Monday, 18 April 2022

BARRICK YADHAMINI KONGAMANO LA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU


Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa makampuni mbalimbali wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa makampuni mbalimbali wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiuliza swali wakati wa wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick
Baadhi ya watendaji waandamizi kutoka makampuni mbalimbali wakisikiliza hoja za wanafunzi wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick

***
Kampuni ya Barrick imedhamini na kushiriki maonesho ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliyoandaliwa na taasisi ya AISEC Tanzania, na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kampasi ya Mlimani.

Kupitia maonyesho hayo wanafunzi huweza kujua jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kujifunza, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Mameneja Waandamizi wa Barrick, walishiriki katika maonesho ya kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake sambamba na mpango wake wa ukuzaji wa vipaji kwa wafanyakazi wake.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 18,2022


Magazetini leo Jumatatu April 18 2022



Share:

Sunday, 17 April 2022

ASKOFU MERY MUTAFUNGWA AWATAKA WANANCHI KUJIEPUSHA NA MAMBO YA UOVU SIKUKUU YA PASAKA

Askofu wa Makanisa ya Mlima wa Bwana Tanzania Mery Mutafungwa akihubiri wakati wa Ibada ya usiku wa mkesha wa Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mlima wa Bwana Tanzania lililopo katika Kata ya Kashai Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Na Mbuke Shilagi Kagera.
Askofu wa Makanisa ya Mlima wa Bwana Tanzania Mery Mutafungwa amewataka wananchi wote wanaposherehekea sikukuu ya Pasaka kujiepusha na mambo ya uovu.

Ameyasema hayo wakati wa Ibada ya usiku wa mkesha wa Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mlima wa Bwana Tanzania lililopo katika Kata ya Kashai Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Askofu Mery amesema kuwa watu wote wanatakiwa kujiepusha na mambo ya uovu pamoja na makundi mabaya katika kipindi hiki cha sikukuu.

Askofu Mery Mutafungwa ameongeza kuwa Sherehe ya Pasaka ni kumbukumbu ya Ufufuko wa Mkombozi wa Ulimwengu Yesu Kristo hivyo watu wanaposherehekea wanatakiwa kusherehekea kwa utulivu na amani kwa kufanya matendo mema na yakumpendeza Mungu.

Amewataka watu wote kuendelea kufanya yale matendo mema ambayo walitenda wakati  Kwaresma na kwamba imekuwepo watu wanapo maliza mfungo wa Kwaresma wanasahau kuendelea na unyenyekevu badala yake wanakuwa na matendo ya yasiyompendeza Mungu.

Ametoa wito kwa wazazi wanap toka na watoto kuelekea katika fukwe za ziwa kuwa na uangalizi mkubwa kwa watoto hao ili kuondoa usumbufu kwa Jeshi la Polisi na kwamba wanapokuwa makini na uangalizi mzuri kwa watoto wanapunguza usumbufu kwa jeshi la polisi pamoja na madhara yanayojitokeza.
Askofu wa Makanisa ya Mlima wa Bwana Tanzania Mery Mutafungwa akihubiri wakati wa Ibada ya usiku wa mkesha wa Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mlima wa Bwana Tanzania lililopo katika Kata ya Kashai Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Askofu wa Makanisa ya Mlima wa Bwana Tanzania Mery Mutafungwa akihubiri wakati wa Ibada ya usiku wa mkesha wa Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mlima wa Bwana Tanzania lililopo katika Kata ya Kashai Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Kushoto ni Mchungaji msaidizi wa Kanisa la Mlima wa Bwana Tanzania lililopo kata ya Kashai mtaa wa Kilimahewa Mch. Frenk Thomas
Kulia ni Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Bwana Tanzania lililopo Kemondo Bukoba vijijini Mch. Seperatus Kashasha
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Bwana Tanzania lililopo kata ya Kashai mtaa wa Kilimahewa Mch.Fransisco Felician akizungumza kanisani
Baadhi ya waumini wa Mlima wa Bwana Tanzania waliohudhuria Ibada ya usiku ya Pasaka

Share:

WIZARA YA AFYA YATANGAZA AJIRA MPYA



Wizara ya Afya nchini Tanzania kupitia kwa Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Abel Makubi imetangaza nafasi za ajira 1650 kwa wataalamu wa kada mbalimbali za afya nchini.


Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa imepata kibali cha kuajiri ambapo wataalamu hao wataajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi ambavyo vipo chini ya uendeshaji wa moja kwa moja wa wizara hiyo.

Miongoni mwa nafasi hizo, zipo za madaktari bingwa (25), madaktari (215), wafamasia(15), maafisa maabara(62), wateknolojia (dawa, maabara, mionzi, macho-155), maafisa uuguzi (140), maafisa uuguzi wasaidizi (467), wauguzi (140), wakemia (2),

Wengine ni madaktari wa afya kinywa na meno (15), tabibu meno (19), watoa tiba kwa vitendo (15), wazoeza viungo kwa vitendo(31), maafisa wazoeza viungo (33), maafisa afya mazingira(40), wasaidizi wa afya (134), wahandisi vifaa tiba (17), wateknolojia vifaa tiba (40) , watunza kumbukumbu wa wfya (10) na madereva (4).
 
Via - EATV
Share:

Saturday, 16 April 2022

GEE KARANGA NDIYO HABARI YA MJINI... KARANGA BORA NA SALAMA KWA AFYA YAKO

Gee Karanga ni watengenezaji na wauzaji maarufu wa Karanga kwa bei ya Jumla na Rejareja ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga. Karanga hizi ni tamu sana, zina mayai na viungo muhimu kwa afya yako .Tunapatikana Mtaa wa Soko B, Old Shinyanga. Wasiliana nasi 0623025708 Instagram @gee_karanga



Share:

BAKWATA, KIVULINI WAENDESHA KONGAMANO LA MAADILI WILAYANI MISUNGWI


Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto (KIVULINI) limeendesha kongamano la kuhamasisha maadili katika jamii wilayani Misungwi ili kusaidia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kongamano hilo limefanyika Jumamosi Aprili 16, 2022 katika Msikiti Mkuu wa Waslamu Misungwi na kuhudhuriwa na waumini mbalimbali wa dini hiyo ambapo lengo ni makongamano ya aina hiyo kufanyika katika Wilaya zote za Mkoa Mwanza.


Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke amesema kongamano hilo la Malezi Bora, Tabia Njema na Misingi ya Ndoa linalenga kujadili na kuandaa mapendelezo yatakayoeleza sababu za kuporomoka kwa maadili katika jamii na kuwasilishwa serikalini kwa ajili ya hatua za utekelezaji.


Amesema kuporomoka kwa maadili katika jamii kunasababisha ufa katika ndoa ambapo matokeo yake ni kuibuka kwa wimbi la watoto wanaokimbilia mtaani kwa sababu ya kukosa malezi bora.


Sheikh Kabeke amekemea tabia ya wazazi hususani akina baba kukosa muda wa kulea watoto akisema wako ‘busy’ na kuacha watoto kulelewa na akina mama pekee ambapo matokeo yake ni kuibuka kwa ufa uitwao liwatwi (ulawiti).


“Baada ya maadili kuporomoka, watoto wadogo wa kindagaten, shule za Msingi, Sekondari na vyuo wanaangukia kwenye hatari ya kuingiliana kinyume na maumbile, mbaya zaidi imefika hatua baadhi ya familia wanawaalika hadi mashoga kusherehesha sherehe zao, je ni kweli tumeupokea ushoga? (sauti zinasikika hapa), huo ni ufa kwenye ndoa”, ameonya Sheikh Kabeke.


Sheikh Kabeke ameongeza kuwa kukosekana kwa maadili katika jamii pia kumesababisha unyanyasaji wa kijinsia kwenye ndoa ambapo imekuwa kawaida mme kumnyanyasa mke na mke kumnyanyasa mme.


“Imefika mahali wanaume hawafanyi kazi wanabaki kwenye kahawa, wanawake ndio asubuhi utakutana nao kwenye daladala wanahangaika na mabeseni kwenda kutafuta hela ya kutunza familia, mme akirudi jioni anaanza kuhoji chakula”, Sheikh Kabeke amekemea tabia hiyo akiwataka wanaume kuwajibika katika ndoa zao.

Pia Sheikh Kabeke ametoa rai kwa wanandoa kuwa na muda wa kukaa pamoja na kuzungumza masuala ya kulea familia, akisema “Mwanamke anatumia kanga kufikisha ujumbe kwa mmewe kwa sababu hakuna muda wa kuongea, inabidi avae kanga, utamaliza mabucha yote lakini nyama ni ile ile. Hivi ni sawa tuwasiliane kwa mfumo huo wa kanga? Tena ndoa za kiislamu? Wanandoa wanawekeza muda mwingi kwenye simu kuliko kukaa pamoja na kujadili masuala ya ndoa.


Katika hatua nyingine Sheikh Kabeke amelipongeza shirika la KIVULINI kwa jitihada zake kubwa za kusaidia kurudisha maadili kwenye jamii, kuwasiaidia watu waliodhalilishwa na wenye matatizo mbalimbali yanayohusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.


“Mungu awape nguvu tuzunguke nao Mkoa mzima wa Mwanza. Tunataka baada ya Ramadhan tutoke na andiko litakalosaidia maadili katika ndoa kwani sisi BAKWATA tunapinga watoto wa mitaani, Kivulini wanapinga na Misungwi naamini mnapinga”, amesema Sheikh Kabeke.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema wimbi kubwa la ndoa zinazofungwa mwezi wa Shaban linapaswa kujadiliwa kwani nyingi hazidumu na matokeo yake zinakuwa chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani.

“Unakuta mwanaume anatafuta mwanamke wa kumtumikisha, ampikie futari, akijinasibu kwamba funga yake itapokelewa. Inabidi wafungisha ndoa, masheikh wetu hili nalo tulijadili, huenda kuna mapungufu mengi katika misingi ya kuzilea na kuzifuatilia hizi ndoa ndio maana hazidumu”, amesema Ally.


Yassin pia amewasihi wanandoa kuishi kwa furaha na kutaniana kwani ukali umezidi miongoni mwa wanandoa tofauti na wapokuwa nje na nyumbani.

 “Unakuta mwanaume akiwa kwa mama ntilie anamtania, leo umependeza ila akiwa kwa mkewe ni mwendo wa kumuamrisha, wewe njoo hapa, chakula kiko wapi” ,amedokeza Ally.


Lakini pia Ally amesisitiza kuwa jukumu la kulea watoto ni la wazazi hivyo ni vyema wakaishi kwa maelewano na kuwalea watoto katika misingi ya maadili inayozingatia kumcha Mungu, kuwapa haki za msingi ikiwemo kupata elimu kwani Serikali imeboresha mazingira ya kuhakikisha kila motto anakwenda Shule.

Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya Misungwi, Sheikh Hussein Hussein amesema wanandoa wanapokuwa na uchumi imara, watoto wanaepuka hatari ya kukimbilia mitaani na hivyo kushauri vijana wa kiislamu kutobweteka na kuunda vikundi vya uzalishaji mali.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo akiwemo mzee Hussein Manyilizu wamesema ndoa nyingi hazidumu kwa sababu vijana hukutana kwenye mitandao ya kijamii na kuoana tofauti na zamani ambapo wazee walikuwa wakifanya utafiti wa familia ya kuoa, akisema “siku hizi wanaangalia utajiri na siyo maadili, matokeo yake ndoa hazidumu”.


Naye Ibrahim Mhebi amewaasa vijana wenzake kufanya kazi badala ya kuamkia kwenye vijiwe vya kahawa na michezo haramu ya kubashiri kwani inadhorotesha uchumi wao na kuzikimbia familia. “Una elfu 50 unaamkia kwenye michezo ya ku-BET unaliwa yote, hapo ndoa Sheikh lazima uikimbie. Mimi naomba BAKWATA ije na mifumo ya kutusaidia vijana kujikwamua kiuchumi hatua itakayotusaidia kutunza familia” ameomba Mhebi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke (katikati) akifungua kongamano la Malezi Bora, Tabia Njema na Misingi ya Ndoa lililofanyika wilayani Misungwi. Kulia ni Sheikh wa BAKWATA Wilaya Misungwi, Sheikh Hussein Hussein na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji shirika la KIVULINI, Yassin Ally.
Sheikh wa BAKWATA Wilaya Misungwi, Sheikh Hussein Hussein (kulia) akizungumza kwenye kongamano hilo. Katikati ni Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally.
Washiriki wa kongamano hilo ambao ni waumini wa dini ya kiislamu wakimsikiliza Sheikh wa Wilaya Misungwi, Sheikh Hussein Hussein.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akichangia mada kwenye kongamano hilo lililoandaliwa na BAKWATA Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na KIVULINI.
Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Ibrahim Mhebi akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Kongamano hilo, pamoja na mambo mengine linalenga kuhamasisha wanajamii kuzingatia maadili bora, kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na kusomesha watoto/ kuondoa utoro mashuleni ambapo baada ya kutamatika katika wilaya zote za Mkoa Mwanza, BAKWATA itaandaa mapendekezo yatakayowasilishwa serikalini kwa ajili ya utekelezaji.
Mmoja wa washiriki akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Mshiriki akichangia kongamano hilo.
Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo lililofanyika katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA wilayani Misungwi.
Jumbe mbalimbali kuhusiana na kongamano hilo.
Share:

JESHI LA POLISI KAGERA LAWATAKA WANANCHI KUSHEREHEKEA KWA AMANI SIKUKUU YA PASAKA


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera ACP William Mwampaghale

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limewataka wananchi hasa waumini wa dini ya Kikristo kusherehekea kwa amani sikukuu ya Pasaka na kwamba jeshi hilo litaimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mkoa.


Haya yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera ACP William Mwampaghale wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwakwe, kuhusu namna gani wamejipanga ili kuhakikisha Sikukuu inaisha salama.

Kamanda huyo amesema kuwa Jeshi la Polisi watakuwa kila mahali ikiwamo katika makanisa, kumbi za starehe, barabarani na kila mitaa ili kuhakikisha usalama unakuwepo.

ACP Mwampaghale ameongeza kuwa wananchi wote watakaokwenda katika maeneo ya fukwe wanapaswa kuwa makini na kusikiliza maelekezo ya askari, na kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.

"Lakini pia wazazi kuweni makini na watoto, msiwaruhusu kwenda ufukweni mwa ziwa peke yao, ni hatari kwa usalama wao, kama mtaona lazima watoto wenu waende huko, basi wawe na mtu mzima ambaye ni mzazi au mlezi", amesema.


Aidha amewataka wananchi kuacha ulinzi nyumbani ili kuepusha vibaka kutumia fursa ya Sikukuu kuvunja nyumba na kuiba.

Amewataka pia madereva wanaojaza abiria na kuendesha magari na pikipiki kwa kasi kuacha tabia hiyo, na kuwataka pia kuepuka kutumia kilevi wakati wa siku kuu ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger