumaa, Aprili 22, 2022) wakati akizungumza na viongozi wa mikoa na wilaya kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye kikao kazi alichokiendesha kwa njia ya mitandao (video conference) kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

“Tumepata malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba bidhaa nyingi zimepanda bei, ninyi ni Wenyeviti wa Kamati za Bei na Kamati za Kodi kwenye mikoa na wilaya zenu. Upandaji wa bei sasa umekuwa holela. Ni jukumu lenu kufanya ufuatiliaji wa bei za mazo katika masoko yenu.”

Waziri Mkuu amesema ziko bidhaa ambazo zinazalishwa nchini kama vile nondo au saruji ambazo hazipaswi kupanda bei hasa baada ya kutolewa tamko na Waziri wa Fedha na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwamba wameshaongea na wenye viwanda na wakakubaliana kuwa bidhaa zote za ndani zinapata nafuu ya kodi.

“Sasa iweje hali iendelee kuwa vilevile?”, amehoji na kuongeza: “Vyakula vinavyozalishwa nchini kama mchele, Shinyanga mchele mwingi, Tabora mchele mwingi, Mbeya nako mchele mwingi kuna sababu gani ya kupadisha mchele wakati unazalishwa nchini?”

“Kama ni mahindi au mihogo inalimwa huko kwenu, umbali wa mazao yanakolimwa mnaujua, iweje bei zipande? Nenda mpite kwenye masoko na kwenye maduka mpate bei za kila siku za maeneo yenu. Kukaa kimya na masoko yako kwenu, na bidhaa ziko kwenu na walaji wako kwenu halafu hamchukui hatua, tutakuwa hatufanyi vizuri.”

“Ninawaagiza, fanyeni ziara kwenye masoko yenu, fanyeni tafiti na mtathmini ni kwa nini bei zinapanda. Mchicha unapandaje bei, ni kwa sababu ya nini? Zungumzeni na tuone mkianza kudhibiti hiyo hali. Na Kama kuna maeneo bei inapanda kiholela, hakikisheni bei inashuka iende kwenye bei halisi ili tuwasaidie wananchi.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao waongeze hamasa kwa wananchi ili waweze kushiriki kwa wingi kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu.

“Hamasa ni muhimu kwa wananchi wa makundi yote. Tutumie wadau mbalimbali kwenye maeneo yetu kama vile Wabunge, madiwani, viongozi wa masoko, viongozi wa vilabu vya michezo na viongozi wa kijamii ili watusaide kuhamasisha wananchi.”

Share:

ALIYEVUNJA VIOO VYA SHULE GAIRO ATUPWA JELA




NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.

Mtu moja aliyevunja vioo vya shule ya sekondari Kibedya iliyopo Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela huku mlinzi wa shule hiyo akihukumiwa miezi sita kwa kosa la kuacha lindo lake na kusababisha uharibifu wa uvunjwaji wa vioo kumi na mbili katika shule hiyo.

Kuvunjwa kwa vioo kumi na mbili vya madarasa sita yaliojengwa kwa fedha za miradi ya Uviko 19 katika shule ya sekondari Kibedya Wilaya ya Gairo kumeisababishia hasara serikali ambapo kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano zimetumika kukarabati madirisha ya madarasa hayo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Kibedya Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bwana Jabiri Makame amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa waliofanya uharibifu huo ikiwemo kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa alivunja vioo hivyo huku mlinzi wa shule hiyo akihukumiwa miezi sita jela.

Aidha makame amesema serikali haitomfumbia macho mtu yeyote atakaye haribu mali za umma katika Wilaya hiyo huku akiitaka taasisi ya kuzuiya na kupambana na rushwa TAKUKURU Wilaya ya Gairo kufanya uchunguzi kwenye miradi ya ujenzi wa shule na kubaini kama kuna ubadhirifu wa wowote wa matumizi ya fedha.

Makame amefikia hatua hiyo ya kuigiza TAKUKURU baada ya kufanya ziara katika shule ya sekondari Kibedya ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,vyoo pamoja na maabara kwa ajili ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kubaini uwepo wa ubadhirifu wa matumizi ya fedha za umma.

“Niwaombe wananchi wa Kata ya Kibedya kuacha tabia kuharibu miundombinu ya miradi ya maendeleo sio kwenye shule tu hata kwenye miradi mingine kwani atakaye fanya uharibifu wowote atachukuliwa hatua za kisheria na niwambie tu serikali inamkono mrefu.” Alisema DC Makame.

“Nilifika hapa niliambiwa viti vipo kwa fundi na vitaletwa baada ya kukamilika lakini leo pia napewa taarifa tofauti na viti sivioni hivyo kwa sintofahamu hii naomba niiagize TAKUKURU kufanya uchukuzi hapa na Wilaya nzima ya Gairo juu ya matumizi ya fedha zilizoletwa na serikali kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.”Alisema

kwa upande wake diwani wa kata ya kibedya Bunditi Masatu amelaani kitendo kilichofanyika cha kuvunjaji wa vioo vya shule hiyo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kuharibu mali za sekali kwani atakaye bainika sheria itafuata mkondo wake.
Share:

Friday, 22 April 2022

RATIBA YA YA KUCHUKU NA KUREJESHA FOMU ZA MAOMBI YA UONGOZI CCM NGAZI YA TAWI


 Ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu za maombi ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya tawi.
i. Mwenyekiti wa CCM wa Tawi.


ii. Katibu wa CCM wa Tawi.


iii. Katibu wa Siasa na Uenezi.


iv. Wajumbe watano(5) wa Mkutano kuu wa CCM ya Kata/Wadi.


v. Wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya CCM ya Tawi.


vi. Mjumbe mmoja(1) wa Mkutano kuu wa CCM wa Jimbo na Wilaya
Share:

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI MWANZA, YATOA ZAWADI KWA WATOTO


Benki ya CRDB imewafuturisha wateja wake jijini Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni wa benki hiyo kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu wanaoishiriki mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Hafla ya Iftar hiyo imefanyika Alhamisi Aprili 21, 2022 katika ukumbi wa Gold Crest mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya Ilemela Hassan Masala na kuhudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza Hassan Kabeke.


Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta alisema benki hiyo imekuwa na desturi ya kujumuika pamoja na wateja wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kupata Futari ya pamoja na kuimarisha mahusiano miongoni mwa pande zote mbili.


Sitta alitumia fursa hiyo waeleza waumini wa dini ya Kiislamu kwamba benki ya CRDB imeanzisha huduma ya Al-Barakah Banking inayoendana na misingi ya dini hiyo ikiwa ni pamoja na mikopo isiyo na riba na hivyo kuwaepusha kuingia kwenye dhambi ya riba.


Mkuu wa Huduma ya Al-Barakah Banking (Islamic Banking), Rashid Rashid alisema uanzishwaji wa huduma hiyo unadhihirisha kauli mbiu ya namna benki ya CRDB isemayo 'Benki Inayomsikiliza Mteja' ambapo kupitia maoni ya wateja wake iliamua kuanzisha huduma ya Al-Barakah.


Rashid aliongeza kuwa akaunti zinazofunguliwa kupitia huduma ya Al- Barakah zina uangalizi maalum unaohakikisha hazitumiki kwenye miamala inayokinzana na maadili ya imani ya kiislamu ikiwemo riba na kuwaondolea changamoto iliyokuwepo zamani ya kuhifadhi fedha kwenye mabenki yanayokinzana na misingi ya sharia.


Naye Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke aliishukuru benki ya CRDB kwa kuwaondolea waislamu na wasio waslamu dhambi ya kuingia kwenye riba baada ya kuanzisha huduma ya Al- Barakah kwani riba ni dhurma kubwa na watu wengi wamefirisika kutokana na kuingia kwenye dhambi hiyo, akisema "yeyote anayeingia kwenye riba ajiandae kupigana vita na Mwenyezi Mungu, CRDB wametutoa huko".


Sheikh Kabeke aliagiza misikiti, Kata na Wilaya zote za Mkoa Mwanza kutii maelekezo ya Mufti wa Tanzania ya kutaka akaunti zote za BAKWATA nchini kufunguliwa ndani ya huduma ya Al- Barakah. "Tumeanzisha mchakato wa kujenga Vituo vya Afya katika Wilaya zote saba za Mkoa Mwanza, akaunti ambayo tumewaomba waislamu na wasiokuwa waislamu wachangie humo michango yao ni akaunti ya Al-Barakah" alisema Sheikh Kabeke.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala alisema Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na benki ya CRDB katika kuwahudumia watanzania kupitia huduma zake zenye ubunifu ikiwemo Al-Baraka Banking inayowapa wasilamu huduma zinazotimiza matakwa ya dini yao.


"Tunatambua kazi kubwa mnayoifanya, miradi yetu mingi, fedha zetu nyingi na biashara kubwa, Serikali inafanya na benki ya CRDB, lakini mmeanzisha huduma ambazo zinagusa makundi mbalimbali kama hii ya Al-Barakah, kwa kweli tunaiona nia yenu njema" alisema Masala wakati akizungumza kwenye Iftar hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Ziwa akizungumza kwenye Iftar hiyo.
Meneja wa benki ya CRDB akizungumza kwenye Iftar iliyofanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa Matawi Benki ya CRDB, Boniventure Paul alisema katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, lisha ya benki hiyo kujumuika pamoja na wateja wake kwenye futari pia hutoa msaada vyakula/ futari kwenye vituo vya kulelea watoto vyenye uhitaji mkubwa ili kuwawezesha watoto na walezi wao kutekeza vyema ibada ya swaum.
Mkuu wa Islamic Banking (Al-Barakah), Rashid Rashid akizungumza kwenye hafla hiyo.
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akizungumza kwenye Iftar hiyo.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwenye Iftar hiyo ambayo aliwahimiza pia waislamu kuendelea kutenda matendo mema, kuswali na kujinyenyekeza mbele za Mwenyezi Mungu nyakati zote na si wakati wa Mwezi Mtukufu tu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akipata riziki ya Iftar iliyoandaliwa na benki ya CRDB jijini Mwanza.
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akiwa kwenye Iftar hiyo.
Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian Massaga akichukua riziki kwenye Iftar hiyo akiwa ameambatana na wateja mbalimbali wa benki ya CRDB.
Wateja wa benki ya CRDB jijini Mwanza wakipata riziki ya Iftar.
Wateja wa benki ya CRDB jijini Mwanza wakiwa kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali akiwemo Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza Hassan Kabeke (katikati) wakipata Iftar iliyoandaliwa na benki ya CRDB jijini Mwanza.
Wateja na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa kwenye Iftar hiyo.
Uongozi wa benki ya CRDB umetumia fursa hiyo pia kukabidhi zawadi ya bidhaa mbalimbali za vyakula kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika Vituo mbalimbali jijini Mwanza.

Share:

WAFAMASIA WATOA TAMKO ZITO WATOA HUDUMA WASIO NA TAALUMA YA DAWA KUHUDUMIA KWENYE MADUKA YA DAWA


Mfamasia na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafamasia Tanzania, Benson Katundu katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Ijumaa Aprili 22,2022 kwa ajili kukemea ukiukwaji wa sheria inayosimamia maduka ya dawa muhimu.
Mfamasia na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafamasia Tanzania, Benson Katundu katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Ijumaa Aprili 22,2022 kwa ajili kukemea ukiukwaji wa sheria inayosimamia maduka ya dawa muhimu


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kufuatia kusambaa kwa video kadhaa mitandaoni zikionesha watoa huduma wasio na taaluma ya dawa wakihudumia katika maduka ya dawa kinyume na miongozo sheria na taratibu zinazoongoza biashara ya maduka ya dawa muhimu nchini, Chama cha Wafamasia Tanzania (Phamarceutical Society of Tanzania PST), kimekemea na kulaani vikali vitendo hivyo kwani ni hujuma kwa afya za Watanzania.


Akizungumza kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari Mjini Shinyanga leo Ijumaa Aprili 22,2022, Mfamasia na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafamasia Tanzania, Benson Katundu amesema wanalaani vitendo vya watoa huduma katika maduka ya dawa au wamiliki wa maduka ya dawa kuajiri watoa huduma wasio na taaluma ya dawa kutoa huduma hizo jambo ambalo ni hatari kwa afya za Watanzania.


Amesema watoa huduma katika maduka mengi wameonekana wakifanya vitendo visivyokubalika katika maduka hayo ikiwemo, uchomaji wa sindano za uzazi wa mpango, kufanya vipimo vya magonjwa mbali mbali kwenye maduka kinyume na utaratibu, uzalishaji wajawazito katika maduka ya dawa, kufanya matibabu yasiyoruhusiwa katika maduka hayo.


Kitundu ameongeza kuwa pia kuna uuzwaji holela wa dawa za moto (antibiotics) zisizoruhusiwa kuuzwa katika maduka hayo ya dawa muhimu ambazo zina athari ikiwemo kusababisha usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, kusababisha ulemavu na hata kusababisha vifo.


“Tunakemea na kulaani vitendo hivi kwani dawa ni sumu ambazo zinaweza kuleta ulemavu wa kudumu ama kupoteza maisha endapo hazitatumiwa kwa usahihi”,amesema Kitundu.


Katibu Mkuu huyo wa PST amesema wanaliomba Baraza la Famasi kuangalia upya mifumo yake ya ukaguzi wa maduka ya dawa muhimu yaliyoko mijini na vijijini kubaini uhalali wake ili kupunguza vitendo hivi vya ukiukwaji wa taratibu za utoaji huduma katika maduka hayo, jambo ambalo ambalo linazuia baadhi ya watu kutopata huduma za afya katika vituo vilivyoidhinishwa kisheria.


“Lengo la uanzishwaji wa maduka ya dawa muhimu ((DLDM) lilikuwa ni kusogeza huduma za dawa kwa wananchi waishio maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji .Tumeendelea kushuhudia utitiri wa maduka ya dawa muhimu yakiendelea kufunguliwa maeneo ya mijini pasipo kufuta utaratibu uliowekwa”,ameongeza Kitundu.


Amebainisha kuwa kada ya ufamasia imegawanyika katika ngazi kuu tatu ambazo ni Wateknolojia dawa wasaidizi wanaosoma kwa miaka miwili 2, Wateknolojia dawa wanaosoma kwa miaka mitatu na Wafamasia wanaosoma kwa miaka minne na kufanya internship kwa mwaka mmoja. hivyo wataalamu wote hawa hutakiwa kufanya mtihani maalumu wa kusajiliwa na baraza la Famasi Tanzania ili kuweza kupatiwa leseni za kutekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali.


Amesema upo ushahidi wa watoa huduma wengi waliopata mafunzo ya utoaji dawa (Accredited Drug Dispensing Outlet- ADDO) wakitekeleza majukumu mengine nje ya uuzaji wa maduka ya dawa huku wakiajiri watu wasio na taaluma ya uuzazi dawa za binadamu katika maduka yao.


“Chama cha Wafamasia Tanzania kinaliomba Baraza La Famasi Tanzania Kutathimini upya kama kuna haja na hitaji la kuendelea kutoa mafunzo ya (ADDO) ilhali wataalam wa dawa wenye mafunzo ya miaka miwili na miaka mitatu na miaka mitano wakiendelea kuzalishwa kutoka vyuo vya kati vya afya 218 vikiwemo vya serikali na binafsi, na vyuo vikuu vya afya vinne vilivyopo nchini”,amesema Kitundu.

“Hakuna kada ya afya inayotoa mafunzo ya mwezi mmoja na watu hao kuingia kuwahudumia watanzania, hivyo Chama cha Wafamasia tunaomba mafunzo haya ya ADDO kusitishwa kwani afya ya mwanadamu haijaribiwi tuwape wataalamu nafasi ya kutekeleza majukumu yao kwa ustawi wa taifa letu”,ameeleza.


Katika hatua nyingine uongozi wa Chama cha Wafamasia Tanzania unawaelekeza wafamasia wa mikoa na wafamasia wa Halmashauri kuongeza weledi katika kusimamia kwa umakini mkubwa uanzishwaji wa maduka ya dawa muhimu katika maeneo yao na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa maduka hayo ili kuhakikisha maduka ya dawa muhimu yanahudumiwa na wataalamu wenye sifa za kutoa huduma za dawa kwa wananchi.


“Uongozi wa Chama cha Wafamasia tunaendelea kuwasistiza wataalamu wa dawa wote nchini kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kufuata miongozo taratibu na kanuni za taaluma bila kuvunja sharia ya nchi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watanzania.

Aidha chama hakitamfumbia macho mtaalamu yeyote atakaethibitika pasi na shaka kukiuka misingi na maadili ya taaluma hii adhimu ya ufamasia atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na tuwaomba wananchi kuwafichua watu wasio na sifa ya kutoa huduma katika maduka ya dawa”,amesema Kitundu.


Katundu ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawateua wafamasia Bi. Rosemary William Slaa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Bohari ya dawa (MSD) na Mfamasia Mavere Tukai kuwa Mtendaji mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) akibainisha kuwa ni imani ya PST kuwa wataongeza ufanisi katika chombo hicho.


“Pia tunaipongeza serikali kutoa nafasi za ajira hususan katika sekta ya afya kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya. Chama kinaziomba wizara zinazohusika katika ajira hizo kutoa kipaumbele pia kwa kuajiri wataalam wa dawa wengi ili kuweza kuongeza ufanisi wa huduma za kifamasia katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kuhakikisha dawa bora na vifaa tiba bora vinapatikana kwa kufanya maoteo sahihi kama wataalam wa dawa ili kuhakikisha matibabu sahihi yanatolewa kwa wagonjwa”,amesema Kitundu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger