Thursday, 15 July 2021

Masauni Aiagiza Benki Kuu Ya Tanzania Bot Kufanya Tafiti Za Kukuza Uchumi Wa Zanzibar


Na Benny Mwaipaja, Zanzibar
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kukuza uchumi wa Zanzibar kupitia sekta za uchumi wa blue pamoja na utalii.

Mheshimiwa Masauni ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kikazi kwenye Tawi la Benki Kuu ya Tanzania lililoko kisiwani Unguja-Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Alisema kuwa Zanzibar inategemea uchumi wa blue ikiwemo masuala ya uvuvi pamoja na sekta ya utalii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake hivyo utafiti katika Nyanja hizo utasaidia kubaini njia bora za kuharakisha ukuaji wa uchumi wake kupitia Sekta hizo muhimu.

"Mazingira ya Uchumi wa Zanzibar ni tofauti na mazingira ya uchumi wa Bara, kuna maeneo ambayo katika uchumi wa Zanzibar yamepewa kipaumbele likiwemo suala la uchumi wa blue,  na utalii,  hivyo kuna kila sababu Benki Kuu ya Tanzania kufanya tafiti katika maeneo hayo ili kuishauri vema Serikali", alieleza Mhandisi Masauni.

Kwa upande wake Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aneyesimamia uthabiti wa sekta ya fedha pamoja na kusimamia Tawi la Benki Kuu-Zanzibar Dkt. Bernard Kibesse amemhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa MHandisi Hamad Yussuf Masauni kwamba maelekezo aliyoyatoa yatatekelezwa.

Alisema kuwa Benki hiyo tayari imeanza mchakato wa kufanya tafiti mbalimbali zitakazo saidia kukukuza na kuimarisha uchumi wa Zanzibar pamoja na kutekeleza sera za fedha kwa manufaa ya nchi hiyo na Taifa kwa ujumla.

"Tumesikiliza maagizo yako hasa ya kufanya tafiti kuhusu hali ya uchumi wa Zanzibar kwa kujikita zaidi katika uchumi wa Blue na utalii maeneo ambayo ndiyo  nguzo kuu za uchumi wa Zanzibar", alieleza Dkt. Kibesse.

Naye Mkurugenzi wa BoT Tawi la Zanzibar Dkt. Camillius Kombe alieleza kuwa Sera imara za fedga zimeiwezesha Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuwa na uchumi imara pamoja utulivu wa mfumuko wa Bei ambao hivi sasa hauzidi asilimia moja.

Alisema kuwa kumekuwepo na utulivu wa bei visiwani Zanzibar kwa muda mrefu, ambao unatokana na Sera za Fedha kuwa na ufanisi kwa upande wa Zanzibar na imetokana na BoT Zanzibar kutoa hali halisi na mikakati ya kukuza uchumi na kuipeleka kwa watoa maamuzi.


Share:

Tanzania yapokea ujumbe wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Umoja wa  Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Shakhboot Bin Nahyan Al Nahyan Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Al Nahyan amemshukuru Rais Samia kwa kuendeleza ushirikiano na Nchi za Falme za Kiarabu na kumkabidhi barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Mfalme wa U.A.E  Sheikh Mohamed Bin Zayed Al Nahyan ambapo pia mfalme huyo ametoa salamu za pole kwa Rais Samia kufuatia kifo cha Hayati Rais Magufuli na kumpongeza kwa kushika nafasi ya uongozi wa nchi.

Amesema U.A.E itaendeleza ushirikiano na uhusiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuunga mkono usawa wa kijinsia na haki za wanawake hasa wakizingatia kuwa Rais Samia ni mfano bora kwa wanawake nchini Tanzania na dunia kwa ujumla.

Aidha, Sheikh Nahyan amesema U.A.E inaunga mkono jitihada za Rais Samia za kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo amesema Umoja wa Falme za Kiarabu upo tayari kuipatia Tanzania chanjo ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Rais Samia ameshukuru Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) kwa kuendeleza ushirikiano na Tanzania na kumuahidi Mjumbe huyo Maalum kuwa Serikali itaendeleza mahusiano mazuri kwa ajili ya  manufaa ya nchi hizi mbili.

Rais Samia amesema U.A.E ni mbia muhimu katika maendeleo ya Tanzania kwasababu wamesaidia kuboresha miundombinu hususan ya barabara  na biashara.

Aidha, Rais Samia  amesema kumekuwa na ongezeko la usawa wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili mwaka hadi mwaka na kuongeza kuwa Tanzania inaendelea kufanya maboresho ya kibiashara ili kuvutia zaidi wawekezaji.

Pia Rais ameshukuru kupokea mualiko wa kuhudhuria maonesho ya biashara ya kimataifa ya Dubai (Dubai Expo) yanayotarajiwa kufanyika mwezi Machi, 2022.
 


Share:

ANAYEDAIWA KUUA WATOTO 10 KWA KUWAFYONZA DAMU AKAMATWA...MWENYEWE ASEMA ALIANZA KITAMBO TU


Masten Wanjala, Mtuhumiwa wa mauaji ya watoto nchini Kenya

Polisi nchini Kenya wanamshikilia Masten Wanjala (20) anayedaiwa kuua watoto kwa nyakati tofauti aliokuwa akiwakuta wakicheza na kuwahadaa kisha kuwaua kwa kuwanyonga ama kuwafyonza damu na kisha miili yao kuitupa na kwamba alianza kutekekeleza unyama huo akiwa na umri wa miaka 16.

Taarifa hiyo imechapishwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya, na kueleza kuwa kijana huyo amewaua watoto takribani 10 kufuatia mwendelezo wa matukio ya utekaji nyara na mauaji ya watoto nchini humo.

Mara baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo aliwaelekeza maafisa upelelezi maeneo baadhi alikoitupa miili ya watoto aliowaua, ambapo amekiri kwamba amekuwa akitumia kemikali inayofanana na unga kwa wathiriwa kwa kuwalazimisha wainywe ama kuwapulizia usoni kabla ya kuwaua kwa kuwanyonga au kuwafyonza damu kupitia mishipa.

Taarifa zimeongeza kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akiwaua watoto wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 13, huku akihusishwa pia na matukio ya aina hiyo yaliyowahi kufanyika siku za nyuma
Share:

WAZIRI MKUU MAJALIWA AISHUKURU BENKI YA AFRIKA

 


Waziri Mkuu Kaasim Majaliwa ameishukuru Benki ya Afrika (BOA) kwa jitihada zake za kuendelea kuisaidia Tanzania katika Sekta mbalimbali za maendeleo.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano Julai 14, 2021) wakati alipozungumza na Rais wa benki hiyo Othman Benjelloun kwenye hoteli ya Sofitel, Rabat Nchini Morocco.

Amesema kuwa uwepo wa Benki hiyo nchini Tanzania umewawezesha wananchi kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo, "kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tunaishukuru Benki ya Afrika kwa jitihada hizi".

Aidha, Waziri Mkuu alimshauri Rais Benjelloun kuendelea kupanua wigo wa huduma za benki hiyo nchini ili kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa katika sekta  za Elimu, Kilimo, Mifugo na Madini.

Waziri Mkuu aliahidi kuwa ataandaa utaratibu wa kuukutanisha uongozi wa Benki hiyo na sekta binafsi nchini Tanzania ili kuona namna watakavyoweza kushirikiana  katika kuwahudumia Watanzania.

Kwa upande wake, Rais Benjelloun amesema lengo la benki hiyo ni kuendelea kukuza uwekezaji wake  nchini Tanzania. "Sisi tupo tayari kuwekeza katika maeneo mbayo viongozi wa taifa la Tanzania watatushauri lengo likiwa ni kutoa mchango wetu katika kujenga uchumi".

Naye, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alisema kuwa benki hiyo isaidie kukuza mahusiano ya Tanzania na Morocco katika sekta ya kilimo hasa kwenye mazao kama vile  Mchele, Tumbaku, kahawa na mazao mengine.

 Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Leila Muhamed Mussa amesema yapo maeneo ya fukwe ambayo hayajawekezwa mpaka sasa hivyo ni fursa kwa wawekezaji kuyatumia na kwamba  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefungua milango kwa wawekezaji.

Pia aliiomba benki hiyo kuona namna ya kuwawezesha wakulima wa viungo ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

SADC Yatoa Dola Milion 6 Ujenzi Wa Reli Ya Kimataifa Ya Mtwara-Mbambabay


 Na. Beatrice Sanga-Maelezo
Jumuiya ya kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wametoa Dola za Kimarekani milioni 6 kwa ajili ya kufanyika upembuzi  yakinifu wa ujenzi  wa reli ya kimataifa ya Mtwara mpaka Mbambabay ambayo inategemewa kufungua fursa nyingi kwa wananchi wa Mtwara na kanda ya Kusini

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha mkutano wa SADC ambao unahusisha mawaziri wa fedha na uwekezaji wa nchi wanachama wa jumuiya ya SADC uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akieleza mambo ambayo yanaendelea kujadiliwa na mafanikio ambayo yamefikiwa kutokana na kikao hicho Waziri jamal Kassim ali amesema kikao hicho kimepata fursa ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sera ya kifedha , za kikodi pamoja na uwekezaji na biashara katika Kanda ya Jumuiya ya SADC ambapo pamoja na hayo fedha zilizotolewa na SADC zinaenda kusaidia upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli hiyo ya Mtwara-Mbambabay ambayo itaenda kufungua uchumi wa Mtwara na kanda nzima ya kusini

“jambo kubwa ambalo ningependa mjue ni kwamba katika mwendelezo wa vikao hivi wenzetu wa SADC wameweza kutupatia takribani Dola milioni 6 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya Mtwara mpaka Mbambabay ambayo itajengwa ili kurahisisha na kuifungua Mtwara na kanda hii ya kusini kiuchumi na mpaka sasa tayari SADC wametupatia pesa hizo” amesema Mh. Jamal Kassim Ali

Mh. Jamal Kassim Ali, ameongeza kuwa  katika vikao vilivyopita mambo mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo wa nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC wenye lengo la kuchochea maendeleo katika nchi wanachama  na kuzitaka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya SADC  kushikana mikono kuhakikisha kwamba mfuko huu muhimu unaanzishwa

“ sisi kama Tanzania kama ambavyo tumekuwa vinara katika kuhakikisha masuala ya ukombozi wa SADC  kisiasa, sasa tunakwenda na ajenda hii tuwe vinara katika ukombozi wa kisiasa lakini pia ukombozi wa kiuchumi. Tunaomba nchi zote wanachama wa Jumuiya ya SADC kwa umuhimu ambao mfuko huu utakuwa katika uchumi wa nchi zetu kuna haja kama nchi zote wanachama wa jumuiya ya SADC tushikane kuhakikisha kwamba chombo hiki muhimu tunakianzisha” amesema Mhe. Jamal Kassim Ali

Aidha ameongeza kuwa kutokana na changamoto ya ugonjwa wa uviko 19 (COVID  19) uchumi wa nchi nyingi ikiwemo Tanzania umeathirika hivyo kupitia vikao hivyo hoja mbalimbali zitafikishwa kupitia jukwaa hilo la SADC kama chombo cha kikanda kuweza kueleza namna gani tunaweza tukasimama pamoja kupeleka sauti zetu na kusema zile changamoto zetu ambazo ni kodi na masharti yaliyotokana na makubaliano yaliyokuwepo.

“ kwa bahati nzuri wenzetu waAfrika Kusini wao ni wanachama katika jumuiya ya G20 ambayo inahusisha nchi nyingi ambazo zinatusaidia kwahiyo kupitia wao tunataka kupeleka ujumbe wetu kwamba katika maeneo muhimu tunaona ipo haja yale mambo au masharti ambayo yamewekwa yatizamwe upya ikiwemo swala la utozaji wa kodi na kuongezeka kwa riba na masharti mengineyo yanayohusu uratibu wa malipo , kwa hiyo kupitisa jukwaa hili la SADC  tutapeleka hii hoja kupitia wenzetu Afrika Kusini ambao ndo nchi pekee kutoka SADC wanaoingia wakapaze sauti hii” amesema Mhe. Jamal Kassim Ali


Share:

Sheikh Sharifu Baruwan: Anatatua Matatizo Ya Watu Kwa Kutumia Maombi na Dawa

SHEIKH SHARIFU BARUWAN. Nisheikh anaewaombea watu maombi kulingana namatatizo yao mbalimbali,Lakini pia anatibia maradhi tofauti kwakutoa dawa mbalimbali zamiti shamba.

Vilevile anazipandisha nyota kwakupitia Pete au Fimbo,Na anazikinga biashara zenye kuzongwa nawizi wa chuma ulete. Na anafungua vifungo kwa aliefungwa aidha asiolewe,,asizae,asipendwe,,NK.

Bila yakusahau shekh sharifu baruwan anao uwezo wakumvuta Mume/mke/mpenzi/mchumba/Aliekukimbia kwa masaa machache,Naanakinga mwili,majumba,viwanja,mashamba,,magari,NK.

Sasa uamuzi niwakwako wakumtafuta shekh sharifu baruwan,Ili aweze kukusaidia kwa shida zako zote.Acha kuteseka pia acha kukata tamaa.Mtafute kwa No:0767 776859 Kwa WhatsApp:0659 551221. SHEIKH SHARIFU BARUWAN,

Anamtibia yoyote Alie karibu na hata Alie mbali Ambae awezi kufika ofisini kwake. SHEIKH SHARIFU BARUWAN Anatoa angalizo; kwamba:Kua makini kwayule uliemchagua akusaidie kwamatatizo yako,Kwani walio wengi siwakweli Nawala hawana khofu yamungu kabisa.

SHEKH SHARIFU BARUWAN Anawakaribisha nyote,Anasema Achagui dini Wala kabila, Pia Achagui mwenye hela naasiekua nahela.Anawaombea nyote ktk Mambo yenu mtanguliwe na M/mungu. Whatsapp 0659 551221 Au 0767 776859.



Share:

MAONESHO YA PILI YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA KUFANYIKA JULAI 23 HADI AGOSTI 1,2021

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akifungua kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkoa wa Shinyanga umeandaa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika uwanja wa kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Julai 15,2021, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary amesema maonesho hayo yanalenga kufungua fursa mbalimbali za biashara na kukuza uwekezaji.

"Tunawakaribisha wafanyabiashara, wajasiriamali na wadau mbalimbali kushiriki katika Maonesho haya ambayo yatasaidia kutangaza mkoa wa Shinyanga na kukuza uwekezaji. Shinyanga tuna fursa nyingi za kiuchumi, tunatamani siku moja Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Kitaifa yafanyike mkoani Shinyanga",amesema Omary.

Akitoa taarifa ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga, Katibu wa Kamati ya Maonesho,  Mhandisi Joseph Kumburu  ambaye ni Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga amesema malengo makuu ni kukuza biashara, viwanda na madini ili kujenga uchumi jumuishi na fungamishi.

“Maonesho haya yanafanyika kwa ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Sekta ya Umma inaongozwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Sekta inaongozwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga”,amesema Mhandisi Kumburu.

Ameyataja baadhi ya malengo ya maonesho hayo kuwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi na taasisi mbalimbali kukutana na wanunuzi kwa lengo la kutangaza bidhaa na huduma wanazotoa, kujifunza masuala ya biashara na teknolojia ya madini kulingana na soko la kimataifa na mifumo ya usambazaji madini katika masoko mbalimbali.

“Malengo mengine ni kutengeneza mitandao ya mawasiliano ya kibiashara na teknolojia ya madini miongoni mwao ili iwasaidie kukuza biashara,kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Shinyanga na kukutanisha wadau wa viwanda, biashara na madini ili kubadilishana uzoefu ili kukuza shughuli zao”,ameongeza Mhandisi Kumburu.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amewahamasisha wafanyabiashara na wajasiriamali kushiriki katika maonesho hayo huku akiwataka kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona kwa kuhakikisha wanavaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kutumia vitakasa mikono 'Sanitizer'.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila na Mwenyekiti wa TCCIA, Dkt. Kulwa Meshack wamesema mafanikio ya Maonesho hayo yatatokana na ushiriki wa wadau hivyo kuwataka wadau wote kushiriki kikamilifu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akifungua kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akifungua kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akifungua kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Kamati ya Maonesho  Mhandisi Joseph Kumburu  ambaye ni Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga akitoa taarifa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika uwanja wa kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa Kamati ya Maonesho  Mhandisi Joseph Kumburu  ambaye ni Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga akitoa taarifa ya Maonesho kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa TCCIA, Dkt. Kulwa Meshack akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa TCCIA, Dkt. Kulwa Meshack akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyangayanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa TCCA Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Kulwa Meshack (kushoto) akiteta jambo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila (kulia) kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akiongoza kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

ULEGA ATAKA SEKTA YA MIFUGO KUJIENDESHA KIBIASHARA

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) aliyechuchumaa akimpa maelezo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete juu ya sifa za malisho ya mifugo yajulikanayo kama JUNCAO kutokea nchini China ambayo yamepandwa katika shamba la malisho ya mifugo lililopo Vikuge katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, ambapo Mhe. Ulega ametaka mbegu za malisho hayo zisambazwa kote nchini hususan vijijini. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (mwenye koti jeusi), akiangalia birika la kunyweshea mifugo maji wakati alipotembelea lambo kwa ajili ya matumizi ya mifugo na binadamu la Chamakweza lililopo Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani na kukabidhi rasmi lambo hilo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze kwa ajili ya matumizi ya wafugaji. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

 

Meneja wa shamba la malisho ya mifugo lililopo Vikuge katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, Bw. Reuben Ngailo (mwenye fulana nyekundu), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka wizarani Prof. Hezron Nonga juu ya aina mbalimbali za mbegu za malisho wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili ya Naibu Waziri Ulega Mkoani Pwani. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Muonekano wa sehemu ya lambo kwa ajili ya matumizi ya mifugo na binadamu ambalo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amelikabidhi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze baada ya kukarabatiwa na serikali kwa zaidi ya Shilingi Milioni 600 na kuagiza kuundwa kwa kamati ya kusimamia lambo hilo. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameagiza shamba la malisho ya mifugo lililopo Vikuge Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, kujiendesha kibiashara na kusambaza mbegu za malisho kutoka nchini China ijulikanayo kama JUNCAO maeneo mbalimbali nchini kwa kuwa ina sifa ya kustahimili sehemu yenye ukame ili wafugaji wapande malisho hayo.

Wakati akihitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo Naibu Waziri Ulega, amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya shamba hilo na kumuagiza Katibu Mkuu anayeshugulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel kuhakikisha aina mpya ya malisho hayo inasambazwa na kusimamia vyema ili mradi huo uweze kuwa na tija kwa taifa hususan kwa wafugaji vijijini.

Mhe. Ulega amesema mbegu za malisho ya JUNCAO zisambazwe kuanzia ngazi ya mikoa wilaya hadi vijiji lengo likiwa kudhibiti mifugo na wafugaji kuhamahama kutafuta malisho.

Amefafanua kuwa hataki kuona mambo yanayoanzishwa kwa ajili ya kunufaisha wananchi yanaishia njiani kwani ni vizuri kukawa na mwendelezo wa teknolojia hiyo ya kilimo hicho kipya cha malisho ya mifugo hata kusambazwa kwa wafugaji hadi vijijini.

Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha mbegu za malisho hayo zinaenea hadi vijijini kwa wafugaji akitaja hususan mikoa yenye ukame kama Dodoma, Singida, Manyara, Shinyanga na iwapo zitasambazwa vizuri  itapunguza tatizo la wafugaji na mifugo yao kuhama hama kutafuta malisho ya mifugo yao.

"Kinachosababisha wafugaji kuzunguka na kuhama hama ni kutafuta chakula cha malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao hivyo kama wafugaji watafikishiwa mahali walipo itawasaidia wafugaji kuwa na uhakika wa malisho." amesema Mhe. Ulega.

“Mbegu hizi nataka zifike kwa haraka na kwa gharama nafuu ambayo kila mfugaji ataweza kununua aweze kuhudumia mifugo yake.” amesema Mhe. Ulega

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo katika uendeshaji wa shamba la Vikuge Meneja wa shamba hilo Bw. Reuben Ngailo  amesema kukosekana kwa vifaa na nguvu kazi katika mipango yao ya kusafisha shamba na kupanua uzalishaji.

Amesema pia eneo hilo la shamba lina visiki vingi ili kuving'oa inagharimu kiasi kikubwa cha fedha jambo ambalo husababisha kuendesha uzalishaji wa malisho katika eneo dogo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameomba malisho yanayozalishwa shambani hapo kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Pwani.

Mhe. Kikwete amesema shamba hilo lipo Mkoa wa Pwani na mkoa huo una migogoro mingi ya wakulima na wafugaji kwa ajili ya kutafuta malisho na maji, hivyo ombi lake ni mbegu hizo zisambazwe haraka kwa wafugaji wa mkoa huo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amekabidhi lambo la kunyweshea mifugo maji la Chamakweza lililopo Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani na kuiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze kuunda kamati kwa ajili ya kusimamia lambo hilo lililokarabatiwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni 600 kwa ajili ya matumizi ya mifugo na binadamu.


Mhe. Ulega amesema ni wakati sasa wafugaji kutumia vyema lambo hilo kwa ajili ya kuboresha mifugo yao ambayo imekuwa ikikosa maji ya kunywa na kuwataka kubadilika na kuanza kufuga kibiashara kwa kuwa na mifugo ambayo wanakuwa wanavuna kila baada ya muda kwa kuuza kwenye viwanda vya kuchakata nyama badala ya kuwa na mazoea ya kuwa na mifugo mingi ambayo haina tija kwao.


Amefafanua kuwa lengo la serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuona mfugaji ananufaika kupitia mifugo yake kwa kufanya biashara na hatimaye kuongeza pato la taifa na mfugaji mwenyewe. 

Naibu Waziri Ulega tayari amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Pwani.

Share:

VIDEO: Nandy – Nimekuzoea

 VIDEO: Nandy – Nimekuzoea



Share:

Waziri Ummy : TARURA Msikae Maofisini


Na. Angela Msimbira KATAVI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mkao Makuu kuacha kukaa 0fisini waende kwenye maeneo ya vijijini ili kuona changamoto na ubora wa barabara.

Ametoa agizo hilo leo alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ya Katuna, Halmashauri ya Wilaya Tanganyika Mkoani Katavi kwa lengo la kujua changamoto zinazozikabili Halmashauri zilizopo pembezoni.

Waziri Ummy alifafanua kuwa TARURA makao makuu wanatakiwa kutoka ofisini watembelee vijijini kujua maeneo ambayo yanachangamoto ya miundombinu ili kuweza kutoa vipaombele zaidi wakati wa kupanga bajeti za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara nchini.

“Haiwezekani TARURA mkakaa ofisini wakati matatizo mengi yanapatikana kwa wananchi hasa wale wanaokaa pembezoni, nawaagiza kuanzia sasa waache kukaa ofisini watoke na kwenda ‘site’ kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi hasa katika maeneo ya vijijini,” alisisitiza Waziri Ummy

Alisema kwa sasa Serikali imejiwekea mkakati wa kuhakikisha inatatua changamoto za miundombinu ya barabara vijijini.
Alielieleza kuwa haiwezekani kukaa ofisini na kugawa fedha bila kujua changamoto za maeneo husika kwa sababu haki itakuwa haitendeki kwa baadhi ya Mikoa ambayo mtandao wao wa barabara ni mkubwa.

“Tumegundua kuwa kuna baadhi ya Halmashauri atuzitendei haki kwa kuwa mtandao wa barabara za TARURA haufiki hata kilometa 200 lakini kuna maeneo ambapo mtandao wao wa barabara ni zaidi ya kilometa 1900. Sasa unaposema Halmashauri zote zipate sawa hii si haki. Tunaenda kuzifumua bajeti za maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa barabara ili kuziwezesha Halmashauri ambazo zinachangamoto kubwa” alisisitiza Waziri Ummy

Naye Mbunge wa Mpanda Vijijini Mhe Selemani Kakoso ameiomba Serikali kusaidia kujenga barabara ya kutoka Sibwesa – Kaduma yenye urefu wa kilometa 25 ambayo ipo katika mtandao wa TARURA.


Share:

NHC Yatakiwa Kubuni Miradi Mipya Morogoro


Na Munir Shemweta, MOROGORO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Tifa (NHC) mkoa wa Morogoro kubuni miradi mipya ya ujenzi wa katika mkoa huo ili kuliwezesha shirika kuingiza fedha badala ya kutegemea nyumba za zamani.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana mkoani Morogoro wakati akizingumza na watumishi wa ofisi ya shirika hilo mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara yake ya kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za ardhi katika mkoa huo.

Alisema haileti maana NHC kutegemea nyumba zake zilizojengwa na mkoloni bila ya kuwa na mipango mipya ya ujenzi itakayowezesha shirika hilo kuwa na nyumba nyingine za kisasa zitakazoliwezesha shirika kujiongezea kipato.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mkoa wa Morogoro bado una uhitaji mkubwa wa nyumba zikiwemo zile za kupangisha hasa kwenye maeneo mapya na kusisitiza kuwa NHC haina budi kuongeza kasi kwa kubuni miradi mipya itakayosaidia shirika kuongeza kipato.

‘’Kumbe ninyi bado mkoa kizamani yaani hamna mradi wa ujenzi wa nyumba mpya na mnategemea zile za zamani? Mnatakiwa kujiongeza kwa kubuni miradi mipya ili muweze kuongeza mapato ya shirika’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula alimtaka Meneja wa NHC Morogoro Constantine Yuda kwenda katika halmashauri za mkoa huo ili kupatiwa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miradi mipya ikiwemo ya nyumba za watumishi kwenye halmashauri za mkoa huo.


Share:

Business Development Manager Singida Branch at NBC Bank

Business Development Manager Singida Branch     NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Summary The main purpose is to drive Loan and Advances, Deposit and alternative product growth at branch. This […]

This post Business Development Manager Singida Branch at NBC Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Personal Assistant at NBC Bank

Personal Assistant    NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Summary To deliver secretarial, general office and administrative support services to manager(s) and or team(s) through the execution of predefined objectives […]

This post Personal Assistant at NBC Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

AMKIMBIA MMEWE BAADA YA KUMFUMANIA NA CHUPI YA MCHEPUKO


Mwanamke mmoja kutoka Nguuni, eneo la Mwingi nchini Kenya  ameamua kumuacha mumewe baada ya kupata chupi ya mwanamke mwingine kwenye mfuko wa koti lake akifua nguo.

 Inasemekana kuwa jamaa alikuwa amerejea nyumbani siku iliyofuata mapema asubuhi akiwa mlevi chakari.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, mrembo alimlaki mumewe na kumkaribisha nyumbani akamvua nguo chafu kisha akamtandikia kitanda alale ili stimu za pombe zimtoke mwilini.

 Inasemekana kwamba mzee alipokuwa akisukuma usingizi mkewe alianza kufua nguo na hapo ndiposa alipata chupi kutoka kwenye mfuko wa koti la mumewe.

Mama alipandwa na mori kutokana na kila alichokiona ambapo alifululiza hadi chumba alichokuwa amelala mumewe na kumwamsha kwa fujo.

“Wewe ulikesha kwa nani na chupi hii ni ya nani? Amka haraka wacha kujifanya hujui ninachokuuliza,” dada huyo alimcheka.

Jamaa aliropokwa kilevi bila kujua njama yake ya kuchepuka na wanawake wengine ilikuwa imefichuka baada ya chupi ya mpango wake wa kando kumsaliti ilipopatikana kwenye koti lake.

Hata hivyo, jamaa alikana chupi ilikuwa ya mpango wake wa kando. “Chupi gani hiyo? Chupi hiyo ni yako si ya mtu mwingine. Wacha kunilaumu bure,” jamaa alisema na kuendelea kulala.

Mwanamke huyo alimgutusha jamaa kwa kumzaba kofi usoni.

 “Amka haraka. Mimi sina chupi ya rangi hii. Wacha kujifanya eti hujui mwenyewe. Tabia yako imenifika kooni na sasa ninaondoka nikuachie mwenye chupi hiyo,” kisura alisema. 

Penyenye zinasema kwamba kipusa huyo alichukua kilichokuwa chake na kuondoka.

Inaarifiwa kwamba kimada wa jamaa aliweka chupi hiyo kwenye mfuko wa koti la jamaa kwa kusudi la kumkosanisha na mkewe.

Chanzo - Tuko News
Share:

Mpyaa : PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOGTUWE TUNAKUTUMIA HABARI BURE MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Share:

Business Development Manager Musoma Branch at NBC Bank

Business Development Manager Musoma Branch NBC   NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Summary The main purpose is to drive Loan and Advances, Deposit and alternative product growth at branch. This […]

This post Business Development Manager Musoma Branch at NBC Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Head of Debt at Absa Bank

Head of Debt     Bring your possibility to life! Define your career with us With over 100 years of rich history and strongly positioned as a local bank with regional and international expertise, a career with our family offers the opportunity to be part of this exciting growth journey, to reset our future and shape […]

This post Head of Debt at Absa Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger