Wednesday, 1 December 2021

TANZANIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MCHEZO WA SOKA KWA WENYE ULEMAVU



******************** 

Na. John Mapepele 

Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Innocent Bashungwa leo Disemba 1, 2021 amewaongoza watanzania kuishangilia Timu ya Tanzania (Tembo Warriors) ambayo imefuzu na kuwa timu ya kwanza miongoni mwa timu nne zinazoingia nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021) na hivyo kupata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Dunia ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon mabao 5-0. 

Timu ya Tanzania ambayo katika kipindi chote cha maandalizi imesimamiwa na Kamati Maalum ya Kitaifa chini ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassani Abbasi ilianza vizuri kutokana hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hasan. 

Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo tembo ilishinda goli 1-0. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mechi hii, Mhe. Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuiisaidia timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri maandalizi ya Kombe la Dunia. 

Aidha, Dkt Abbasi amesema kwa kuwa safari ya kuelekea kombe la dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa kombe linabaki Tanzania. 

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na Alfan Kyanga dakika ya 2 na 15 , Ramadhan Chomole dakika ya 18, na Frank Ngailo dakika ya 36 na 44. 

Mchezo huo pia umeshuhudiwa na Rais wa Mashindano hayo duniani Mateus Wildack.
Share:

Wachimbaji Madini Waaswa Kujikinga Dhidi Ya Maambukizi Ya Ukimwi- Waziri Biteko


 Na MWANDISHI WETU,TABORA
Katika kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Waziri wa Madini Doto Biteko ameitumia fursa hiyo kuwaasa wachimbaji wote wa Madini Nchini kuhakikisha wanalinda afya zao kwa kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
 

Waziri Biteko ameyasema hayo baada ya kutembelea mgodi wa wachimbaji wadogo wa Nsungwa uliopo wilayani Kaliua Mkoa wa Tabora ambako kumeibuka mfumuko wa Madini ya Dhahabu (Rush).
 

Aidha, Waziri Biteko amewataka wachimbaji hao kuhakikisha wanatunza akiba ya kipato wanachokipata na kutunza familia zao ikiwemo kuwekeza katika sekta nyingine hususan katika Sekta ya Biashara na Kilimo.
 

“Hela unayoipata usiidharau hata kama ni kidogo weka akiba ili ije ikusaidie kesho ukiwa huna nguvu, leo unanguvu unaingia duarani lakini baada ya miaka kadhaa hautaweza, utaitaji watu wa kukusaidia, nguvu ya leo uiweke akiba kwa ajili ya kesho ili ikusaidi kuwa na kesho nzuri usije ukawasumbua watu,” amesema Waziri Biteko.
 

Waziri Biteko amesema Wilaya ya Kaliua inafahamika kwa Kilimo cha Tumbaku ambapo kwa sasa umetokea mlipuko wa Madini ya Dhahabu katika eneo hilo na kusababisha Wilaya hiyo kuingia kwenye orodha ya Wilaya zinazochimba Madini ambapo amewataka Wachimbaji hao kuendelea kuwa watulivu na kufuata Sheria katika uchimbaji wao.
 

Pia, Waziri Biteko amesema haki zipo nyingi kuna Haki ya Ardhi, Haki ya Anga, Haki ya Madini na kadhalika, unaweza ukawa na shamba lakini mmiliki mkuu wa shamba hilo ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenye mamlaka ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama kwenye shamba hilo kuna Madini hairuhusiwi yachimbwe mpaka kuwe na leseni katika eneo hilo.
 

“Yoyote anayepewa leseni ya Madini kazi yake ya kwanza ni kwenda kwa mwenye shamba sababu huwezi kuyachimba Madini mpaka ukubaliane na mwenye shamba na kuna makubaliano ya aina mbili ya kwanza ni kumlipa fidia mwenye shamba ili akupishe na aina ya pili ni mwenye shamba kuingia shea kwenye leseni husika,” amesema Waziri Biteko.
 

Pia, Waziri Biteko amewasisitiza wachimbaji wadogo kuachana na suala la kutorosha madini ambapo amewataka kuchimba kwa kufuata Sheria na kuhakikisha kodi ya Serikali inalipwa.
 

“Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anataka kuona Uchumi wa Madini unamilikiwa na Watanzania wa kawaida pia wachimbaji wote walioko sehemu mbalimbali ikiwemo Kaliua wanabadilisha maisha yao kwa rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu amewabariki,” amesema Waziri Biteko.



Share:

Vijana Watakiwa Kujitokeza Kupima UKIMWI


NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewaasa vijana kujitokeza kupima Virusi vya UKIMWI ili kujua hali zao na kuishi kwa malengo.

Ametoa kauli hiyo  Novemba 30, 2021 wakati akihutubia vijana katika kuadhimisha siku ya vijana katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani tarehe 01 Disemba, 2021 yatakayofanyika katika Uwanja ya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya. Kaulimbiu ya Maadhimisho kwa mwaka huu inasema “Zingatia Usawa. Tokemeza UKIMWI, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

Alieleza kuwa, Kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kutoa msukumo kwa Watanzania wote kujitokeza kwa ajili ya upimaji wa hiari wa VVU baada ya ushauri nasaha, ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia dawa za kufubaza VVU (ARV) mapema kwa watakaogundulika kuwa na mambukizo ya VVU. Kauli mbiu hii inakwenda sambamba na jitihada za nchi katika kufikia malengo ya Kidunia ya Sifuri TATU ambayo tumeyaridhia.

Akieleza umuhimu wa kundi la vijana nchini, alisema ni kundi linalotegemewa kwa asilimi kubwa hivyo ni vyema wakawa na desturi za kupima hali zao ili kuishi kwa malengo na kutimiza ndoto zao.

“Vijana ndio nguzo katika ujenzi wa Taifa imara. Katika Taifa letu vijana ni zaidi ya asilimia 68 ya nguvu kazi ya Taifa letu, hii ni kwa mujibu wa takwimu za makadirio ya ongezeko la idadi ya watu nchini ambayo imeonesha kuwepo na ongezeko kubwa la vijana na watoto, hivyo hakuna namna tunayoweza kufanya shughuli za maendeleo pasipo kutambua nafasi ya vijana ndani ya jamii yetu na kufahamu vipaumbele vyao ikiwa ni pamoja na afya bora,”alisema waziri Mhagama.

Waziri Mhagama alisema utafiti wa Viashiria vya UKIMWI wa mwaka 2016/17 hapa nchini, ulibaini kuwa moja ya makundi yaliyo nyuma katika kufikia malengo yaliyowekwa ni kundi la VIJANA ambapo inaonesha vijana wengi wenye umri wa miaka 15 hadi 24 hawajui hali zao za maambukizo ukilinganisha na watu wenye umri mkubwa. Hali hii inapelekea vijana hawa kutoanza dawa za ARV mapema kwani hawajui hali zao na hivyo kutoweza kufubaza VVU.

“Nitoe rai kwa vijana wote nchini, tujitokeze kwa wingi katika huduma za upimaji wa VVU kwa hiari zitolewazo sehemu mbalimbali nchini, ili wale wote watakaogundulika kuwa wana maambukizo ya VVU waweze kuanza dawa za ARV mapema na hivyo kutimiza kwa vitendo kauli mbiu ya mwaka huu,”alisisitiza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana wanaoishi na VVU Nchini Bi. Pudenciana Mbwiliza akitoa salamu wakati wa maadhimisho hayo alieleza ni vyema vijana wakajitokeza kupima na kujua hali zao ili kuendelea kuunga mkono jitihada za mapambano haya.

Aidha akibainisha changamoto zao alisema ni wakati sahihi kuwa na mikakati ya kuendelea kutokomea vitendo vya kikatili na kuendelea kuwafikiwa vijana kupitia miradi mbalimbli inayotekelea afua za masuala ya UKIMWI nchini.

Pia alizitaja changamoto wanazokabiliana nazi ikiwemo ya kasi ya maambukizi mapya hasa kwa wasichana walio katika umri balee, unyanyapaa katika jamii hususan ule wa mtu binafsi, ukatili wa kijinsia, ufuasi hafifu wa utumiaji wa dawa za ARV, elimu duni kwa vijana walio mashuleni hasa katika shule za bweni, matumizi yasiyosahihi ya kondom na mwamko mdogo wa watu kujitokeza kupima na kujua hali zao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI Mhe. Fatma Taufiq alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika mapambano dhiti ya UKIMWI na kuahidi kuendeleza ushirikiano kadiri inavyotakiwa.

“Kweli bajeti tunayoipitisha bungeni inafanya kazi kwa haya tuliyoona na mwitikio huu wa vijana na kuona kundi hili linashirikishwa kwa namna kubwa na hii ni ya kupongeza sana. Naamini Taanziania bila UKIMWI inawezekana na Tanzania bila unyanyapaa inawezekana,”alieleza Mhe. Fatma

Aliongezea kwamba, Kamati itaendela kuishauri Serikali kuwa na sera na sheria imara kuhakikisha kundi ka vijana linapata fursa nzuri na kuone namna bora ya kuweka mipango thabiti ili kuendela kulivusha kundi hili.


Share:

Global SaaS Business Development Manager at LocoNav

Global SaaS Business Development Manager   LocoNav  Dar es Salaam, Tanzania Remote 19 hours ago  174 applicants Full-time · Associate About Loconav : Loconav is the World’s fastest growing Vehicle Management & IOT platform and is currently used to track over 500,000 assets across the globe. LocoNav is bringing together the power of its proprietary […]

This post Global SaaS Business Development Manager at LocoNav has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Accountant Cum Sales at Fast Link Safaris & Tours

Accountant Cum Sales   Summary: We are looking for an Accountant to manage all financial transactions, from fixed payments and variable expenses to bank deposits and budgets. Job Description:   Accountant responsibilities include auditing financial documents and procedures, reconciling bank statements, and calculating tax payments and returns. To be successful in this role, you should […]

This post Accountant Cum Sales at Fast Link Safaris & Tours has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Enterprise Account Manager at Value Data

Enterprise Account Manager   Value Data Main Characteristics and Expertise.   Experience in key account management within a fast-paced and highly competitive business environment. Experience in high-value client acquisition, satisfaction, and retention working as a Enterprise Account Manager. Experience of having driven sales initiatives and achieving or surpassing business targets. Experience developing, negotiating and maintaining […]

This post Enterprise Account Manager at Value Data has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Consultant at Sustainable Agriculture

Consultant   Sustainable Agriculture, Tanzania  Morogoro, Tanzania CALL FOR EXPRESSION OF INTEREST FOR EXTERNAL PROJECT EVALUATION OF CURRICULUM IMPLEMENTATION SUPPORT FOR TRAINING INSTITUTES (CISTI) PROJECT GENERAL INSTRUCTIONS Introduction Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) is seeking to hire a consultant(s) to conduct a comprehensive external evaluation for the Liechtenstein Development Service (LED) funded project “Curriculum Implementation Supports […]

This post Consultant at Sustainable Agriculture has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Business Development Managers (Hotel Software) at SciTech Placements

Business Development Managers (Hotel Software)   SciTech Placements,  Dar es Salaam, Tanzania About the job Our International Client in the Hotel & Hospitality Technology sector requires a Business Development Managers to be based in Dar es Salaam, Tanzania Responsibilities:   Business development for our Hospitality / Hotel Technology services Travel to clients Expanding the business in […]

This post Business Development Managers (Hotel Software) at SciTech Placements has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 1, 2021




Magazetini leo December mosi 2021












Share:

Tuesday, 30 November 2021

Jeshi la Uganda lafanya mashambulio ya anga dhidi ya waasi wa ADF huko DRC


Jeshi la Uganda limeanzisha mashambulizi ya pamoja ya anga na ardhini dhidi ya kundi la waasi la Allied Democratic Forces -ADF, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Uganda Brigedia Jenerali Flavia Byekwaso amethibitisha hayo kupitia akaunti yake rasmi ya twitter.

Alisema kuwa operesheni hizo zilifanywa na washirika wa Congo, dhidi ya kambi za ADF, lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu maeneo ambayo mashambulizi hayo yamefanywa.

Mamlaka ya Uganda inalaumu ADF, ambayo inashirikiana na Islamic State (IS) kwa msururu wa mashambulizi ya mabomu nchini humo tangu Oktoba.

Wiki mbili zilizopita, IS ilidai kuhusika na milipuko miwili ya mabomu nje kidogo ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Kampala na karibu na Bunge.

Takriban watu watano wameuawa katika milipuko hii ya mabomu, baadhi ya mashambulizi yakiwa ya kujitoa mhanga, kwa mujibu wa Polisi wa Uganda.


Share:

NIC KUDHAMINI MBIO ZA UDSM MARATHON 2021

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakionesha jezi ambayo itatumika katika mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Disemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakipongezanawakisaini mkataba wa makubaliano NIC kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakionesha mkataba uliosainiwa NIC kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya wakipongezana mara baada ya NIC kusaini mkataba wa makubaliano kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano na NIC kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajia kufanyika Novemba 4,2021 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) wameingia mkataba wa makubaliano wa kudhamini mbio za UDSM Marathon ambazo zinatarajiwa kutimua vumbi Disemba 04, 2021 kuanzia na kumalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule amesema wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika sekta ya michezo kwa lengo la kukuza vipaji kwa watanzania na pia kujiepusha na magonjwa nyemelezi.

Amesema wanakila sababu ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa maana wamekuwa wadau wakubwa kwao katika biashara pia ndio kitivu cha elimu hapa nchini.

"Ni mara yetu ya kwanza kusapoti UDSM Marathon na haitakuwa mara ya mwisho kufanya hivyo, tutaendelea kushirikiana kama  ambavyo wamekuwa wadau wakubwa kwetu kwa muda mrefu". Amesema Bw.Mwakifulefule.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa UDSM Marathon Bi.Lulu Kaaya amesema katika mbio hizo wanatarajia kuwepo kwa mgeni rasmi ambaye atakuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia atashiriki kukimbia Kilomita 5.

Amesema mbio hizo zitakuwa na ruti kubwa tatu ambazo ni ruti ya Kilomita 21.1, ruti ya kilomita 10 na ruti ya kilomita 5 ambayo ruti hiyo mgeni rasmi atashiriki 

'Lengo kuu la mbiu hizi ni kwaajili ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kuboresha maisha ya wanachuo. Kwasasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo katika ujenzi wa kituo cha wanafunzi (Student Center) inayojengwa kwenye Campus ya Mwalimu Nyerere Mlimani Jijini Dar es Salaam ambacho ni mahususi kwa kutoa mazingir mazuri ya mapumziko kwa wanafunzi". Amesema

Share:

CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO CHAPONGEZWA KUWA NI KISIMA CHA UTOAJI MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani akifungua mafunzo elekezi ya siku tano yanayowashirikisha Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama ambayo yanafanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akisistiza jambo alipokuwa anatoa mada katika mafunzo hayo.
Kaimu Mkuu wa Chuo, Prof. Fatihiya Massawe, ambaye pia ni Naibu Mkuu wa IJA, Mipango, Fedha na Utawala akitoa neno la ukaribisho kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayowashirikisha Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama ambayo yanafanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA). ,Mafunzo hayo yamefunguliwa leo tarehe 29 Novemba, 2021 na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani.
Sehemu ya Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel.
***

Na Faustine Kapama na Rosena Suka, Mahakama-Lushoto

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani leo tarehe 29 Novemba, 2021 amefungua mafunzo elekezi ya siku tano kwa Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama ambapo amekisisifia Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa mchango mkubwa kinachofanya na kujenga taaluma bora kwa watumishi wa Mahakama na wananchi wengine kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tano yanayowashirikisha viongozi hao, Mhe. Siyani amebainisha kuwa Chuo kwa kushirikiana na Kitengo cha mafunzo cha Mahakama ya Tanzania wamekuwa wakifanya kazi nzuri kwa kutoa mafunzo mbalimbali elekezi na endelevu kwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

“Kama ilivyo kwa wengine, mimi nina imani kuwa chuo hiki kweli ni kitovu na kisima cha elimu bora. Kimsingi, chuo hili kina uwezo wa kujenga taaluma na kufanya leo hii tuna Wasajili ambao kesho ni Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kwa hiyo, mimi niwapongeze sana na nifikishie salamu zangu kwa Mkuu wa Chuo,” Jaji Kiongozi alimweleza Kaimu Mkuu wa Chuo, Prof. Fatihiya Massawe, ambaye pia ni Naibu Mkuu wa IJA, Mipango, Fedha na Utawala.

Amesema kuwa mafanikio katika utoaji wa mafunzo elekezi ya awali na mafunzo endelevu ya kimahakama ni mojawapo ya matunda ya kazi nzuri yanayofanywa na IJA kwa kuzingatia Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya mwaka 2019 ambayo inakitambua Chuo hicho kama kitovu au kisima cha utoaji mafunzo kwa watumishi wa Mahakama, lakini vile vile utafiti wenye lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji wa Mahakama ya Tanzania.

Jaji Kiongozi aliwakumbusha washiriki kuwa mafunzo ambayo yameandaliwa kwa ajili yao yamelenga kuwapa mbinu na nyenzo sahihi za kuweza kukabili changamoto mbalimbali za kiutendaji. “Hivyo muwe wazi kuuliza maswali na kuchangia uzoefu kila mmoja kwa namna ambayo mnaona italeta matokeo chanya katika utendaji kazi wenu. Shabaha ya kila mmoja wetu iwe ni utoaji wa haki na kuliletea maendeleo taifa letu na kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Huduma kwa Mteja,” amesema.

Mhe. Siyani alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha washiriki wa mafunzo hayo kuwa wapo katika kipindi cha mapinduzi ya nne ya viwanda na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amekuwa akisisitiza watumishi wa Mahakama kujinoa zaidi kwenye eneo la TEHAMA ili waweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia hivi sasa.

Amebainisha kuwa miongoni mwa mada zitakazotolewa katika mafunzo hayo inahusu TEHAMA, hivyo ni imani yake kupitia mada hiyo washiriki wote watapata nafasi ya kujifunza juu ya nafazi zao katika usimamizi wa mashauri kwa njia za kielektroniki. Aliwaomba kutumia fursa hiyo kupata kitu cha nyongeza katika eneo hilo na kwamba kila mmoja wao awe mfuasi wa karibu wa TEHAMA kama dunia inavyowataka hivi sasa.

“Tambueni kwamba tunakoelekea hakutakuwa na nafasi kwa Msajili au Mtendaji asiye na uelewa wa TEHAMA katika Mahakama yetu. Hiyo ni dhahiri kwa sababu ninyi ni wasimamizi wa mifumo ikiwemo ya TEHEMA na bila shaka msimamizi bora ni yule anayefahamu anachokisimamia,” aliwaambia viongozi hao wa Mahakama ya Tanzania.

Awali akitoa neno la ukaribisho, Kaimu Mkuu wa Chuo, Prof. Fatihiya Massawe alisema kuwa mafunzo yanayotolewa kwa Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama siyo ya kwanza kutolewa hapo Chuoni, kwani IJA imekuwa ikitoa mafunzo elekezi (Induction) kwa wahesimiwa Majaji wote wapya wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na mafunzo ya awali na elekezi kwa Majaji wote wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Zanzibar wanapoteuliwa kwenye wadhifa huo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani pamoja na Rais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa Prof. Massawe, vilevile IJA imekuwa ikiendesha mafunzo elekezi kwa Mahakimu wote mara wanapoajiriwa kujiunga kwa mara ya kwanza na utumishi wa Mahakama kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutenda haki kwa wote na kwa wakati kwa kuzingatia misingi ya sheria na uadilifu.

“Hii ni mara ya kwanza mafunzo ya namna hii yametolewa kwa Naibu Wasajili na hata kwa Watendaji. Tunapenda kuipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kulisimamia hili. Tunaamini mafunzo haya elekezi ni mwanzo tu wa mafunzo endelevu ambayo washiriki hawa wataendelea kupata kama watumishi wa Mahakama. Chuo kinaahidi kitaendelea kutayarisha programu za mafunzo kulingana na uhitaji kadri watakavyoendelea kutekeleza majukumu yao na kubaini changamoto katika maeneo ya uhitaji wa mafunzo,” alisema.

Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali zitawasilishwa na waezeshaji waliobobea katika maeneo mbalimbali, akiwemo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, Jaji Mkuu Mstaafu ,Mohamed Chande Othman, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. January Msoffe, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na watendaji wengine waandamizi wa Mahakama.

Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa kwenye mafunzo hayo zinajumuisha Uongozi wa Kimkakati, Stadi za Uongozi na Uwezo wa Kukabili Mabadiliko, Wajibu wa Mahakama, Utamaduni wake na Uhusiano wake na Mihimili Mingine ya Dola, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama na Uboreshaji unaofanywa na Mahakama, Maadili ya Watumishi wa Umma na Maadili ya Kimahakama, Usimamizi wa fedha na Manunuzi ya Umma pamoja na Usimamizi wa Nyaraka.


Share:

REA YAVUKA MALENGO KUWAFIKIA WANANCHI VIJIJINI

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Nishati leo Novemba 30,2021 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Nishati leo Novemba 30,2021 Jijini Dar es Salaam.Kamishna Msaidizi wa umeme, Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Nishati leo Novemba 30,2021 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imesema imevuka malengo iliyojiwekea ya asilimia 50 katika kuwafikishia wananchi huduma ya umeme viijini ambapo hadi kufikia Juni 2021 asilimia 69.6 ya vijiji vilikuwa vimefikiwa na huduma hiyo.

Akiongea leo Novemba 30, 2021 katika ukumbi wa Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Seif Saidy alisema kuwa wakati Taifa linaelekea kuadhimisha miaka 60 ya uhuru, hali ya maisha ya wakazi wa vijijini imebadilika ambapo mwaka 2007 wakati Wakala inaanzishwa asilimia 2 tu ya vijiji walikuwa wamefikiwa na huduma ya umeme.

“ Kuna mafanikio mengi tuliyoyapata kutokana na usanifu, utekelezaji na usimamizi wa miradi inayotekelezwa na wakala tangu kuanziswa kwake ambapo miradi hiyo imewezesha ujenzi wa jumla ya kilomita 38,296.56 za umeme msongo wa kati na kilomita 35,253.43 za umeme msongo mdogo lakini pia kuna jumla ya wateja 716,847 waliounganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi bilioni 2,661.93 kwa kipindi cha miaka 14 tangu kuanzishwa kwake”, alisema Mhandisi Saidy.

Mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kutengeneza masoko kwa viwanda vya ndani vinavyozalisha vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miradi ya umeme, kuwezesha uboreshwaji wa kilimo cha umwagiliaji katika mashamba likiwemo shamba la Mtakuja Kilimanjaro na Zuzu Dodoma.

Aidha, kufunga mifumo ya umeme katika nyumba za wafanyakazi takribani 831 kwenye sekta ya afya na elimu katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Kagera, Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma na Tabora, wakati huo huo hali ya kuboresha mazingira ya makazi vijijini ambayo imepelekea kupunguza uhamiaji wa vijana kutoka vijijini kwenda mjini kwa kuwa umeme umewamewezesha kufanya shughuli za kiuchumi kwenye makazi yao.

“ Vijana wengi sasa wanatulia vijijini kwani wameweza kuanzisha viwanda vidogo na vya kati katika juhudi za kujikwamua kiuchumi. Vitu kama vile mashine za kusaga, kuchomelea, viwanda vya uselemara pamoja na saloni za kike na kiume vinapatikana hadi vijijini siku hizi, lakini pia upatikanaji wa taarifa na burudani kwa wepesi kama vile televisheni na redio vimeongeza utulivu kwa vijana wengi hapa nchini”, aliongeza.

Kwa upande wake kamishna Msaidizi wa umeme, Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila alisema kwamba katika kuhakikisha mtu mmoja mmoja anafaidika na uwepo wa umeme, Serikli inahamasisha wananchi wengi waone umuhimu wa kuunganishiwa umeme kwenye makazi yao ili kufaidi fursa zinazoletwa na nishati hiyo.

“ Tunaondoka kwenye hatua ya kuhakikisha umeme unafika kijijini, na hivi sasa tunawahamiasisha wakazi wa eneo husika kuhamasika kuunganishiwa umeme huo kwenye makazi yao. Mwamko ni mkubwa na tunapokea maombi mengi na hivi sasa tunahamasisha ushiriki wa sekta binafsi, taasisi za fedha katika uwekezaji wa miradi ya Nishati vijijini na tunaendelea kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya nishati jadidifu kutoka vyanzo vya asili vinavyopatikana maeneo ya vijijini na kwenye visiwa”, alisema Mhandisi Rwebangila.

Wakala wa Nishati Vijiji ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Nishati vijijini Na. 8 ya mwaka 2005 na kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yake mwezi Oktoba, 2007 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa iliyokua Sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2003.
Share:

Balozi Mulamula Akutana Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa China


Na mwandishi wetu,  Dakar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi jijini Dakar nchini Senegal.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea kuridhishwa kwao na ushirikiano na uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na China na kuahidi kuendeleza uhusiano huo kwa faida ya pande zote mbili.

Waziri Mulamula amemuhakikishia Waziri Yi utayari wa Serikali  kuendelea kushirikiana na China katika kuhakikisha Tanzania inafikia maendeleo ya kweli kwa ufanisi mkubwa.

Amemshukuru Waziri huyo kutokana na ahadi iliyotolewa awali na Rais Xi Jinping wa China wakati wa ufunguzi wa mkutano wa FOCAC ya kutoa dozi bilioni moja zaidi za chanjo ya virusi vya Covid 19 kwa bara la Afrika kwani kitendo hicho kitazisaidia nchi za Afrika kutoa chanjo ya ugonjwa huo kwa watu wengi zaidi.

Pia ameishukuru China kwa kuwa soko la bidhaa za Tanzania na amemuhakikishia Waziri huyo kuwa Tanzania iko tayari kutumia fursa ya soko la China la kuuza mazao yake ya mbogamboga na matunda ili kuongeza ujazo wa biashara na hivyo kukuza uchumi.

Pia ameelezea ambavyo Tanzania inafarijika na utayari wa China katika kuisaidia kwenye miradi mbalimbali kama ile ya  ya ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme utokanao na maji kama ya Ruhuji, mradi wa uendelezaji wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji , upanuzi wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete  na ujenzi wa barabara kuu katika Visiwa vya  Zanzibar miradi ambayo amesema itasaidia kuinua na kukuza uchumi wa nchi.

Naye Waziri Yi kwa upande wake ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono China na kuahidi kuendelea na harakati za kusaidia nchi zinazoendelea na kuongeza kuwa China itaendelea kuisadia Tanzania katika kufanikisha miradi mbalimbali ya kimkakati na kuielezea Reli ya TAZARA kama moja ya kielelezo cha ushirikiano huo.

Amesema China itaendelea kuunga mkono jitihada za Tanzania katika kujikwamua kiuchumi na kuahidi kuendelea kutoa misaada ya fedha na  kitaalamu ili  kukamilisha miradi ya ujenzi, uanzishwaji wa kituo cha mfano kwa ajili ya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo wadogo nchini.

Mawaziri hao wako Senegal kuhudhuria  Mkutano wa Nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika nchini Senegal ulioanza tarehe 29  hadi 30 Novemba  2021.


Share:

Infinix Kuja na Toleo Jipya lenye ukubwa mara mbili zaidi ya matoleo ya awali.....Bofya Hapa Kujua Zaidi


  Je ni kweli baada ya Infinix Zero X pro sasa kampuni ya simu za mkononi Infinix kuja na simu ya kwanza kwenye toleo la NOTE kuwa na ukubwa mara mbili zaidi ya matoleo ya awali ya NOTE?
 

Hivi punde picha yenye muonekano wa simu ikiwa imeandikwa ‘THE NEXT NOTE PLAY BIG’ imeonekana kuvuja kwenye mitandao ya blog za tech lakini pia kwenye kurasa ya @infinixmobile Infinix imetupia picha inayoashiria ujio wa simu mpya kupitia post inayosema ‘FIRST 11, ARE YOU READ FOR THE FIRST ROUND? Kushabihiana kwa hizi sentensi mbili mashabiki wametafisiri kuwa huenda hii ni simu mpya aina ya NOTE 11.
 

 Simu za toleo la Infinix NOTE hukubalika zaidi kutokana na muonekana mzima wa simu hizi ambao ni imara na wenye kuvutia lakini kivutio kikubwa zaidi kwa simu hizi ni ubora wake wa camera zenye teknolojia ya AI. 

Kamera za simu za toleo la NOTE huimarishwa kwa kila toleo jipya kama ilivyokuwa kwa NOTE 8 ikiwa na camera yenye MP48 na NOTE 10 ikiwa na MP64.

 Tetesi zinadai kuwa simu hii huenda ikaja na kioo cha aina ya AMOLED na hii ni baada ya kampuni hiyo kuonyesha kuwa inawezekana kutumia teknolojia ya hali ya juu na bado simu ikiwa na bei rafiki kama ambavyo tumeliona hili kwa Zero x pro.
 

Je ni sifa gani nyengine ya kipekee kuja katika simu hii  https://bit.ly/3BHedZw?...

Tembelea;  https://www.infinixmobility.com/smartphone/note-11-pro/ kupata majibu kamili ya simu hii mpya ya Infinix NOTE 11.



Share:

DC KIBAHA AIPONGEZA TBS KUTOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA MAZIWA KATIKA MKOA WA PWANI

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Sara Msafiri akifungua mafunzo kwa wajasiriamali wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa wilayani Kibaha Mkoani Pwani. 

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe Sara Msafiri (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa. 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa wilayani kibaha wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. 

*************** 

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wametoa mafunzo ya Udhibiti ubora kwa wajasiriamali ambao niwasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa mkoani Pwani. 

Akizungumza na washiriki wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Sarah Msafiri alisema amefurahishwa sana na uamuzi wa TBS kuamua kutoa mafunzo kwa wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa na kuichagua wilaya ya Kibaha kuwa sehemu ya kwanza kabisa kupokea mafunzo hayo na nimatarajio yake kuwa wadau hawa watatumia vizuri fursa hii ya mafunzo ambayo itapelekea kuwa na uzalishaji wa maziwa na bidhaa za maziwa zitakazokidhi matakwa ya viwango. 

Alisema anatambua nafasi walionayo wadau wa maziwa na bidhaa za maziwa katika kuchangia uchumi wa taifa hivyo basi kama watakuwa wasikivu katika mafunzo hayo mahususi kwa ajili yao ili kuwajengea uwezo na hatimaye kuwa bidhaa zitakazoweza kuuzwa ndani na nje ya nchi. 

Kwa upande wake Bw. Hamisi S. Mwanasala mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (TBS) alisema kuwa mafunzo haya yanafanyika katika wilaya Kihaha na Bagamoyo ( Pwani) na Kilosa na Bagamoyo ( Morogoro) na yanatarajia kuwa endelevu kwa Tanzania nzima 

Alifafanua kuwa mafunzo haya yatawanufaisha washiriki kwa kutambua faida na matakwa ya viwango vya maziwa na bidhaa za maziwa, kanuni bora za usindikaji wa maziwa, kanuni bora za afya, teknolojia mbalimbali za usindikaji wa maziwa, utaratibu wa uthibitishaji ubora wa bidhaa, usajili wa majenngo ya kusindikia vyakula na kanuni bora za ufugaji. 

Bw. Mwanasala alisema mafuzo hayo yamejumuisha wakufunzi kutoka taasisi mbalimbali kama vile TBS, SIDO, Bodi ya Maziwa , Afisa Biashara, Afisa Afya na Afisa maendeleo ya jamii. 

Lengo la kutumia wakufunzi kutoka taasisi mbalimbali ni kuhakikisha kuwa mafunzo haya yanaleta tija kwa washiriki kwa kupata elimu juu ya taratibu na kanuni za uzalishaji bora wa maziwa na bidhaa za maziwa.
Share:

Chuo Cha Ardhi Morogoro Chatakiwa Kuweka Mikakati Kukamilisha Urasimishaji Makazi


Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekitaka Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) kujipanga na kuhakikisha kinamaliza kazi ya urasimishaji makazi katika maeneo waliyopewa kazi hiyo.

Hatua hiyo inafuatia Naibu Waziri Dkt Mabula kuelezwa na Mkuu wa Chuo cha ARIMO   Huruma Lugalla kuwa, moja ya changamoto kubwa katika zoezi zima la urasimishaji makazi maeneo mbalimbali ambayo chuo hicho imechukua kazi hiyo ni kasi ndogo ya uchangiaji gharama kutoka kwa wananchi.

‘’Mhe. Naibu Waziri uchangiaji katika zoezi la urasimishaji makazi katika maeneo mbalimbali nchini tunayoyafanyia kazi hasa hapa Morogoro ni mdogo sana pamoja na gharama ya zoezi hilo kupungua kutoka shilingi 150,000 hadi 130,000/=’’ alisema Lugala

Hata hivyo, pamoja na kuelezwa changamoto, hiyo Dkt Mabula ambaye alikuwa akizungumza na Uongozi wa Chuo cha Ardhi Morogoro tarehe 29 Novemba 2021, alikitaka chuo hicho kuhakikisha kinachukua maeneo machache ya kuyafanyia kazi badala ya kuchukua maeneo mengi aliyoyaeleza kuwa yanaweza kuwashinda kukamilisha kazi kwa wakati.

‘’ Ni vizuri mkajipanga katika zoezi zima la urasimishaji, baada ya kufanyika kosa la awali nyuma sasa msirudie tena kosa maana haitaleta picha nzuri kwa chuo na mnachotakiwa ni kujipanga na kuwa na mkakati wa kukamilisha kazi’’ alisema Dkt Mabula

Mkuu wa koa wa Morogolo Martine Shigela alishangazwa na maelezo kuwa, baadhi ya wananchi katika mkoa wake wanakuwa wazito kuchangia gharama za urasimishaji makazi holela wakati wanaweza kujenga nyumba ya milioni 20 huku akishindwa kuchangia shilingi 130,000/

‘’Yaani wananchi wanashindwa kuchangia gharama za urasimishaji wakati wanajenga nyumba kwa gharama kubwa kama milioni 10 mpaka 20? Hii haina afya kabisa’’alisema Shughela.

Awali Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro Huruma Lugalla alimueleza Naibu Waziri Dkt Mabula kuwa Chuo chake kinaendelea na utekelezaji miradi ya urasimishaji makazi katika mitaa 61 nchini kwa kushirikiana na halamashauri na wananchi wanaomiliki ardhi ya makazi yaliyoendelezwa kiholela.

Kwa mujibu wa Lugalla, jumla ya viwanja 30,188 vimeidhinishwa kufanyiwa kazi ya urasimishaji makazi, iwanja 129, 761 vimetambuliwa huku michoro 218 ikisanifiwa  na takriban Shilingi Bilioni 2.553 ikiwa imetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Aidha, Mkuu huyo wa Chuo cha ARIMO aliwasilisha ombi la chuo chake kutaka kusaidiwa uendelezaji eneo la ekari 33 lililoko Mlimakola Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kupanua wigo wa mafunzo, miundombinu sambamba na kuongeza udahili wa wanafunzi.

Kufuatia ombi hilo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shigela alisema, ni vyema taasisi za umma zinapoomba msaada wa uendelezaji maeneo yake zikafikiriwa kusaidiwa na kuongeza kuwa, mkoa wake uko tayari kusaidia pale utakapoona mipango ya chuo kuhusu uendelezaji eneo hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shighela alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kufikiria namna ya kuwekeza miradi katika mkoa huo ukiwemo ule wa eneo la maduka (MALL) kwa lengo la kurahisisha upatikanani huduma.

Akizungumza na Menijementi ya NHC iliyomtembelea ofisini kwake wakati wa kikao chake na Jukwaa la Wahariri Tanzania mkoani Morogoro kilichofunguliwa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, Shighela alisema, kwa sasa mkoa huo hauna maduka (Mall) kwa ajili ya kuwaewezesha wananchi wa mkoa huo kupata huduma eneo moja kama ilivyo Dar es Salaam wakati mkoa huo unaendelea unapanuka.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Numba la Taifa Dkt Maulid Banyani alimhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kulifanyia kazi suala hilo na katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika haraka Shigela na timu ya NHC walitembelea eneo la Kingo Sabasaba katika manispaa ya  Morogoro kuona namna ya kufanya uwekezaji kwenye eneo hilo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger