Tuesday, 12 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 12,2022

Magazetini leo Jumanne April 12 2022
Share:

BONDIA WA TANZANIA HASSAN MWAKINYO AVULIWA TAJI LA UBINGWA

Bondia wa Tanzania Hassan Hamza maarufu kama Mwakinyo amevuliwa taji lake la ubingwa wa Afrika (African Boxing Union) mara baada ya muda kupita bila kutetea taji hilo.

Kuvuliwa kwa taji hili kunakuja ikiwa imepita miezi michache tangu avuliwe taji lingine la ubingwa wa mabara la WBF.

Mwakinyo alitwaa ubingwa wa Afrika baada ya kumchapa Muangola Maiala Antonio, mwezi mei mwaka jana.

ABU ilimuondoa Mwakinyo kwenye orodha ya mabingwa na kumshusha hadi nafasi ya tatu ya ubora kwenye uzani wa super welter, nafasi ya kwanza ikishikwa na Wale Omotoso kutoka Nigeria, namba mbili ikishikiliwa na Patrick Alotey kutoka Ghana.

ABU pia imeweka wazi nafasi ya ubingwa.

Mwakinyo sasa hana taji la ubingwa analoshikilia. Lakini mbali na kuvuliwa ubingwa huo bado anashikilia nafasi ya 14 duniani kwenye uzito wake wa super welter.

Chanzo - BBC Swahili
Share:

Monday, 11 April 2022

RAIS SAMIA AFUTARISHA VIONGOZI NA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akifutari pamoja na Viongozi wa Dini, Wanasiasa, Wazee na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Futari aliyoiyandaa Jana 10 April 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Share:

NEMC YAANDAA MKUTANO WA KAMATI YA TAIFA YA BINADAMU NA HIFADHI HAI.


Mgeni Rasmi Dkt. Menan Jangu ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira(NEMC) akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kupitia na kuidhinisha (kuridhia) uteuzi wa eneo la Rufiji, Mafia na Kilwa(RUMAKI) kuingia katika mtandao wa dunia wa binadamu na Hifadhi hai uliofanyika mjini Morogoro. Waliokaa kulia ni Meneja wa Tafiti za Mazingira kutoka NEMC Bi Rose Mtui na kushoto ni Dkt. Henry Ndangalasi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria Mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani) alipokua akifungua Mkutano wa kupitia na kuidhinisha (kuridhia) uteuzi wa eneo la Rufiji, Mafia na Kilwa(RUMAKI) kuingia katika mtandao wa dunia wa binadamu na Hifadhi hai mjini Morogoro.


Mgeni Rasmi katika Mkutano huo Dkt Menan Jangu (wa pili kushoto) ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Binadamu na Hifadhi Hai wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati hiyo uliofanyika mjini Morogoro.

****************************

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeandaa Mkutano wa kupitia na kuidhinisha uteuzi wa eneo la Rufiji, Mafia, Kibiti na Kilwa(RUMAKI) kuingia katika mtandao wa dunia wa binadamu na Hifadhi hai.

Mkutano huo umefunguliwa na Dkt Menan Jangu aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NEMC na umefanyika mjini Morogoro na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Binadamu na Hifadhi hai kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali.

Aidha akiongea katika Mkutano huo Dkt. Jangu amesema dhumuni kubwa la mkutano huo ni kupitia kwa pamoja na kuridhia mapendekezo ya uteuzi wa eneo la RUMAKI kuingia katika mtandao wa dunia wa binadamu na hifadhi hai kwani kufanya hivyo ni muhimu kwa ustawi wa mazingira.

“Lengo la Mkutano huu ni kupitia mapendekezo na kujiridhisha kwa ajili ya maandalizi ya kuridhia RUMAKI kuingia katika mtandao wa dunia wa Binadamu na hifadhi hai”

Naye Meneja wa Tafiti za Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bi Rose Salema amesema kuwa Hifadhi hai za Taifa ni muhimu sana kwani zinamshirikisha binadamu katika maeneo yake na pia Binadamu atafaidika kwa hizo Hifadhi hai. “Hifadhi hai za Taifa ni muhimu sana na kwa mfano hili la RUMAKI wananchi wa maeneo hayo tutawatafutia miradi na kazi mbadala ili waweze kuondoa uharibifu katika mazao ya bahari”

Kamati ya Taifa ya Binadamu na Hifadhi hai Nchini inaundwa na wajumbe kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali kama vile Hifadhi za Taifa (TANAPA), Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakal wa huduma za misitu (TFS),Chuo Kikuu cha Das es Salaam, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Taasisi ya Tafiti za Misitu (TAFORI), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) na Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA)

Share:

KIKAO UIMARISHAJI MPAKA TZ NA KENYA CHAANZA TARIME

Mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Kanali Michael Mangwela akifungua kikao cha pamoja cha Wataalamu wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime tarehe 11 April 2022. Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Hamdouny Mansoor (Kulia) Mkuu wa ujumbe kutoka Kenya Juster Nkoroi (Katikati) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Balozi Joseph Ungo (kushoto) wakiwa kwenye kikao cha pamoja cha wataalam wa mipaka wa Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 11 April 2022.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Balozi Joseph Vungo akizungumza kwenye kikao cha pamoja na wataalam wa mipaka wa Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 11 April 2022.

Ujumbe wa Tanzania na Kenya ukiwa kwenye kikao cha Pamoja cha Wataalamu wa mipaka wa nchi hizo mbili kinachoendelea wilayani Tarime tarehe 11 April 2022.

Mratibu Msaidizi wa Uimarishaji mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Kenya Joseph Ikorongo akiwasilisha taarifa wakati wa kikao cha pamoja cha wataalamu wa mipaka kutoka Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime tarehe 11 April 2022. Sehemu ya washiriki kutoka Tanzania

Mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Kanali Michael Mangwela akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa mipaka wa Tanzania na Kenya wakati wa kikao cha kujadili uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili tarehe 11 April 2022 wilayani Tarime mkoani Mara. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

************************

Na Munir Shemweta, WANMM TARIME

Kikao cha Kamati ya pamoja ya Wataalamu wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya kimeanza leo tarehe 11 April 2022 wilayani Tarime mkoa wa Mara.

Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili kinachotarajiwa kumalizika April 15, 2022 wilayani humo kitapokea mawasilisho ya kazi iliyofanyika na kutoa muongozo juu ya namna bora ya kutekeleza kazi iliyobaki.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 11 April 2022 kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mangwela alisema uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya Tanzania na Kenya ulenge kuimarisha mahusiano ya nchi hizo pamoja na kujadili changamoto za maeneo ya mipakani.

"Pamoja na kuimarishwa mipaka kati ya Tanzania na Kenya lakini bado kuna maeneo ambayo baadhi ya wananchi kutoka kila upande wanaingia na kuendesha shughuli zao hivyo mjadili changamoto hizi kwa kina na kuja na maamuzi yatakayoleta tija" alisema Kanali Mangwela.

Timu ya wataalamu wa Tanzania na Kenya imefanikiwa kukamilisha uimarishaji mpaka wa kimataifa wa awamu ya kwanza na kuanza awamu ya pili iliyosimama kutokana na changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Kenya Balozi Joseph Vungo aliwataka wataalamu wanaoshiriki kikao hicho kuhakikisha wanajadili na kuzitolea maamuzi changamoto kwa amani hasa wakizingatia nchi ya Tanzania na Kenya zimekuwa na mahusiano mazuri

Kwa mujibu wa Balozi Vungo, maamuzi yoyote yatakayoamuliwa katika kikao hicho yalenge kuleta tija na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo

Zoezi la uimarishaji mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya awamu ya kwanza limeanzia hifadhi ya Serengeti / Masai Mara kipande cha Kilomita 60 hadi eneo la Ziwa Natron kilomita 23 na awamu ya pili inaanzia Ziwa Natron hadi Namanga eneo la Kilomita 110.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 11,2022


Magazetini leo Jumatatu April 11 2022






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger