Tuesday, 13 July 2021

Wanachama Wa NHIF Tumieni Kadi Zenu Kwa Matumizi Halali Ya Matibabu - Dkt. Godwin Mollel


Na WAMJW - Moshi, Kilimanjaro.
Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wametakiwa kuhakikisha wanatumia kadi za uanachama wao katika kufanya malipo halali ya huduma wanazopata katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel alipokuwa ziara katika Mkoa wa Kilimanjaro na kupokea ripoti ya ubadhirifu wa NHIF unaofanywa na wanachama pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.

"Kila Mtanzania ahakikishe kadi yake ya bima ya afya inatumika kufanya malipo halali tuu, kila mwenye duka la dawa ahakikishe anaposaini fomu za bima ya afya na anapopokea na kudai madai, adai malipo halali tuu" amesema Dkt. Mollel

Dkt. Mollel amezitaka taasisi za umma na binafsi zinazotoa huduma za afya nchini kuhakikisha kadi za bima ya afya zinatumika kwenye malipo halali huku wakiwasimamia vyema watumishi hao wasijiingize katika vitendo vya wizi kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Amesema kuwa wanachama pamoja na watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo vya wizi kwa mfuko watatakiwa kurejesha fedha zote walizosababishia hasara NHIF pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria chini ya vyombo vya dola.

Dkt. Mollel amesema kuwa tusipokuwa matumizi mazuri na kuwa na uadilifu ndani ya mfuko wa bima ya afya huku ubadhirifu ukiendelea, adhma ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ya kuwa na mfuko imara wa bima ya afya kwa wote hapa nchibi hatutoifikia.

"Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 148 kwa ajili ya mfuko wa bima ya afya kwenda kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo kuwa na uhakika wa bima, sisi tunaosimamia mifumo, tusiposimamia kuondoa uchafu na ubadhirifu wote mfuko huu utakufa" amefafanua Dkt. Godwin Mollel.

Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa wataenda kuchunguza pia watumishi wa afya katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF na endapo watabainika kujihusisha na vitendo hivyo vya ubadhirifu hatua kali za kisheria zitatumika dhidi yao.

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kigaigai amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na NHIF pamoja na vyombo vya usalama umebaini ubadhirifu wa shilingi milioni 520 uliosababishwa na vituo 12 vya kutolea huduma za afya, watumishi wa aya kutoka hospitali 38 na wanachama 6 wa mfuko huo.

"Ubadhirifu huu haukubaliki, natoa maelekezo kwa vyombo vya usalama wachukue hatua za haraka sana kuhakikisha kwamba fedha hizo zinarejeshwa na kuchukuliwa hatua za kisheria" amesema Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai.


Share:

Serikali Yakiri Kutambua Umuhimu Wa Sekta Ya Usafirishaji Nchini


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene amesema serikali inatambua umuhimu wa sekta ya usafirishaji nchini na kwamba pamoja na umuhimu huo pia serikali imeahidi kufanyia kazi changamoto zilizopo ikiwemo muingiliano wa kimamlaka kati ya Jeshi la Polisi na LATRA.

Waziri Simbachawene amesema hayo jana wakati akizungumza na wadau wa sekta ya usafirishaji nchini kwenye kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es salaam na kuhusisha wadau mbalimbali katika sekta hiyo kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi hilo limeanza kushughulikia maombi kadhaa yaliyowasilishwa na wadau wa sekta ya usafirishaji ambapo kati ya maombi hayo ni pamoja na mabasi kuruhusiwa kutoka saa kumi na moja alfajiri sambamba na kuwepo kwa kituo cha maalum cha  ukaguzi katika stendi kuu ya mabasi iliyopo Mbezi jijini Dare s salaam.

Kwa upande wake mdau wa sekta ya usafirishaji amesema Jeshi la Polisi linajitahidi katika kutatua changamoto za usalama barabarani lakini ameelekeza kuwepo kwa changamoto kwa LATRA kwa kutotoa ushirikiano kwa wadau hao wa usafirishaji na hivyo kukwamisha baadhi ya mambo muhimu.


Share:

Serikali Yakutana Na Taasisi,mashirika Na Mabalozi Kujadili Mapato Na Matumizi Ya Bajeti


 Na Mwandishi wetu
Katika kukuza Diplomasia ya Uchumi, kuimarisha na kushirikisha Jumuiya za Kimataifa Serikali imekutana na Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mbinu za pamoja za kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19.

Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wizara za Kisekta zikiwemo Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Afya, Maliasili na Utalii, Uwekezaji na Wizara ya Fedha na Mipango – Zanzibar pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa 54 kutoka nchi na taasisi mbalimbali.

Lengo la Mkutano huo pamoja na mambo mengine, ni kuwapitisha Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kwenye Bajeti ya Serikali ya 2021/22, Mipango ya Utekelezaji wake na Maeneo ya Ushirikiano.

Akiongoza Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametaja sababu za Serikali kukutana na Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa ambao pia ni wadau wa maendeleo ili kuwajengea uelewa katika mipango na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya 2021/22 pamoja na maeneo ya Ushirikiano.

“……………………tumeona tuweke utaratibu wa kukutana na wadau hawa wa maendeleo ili kujenga uelewa wa pamoja katika maeneo muhimu yaliyoainishwa katika bajeti ya Serikali ili waweze kupata picha halisi ya mipango na mikakati ya Serikali katika utekelezaji wa Bajeti,” amesema Balozi Mulamula

Kwa Upande wake Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti amesema uamuzi wa Serikali wa kukutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa umekuwa mzuri sana umesaidia kufahamu mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali katika utekelezaji wa bajeti yake ya 2021/22.

“Kupitia mkutano wa leo tumeweza kupata picha halisi ya ushirikiano wetu na Tanzania na umezidi kuimarika lakini pia tumeweza kuona na kujadili baadhi ya vipaumbele vya bajeti ya Serikali ya Tanzania, mipango ya maendeleo jambo ambalo sisi kama wadau wa maendeleo limetuhamasisha kuendelea kushirikiana kwa ukaribu n a uwazi zaidi,” amesema Balozi Fanti   

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigula Nchema (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango kutoka Serikalini ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, Pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji Mhe. William Tate Olenasha (Mb).  

Pamoja na Mambo mengine, Mawaziri hao wamepata fursa ya kutoa ufafanuzi katika maeneo yanayohusu wizara zao ikiwa ni pamoja na mipango ya Serikali katika kukuza uchumi, kukusanya mapato, kukuza Viwanda, kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji, kukuza utalii na jinsi Serikali inavyojipanga kuboresha sekta ya afya nchini hasa katika kupambana na janga la UVIKO 19.


Share:

Naibu Waziri Dkt Mabula Awashukia Wenyeviti Wanaouza Ardhi Kilosa


Na Munir Shemweta, WANMM KILOSA                                       

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewajia juu na kutoa onyo kwa wenyeviti wa vijiji wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro wanaojihusisha na kuuza ardhi ya vijiji bila kufuata taratibu.

Dkt Mabula alitoa onyo hilo tarehe Julai 12, 2021 alipozungumza na wananchi wa kata ya Dumila wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara yake ya kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za ardhi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara katika mkoa huo.

Akiwa mkoani Morogoro hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Dumila wilayani Kilosa kuhusiana na migogoro ya ardhi waliyoieleza kuwa imekuwa ikisababisha kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji mali.

Dkt Mabula alisema, migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikisababishwa na wenyeviti wa vijiji hasa katika suala zima la ugawaji ardhi na kusisitiza kuwa, jukumu la kugawa ardhi ya kijiji kwa mujibu wa sheria ni mkutano wa kijiji na siyo mwenyekiti.

 ‘’Naomba muelewe kuwa mwenyekiti wa kijiji haruhusiwi kugawa ardhi na yeyote atakayepewa ardhi na mwenyekiti wa kijiji basi ajue imekula kwake’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi alimuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro Frank Minzikuntwe kuwapitisha katika sheria ya ardhi ya usimamizi viijiji wenyeviti wa vijiji ili waweze kuielewa na kusimamia vizuri ardhi katika maeneo yao.

“Kasimamieni vizuri vijiji vyenu na mhakikishe ardhi katika maeneo yenu inapangwa, inapimwa na kumilikishwa maana upangaji ardhi katika maeneo yenu utapunguza migogoro ya ardhi ” Alisema Dkt Mabula.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shigela alimhakikishai Naibu Waziri Mabula kuwa atahakikisha sheria za usimamizi wa ardhi katika mkoa wake zinasimamiwa vizuri ili kuhakikisha migogoro ya ardhi katika mkoa huo inapungua au inakoma kabisa.

Awali Dkt Mabula alianza utekelezaji maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kikao cha ndani na viongozi wa wilaya ya Kilosa kwenye ofisi ya Kata ya Dumila wilayani Kilosa na kuhusisha wenyeviti wa vijiji, watendaji wa mitaa, madiwani pamoja na wananchi waliowasilisha malalamiko kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika kikao hicho, wenyeviti wa mitaa wakiongozwa na madiwani walimueleza Naibu Waziri kuwa, migogoro ya ardhi katika maeneo yao inahusisha mipaka kati ya vijiji, kubomolewa kwa baadhi ya nyumba za wananchi, kutopimwa baadhi ya vijiji, wananchi kuzuiwa kuendelea na shughuli za kiuchumi na wanaodaiwa wamiliki halali pamoja na mgogoro ya uvamizi wa maeneo.

Akieleza suala la migogoro ya mipaka, Dkt Mabula alisema, suala la kupima mipaka ni la halmashauri kwa kutenga fedha kwa ajili ya kazi hiyo na kuhakikisha vijiji vinapimwa na kupatiwa vyeti na alitaka utengaji fedha ufanyike kila mwaka.

“Sisi kama Wizara hatuna wajibu wa kupima mipaka ya vijiji, madiwani mtekekeze majukumu yenu kwa kusimamia upimaji vijiji na msipotekekeza kilosa haitakaa itulie na RAS aunde timu yake chini ya usimamizi wa mpima wa mkoa na kuweka kambi vinginevyo hatuwezi kufika” Dkt Mabula.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wtumishi watatu wa wizara hiyo walioshindwa kuripoti katika kituo chao kipya cha kazi kwenye halmashauri ya wilaya ya Kilosa.

‘’Kama mtakumbuka tulifanya maamuzi magumu kwenye mkoa wa Morogoro kwa kuhamisha asilimia 90 ya watumishi wa sekta ya ardhi na wapo watumishi watatu waliopangiwa kufanya kazi hapa Kilosa lakini mpaka sasa hawajaripoti, namuagiza kamishna wa Ardhi awasiliane na  Katibu Mkuu ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao’’ alisema Dkt Mabula.


Share:

Ngoma Mpya Kabisa!! NYANDA MADIRISHA OBHADO 'MALIGANYA - BHUJINGI 'UTONGOZAJI'


Msanii wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kutazama video yake Mpya inaitwa Bhujingi..... Bhujingi ni neno la Kisukuma lenye maana ya 'Utongozaji'. Tazama video hii hapa chini iliyotengenezwa na Director maarufu Manwell

Share:

LHRC YATOA POLE KWA WALIOATHIRIWA NA TUKIO LA SOKO LA KARIAKOO KUUNGUA MOTO



Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesikitishwa na tukio la moto lililotokea katika Soko Kuu la Kariakoo na kusababisha uharibifu wa vitu mbalimbali vyenye thamani. LHRC inawapa pole wote walioathirika na tukio hili kwa namna yoyote.

Share:

Head Of Risk and Compliance (Re- Advertised) at TADB

Background of TABD   Tanzania Agricultural Development Bank Limited (TADB) is a government institution operating under the Ministry of Finance and Planning. Established in 2012 TADB is registered under the Companies Act, 2002 and licensed under the provisions of the Banking and Financial Institutions Act No 5 of 2006 and the Banking and Financial Institutions […]

This post Head Of Risk and Compliance (Re- Advertised) at TADB has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Driver at TADB

Background of TABD   Tanzania Agricultural Development Bank Limited (TADB) is a government institution operating under the Ministry of Finance and Planning. Established in 2012 TADB is registered under the Companies Act, 2002 and licensed under the provisions of the Banking and Financial Institutions Act No 5 of 2006 and the Banking and Financial Institutions […]

This post Driver at TADB has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

NAIBU WAZIRI KASEKENYA ATOA SIKU 10 MIZANI YA NYAKAHURA, KAGERA KUKAMILIKA

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akiongea na wakazi wa kata ya Rulenge Wilayani Ngara, aliposimama kuzungumza nao wakati akikagua barabara ya Omubuga, Rulenge hadi Murugarama (KM 32), iliyotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro (mwenye suti ya bluu), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (kushoto), wakati akikagua barabara ya Omubuga, Rulenge hadi Murugarama (KM 32), iliyotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto kwa mbunge huyo ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara Col. Mathias Kahabi.

Ukarabati wa miundombinu ya mizani ya Nyakahura iliyoko wilaya ya Ngara mkoani Kagera, ukiendelea kwa kasi. Mizani hiyo inatumika kupima magari makubwa ya mizigo zaidi ya 400 kwa siku, yanayofanya safari zake kati ya Tanzania, Burundi na Rwanda.

Ujenzi wa daraja la kudumu la Kitengule lenye urefu wa meta 140 ukiendelea. Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutaziunganisha wilaya za Karagwe na Misenyi Mkoani Kagera

Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Kagera Mhandisi Ntuli Mwaikokesa, akimkumbusha jambo Mhandisi Mkazi Charles Romisha, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa daraja la Kitengule na barabara unganishi (KM18). Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati akikagua ujenzi wa daraja la Kitengule lenye urefu wa meta 140, na barabara unganishi (KM18), kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Col. Sakulo akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.

PICHA NA WUU

.......

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ametoa siku 10 kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Kagera, kuhakikisha anamsimamia mkandarasi anayejenga mizani ya Nyakahura mkoani humo, kumaliza ujenzi na kuanza kutolewa huduma za upimaji wa magari katika mizani hiyo kama zamani.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya barabara, mizani na madaraja mkoani humo, Naibu Waziri Kasekenya, amesema kuwa kusimama kwa huduma za upimaji wa magari katika mizani hiyo kunaisabibishia Serikali hasara kubwa, kwani kupitia fursa hiyo magari yanaweza kuzidisha uzito na kupelekea kuharibu barabara.

“Ujenzi wa mizani hii inabidi ukamilike mapema iwezekanavyo, nimeambiwa hapa kwa siku yanaweza kupita magari zaidi ya 500, hivyo magari kutokupima hapa inaweza ikawa sababu ya wasafirishaji kuzidisha uzito na kupelekea kuharibu barabara zetu ambapo Serikali inatumia kiasi kikubwa cha fedha ili kuzijenga”, amesema Kasekenya.

Aidha, amemuagiza Meneja huyo kufanya utaratibu wa kuandaa mchoro wa mizani nyingine ya pili, pembezoni mwa mizani ya kwanza ili kuepusha msongamano amabao unaweza kujitokeza.

“Haiwezekani sehemu inayopitisha magari mengi kama hii ikawa na mizani moja ya kupima magari yanayotoka na yanayoingia nchini, hivyo nakuagiza tena Meneja kuandaa mchoro na kuuwasilisha Wizarani ili tutenge fedha kwa ajili ya mizani ya pili”, amesisitiza Kasekenya.

Kuhusu suala la barabara katika mkoa huo, Kasekenya amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 12.8 kwa ajili ya ukarabati mdogo wa barabara ya Lusahunga – Rusumo (Km 92), huku ikisubiri taratibu za manunuzi ya kumpata mkandarasi wa kufanya ukarabati mkubwa.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kasekenya, amekagua daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140 na barabara za maingilio zenye urefu wa kilometa 18 ambapo ameridhishwa na kasi ya ujenzi ya mradi huo unaojengwa na mkandarasi M/s China Henan.

Amebainisha kuwa daraja hilo ambalo linaunganisha wilaya ya Karagwe na Misenyi, litakuwa ni njia ya mkato kati ya wilaya hizo mbili na hivyo kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa wilaya hizo na mwekezaji wa kiwanda cha sukari kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Ngara, Mheshimiwa Ndaisaba Ruhoro, ameipongeza Serikali kwa kutoa shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami za Nyakahura – Kumubuga – Murusugamba (Km 75), Kumubuga – Rulenge – Mururama (Km 32) na Rulenge - Kabanga Nickel (Km 34) ambapo amesema kuwa kukamilika kwa barabara hizo kutarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kutoka wilaya hiyo kuelekea wilaya jirani na hata nchi jirani za Rwanda na Burundi.

Naye, Msimamizi wa Daraja la Kitengule, Charles Rumisha, amesema kuwa mradi ulianza mwezi Oktoba, 2018 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu ambapo amesisitiza kuwa mpaka sasa wamefika katika hatua nzuri.

Amefafanua kuwa kwenye upande wa barabara ujenzi umefika asilimia 88 na kwa upande wa daraja mkandarasi tayari keshakamilisha ujenzi wa nguzo zote nne, kilichobaki ni kuweka usawa wa juu wa barabara.

Naibu Waziri Kasekenya, yupo katika ziara ya siku Tatu mkoani Kagera ambapo atakagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na na Wizara hiyo ili kujionea maendeleo yake.

Share:

PROF.MKUMBO AFANYA UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA TANTRADE

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), kwa Mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa Sheria ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ya 2009, Kifungu cha 6(2) ameteua Wajumbe saba (7) wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Wajumbe hao walioteuliwa kwa kushauriana na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban ni kama ifuatavyo:

    1. Bw. Ally Senga Gugu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara;
    2. Dkt. Salim Hamad Suleiman kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda (SMZ);
    3. Bi. Vumilia Lwoga Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo;
    4. Bw. John Marato Sausi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango;
    5. Bi. Dorice John Mgetta kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA);
    6. Bw. Ahmed Suleiman Nassor kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA); na
  • Bi. Jackline David Mkindi kutoka Taasisiya Wafanyabiashara wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA).

Uteuzi wa Wajumbe hao unaanza mara moja.

Share:

31 New FORM FOUR and Above Job Vacancies at Dar es Salaam University College of Education (DUCE) – Various Transfer Posts

About DUCE The Dar es Salaam University College of Education (DUCE) is a public institution established in 2005 through the Government Notice No. 202 published on 22nd July 2005. The establishment of the College was a priority response by the Government of Tanzania to address the problem of acute shortage of graduate teachers and experts […]

This post 31 New FORM FOUR and Above Job Vacancies at Dar es Salaam University College of Education (DUCE) – Various Transfer Posts has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Country Human Resources and Operations Manager (COM) at SNV

Company Description SNV is a not for profit international development organisation founded in the Netherlands nearly 50+ years ago. SNV has built a long-term, local presence in 25 of the poorest countries in Africa, Asia, and Latin America. Established in Tanzania in 1971, SNV Tanzania works with locally-based development partners including national and local government, […]

This post Country Human Resources and Operations Manager (COM) at SNV has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

ULEGA ATAKA KUMALIZIKA KWA MIGOGORO NA CHANJO KUFIKISHWA VIJIJINI

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumza mara baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuanza rasmi ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo ambapo ameusisitiza uongozi wa mkoa huo kuwa na mkakati wa kumaliza migororo ya wakulima na wafugaji ikiwemo njia ya kuhamasisha wafugaji kuvuna mifugo yao na kuuza viwandani ili viwanda hivyo vipate malighafi kwa ajili ya kuuza nyama ndani na nje ya nchi. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge akibainisha mikakati ya mkoa katika kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji wakati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alipofika ofisini kwake kabla ya kuanza rasmi ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, ambapo Mhe. Kunenge amewataka wakazi wa mkoa huo kutochukua sheria mkononi na kuvielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kutenda haki vinapopata taarifa juu ya migogoro hiyo. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akioneshwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi, sehemu ya eneo la Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani ambalo limevamiwa na baadhi ya wananchi na kujenga makazi. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, (wa tatu kutoka kushoto) akioneshwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi moja ya mitambo inayotumiwa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akiangalia moja ya mitambo katika kiwanda cha kuzalisha chanjo za mifugo cha HESTER kilichopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani na kusisitiza chanjo zinazozalishwa nchini zinapaswa kufikishwa maeneo ya vijijini ili wafugaji wakinge mifugo yao dhidi ya magonjwa mbalimbali. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

 Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) ameusisitiza uongozi wa Mkoa wa Pwani kutumia mkakati wa uvunaji wa mifugo kama mkakati wa kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima pamoja na kuondokana na tatizo la uhaba wa malighafi katika viwanda vya kuchakata nyama mkoani humo.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo leo (12.07.2021) alipokutana na uongozi wa mkoa huo ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, wakati akitoa taarifa ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Pwani na kufafanua kuwa ni vyema uongozi huo ukafanya tathmini ya kina kwa kuunda kamati maalum ili kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji mkoani humo.

Amesema viongozi ndani ya mikoa yote nchini ni vyema wakaunda kamati maalum za wataalamu kwenda wilayani hadi vijijini ili kutafuta ufumbuzi wa haraka na kudumu wa kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji, ukiwemo mkakati wa kuhakikisha wafugaji wanavuna mifugo yao kwa kuuza katika viwanda vya kuchakata nyama ili vipate malighafi na kuuza nyama ndani na nje ya nchi.

Mhe. Ulega amesema serikali inalichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa kwa kutumia kamati maalum kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Amesema wizara ilishatuma timu ya kushughulikia jambo hilo kwa ngazi ya taifa na imetoka na mapendekezo kadhaa kwa hatua zaidi.

Mhe. Ulega amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi inasisitiza mikoa kuunda kamati ya wataalam kubaini mambo kadhaa ili kuchukua hatua ili jambo hilo lisijitokeze katika maeneo mbalimbali nchini.

"Timu hizo zitabaini maeneo ya mifugo vamizi, wafugaji wakorofi ili waweze kuchukuliwa hatua kali sambamba na kubainisha mahitaji halisi ya miundombinu ya mifugo, kuwepo kwa taarifa kamili za mifugo ilipo pamoja na kuhamasisha kuwa na utamaduni wa kuuza mifugo kwenye viwanda vya kuchakata nyama ili vipate malighafi." amesema Mhe. Ulega

Akizungumzia hali halisi ya hatua zilizochukuliwa na Mkoa wa Pwani kukabiliana na kero hiyo mkuu wa mkoa huo Mhe. Abubakar Kunenge amewataka wakazi wa Mkoa wa Pwani kutochukua sheria mkononi na kuviasa vyombo vya ulinzi na usalama kutenda haki wanapopata taarifa ya migogoro hiyo.

Mhe. Kunenge amefafanua kuwa mkoa huo tayari umeanza kufanya sensa ya mifugo katika wilaya zote na Wilaya ya Rufiji kwa sasa ipo hatua za mwisho kukabidhi mapendekezo yao.

Ameongeza kuwa taarifa hiyo ya sensa wamebaini kuna wafugaji wengi waliopo katika wilaya hiyo hawajasajiliwa na hawana taarifa zozote za wanakotoka wala wanakokwenda.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani ameagiza uongozi huo pamoja na wizara wanaohusika na masuala ya chanjo kuhakikisha chanjo zinazozalishwa na taasisi hiyo zinawafikia wafugaji waliopo vijijini badala ya kuanza kufikiria kusambaza chanjo hizo nje ya nchi.

Mhe. Ulega amesema kuna mifugo mingi kama kuku, ng'ombe na mbuzi wanaokufa kwa kuwa wafugaji hawajui kama kuna chanjo zinazozalishwa hapa nchini ingawa kuna maeneo mengine chanjo hizo hazijafika kabisa.

Ametaka viongozi hao kuhakikisha chanjo zinafika maeneo mbalimbali nchini hususan maeneo ya vijijini ili wafugaji waweze kukinga mifugo yao dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Mhe. Ulega ametembelea pia kiwanda cha kuzalisha chanjo za mifugo cha HESTER kilichopo Wilayani Kibaha na kujionea namna kiwanda hicho kikiwa tayari kuanza kuzalisha chanjo ambazo zitakuwa zikiuzwa ndani na nje ya nchi.

Akiwa kiwandani hapo ameendelea kusisitiza chanjo za mifugo kufikishwa maeneo mbalimbali nchini hususan ya vijijini ili mifugo iwe na afya bora na wafugaji waweze kunufaika kupitia ufugaji

Share:

Head Teacher at Geita Gold International School

ABOUT GEITA GOLD INTERNATIONAL SCHOOL (GGIS)   Geita Gold International School (GGIS) is owned and maintained by Geita Gold Mining Ltd, located at Geita Region within the mine license area. The school is accredited by the Council of International Schools (CIS) and affiliated to Association of International Schools in Africa (AISA) and Tanzania International Schools […]

This post Head Teacher at Geita Gold International School has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Graduate Trainee-Bank Officer at KCB Bank

Job Summary:   The incumbent will be contact person to customers on banking solutions. Responsible for advising bank customers on financial related issues. He/she will handle customers in a professional manner Key Responsibilities:   Advise customers on financial related issues Respond to customers on and about Banking Products and related customer queries Offer quality cash […]

This post Graduate Trainee-Bank Officer at KCB Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Engineer, Software at Standard Bank

Job Purpose   To design, code, test, debug and correct programs in development environments within the Continuous delivery pipelines as well as provide support and maintenance of computer systems and programmes.  In addition, produce program specifications in accordance with the Cyclomatic complexity conducive to a technical area, and implement applicable enhancements as well as work […]

This post Engineer, Software at Standard Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Country Finance Manager at Sokowatch

Country Finance Manager   Country Finance Manager Role Description About Us: Sokowatch is transforming communities across Africa by revolutionizing access to essential goods and services. By connecting small shops to the digital economy, we fix inefficient supply chains and provide services that were previously unavailable. Sokowatch aims to provide everything a retailer needs, no wholesalers […]

This post Country Finance Manager at Sokowatch has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger