Friday, 16 July 2021

RAIS SAMIA AWASILI NCHINI BURUNDI KUANZA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU MBILI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Melchion Ndadaye Jijini Bujumbura Burudi kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa ya siku mbili leo Julai 16,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Burundi Mkuu wa Burundi Mhe. Prosper Bazombanza alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Melchion Ndadaye Jijini Bujumbura Burudi kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa ya siku mbili leo Julai 16,2021.(Picha na Ikulu)

Mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Melchion Ndadaye Jijini Bujumbura Burudi kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa ya siku mbili leo Julai 16,2021.
Share:

MKAKATI WA KOPA MBUZI LIPA MBUZI KUANZA, CHANJO ZA MIFUGO ZATAKIWA VIJIJINI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (kushoto) akipewa maelezo na mmoja wa wanasanyansi wanaotengeneza chanjo ya Tatu Moja Prof. Phillemon Wambura namna chanjo hiyo inayodhibiti magonjwa ya mdondo, ndui na mafua ya kuku isivyoweza kughushiwa kwa namna yoyote ile kwa kuwa imewekewa rangi maalum ya kubaini endapo ikiwa imeghushiwa. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akionesha namna chanjo ya Tatu Moja inayozalishwa na kampuni ya Nobel Vaccine Bioscience (NOVABI) inavyotumika kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya mdondo, ndui na mafua ya kuku kupitia njia ya kwenye macho ya mifugo hiyo. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akitoa maelekezo kwa uongozi wa Ranchi ya Mkata iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, kuhakikisha wanazalisha mbuzi wengi zaidi kwa ajili ya mkakati wa kopa mbuzi lipa mbuzi ili wananchi wengi zaidi waweze kuingia katika ufugaji wa kisasa na kibiashara. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)



Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa ameshika moja ya aina ya mbuzi wanaozalishwa kwenye Ranchi ya Mkata iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogororo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja katika ranchi hiyo na kuagiza ranchi hiyo kuendeleza uzalishaji wa mbuzi kwa ajili ya kufuga kibiashara. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Na. Edward Kondela



Serikali imesema Ranchi ya mifugo ya Mkata iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro itakuwa sehemu ya kuzalisha mbuzi kwa wingi kwa ajili ya mkakati wa kopa mbuzi lipa mbuzi ambao unatarajia kuanza hivi karibuni lengo likiwa ni kuwa na mbuzi wa kutosha kwa ajili ya soko la nje ya nchi.

Akizungumza na uongozi wa ranchi na Wilaya ya Kilosa, wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja katika Ranchi ya Mkata, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalllah Ulega amesema ni muhimu kuangalia namna bora ya kufanya ufugaji wa kibiashara katika ranchi hiyo.


Amesema serikali imechagua Ranchi ya Mkata kuwa kituo cha kuzalisha mbuzi kwa wingi ambacho watakuwa wanasambaza katika maeneo mbalimbali nchini.


"Tutakayempa tutataka tujue yupo wapi na ana mbuzi wangapi ili tuwatambue na tuwaingize katika mfumo wetu wa takwimu za kibiashara ili iwapo tunapata mteja wa kilo 50 kwa mwezi kweli tuwe na uhakika wa kupata kilo hizo 50 kwa mwezi.” Amesema Mhe. Ulega

Kutokana na mkakati huo wa kopa mbuzi lipa mbuzi mahitaji ya mbuzi yatakuja kuwa makubwa nchini hivyo ameitaka ranchi hiyo kuzalisha mbuzi kwa wingi ili kuweza kutosheleza soko la ndani na nje ya nchi.

Aidha Mhe. Ulega amesema wafugaji wa mbuzi wafuge kibiashara ili kuweza kutimiza vigezo na masharti ya wateja wa kimataifa kama nchini hizo na kutolea mfano wa nchi za uarabuni ambazo wanataka mbuzi wenye uzito wa kilo kati ya 8 hadi 10 ambao hawajakomaa sana.

Kwa upande wake Meneja wa Ranchi ya Mkata Bw. Oscar Magete amesema ranchi ilianzishwa na serikali kwa madhumuni ya kuendeleza na kueneza ufugaji bora wa mbuzi, kondoo na ng'ombe ambapo ranchi hiyo kwa sasa ina mbuzi 609 kondoo 116 na ng'ombe 47.


Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ulega ametembelea kiwanda cha kuzalisha chanjo cha Nobel Vaccine Bioscience (NOVABI) kilichopo Mkoani Morogoro kinachozalisha chanjo aina ya Tatu Moja kwa ajili ya ya mdondo, ndui ya kuku na mafua ambayo yanaathiri mfumo wa upumuaji na yamekuwa chanzo kikuu cha vifo vya kuku na kuwatia hasara wafugaji.


Akiwa kiwandani hapo Naibu Waziri Ulega ameelekeza chanjo hiyo ya kipekee isambazwe maeneo mbalimbali nchini hususan vijijini ambapo kuna wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji ili waweze kuipa mifugo yao chanjo kuondokana na hasara ambayo wamekuwa wakipata ya kuku kufa kutokana na magonjwa hayo.

Ameongeza kuwa ni vyema uongozi wa wizara kuhakikisha chanjo mbalimbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi zinawafikia walengwa hususan waliopo vijijini ili waweze kufuga kibiashara na waweze kunufaika kupitia mifugo yao.





 


Share:

WAZIRI JAFO AUPA 5 MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE

Mhandisi Mkazi kutoka Taasisi ya TEKU - TANROADS John Mageni akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi kwa lengo la kukagua uzingatiaji wa masharti yaliyowekwa katika Cheti cha Tathmini ya Mazingira katika ujenzi wa Mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Julius Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samwel Gwamaka
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua na kutoa maelezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kufua umeme wa Mwalimu Julius Nyerere juu ya uzingatia wa Kanuni za Mazingira za Udhibiti wa Taka hatarishi na Taka za Kielekroniki za mwaka 2021. Waziri Jafo ameelekeza taka hizo ikiwa ni pamoja na chuma chakavu kuuzwa wa wafanyabiashara wenye vibali tu
Picha zikionyesha hatua mbalimbali za ujenzi wa Mradi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere. Ujenzi huo umefikia asilimia 54 ya utekelezaji kati ya asilimia 59 zilizokusudiwa na unaratajiwa kukamilika tarehe 14/06/2022.

.......................................

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na uzingatiaji wa Sheria ya mazingira katika kutekeleza Mradi wa Kimkakati wa kufua umeme katika bonde la Mto Rufiji.

Waziri Jafo amesema haya leo mara baada kufanya ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa masharti yaliyowekwa katika cheti cha Tathmini ya Athari kwa mazingira kinachotolewa na Ofisi yake.

Amesema ameridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Mhandisi Mkazi wa TEKU John Mageni kuhusu hatma ya mashimo yanayochimbwa kwa ajili ya upatikanaji wa madini ujenzi ikiwemo mawe, kokoto na mchanga.

"Nnimeridhika na maelezo ya wataalamu wetu kuwa mashimo haya yatatumika kama chanzo cha mazalia ya viumbe hai wa majini baada ya mradi kukamilika, nimefarijika sana" Jafo alisisitiza.

Jafo amemuagiza Mhandisi Mkazi na wakandarasi kuhakikisha kuwa vyuma chakavu na taka za kielektroniki zinazozalishwa katika mradi huo zinafuata taratibu za kimazingira na kuuzwa kwa wafashabiashara wenye vibali vya Serikali vya mazingira ikiwa ni pamoja na kibali cha ukusanyaji, kibali cha kuhifadhi na kibali cha kusafirisha taka na kusisitiza kuwa taka zote zinazozalishwa eneo la ujenzi ni lazima kukidhi matakwa ya kimazingira.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano ma Mazingira Mhe. Selemani Jafo amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka kusimamia kwa ukaribu na kufuatilia ajenda ya mazingira, uhifadhi na usimamaizi wa Mazingira katika ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere.

Akikagua mfumo wa Maji taka katika eneo la ujenzi, Waziri Jafo ameagiza Afisa Mazingira wa Mradi huo kuhakikisha anatunza takwimu za kiasi cha maji taka yanayozalishwa katika eneo hilo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samwel Mafwenga amesema.ameyapikea maagizo yaliyotolewa na Waziri Jafo kwa Taasisi yake ya kuhakikisha inafuatilia masuala yote ya takwa la kimazingira katika mradi huo. " Tumepokea maelekezo ya Mheshimiwa Waziri na tutaendelea kuusimamia huu mradi mkubwa wa ufuaji umeme katika masuala yoye ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira"

Awali Meneja wa Mradi huo Mhandisi Mkazi John Mageni amesema shughuli zote zinazoendelea zimezingatia takwa na mahitaji ya Sheria ya mazingira kwa mujibu wa cheti cha mazingira walichopewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Waziri Jafo ametembelea mradi huo wa kufua umeme kwa lengo la kujionea masuala mbalimbali yanayohusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Ujenzi huo wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere umefikia asilimia 54 ya utekelezaji kati ya asilimia 59 zilizokusudiwa na unaratajiwa kukamilika tarehe 14/06/2022.

Share:

TGNP YATOA MAFUNZO KWA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA DAR ES SALAAM, SANGAI ATAKA WATAMBUE RASILIMALI ZA NCHI


Afisa wa Programu ya Mafunzo na Ujenzi wa Nguvu katika Jamii wa TGNP Bi. Anna Sangai akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wanajamii kutoka vituo vya taarifa na maarifa vya mkoa wa Dar es salaam.

***
Wanajamii wametakiwa kuamka na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo yao kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.

Hayo yameelezwa jana Julai 15,2021 na Afisa wa Programu ya Mafunzo na Ujenzi wa Nguvu katika Jamii wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Anna Sangai wakati akitoa mafunzo kwa baadhi ya vituo vya Taarifa na Maarifa vya mkoa wa Dar es salaam.

Akiongea katika mafunzo hayo ya siku moja yaliyofadhiliwa na Chuo cha COADY International kupitia mradi wake wa Engage: Woman Empowerment and active Citizen, wenye lengo la kuisaidia jamii kuweza kuzitambua na kuzitumia fursa mbalimbali walizonazo katika maeneo yao kwa kutumia moduli ya ABCD.

Afisa huyo amesema kuwa moduli hiyo licha ya kuwasaidia wanajamii kuweza kutambua fursa mbalimbali ndani ya jamii yao, lakini pia itawasaidia kuweza kupigania usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuhimiza serikali kuweza kutenga bajeti yenye mlengo wa kijinsia.

Amesisitiza kuwepo na bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa kuwa itakuwa ni bajeti inayolenga makundi yote lakini pia inahakikisha rasilimali fedha zinazokwenda kutumika kwenye miradi ya maendeleo zinatumika kama zilivyokusudiwa.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo ya ABCD yamewakutanisha wanajamii kutoka katika vituo vya Taarifa na Maarifa Kipunguni, Majohe, Saranga Mabwepande, Mabibo na Kivule ambapo vituo hivi vilifanyiwa uraghibishi mwezi Machi mwaka huu, na hii ni kuendelea kuwajengea uwezo ili waweze kuendelea kutekeleza mpango kazi waliyouandaa baada ya mafunzo yaliyopita.

Aidha Sangai amesema kuwa mafunzo hayo pia ni fursa ya wanajamii hao kuweza kubadilishana uzoefu wakati wa utekelezaji mpango kazi huo, kwa kushirikishana na kusaidiana endapo kituo kimoja kitakuwa kimekwama au kinapitia kwenye changamoto ama nyingine.

Amesema kuwa matarajio yao baada ya mafunzo haya ni kwamba watakuwa wameweza kuzalisha waraghibishi wazuri na wengi ambao wataweza kuwa mabalozi wazuri wa kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawajaweza kupata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo.

Afisa wa Programu ya Mafunzo na Ujenzi wa Nguvu katika Jamii wa TGNP Bi. Anna Sangai akiwezesha katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wanajamii kutoka vituo vya Taarifa na Maarifa vya Dar es salaam.
Baadhi ya wanajamii wakisikiliza kwa umakini mafunzo ya ABCD.
Mshiriki kutoka kituo cha Taarifa na Maarifa Kipunguni Fatma Abdulahman akichangia mada katika semina ya ABCD iliyoandaliwa na TGNP.
Baadhi ya wanajamii walioshiriki mafunzo ya ABCD yaliyoandaliwa na TGNP wakiwa katika kazi za makundi.
Mwanaharakati kutoka kituo cha taarifa na maarifa Majohe Joseph Safari akitoa ufafanuzi wa jambo katika semina ya ABCD.
Semina ikiendelea
Share:

Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADO 'MALIGANYA' - JIRANI


Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo kutoka Kahama Mkoani Shinyanga inaitwa Jirani.

Tazama Video hapa chini
Share:

Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADHO 'MALIGANYA' - MITIHANI YA DUNIA


Msanii wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kutaza video yake mpya inaitwa Matatizo ya Dunia
Share:

KAY JAY :KUTOKA KUANDIKIA WASANII WENZAKE MPAKA KUWA "ORDINARY GUY"

Kay Jay

Kayjay ni Mwandishi wa nyimbo na mwimbaji kutoka nchini Nigeria ambaye amewahi kuwaandikia wasanii wakubwa kama vile TundeEdnut ('Catching Cold'), Iyanya ('IyanuMashele'), KCEE ('Burn' & 'Psycho'), Naeto C, Kach ('Olo'), Chuddy K ('Nenda chini'), Stunna ('Balance' akishirikiana na Iyanya), Samklef, Tillaman, BimbiPhiliphs (Duro Dada).

Licha ya hivyo Kayjay amefanikiwa kushirikiana na wasanii wengi kama vile Shaydee,skales ,Samklef na wengine.

Lakini kwa sasa ameachia kazi yake mpya ambayo inapatikana katika mitandao kama vile Spotfiy ,Itunes ,Boomplay,Audiomack ,Youtube na kwingine.

Unaweza Kusikiliza na kudownload kazi yake "Ordinary Guy" @kayjayogbonna
Share:

SERIKALI IWEKE JITIHADA KWENYE KUWEZESHA VIFAA VYA MASOMO YA SAYANSI


Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete wakati mkutano wao baina yao na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kueleza  siri iliyowafanya kung’ara kwenye matokeo ya kidato cha sita 2020/2021 kushoto ni Mwalimu wa Taaluma Msaidizi wa Shule ya Sekondari Coastal High Shool Moses Mhina
Mwalimu wa Taaluma Msaidizi wa Shule ya Sekondari Coastal High Shool Moses Mhina akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete
Mwalimu wa Michezo na Klabu za Jamii kwenye shule  hiyo akieleza namna michezo inavyochangia ufaulu kwa wanafunzi Salim Mwakumuna kushoto ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete
Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Coastal High School wakiendelea na majukumu yao kama walivyokutwa
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete akikagua madaftari ya wanafunzi kama inavyoonekana


SERIKALI imeshauri kuweka juhudi kubwa kuwezesha vifaa vya kufundishia ambavyo vitasaidia kuwa na wanasayansi halisi kwa kusoma kwa vitendo ili kuweza kuendana na uchumi wa viwanda.

Iwapo vifaa vya masomo ya sayansi vitakuwepo kwenye shule mbalimbali hapa nchini itawawezesha wanafunzi kuweza kusoma kwa vitendo na hivyo kuongeza ufaulu na hatimaye kuwa na wataalamu wengi

Hayo yalisema na Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete wakati mkutano wao baina yao na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kueleza  siri iliyowafanya kung’ara kwenye matokeo ya kidato cha sita 2020/2021..

Shule hiyo imefanya vizuri katika matokeo hayo  baada ya Wanafunzi kuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza na Pili tu (Division I na II)yaliyopatikana shuleni hapo na kuifanya kuwa ya kwanza katika wilaya ya Tanga.

Alisema matokeo hayo yamewawezesha kuendelea kuwa shule ya kwanza(Namba 1)katika wilaya ya Tanga mjini huku wakiwa shule ya nne(Namba 4) kwa mkoa wa Tanga.

Aidha alisema mafanikio hayo yamechagiwa na uongozi pamoja na walimu walio bora ikiwemo kujituma bila kuchoka na wanafunzi kuwa na ari katika masomo.

"Kwanza ni ushirikiano kutoka kwa Mkurugenzi wa Shule hii Mathew Marupa kuwa na walimu bora na wanajitoa kwa muda wote hali hii imesaidia kuwezesha kupata matokeo mazuri”Alisema

Alisema pia ni kuwekwa kwa bidii kwenye masomo wanayosimamia pamoja na kuwa na wanafunzi wanaojitambua ambapo pale wanapofika wanapewa malengo ya shule kuwa hautakiwi kufeli unapokua kwenye shule hii"alisema Kifwete.

Aidha alisema kwa miaka minne mfululizo shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kujifunza na hivyo kupelekea kuelewa kila wanachofundishwa.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Mwalimu Msaidizi wa Taaluma Moses Mhina ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Sayansi anafundishi masomo ya Kemia na Biologi alisema matokeo ya kidato cha sita wanakuwa wakifanikiwa kutokana na uwepo wa nidhamu ya hali ya juu ambalo kwao ndio jambo la kwanza kabla ya taaluma.

Alisema wanafunzi wanapofika shuleni jambo la kwanza ni nidhamu,la pili ni ushirikiana kati ya walimu na wafanyakazi wengine,kujitoa ni jambo ambalo ni kubwa sana kwao na wakati mwengine kufanya kazi nje ya muda wa kazi na kuwafundisha wanafunzi kwa waledi ambao unawatengenezea ujasiri.

“Lakini pia ushirikiano walimu na watu wa nje ambao sio walimu hasa wazazi na walezi kwa sababu kunaweza kutokea changamoto ya utoro lakini tunapokutana na wazazi na kuwaeleza utoro unavyokwamisha matokeo mazuri na hivyo wao kutupa ushirikiano “Alisema

Alisema siri nyengine ambayo imewasaidia wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kufanya vizuri ni kuwatengenezea mtazamo chanja unajua kwenye malezi wanayolelewa mtu tangia akiwa mdogo anasikia habari kwa kaka zake kwamba sayansi ni ngumu lakini wao wanafunzi wanapofika shuleni wanawaelezwaa namna wanavyuoweza kufanya masomo hayo bila woga na hivyo kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo .

Mwalimu huyo alieleza kwamba hatua inayoondolea woga kwao na hivyo kuwajengea namna ya kujiamini na kumtengeneza ujasiri wa kujibu maswali na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri wanapokuwa kwenye mitihani yao.

“Lakini pia tumekuwa tukifanya ziara ya kutembelea kwenye viwanda na hivyo kuona namna sayansi inayoweza kufanya kazi na hivyo kuwawezesha wanafunzi kupata uelewa mpana “Alisema

Hata hivyo pia siri nyengine ni wao kujitahidi kufundisha kwa waledi na kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi yanayowapa ujasiri wa kutambua mambo mengi na hivyo kuwawezesha kutimiza ndoto zao za kufanya vizuri.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 16,2021

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger