Monday, 19 July 2021

CCM WAIBUKA BAADA YA RAIS SAMIA KUTOA AGIZO TOZO YA MIAMALA YA SIMU...WASEMA 'AMEDHIRISHA USIKIVU NA HEKIMA ZAKE'


 Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuona haja ya kuangalia namna ya kufanya mapitio upya ya Sera na sheria za kodi ili kuliweka vyema jambo hilo na kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kwa jamii.

Hatua imekuja baada ya uamuzi wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wa kutaka tozo za miamala ya simu kuangaliwa upya na kuweka unafuu kwa wananchi.

Katibu wa Itikadi siasa na Uenezi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema hayo wakati akiongea na Vyombo vya habari Jijini hapa ambapo  amesema kwa mara nyingine Rais Samia amedhihirisha hekima, usikivu wake, uzalendo, umakini katika utendaji wake.

Akiongea katika Mkutano huo Shaka amesema,"Lakini zaidi Mama amedhihirisha kwa namna ambavyo amekuwa akiguswa moja kwa moja na changamoto za Watanzania na haki hii  ni kielelezo tosha kuwa huyu ni Rais wa watu lakini na nao watu wana rais wao ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema.

Pamoja na mambo mengine amezitaka pia Serikali ya Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia kuona namna gani zitafanya mapitio ya sera, sheria za kodi ili kuliweka vyema jambo hili katika utekelezaji wake.

Katika hatua nyingine Shaka amezungumzia kuhusu ushindi kwenye jimbo la Konde,na  kusema "Ni faraja iliyoje, namna gani mgombea wa CCM katika jimbo la Konde alivyoweza kukubalika na makundi yote,hii ni kwa sababu wananchi Wana imani na Serikali iliyopo madarakanai,"amesema na kuongeza;.

“Kwa niaba ya chama niwahakikishie kuwa hawatajuta juu ya uamuzi wao wa kukipa ushindi chama cha Mapinduzi, wamekikopesha chama Imani na tutalipa Imani katika kuwaletea maendeleo endelevu,”amesema.

Aidha amesema kuwa chama kimekuwa mstari wa mbele katika kuwasimamia viongozi katika ngazi zote ili kuhakikisha kuwa wanatimiza dhamira na matakwa ya wananchi  katika kuwaletea maendeleo.

Kadhalika ,Katibu huyo Mwenzezi wa CCM amegusia  malalamiko ya ACT Wazalendo ya kuchezewa rafu katika uchaguzi huo ambapo amesema vyama vya upinzani vimejisahau kwa kuhamishia siasa zao katika mitandao, matusi na kejeli na kusahau kuwa Watanzania  wanataka maendeleo na si vinginevyo.

"Matusi hayawasaidii wananchi,wananchi wameelimika ,na hii imeonuesha dhahiri kwenye uchaguzi huo  kuwa ni namna gani Watanzania na wapemba wameamka katika kujua ipi nyeupe na nyekundu katika kusimamia suala la maendeleo,"amesisitiza Shaka

Share:

MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA YANAANZA JULAI 23... WANAOTAKA MABANDA GHARAMA HIZI HAPA


Share:

RAIS SAMIA AGUSWA NA MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU TOZO ZA MIAMALA YA SIMU...ATOA MAAGIZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
****
Rais Samia Suluhu Hassan ameguswa na malalamiko ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya simu iliyoanza kutumika hivi karibuni na kuwaagiza mawaziri husika kutafuta suluhisho.


Hayo yamesemwa leo Julai 19,2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kupitia televisheni ya Channel Ten, akisema pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa na kikao na mawaziri husika ili kutafuta suluhisho.

“Tayari Mheshimiwa Rais ameshaguswa na jambo hili amesikia maoni ya Watanzania wote na amesema tuyafanyie kazi jambo hili,” amesema Waziri

Dk Mwigulu ameongeza kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na Waziri Mkuu. “Vilevile Waziri Mkuu ameitisha kikao kitakachofanyika kesho (Julai 20) kuendelea kupitia jambo hilo hilo.”

Amesema Serikali imesikia kilio cha wananchi na kuna mambo watakayoyafanyia kazi na mengine wataendelea kuwaelimisha wananchi.

“Tumepokea maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa uelewa zaidi kwa maana ya uelimishaji zaidi ili kuwa na uelewa wa pamoja, ikiwa pamoja na viwango vinavyokatwa, yupi anayekatwa, ukataji wakati wa kutoa na mantiki ya jambo hili zima kwa ujumla,” amesema.

SOMA ZAIDI HAPA
CHANZO MWANANCHI

Share:

DORIA YA KUFUKUZA TEMBO KUANZA LEO NACHINGWEA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) akisikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Ngulichile wilayani Nachingwea mkoani Lindi ambapo ameagiza doria za askari wa wanyamapori kuanza leo ili kufukuza tembo waliovamia makazi ya wananchi.
Wananchi wa Kijiji cha Ngulichile wakielezea kero yao ya tembo waliovamia makazi yao kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) wakati wa ziara yake a kikazi ya kusikiliza kero za wananchi wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi.


Na Happiness Shayo, WMU
Doria ya Askari wa Wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inatarajiwa kuanza leo ili kufukuza tembo waliovamia Kijiji cha Mbute na Ngulichile wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza changamoto za wananchi iliyofanyika leo wilayani Nachingwea.

“Ninawaagiza askari wa wanyamapori kuhakikisha mnaweka kambi katika vijiji hivi na kuanzia leo mfanye doria ya kuangalia tembo walipo ili kuwarudisha katika maeneo yao ya hifadhi,” Mhe. Masanja amefafanua.

Amesema, doria hizo zitakuwa mwarobaini wa kutatua tatizo la tembo waliovamia makazi ya wananchi katika vijiji hivyo.

“Kambi hii a askari wa wanyamapori katika maeneo haya iwe ya kudumu lakini naelekeza askari waje leo kufukuza tembo ili wananchi waishi kwa amani,” amesisitiza mhe. Mary Masanja.

Mhe. Masanja amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea pamoja na wananchi wa Wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kukamilisha zoezi hilo.

Aidha, Mhe. Mary Masanja amewaagiza wananchi hao kuanza utamaduni wa kufuga nyuki ili kukabiliana tembo.
“Nawaagiza watakapokuja wakufunzi kutoka Wizarani kuwafundisha mbinu mbalimbali za kukabiliana na tembo, mkubali njia hii ya kufuga nyuki kwa sababu nyuki ni adui wa tembo, sehemu ambayo nyuki yupo tembo hawezi kukaa,” Mhe. Mary Masanja ameongeza.

Amefafanua kuwa, ufugaji nyuki utasaidia kurutubisha mazao yao korosho wanayolima ili yaweze kukua vizuri.

Akizungumzia kuhusu changamoto ya tembo, Diwani wa Kata ya Ngulichile, Mhe. Said Mwakayola amesema kuwa wananchi wanaogopa kwenda kwenye maeneo yao ya shughuli za kila siku kama kisimani na mashambani kutokana na tatizo hilo la tembo.

“Zoezi hili la kufukuza tembo naomba lianze haraka iwezekanavyo kwa sababu watu wanashindwa kwenda hata kwenye mashamba ya mikorosho kuangalia mazao yao kwa sababu ya tembo hawa,” amefafanua Mhe. Mwakayola.

Pia, Mhe. Mwakayola ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa askari wa wanamapori watakaoanza zoezi hilo la kukabiliana na tembo.

Ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi za kutatua changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kama tembo wanaovamia makazi ya wananchi katika sehemu mbalimbali nchini.

Share:

WATU 13 WAFARIKI DUNIA BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA


Watu wapatao 13 wamefariki dunia baada ya tangi la mafuta ya petroli kulipuka huko magharibi mwa Kenya, usiku wa kuamkia Jumapili.

Ajali hiyo imeripotiwa kutokea wakati dereva alipojaribu kupishana na lori lingine katika barabara ya Kisumu na Busia.

Watu hao walikimbilia eneo la tukio wakiwa na madumu ya kujimiminia mafuta wakati lori hilo lilipopinduka lakini ghafla likawaka moto.

Watu wapatao 11 wakiwemo watoto, wapo hospitalini wakiwa na hali mbaya baada ya kuungua.

Iliwachukua saa mbili kwa kikosi cha zima moto kufika katika eneo la tukio karibu na mji wa Malanga katika kaunti ya Siaya yapata kilomita 315(195 miles) kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi.

"Hatukuweza kupata kituo za kuzima moto kaunti ya Siaya kwa kuwa ni Nairobi," afisa polisi Moreso Chacha alisema.

Vikosi wa kuzima moto walitokea katika kaunti za jirani , alisema.
Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

1px transparent line


Lori lilikuwa limebeba maziwa kutoka Busia, karibu na mpaka wa Uganda kuelekea Kisumu wakati lilipogongana na lori la mafuta lililokuwa linaelekea eneo tofauti, kamanda wa polisi amesema.

Ajali za barabarani si jambo geni katika mataifa ya Afrika Mashariki , ambapo malori na magari mengine yanapogongana kutokana sababu mbalimbali ikiwemo ya mwendo kasi.

Watu wapatao 3,000 ufariki kutokana na ajali za barabarani ,kila mwaka nchini Kenya.

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

KALEMANI ASHUSHA UMEME TOKA 3700/- MPAKA 100/- KWA UNIT VISIWANI - MWANZA


Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani Julai 18, 2021 amefanya Ziara katika kisiwa cha Maisome kilichopo wilaya ya Sengerema jijini Mwanza na kuagiza kampuni binafsi ya Jumeme inayosambaza Umeme katika kisiwa hicho kutoza bei elekezi na Serikali ya Umeme Vijijini ya shilingi 100 kwa unit moja badala ya shilingi 2,000/- mpaka 3,700/- iliyokuwa ikitozwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Kanoni kisiwani Maisome, Waziri Kalemani alieleza kuwa tayari Serikali imetoa bei elekezi ya umeme nchi nzima ambayo inasimamiwa na EWURA na ndio inayotumika na TANESCO katika kuuzia umeme wananchi hivyo ni vyema wawekezaji wote wakaifuata na kuizingatia.

Bei ya kuwauzia umeme wananchi ni moja ambayo inatumika na TANESCO na kusimamiwa na EWURA, hivyo naagiza Kampuni ya Jumeme iwashushie wananchi wa kijiji hicho bei na ifanane na ile inayotozwa na TANESCO katika maeneo mengine na huduma ziboreshwe, umeme usikatike mara kwa mara bila sababu za msingi” alisema Waziri Kalemani. 

Waziri Kalemani aliendelea kwa kuagiza kampuni hiyo yenye ofisi zake jijini Mwanza kuhakikisha inafungua ofisi za kuhudumia wateja katika visiwa hivyo kwa huduma za dharura ili kuboresha huduma kwa wateja wanaohudumiwa na kampuni hiyo katika visiwa hivyo. 

Naye Mwakilishi wa bodi ya Wakurugenzi ya kampuni hiyo ya Jumeme, Profesa Isack Safari, alipotakiwa kutoa maelezo ya utekelezaji wa agizo hilo, alieleza kuwa tayari wameanza kulifanyia kazi kwa kushusha bei ya umeme mpaka kufikia bei elekezi ya Serikali kama ilivyoagizwa pamoja na kubadilisha Uongozi wa kampuni hiyo.

“Mheshimiwa Waziri, Kufuatia maelekezo yako uliyoyatoa mara kwa mara ya kututaka tuzingatie bei elekezi ya Serikali katika mauzo ya umeme tayar tumeyazingatia na hivi leo ulivyokuja kujiridhisha umekuta tayari tulishajipanga na tulishaanza kutekeleza maagizo hayo toka siku tutu zilizopita”, alisema Profesa Safari 

Waziri Kalemani alimalizia kwa kuiagiza TANESCO kuanza taratibu za kupeleka umeme wa gridi ya Taifa katika visiwa hivyo kwa kutumia Miundombinu inayopita chini ya maji ili kuwaondolea adha ya umeme wanayopata wakazi wa visiwa hivyo vilivyoko ziwa victoria vikilizunguka jiji la Mwanza.

Share:

TBS Internship Programme For Graduates – 54 Posts

OPPORTUNITIES FOR INTERNSHIP PROGRAM   Background Tanzania Bureau of Standards (TBS) is Tanzania’s sole Standards body, formerly established by the Standards Act No. 3 of 1975, which was repealed and replaced by the Standards Act No. 2 of 2009. It is a Parastatal Organization under the Ministry of Industry and Trade. TBS introduced internship programs […]

This post TBS Internship Programme For Graduates – 54 Posts has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Business Development Director at ZOLA

Business Development Director    Do you want to impact global energy accessibility? ZOLA Electric (formerly Off Grid Electric) is the leading clean energy technology brand in Africa.  Through our distribution partners, ZOLA products bring light and power to homes, small businesses, and whole communities.  Our products help people stay connected and expand opportunities for work […]

This post Business Development Director at ZOLA has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Behavioral Insights Coordinators at International Rescue Committee (IRC)

Job Title: Behavioral Insights Coordinator   5 Locations Available | req19028 Job available in these locations: Dakar, Senegal Dar es Salaam, Tanzania, United Republic of Kampala, Uganda Abuja, FEDERAL CAPITAL, Nigeria Nairobi, NAIROBI MUNICIPALITY, Kenya Requisition ID: req19028 Sector: Research & Development Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: Yes Job Description The […]

This post Behavioral Insights Coordinators at International Rescue Committee (IRC) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Analyst at citi Bank

Analyst     The Analyst is an intermediate-level position responsible for assisting clients in raising funds in the capital markets, as well as in providing strategic advisory services for mergers, acquisitions and other types of financial transactions in coordination with the Institutional Banking team. The Analyst also serves as an intermediary in trading for clients. The […]

This post Analyst at citi Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Billing Administrator: Application Support at Vodacom

Billing Administrator: Application Support    At Vodacom, we’re working hard to build a better future. A more connected, inclusive and sustainable world. As a dynamic global community, it’s our human spirit, together with technology, that empowers us to achieve this. We challenge and innovate in order to connect people, businesses, and communities across the world. […]

This post Billing Administrator: Application Support at Vodacom has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Specialist Network Security at Vodacom

Specialist Network Security    At Vodacom, we’re working hard to build a better future. A more connected, inclusive and sustainable world. As a dynamic global community, it’s our human spirit, together with technology, that empowers us to achieve this. We challenge and innovate in order to connect people, businesses, and communities across the world. Delighting […]

This post Specialist Network Security at Vodacom has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 19,2021






















Share:

Sunday, 18 July 2021

DC KISWAGA AMALIZA SAKATA LA MGAMBO NA MACHINGA KAHAMA.... "VIJANA MSISHINDANE NA SERIKALI"


Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga

Na Malunde 1 blog - Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ameelekeza kuachiwa huru kwa Wafanyabiashara wawili wa Matunda Rasta na Jofley walioshikiliwa kwa kosa la kushambulia askari wa Manispaa ya Kahama waliokuwa wakitimiza wajibu wao.

Mhe. Kiswaga ametoa msamaha huo mapema leo Jumapili Julai 18,2021 alipotembelea na kuongea na wajasiriamali wa Soko la Matunda na Machinga lililopo eneo la CDT Mjini Kahama.

"Nimetoa msamaha kwenu ili iwe funzo kwenu na kuwapa nafasi ya kujirekebisha, serikali ina malengo makubwa kwa vijana.. Serikali inataka muwe pamoja, muunde vikundi vingi ili kama hamna mitaji iwakopeshe, na mikopo inayotolewa na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan haina ubaguzi wa itikadi za vyama, uwe Chadema, iwe CUF, NCCR au CCM wote ni wa Tanzania, ni marufuku kwa machinga kufirisika.. " amesema Kiswaga.

Mhe. Kiswaga amesema ziara yake kwenye eneo hilo imetokana na kuona kipande cha Video kilichokuwa kinasambaa mitandaoni kikionesha Mgambo wa Manispaa ya Kahama wakibeba bidhaa za muuza matunda aliyekuwa akifanya biashara pembezoni mwa barabara.

"Unajua mitandao ya Kijamii ina nguvu sana, na jambo linasambaa kwa haraka sana kupitia mitandao hiyo, nlipoona hiyo video hiyo nikawasiliana na viongozi lakini sijaridhishwa na maelezo yao na ndiyo maana nimekuja hapa, ila kwa maelezo ya Mheshimiwa Diwani na viongozi wa Machinga nimejiridhisha kuwa wale vijana walikuwa na makosa, ila tunawapa nafasi nyingine..na nakuagiza kiongozi wa eneo hili kuwapatia hawa eneo la kufanyia biashara zao ndani ya eneo hili ambalo lipo rasmi kwa kazi hiyo..na Mkurugenzi ameweka wazi kuwa ikifika saa moja jioni mnaruhusiwa kwenda huko barabarani lakini asubuhi na mchana eneo la biashara ni hili.." amesema Kiswaga.

Amewataka wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wauza matunda kufuata sheria walizozitunga na kutokuwa na tabia ya kushindana na serikali kwa maamuzi ambayo yanaweza kuwahatarishia uchumi wao.

Katika hatilua nyingine Mhe. Kiswaga amewaasa askari wa Manispaa ya Kahama kufanya jukumu lao la msingi la kulinda wafanyabiashara wafanye biashara kwa amani badala ya kuwabughudhi na kuwapa hofu na inapotokea changamoto kabla hawajachukua hatua wawasiliane na viongozi kwanza.

Kwa upande wao wafanyabiashara hao waliokumbwa na hiyo kadhia wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa Msamaha na wameahidi kutii na kufuata sheria zilizowekwa na Serikali.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Underson Msumba amesema serikali ipo kwajili ya wananchi kwa kuboresha miundombinu rafiki na kuwataka wakulima kwenda kuchukua pesa za mikopo ili kukuza uchumi wao.

Share:

MAMA APATA MSHTUKO BAADA YA KUBAINI ANAISHI NA FAMILIA YA NYOKA CHINI YA KITANDA CHAKE



Mfano wa nyoka

Je utahisi vipi ukigundua umekuwa ukilala na nyoka chumbani mwako? Haya yamempata mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani ambaye amepigwa na bumbuwazi baada ya kutambua amekuwa akiishi na nyoka 18 chini ya kitanda chake.

Trish Wilcher alishtuka sana alipogundua kuna familia ya nyoka hao waliokuwa wakiishi katika chumba chake cha kulala nyumbani kwake Augusta, Georgia, Marekani. 

Katika posti kwenye mtandao wa Facebook, mnamo Jumatatu, Julai 12, Trish alipakia picha ya nyoka hao akisema kuwa: “Angalia nyoka wote hawa waliopo katika chumba changu cha kulala. yaaani nimechanganyikiwa.”

Kulingana na Trish, hii ni baada ya mumewe Max kugeuza kitanda chao cha kulala juu chini kuangalia kilichotokea na kisha walishtuka kupata watoto 17 wa nyoka na mama yao. 

Trish alisema huenda nyoka hao waliingia nyumbani kwao kutokana na shughuli ya ujenzi uliokuwa unaendelea mkabala na makazi yao hivyo nyoka hao walikimbia humo kutafuta hifadhi.
Share:

SIMBA YAUNGURUMA KWA MSIMU WA NNE, WAIPIGA NAMUNGO 4-0


Wachezaji wa Simba wakishangilia ubingwa walioutwaa msimu wa 2020/21

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara imefikia tamati hii leo kwa michezo tisa kupigwa katika viwanja tofauti, huku katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam mabingwa mara nne mfululizo klabu ya Simba wamepata ushindi wa magoli 4 kwa 0 dhidi ya Namungo.

Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wake Medie Kagere, Chris Mugalu aliyefunga mara mbili na John Bocco akifunga moja.

Simba imemaliza msimu ikiwa na alama zake 83 wakati waliokuwa wapinzani wao wa karibu Yanga ambao jioni ya leo wametoka suluhu na Dodoma Jiji huko katika dimba la Jamhuri, wamemaliza katika nafasi ya pili wakiwa na alama 74.

Washindi wa tatu Azam Fc wameshinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ,shukrani kwa nyota wake Mudathir Yahya na wamemaliza msimu wakiwa na alama 64.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo katika kumaliza msimu wa ligi kuu Tanzania bara 2021/22 ni;

Ruvu shooting 0 – 1 Azam FC
Mbeya City 4 – 0 Biashara United
KMC FC 1 – 0 IHEFU FC
JKT Tanzania 2 – 1 Mtibwa Sugar
Tanzania Prisons 1 – 1 Gwambina FC
Polisi Tanzania 1 – 0 Mwadui FC
Coastal Union 3 – 1 Kagera Sugar

Kwa matokeo haya sasa Coastal Union na Mtibwa Sugar watakwenda kucheza mtoano kugombea kusalia ligi kuu, Huku timu za JKT Tanzania, Gwambina FC, Ihefu FC na Mwadui FC wao wameshuka daraja moja kwa moja.

CHANZO - ETV
Share:

Tanzia : ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ALLY NASSORO RUFUNGA AFARIKI DUNIA

Ally Nassoro Rufunga enzi za uhai wake

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga amefariki dunia leo Jumapili Julai 18,2021.

Taarifa za chanzo cha kifo chake bado hazijajulikana na mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari)  katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Ally Nassoro Rufunga alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2016.

R.I.P Rufunga

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger