Sunday, 18 July 2021

Mashuhuda waeleza tukio la Gift Mushi alivyopigwa risasi na Alex Karosso


Mashuhuda wameeleza kuwa Gift Mushi aliyepigwa risasi jana alikumbwa na tukio hilo, baada ya kumshauri Alex Korosso aache tabia ya kuwatishia watu kuwapiga risasi  wakati wakipata kinywaji.

Tukio hilo la kusikitisa lilitokea jana Julai 17,2021 katika baa ya New Lemax  iliyopo maeneo ya Sinza kwa Remmy

Mashuhuda wamesema siku ya tukio Korosso alifika kwenye baa hiyo aliyezoea  kunywa akiwatisha wenzake na kwamba anatamani kuua mtu.

"Gift Mushi alipigwa risasi moja ya mguu, mbili za tumboni baada ya kumuona anaendelea kuangaika chini alienda kummalizia kwa kumpiga risasi  tatu kichwani na baadaye kurudi kwenye kiti alichokaa kujimalizia mwenyewe kwa kujipiga risasi moja kichwani," amesema Karim Hussen.

"Alikuja toka asubuhi akiwa na gari yake ambayo alimpa ufunguo aitengeneze huku mwenyewe akiwa anaendelea kunywa na kuwatisha wenzake muda wote na baadae Gift Mushi ambaye ni marehemu akamfuata kumshauri aache kuwatisha wenzake wakati wakinywa."

"Baadaye kuna jamaa mmoja alikuwa anakunywa  naye silijui jina lake akamuambia kwamba kuwa yeye ni usalama wa taifa na kumuonesha kitambulisho baadae alitulia na kuanza kuomba msamaha, alikaa kimya kwa muda akawa anajishauri ghafla alitoka kwenye kiti alichokaa na kwenda hadi kwa DJ kumuambia azime muziki nako alikataliwa" amesema Lema.

Lema amesema "Kossoro baada ya kukataliwa kuzima muziki alianza kuongea kwa sauti kubwa na kusema  watu katika baa wanajifanya usalama na kuchomoa bunduki yake kuanza kupiga risasi juu baadae Gift Mushi alipomfuata kumshauri alipigwa risasi ya mguu kabla ya hajakaa sawa alipigwa risasi mbili za tumboni  na akuanguka chini  na watu wengine walikuwa wanakunywa walianza kukimbia," amesema.

Amesema wakati huo Gift Mushi alikuwa chini anahangaika baadae alimfuata tena kumpiga risasi tatu kumalizia kumuua na baadae alitoka nje ya baa na kwenda kwenye gari yake kufungua mlango alikuta umefungwa.

Husseni anaeleza "baada ya kuona mlango haufunguki alirudi tena kwenye baa na kukaa kwenye siti yake kisha kujipiga risasi ya kichwa na baadae sisi tulijitokeza,"

Husseni amesema siku hiyo Gift Mushi hakulewa isipokuwa Alex Korosso alikuwa amekuwa na tabia ya kuwatisha watu kwenye baa hii toka miezi miwili alipoanza kumiliki silaha hiyo yenye magazini 16," amesema.

 

Credit:Mwananchi



Share:

Watanzania Watakiwa Kutumia Fursa Za Ujenzi Bomba La Mafuta


Hafsa Omar-Kagera
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka Wananchi watakaopitiwa na ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kujitokeza na kuzitumia fursa mbalimbali ambazo zitapatikana wakati wa ujenzi wa bomba hilo.

Ameyasema hayo, Julai 17, 2021 wakati wa Mkutano na wadau mbalimbali kujadili fursa za Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta, uliofanyika katika Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagera.

Dkt. Kalemani amezitaja fursa hizo,ambazo ni ujenzi wa viwanda mbalimbali vitakavyozalisha bidhaa ambazo zitatumika katika ujenzi wa mradi.

Pia, amesema Watanzania zaidi ya 15,000 watajiriwa katika kipindi cha ujenzi wa bomba hilo, na  kuwataka pia kuchangamkia fursa za kufanya biashara mbalimbali ambazo zitawaingizia kipato.

Amesema, lengo la Mkutano huo ni kujenga uelewa na kuwaeleza wananchi wajibu wao ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali wakati wa ujenzi husika, ambapo ameeleza kuwa zaidi ya asilimia 80 kazi za mradi huo zitafanywa na Watanzania.

 “Mradi huo wakati wa ujenzi utaoa fursa kwa Watanzania wengi tunawaomba Watanzania kuchukua nafasi hii kuwekeza katika sekta mbalimbali, na kwa wale ambao hawana mtaji tunaongea na mabenki ili waweze kuwakopesha mikopo ya masharti nafuu ”alisema.

Aidha, amesema utekelezaji wa mradi umeanza na upo kwenye hatua za mwisho za ulipaji wa fidia, na baadhi ya maeneo tayari ujenzi wa barabara za kuelekea kwenye mradi umeanza.

Ameongeza kuwa, ujenzi wa mradi huo utachukua takribani miaka mitatu na utagharimu dola za kimarekani bilioni 3.5.

Waziri Kalemani, pia ameeleza manufaa  ya mradi huo kwa kufafanua kuwa katika Mikoa ya Singida, Tabora na Simiyu, maeneo hayo ambayo bomba linapita yanatarajiwa nayo kutoa mafuta  ambapo amesema nchi itatumia bomba hilo kupitisha mafuta hayo.

Pia, amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali pamoja na wawekezaji na kushiriki katika ulinzi wa bomba hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amesema, ujenzi wa mradi huo utainua uchumi wa Mkoa wa Kagera na kwa nchi kiujumla.

Vilevile, amesema atahakikisha mradi utajengwa na kusimamiwa kwa umakini, na mataifa mengine yatajua kuwa Watanzania ni watu makini na wazalendo na hilo litasadia nchi kuendelea kupata fursa mbalimbali za miradi kutoka kwenye mataifa ya jirani.

Pia, amesema kuwa uongozi wa Mkoa huo utahakikisha mradi huo unalindwa na utakuwa kuwa salama mda wote wa ujenzi na hata ukikamilika.

Nae, Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua fursa mbalimbali ambazo zitakazopatikana kwenye ujenzi wa mradi na kuwataka kujivunia ujenzi huo kwani unaenda kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.


Share:

Scholarships for Tanzanian Students| Ufadhili wa Kusoma Nje ya Nchi (Unalipiwa Kila Kitu)

πŸ“š FURSA ZA UFADHILI  WA KUSOMA NJE YA NCHI

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

    πŸŽ“ Tanzanian Scholarships


Kama wewe ni Mtanzania mwenye Ndoto ya Kusoma nje ya Nchi lakini hukuwa na uwezo, basi hii ni Nafasi yako. Kuna Nafasi Nyingi sana za Ufadhili zimetangazwa (Scholarships)


 Zote Hizo ni Full Funded( Unalipiwa kila Kitu) Japo kuna zingine utachangia kidogo 

_______________________ 

Bado hujachelewa, Deadline ni kuanzia Mwezi huu wa  saba na   hadi Mwakani-2022...BOFYA Hapo ChiniπŸ‘‡πŸ‘‡
._______________________ 


1.Jim Ovia Foundation Scholarships for African Students [ Fully Funded]…Apply by 29th July 2021

2. Africa Grants for Young Scientists..Apply by 27th July 2021

3.University of Pretoria MasterCard Scholarships in South Africa (Fully Funded for African Students)

4.Carl Duisberg Medicine Scholarships (Fully Funded )

5.IMD MBA Scholarships – Switzerland 2021 [ Fully Funded]… Apply by 1st September 2021

6.Japan Africa Dream Scholarships

7.Narratives of Africa Grants for Individuals and Organizations

8.LLM Scholarships in Intellectual Property

9.PhD Scholarships for Commonwealth Countries 2021/2022 [Fully Funded]

10.Germany Master Scholarships for Public Policy and Good Governance 2021 – [Fully Funded Scholarships]

11.Pan African University Scholarships 2021/2022 (Masters & PhD) for African Students [Fully Funded]
 
Bofya hapo chini kujua zaidi
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 


Share:

MHASIBU WA CHAMA WAIGIZAJI TANZANIA AUA KISHA KUJIUA KWA RISASI BAA


Alex Korosso kwa jina maarufu la Simba anayedaiwa kuua na kisha kujiua, alikuwa mhasibu wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA),imeelezwa.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Julai 18, 2021 na mwenyekiti wa chama hicho,Chiki Mchoma maarufu kwa jina la Chiki katika mahojiano yake na Mwananchi.

Tukio la Korosso kujiua lilitokea jana baa ya Lemax maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka mabishano kati yake na mtu aliyetambulika kwa jina la Gift ambaye alimpiga risasi na kisha naye kujipiga na kufariki hapohapo.

Via Mwananchi
Share:

RAIS SAMIA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI BURUNDI,AREJEA NCHINI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakati akitokea nchini Burundi leo tarehe 17 Julai, 2021 baada ya ziara yake ya siku mbili nchini humo. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi mbalimali wa Serikali ya Burundi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye Jijini Bujumbura Burundi baada ya kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili Nchini Burundi leo Julai 17,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye Jijini Bujumbura Burundi baada ya kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili Nchini Burundi leo Julai 17,2021. (Picha na Ikulu)
Share:

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIPONGEZA BANK OF AFRICA KWA KUSAIDIA KUKUZA SEKTA MBALIMBALI ZA MAENDELEO NCHINI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akiongea na Rais wa Benki ya Afrika, Othman Benjelloun, katika Hoteli ya Sofitel, Rabat nchini Morocco
alipofanya ziara ya kikazi nchini humo.

****
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, ameishukuru Bank of Afrika (BOA), kwa juhudi zake inazofanya kusaidia Tanzania katika sekta mbali mbali za maendeleo Mh. Kassim Majaliwa, alitoa pongezi hizo za shukrani Jumatano Julai 14, 2021 alipofanya mazungumzo na Rais wa Bank of Africa, Othman Benjelloun, katika Hoteli ya Sofitel, Rabat nchini Morocco.

Alisema kuwa uwepo wa Benki hii nchini Tanzania umewezesha wananchi kufaidika na huduma mbali mbali zinazotolewa na Benki hiyo, "Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Rais Samia Suluhu Hassan tunaishukuru Bank of Africa kwa juhudi hizi ".

Aliongeza kwa kumshauri Rais Benjelloun, kuendelea kupanua wigo wa huduma za benki hiyo nchini ili kuwafikia Watanzania wengi, hususani katika sekta za Elimu, Kilimo, Mifugo na Madini.

Waziri Mkuu aliahidi kuwa ataandaa utaratibu wa kukutanisha uongozi wa Benki na sekta binafsi nchini Tanzania ili kuona ni jinsi gani wanaweza kufanya kazi pamoja kuwahudumia Watanzania. Kwa upande wake, Rais Benjelloun alisema lengo la benki hiyo ni kuendelea kukuza uwekezaji wake nchini Tanzania.

"Tuko tayari kuwekeza katika maeneo ambayo viongozi wa kitaifa wa Tanzania watatushauri kwa lengo la kutoa mchango wetu katika kujenga uchumi."

Naye Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, alisema kuwa benki hiyo inapaswa kusaidia kukuza uhusiano wa Tanzania na Morocco katika sekta ya kilimo hususani katika mazao kama mpunga, tumbaku, kahawa na mazao mengine.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Leila Muhamed Mussa, alisema kuna maeneo ya pwani ambayo hayajafanyiwa uwekezaji hadi sasa, hivyo ni fursa kwa wawekezaji kuyatumia na kwamba Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amefungua milango kwa wawekezaji.

Aliitaka benki kuona jinsi ya kuwezesha wakulima utekelezaji shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Pamoja na ushiriki wa benki katika miradi mbalimbali ya maendeleo, benki imeonyesha dhamira yake katika kusaidia Biashara Ndogo na za Kati (SMEs) kwa kutoa bidhaa na huduma zinazovutia wateja wake. Kama benki ya biashara Imekuwa ikihudumia wateja wa makundi ya wateja wa Rejareja, Biashara Ndogo na za Kati (SMEs) na wateja wa Makampuni.
Share:

WANANCHI KONDE WAPIGA KURA LEO KUMCHAGUA MBUNGE WAO


Mkazi wa Msuka akionesha kidole baada ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 18,2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo. (Picha na NEC).
Mkazi wa Konde akipiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 18,2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Mkazi wa Konde akipiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 18,2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Mkazi wa Konde akipiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 18,2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Mpigakura akiwekwa wino baada ya kupiga kura
Wananchi wakihakiki majina yao katika daftari la mpiga kura kabla ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 18,2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Mpigakura akitoa kitambulisho chake na kuhakikiwa katika Daftari la Mpiga kura
Wakazi wa Konde wakiwa kawa katika foleni ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 18,2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Wakazi wa Konde wakiwa kawa katika foleni ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 18,2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Share:

VIJANA WA CCM SHINYANGA WAMUOMBA RAIS SAMIA KUTAZAMA UPYA SUALA LA TOZO YA MIAMALA YA SIMU...'LINAUMIZA'


Mwenyekiti wa UVCCM, Baraka Shemahonge akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga likiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Baraka Shemahonge wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulitazama kwa taswira mpya suala zima la tozo za miamala ya simu kwa manufaa ya wananchi wa hali ya chini na Ajira za vijana wengi wanaojipatia kipato kutokana na shughuli za kutuma miamala kwani mzunguko miamala ya simu za mkononi utapungua.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Baraka Shemahonge Julai16,2021 katika kikao cha Baraza la Vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga ambacho kimehudhuriwa na mkuu wa mkoa huo Dkt. Philemon Sengati aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho pamoja na Naibu Waziri wa Vijana Kazi na Ajira, Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Mbunge wa Kundi la Vijana Mwasi Kamani.

“Baraza la Vijana linampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya tangu kuingia kwake madarakani ikiwemo kukuza maendeleo pamoja na kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati nchini .Tangu kuingia kwake madarakani upo mwanga na matumaini kwa wananchi. Tunamuomba Mhe. Rais kulitazama kwa taswira mpya suala zima la tozo za miamala ya simu”,amesema Shemahonge.

Shemahonge amesema wanamuomba Mhe. Rais Samia alitazame upya jambo la Tozo za miamala ya Simu akibainisha kuwa wana imani kila Mtanzania yuko tayari kuchangia maendeleo ya nchi yake kwani Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe lakini tozo imekuwa kubwa kidogo.

“Tunaona vijana wengi watakosa ajira kwa sababu mzunguko wa miamala ya simu utapungua lakini wazee na wananchi waliopo vijijini wataathirika kwa sababu kule hakuna Benki, wengi wao wanatumia Simu kutuma na kutumiwa fedha. Kwa makato haya yanakwenda kuathiri moja kwa moja wananchi wenye kipato chaa chini”,amesema Shemahonge.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati amewaomba vijana wa UVCCM Mkoa kuendelea kuhamasisha Falsafa ya kujitegemea kiuchumi kwa vijana na kuwa wabunifu wa fursa mbalimbali huku akiafiki ombi la ujenzi wa Chuo Kikuu ambacho kitakuwa kichocheo cha uchumi wa mkoa wa Shinyanga.

Dkt. Sengati pia amechangia Shilingi milioni 2.5 kwa ajiri ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga.

Kuanzia Alhamisi Julai 15, 2021, watumaji na watoaji fedha kupitia simu za mkononi, walianza kulipa kodi ya uzalendo iliyopandisha gharama za kutuma na kutoa fedha mara 11 ya ilivyokuwa mwanzo, hali iliyoelezwa kuacha maumivu kwa wengi.

Kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wamesema tozo mpya ni mzigo mwingine kwa wenye kipato cha chini, hasa vijijini ambako simu za mkononi ni mkombozi wa huduma za fedha kutokana na kutokuwepo kwa huduma za benki.

Wamesema tozo hizo ni kubwa na zinashawishi watu kukwepa miamala ya simu na k kuejielekeza katika huduma za benki wakibainisha kuwa Tozo mpya ni maumivu kwa wananchi wa kipato cha chini ambao ndio watumiaji wakubwa wa miamala ya simu huku wengine wakidai kodi hiyo ni ishara ya kutowafikiria wananchi wa kawaida.
Share:

Naibu Waziri Mabula Apiga Marufuku Wanaoshitakiana Mabaraza Ya Ardhi Kugharamia Usafiri


Na Munir Shemweta, SONGWE
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amepiga marufuku wananchi wanaoshitakiana kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya kugharamia usafiri wa kwenda uwandani wakati wa kusikiliza mashauri ya ardhi.

Akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya, mkoa wa Songwe jana  Dkt Mabula alisema, asingependa kuona wananchi  wanaoshitakiana katika kesi ya ardhi mmoja wao atoe fadhila ya usafiri wa kwenda uwandani.

‘Tusingependa wale wanaoshitakiana mmoja wao atoe fadhila ya usafiri maana baada ya hapo mara nyingi wazee wa Baraza wanashawishika na kuona anayetoa usafiri kuwa amekuwa ni msamamaria mwema kwa hiyo wanamlipa fadhila hata kama hana haki ya kupata ushindi’ alisema Naibu Waziri Mabula.

Aliwataka Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi kuandaa ratiba za mashauri ya Ardhi kwenye maeneo yao na kuzipeleka kwa wakuu wa wilaya aliowaeleza kuwa watashirikiana na wakurugenzi wa halmashauri kuangalia ratiba na kutoa usafiri kwa wazee wa mabarza   ili kwenda uwandani wakati wa mashauri.

Naye Kamishna wa Ardhi Nchini Methew Nhonge alisema pamoja na kuwa sheria ya ardhi imeanisha utaratibu mzuri wa kisheria katika kushughulikia migogoro ya ardhi lakini halmashauri na ofisi za ardhi za mikoa zinao wajibu mkubwa wa kuhakikisha migogoro ya ardhi kabla haijaenda mahakamani inatatuliwa kwa njia ya kiutawala.

‘Bahati nzuri katika wizara tumeweka utaratibu kwa nchi nzima kuhakikisha kwamba viongozi wa ardhi wa mkoa pamoja na halmashauri kupitia watendaji wa sekta wanaenda kwenye ngazi za halmashauri na mitaa kutoa elimu na kushughulikia migogoro ya wananchi kiutawala’’ alisema Nhonge.

 Kwa upande wake Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya nchini Stela Tullo aliushurukuru uongozi wa mkoa wa Songwe kwa kusaidia kupata jengo la Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya na kueleza kwamba, uanzishwaji baraza hilo utasaidia kuondoa usumbufu waliokuwa wakiupata wananchi wa Songwe kusafiri  umbali mrefu kufuata huduma za Baraza mkoani  Mbeya.

‘Ninawasihi wananchi wa Songwe kulitumia vizuri baraza la ardhi la mkoa wa Songwe kupata huduma, ile migogoro ya ardhi iliyoshindwa kusuluhishana nyumbani hata katika ngazi ya familia na mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata basi serikali imewasogezea huduma kwenye baraza la ardhi na nyumba la wilaya  mkoa wa Songwe’’ alisema Stela Tullo.

Kabla ya uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, mkoa wa Songwe, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alizindua Baraza kama hilo  wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambapo aliagiza mashauri ya ardhi yasikilizwe na kuisha katika kipindi kisichozidi miaka miwili.


Share:

Hospitali ya Maswa Yapinga habari za uhaba wa dawa.


Samirah Yusuph.
Maswa.
Kufuatia tetesi zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kukosekana kwa dawa hata "Panadol"  katika hospitali ya wilaya ya Maswa, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Fredrick Sagamiko amesema taarifa hiyo sio sahihi.

Sagamiko amesema kuwa hali ya upatikanaji wa madawa katika hospital ya wilaya hiyo ni asilimia 98 na upatikanaji wa madawa muhimu ni 100 na kuwa halmashauri hiyo inaduka la madawa bora miongoni mwa maduka yote ya madawa nchini.

"Taarifa hiyo haina ukweli, kuna dawa za kutosha na duka la dawa linalo milikiwa na hospital ya wilaya ya Maswa ndilo duka linalouza dawa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali zote za Mkoa wa Simiyu pia tuna mfumo wa "hospital protocol" unaowezesha ofisi ya mkoa kupata taarifa za utoaji wa dawa kwa kila wiki kwa hospitali zote"

Ameongeza kuwa hapo mfumo wa utoaji taarifa za dawa katika ofisi ya mkuu wa wilaya imesaidia kuondoa kwa kiasi kikubwa upotevu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo dawa stahiki zinawafikia wahitaji bila kuwa na shaka.

Aidha kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali hiyo James Bwire alisema kuwa mahitaji ya dawa katika hospitali hiyo yanajitosheleza na kuwa hospitali hiyo inamaduka matatu ya dawa ambalo ni duka la wateja wa bima, duka linalo hudumia zahanati, vituo vya afya na hospitali nyingine pamoja na duka la hospital.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Binza Aroni Joseph Mboje alisema kuwa shida na madawa ilikuwepo kipindi cha nyuma lakini kwa sasa haipo tena mambo yanayo jitokeza katika mikutano sio uhalisia kwa sasa dawa zipo za kutosha.

"Vitu wanavyovisema wananchi hawana uhakika navyo baada ya taarifa hiyo nilifika hospitali kuja kujionea lakini kuna dawa nyingine wanaandikiwa wakachukue maduka ya nje hivyo wanasema hospitali haina dawa lakini dawa zipo za kutosha".

 Mwisho.


Share:

TCRA Na UCSAF Wapewa Mwezi Mmoja Kuja Na Mapendekezo Kutatua Changamoto Za Mwingiliano Wa Mawasiliano Mipakani


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew ametoa mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa maelezo ya kinachosababisha mwingiliano wa mawasiliano katika maeneo ya mipakani  na namna bora ya kutatua changamoto hiyo

Mhandisi Kundo amezungumza hayo katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya mipakani alipotembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa upande wa lango la Machame la kupandia mlima huo lililopo Wilayani Hai

“TCRA na UCSAF nawapa mwezi mmoja mje na majibu ya kutatua changamoto za mwingiliano wa mawasiliano katika maeneo ya mipakani ikiwa ni pamoja na maeneo ya hifadhi za Taifa kwa kuwa kuna maeneo ya mipakani kama Namanga minara ipo lakini bado kuna tatizo la mwingiliano wa mawasiliano”, alizungumza Mhandisi Kundo

Aliongeza kuwa ni muhimu kujiridhisha kama sababu ni nchi ya Tanzania kutii sheria, kanuni na miongozo ya Shirika la Kimataifa linalosimamia Mawasiliano (ITU) kuhusu uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano katika maeneo ya mipakani na hatua zilizochukuliwa za kutatua changamoto hiyo ili nchi jirani nazo zifuate utaratibu uliowekwa na ITU

Alisema kuwa eneo la hifadhi ni eneo nyeti sana kwasababu ni maliasili ambayo nchi inajivunia kama kivutio cha Taifa, chanzo cha ukusanyaji wa mapato kutokana na shughuli za utalii na pia ni urithi wa vizazi vijavyo hivyo ni eneo muhimu kuwa na mawasiliano ya uhakika

Aidha, katika hatua nyingine Mhandisi Kundo ameutaka uongozi wa hifadhi hiyo kuharakisha mchakato wa utoaji wa vibali vya ujenzi wa minara ya mawasiliano katika maeneo ya hifadhi kwa sababu ni moja ya maeneo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na watoa huduma kwa kuchelewesha au kukwamisha ujenzi wa minara katika maeneo hayo

Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa KINAPA Angela Nyaki amesema kuwa wapo tayari kushirikiana na watoa huduma katika  kufanikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya hifadhi kwa kuharakisha mchakato wa kutoa vibali sambamba na kuwapa watoa huduma maeneo ambayo wanaweza kujenga minara ya mawasiliano bila kuathiri uoto wa asili au viumbe hai vilivyopo katika hifadhi hiyo

Ameongeza kuwa watalii wengi wanaofika mahali hapo kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro wamekuwa wakishindwa kutumia huduma ya live streaming wakiwa juu ya mlima  kutokana na mwingiliano wa mawasiliano na mtandao wa Safaricom wa nchini Kenya kitu kinachosababisha watalii kukosa mawasiliano wanapopanda mlima kwasababu simu zao zinakuwa zinasoma mtandao wa nchi jirani.

Kwa upande wa Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard amesema kumekuwa na malalamiko mengi ya watoa huduma kuhusu ucheleweshaji wa vibali vya ujenzi wa minara ya mawasiliano katika maeneo ya hifadhi za Taifa nchini kitu ambacho kinachangia kwa kiasi kikubwa kwa watoa huduma kuamua kwenda kujenga mnara katika maeneo ambayo hayana changamoto za utoaji wa vibali

Aidha, watendaji wa TCRA, UCSAF, KINAPA pamoja na wawakilishi wa Makampuni ya simu nchini wamekiri kupokea maelekezo ya Naibu Waziri na kuahidi kuyafanyia kazi kama alivyoelekeza kwa lengo la kutatua changamoto ya mwingiliano wa mawasiliano  katika maeneo ya mipakani na maeneo ya hifadhi za Taifa nchini

Katika ziara hiyo Mhandisi Kundo aliambatana na watendaji kutoka katika taasisi za mawasiliano ambazo ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) pamoja na wawakilishi wa makampuni ya simu ya Vodacom, Tigo, Airtel, TTCL, Halotel na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Hai kwa lengo la kukagua ujenzi, ubora, uwezo na upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya mipakani.


Share:

Waziri Gwajima Ateta Na Uongozi Moi, Aupongeza Kwa Kutoa Huduma Bora Kwa Watanzania


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima jana amekutana na kufanya kikao na Uongozi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI).

Dkt. Gwajima ameipongeza Taasisi ya Mifupa MOI kwa kendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania kwa kipindi cha miaka 25.

“ Hongereni mnafanya kazi nzuri, nimekuja hapa tujadiliane ili tuone ni namna gani MOI itafikisha miaka 30 ikiwa bora Zaidi, kueni huru kuchangia mada ili tusonge mbele Zaidi.” Alisema Dkt Gwajima

Amesema pamoja na huduma nzuri nafahamu kwamba Kuna changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa ili tuendelee kutoa huduma Pamoja na mambo mengine.

Dkt. Gwajima amepokea maoni, michango pamoja na changamoto mbalimbali zinazolenga kuboresha hali ya utoaji huduma katika Taasisi yaTiba na Mifupa (MOI).

Hata hivyo Dkt.Gwajima amewapa siku kumi Taasisi hiyo kuandaa taarifa watashughulikiaje changamoto zilizo ndani ya uwezo na kuziwasilisha kwake.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI Prof. Charles Mkonyi amesema Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI) ina mpango wa kuanzisha kliniki katika wilaya za mkoa wa DSM ili kuwasogezea huduma Wananchi.

“Pamoja na kuanzisha hizi kliniki pia tunalenga kujenga hospitali ya kisasa ya utengamao katika kiwanja cha MOI kilichopo Mbweni Mpiji jiji Dar es. Salaam, Alisema Prof. Mkonyi.

Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema Taasisi ya MOI imeendelea kusogeza huduma kwa wananchi ili kupunguzia adha ya kusafiri kufuata huduma Dar es Salaam.

“Tumesogeza huduma za kibingwa za ubongo KCMC pamoja na Bugando tumesogeza huduma za Mifupa, Hospiali ya kanda Mbeya na Nyangao Lindi Alisema Dkt. Boniface.

Dkt. Boniface amesema Maabara ya kisasa ya Ubongo (Angio Suit) iliyoanzishwa hivi karibuni tayari wagonjwa 27 wameshafanyiwa upasuaji.


Share:

Waziri Kabudi Awataka Watumishi Wa Wizara Yake Kushiriki Katika Majukumu Na Kutathmini Utekelezaji Wake


Na mwandishi maalum, Morogoro.
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amewataka watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kushiriki katika utekelezaji wa majukumu ya wizara na kutathmini mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu hayo kwa pamoja ii kuleta tija na ufanisi ndani  ya Wizara.

Prof.Kabudi alikuwa akizungumza na watumishi hao alipokuwa akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika mkoani Morogoro.

“Ni vyema kila mtumishi akashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa pamoja kama timu na kutathmini mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara,” alisema.

Prof. Kabudi pia amewataka watumishi hao kuhakikisha wanasoma na kuielewa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 -2025 na kupanga kuitekeleza, kufahamu vipaumbele vya serikali ya Awamu ya Sita na jinsi vinavyopaswa kutekelezwa, kujitambua, kutambua nafasi  na majukumu yao ndani ya Wizara na kuwa na  utendaji kazi wa pamoja kama timu.

Prof Kabudi pia ametaka kila mtumishi  wa Wizara  kushiriki katika utendaji kazi wa pamoja na kushiriki katika ujengaji wa taswira ya Wizara ili kuwa na taswira inayoendana na mabadiliko ya nchi inavyokwenda ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ili umma upate kufahamu.

Amewataka watumishi hao kuhakikisha wanazingatia na kufuata sheria, taratibu na kanuni za Serikali kuwa waadilifu katika mawasiliano na kuongeza na kuimarisha mawasiliano na mashauriano ya kazi ndani ya Wizara ili kumfanya kila mtumishi kuelewa mambo yanayotekelezwa.

Prof. Kabudi pia amewapongeza watumishi hao kwa kutembelea ili kujionea kwa pamoja utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere huko Rufiji mkoani Pwani na Ujenzi wa Reli ya Kisasa kutokea  mkoani Morogoro – Kilosa hadi Dodoma na kuwasihi wawe mabalozi wazuri kuelezea yanayoendelea katika miradi hiyo na kuendelea kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria walitembelea miradi ya ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere huko Rufiji mkoani Pwani na walipokuwa njiani kurejea jijini Dodoma walitembelea Ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea kutokea Morogoro – Kilosa hadi Dodoma


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo July 18



Share:

Saturday, 17 July 2021

AVIMBA SEHEMU ZA SIRI BAADA YA KUPAKUA ASALI YA MKE WA MGANGA WA JADI

Kijogoo mmoja kutoka mtaani Kabiria, Nairobi nchini Kenya amelazimika kujifungia chumbani kwa siku saba bila kuona jua baada ya sehemu zake za siri kurefuka na kufura alipochepuka na mke wa mganga wa kienyeji.

Inaarifiwa kwamba jamaa alijua kwamba jirani yake aliyekuwa mganga na wake wanane hangeweza kuwahudumia wote naye akajitolea kumsaidia. 

“Ni mzee sana. Gemu ya wanane haiwezi! Yatushinda sisi vijana sembuse mzee asiye na meno?” jamaa alijisifu jinsi alivyonukuliwa na Taifa Leo. 

Penyenye zinasema kwamba mpiga ramli huyo alikuwa kipofu jombi alianza kuchezea mechi nyumbani kwa mganga huyo bila aibu. 

Asali ilikuwa tamu kwa kuwa hata baada ya kuonywa, lofa alizidi kuipakua kila alipotaka.

 Hata hivyo siku ya kioja ilipofika, baada ya jamaa kurina asali ya mke wa mganga alishindwa kuvalia suruali kwani sehemu zake za siri zilivimba zikajaa na kujaza suruali kupindukia. 

Ilimbidi aende kwake usiku akiwa amejifunga leso ya mke wa mganga huyo. “Jamani nala kiburi na ujeuri wangu. Kipi nilichovuna kwa mke wa mtu isipokuwa haya maradhi yasiyo ya kawaida,” lofa alilia.

Duru zinaarifu kwamba jamaa alikimbizwa katika hospitali zote lakini madaktari wakasema wasingeweza kuutibu ugonjwa wake.

 Jamaa alianza kujuta na kuamua kwenda kwa mpiga ramli kukiri makosa yake na kuomba msamaha ili amgangue apone.

 “Nafa! Nitaenda kuomba msamaha kwa jirani yangu,” jamaa alisema akielekea kwa mganga ambaye inasemekana alikuwa akimsubiri. 

“Mimi nimekusamehe na ugongwa huu uishe. Hata hivyo lazima unihakikishie kwamba hautamgusa mke wangu siku nyingine tena! Wake zangu wote ni waya ya stima ukikanyaga nawe utalia,” mganga alisikika akimuonya jamaa huku wawili hao wakikumbatiana. 

“Ukitamani mke wangu, njoo uniombe ruhusa kwanza,” mpiga ramli alimweleza kwa kejeli kijogoo. Jamaa alirejea kwake akiwa mzima na mwenye afya baada ya mganga huyo kumnasua kutoa kwenye ndumba yake.

Chanzo - Tuko News

Share:

WAFICHA MAITI NA KUJIZUIA KULIA KUKWEPA GHARAMA ZA KWENDA MOCHWARI



Miguu

Wananchi wa Kijiji na Kata ya Lupanga, wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamesema wamekuwa wakilazimika kuficha maiti, kuzuia matangazo na kujizuia kulia unapotokea msiba jioni au mchana majumbani mwao ili kuepuka gharama za kusafirisha maiti kwenda mochwari.

Wananchi wa Kijiji hicho wameeleza changamoto hiyo katika mkutano wao na mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga, alipofika katika Kijiji hicho ikiwa ni ziara yake anayoifanya katika kila Kijiji ili kupata changamoto na kuzifanyia kazi.

Zebedayo Mgaya ni mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho aliyeeleza changamoto hiyo huku akibainisha kuwa hivi karibuni alifiwa na ndugu yake na kulazimika kukaa kimya na maiti nyumbani kwake akihofia kutangaza kwa kuwa uongozi wa Kijiji hicho ungemtaka kufikisha mwili wa marehemu mochwari iliyopo umbali wa zaidi ya Km 10 kutoka kwenye kijiji hicho huku gharama za usafirishaji pekee zikiwa ni shilingi 40,000 hadi 50,000.

"Gharama za kusafirisha mwili kutoka hapa mpaka mochwari iliyopo Mlangali ni zaidi ya Km 10 na gharama zake ni 50,000 na sijui kwanini gharama ya kusafirisha maiti ni kubwa kuliko kusafirisha mahindi, nashauri kama Mochwari ni mradi mzuri kwa Wizara ya Afya au Halmashauri basi wajenge kila kijiji mahali ambapo mtu anaweza kufikisha maiti na kurudisha nyumbani, "amesema Zebedayo Mgaya.

Aidha, wananchi wa kijiji hicho wamesema wamekuwa na hofu wanapopata msiba na kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji kwa kuwa imekuwa ikiwalazimu kufikisha maiti katika mochwari kutokana na kutoruhusiwa kulala na maiti huku wengi wao wakiwa hawana ada ya mochwari kwa wakati huo.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Baraka Mfaume, aliyeongozana na mbunge katika mkutano huo amesema chama kimepokea changamoto hiyo na kuelekeza ofisi ya mkuu wa wilaya kuifanyia.

CHANZO - EATV
Share:

SI WOTE WATUMIAJI WA POMBE NA DAWA ZA KULEVYA NI MATAKWA YAO,SOMA STORY HII

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger