Friday, 2 July 2021

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Lalaani Manara kumdhalilisha mwandishi wa habari

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesikitika na kulaani kitendo cha msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara kumdhalilisha mwandishi wa Habari wa Redio Clouds FM, Prisca Kishamba.

Taarifa iliyotolewa na jukwaa hilo leo Ijumaa Julai 2, 2021  na mwenyekiti wake, Deodatus Balile inaeleza kuwa udhalilishaji huo ulioambatana na maneno ya kashfa ulifanywa  kwenye mkutano wa Simba na waandishi wa habari uliofanyika Juni 30, 2021 mkoani Dar es Salaam.

TEF imemtaka Manara kuacha mara moja tabia ya kutumia mikutano ya klabu ya Simba na hata mitandao ya kijamii kuwadhalilisha wanahabari.

Limesema ikiwa kuna suala lolote ambalo mwandishi wa habari amelitenda kinyume cha maadili na miongozo ya taaluma, wahusika wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwa taasisi za kihabari au kwa mwajiri wa mwandishi husika ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Kupitia taarifa hiyo,  TEF imeuomba uongozi wa timu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kumuonya Manara kuacha tabia hizo mara moja kwani  hazina afya na haziongezi thamani yoyote kwa Simba wala taaluma  ya habari.


Share:

Picha : SHEMAHONGE AFUNGUA SHINA LA WAKEREKETWA, OFISI YA CCM TAWI LA NEGEZI - MWAWAZA.... ASEMA VIJANA CCM HAWANA MPANGO NA KATIBA MPYA


Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amefungua Rasmi Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga huku akiweka wazi kuwa Vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga hawana mchakato wala mawazo ya Katiba Mpya zaidi ya kujenga chama na nchi.

Akizungumza leo Ijumaa Julai 2,2021 wakati wa ufunguzi wa shina la wakereketwa na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga, Shemahonge amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakina ajenda ya katiba mpya sasa.

“Sisi Chama cha Mapinduzi hatuna ajenda ya Katiba Mpya kwa sasa,huo ndiyo msimamo na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hivi sasa anajenga nchi, anajenga uchumi. Sasa vile vyama ambavyo havina malengo wala ajenda ndiyo vinalazimisha katiba mpya.

“Hivi sasa hatuna mchakato wala mawazo na Katiba Mpya, wazo letu ni kujenga chama na nchi.Sisi vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga tunaungana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwamba mchakato wa Katiba kwa sasa haupo, sasa hivi tunajenga chama, tunajenga nchi iweze kuwa na uchumi tukiangalia uchumi wa nchi yetu umeyumba kutokana na ugonjwa wa Corona ambao umeikumba dunia nzima”,amesema Shemahonge.

Baraka amewataka vijana wa CCM kumuunga mkono Rais Samia Suluhu akisema katika kipindi cha siku 100 amefanya mambo makubwa akionesha kwa vitendo kuwa wanawake wanaweza kuongoza nchi.

“CCM tembeeni kifua mbele kuwa wanawake wanaweza. Rais wetu Mpendwa Mhe. Samia Suluhu amefanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi. Tuendelee kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii, kuwa waadilifu, waaminifu, kumlinda na kulinda amani ya nchi huku tukieleza na kuyasemea mambo mema anayofanya katika kujenga nchi yetu”,amesema Shemahonge.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoa wa Shinyanga ametumia fursa hiyo kumpongeza kada wa CCM, Edwin Masha Charles kwa kutoa jengo la nyumba yake litumike kama ofisi za Chama Cha Mapinduzi tawi la Negezi kata ya Mwawaza kwa ajili ya shughuli za chama hicho.

“Nimefarijika kuona kijana mwenzetu Edwin Masha Charles kwa kutoa mali yake itumike kwa shughuli za chama. Tunamshukuru kwa kujitolea kukijenga chama. Hii ni kazi ya chama kwani chama kinajengwa na vijana.Najua kuna mambo mengi yataibuka kwamba kwanini amefanya hivi labda anataka uongozi. Nikusihi ndugu ya Edwin usikatishwe tama na maneno ya watu, umefanya kazi ya kizalendo kujenga chama”,amesem Shemahonge.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua mbali na kumpongeza kada wa CCM Edwin Charles kutoa jengo lake litumike kama ofisi ya CCM pia amewaomba vijana kuendelea kujenga chama na kukipambania huku akiwasihi vijana kuendeleza umoja na mshikamano walionao.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu amesema ofisi hiyo ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza itatumiwa na chama na Jumuiya zote za CCM wakati CCM inaendelea na mchakato wa kujenga ofisi zake katika eneo hilo.

Bashemu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa serikali za mitaa pamoja na Madiwani kufanya mikutano ya hadhara na kuwaeleza wananchi kuhusu miradi na kazi wanazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi huku akiwataka vijana kujitokeza kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyoo na vyumba vya madarasa shuleni.

Kwa upande wake, Edwin Masha Charles amekishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kukubali ombi lake la kutoa chumba cha nyumba yake kitumike kama ofisi ya CCM huku akibainisha nia yake ilikuwa ni jengo hilo litumike kwa shughuli za UVCCM kwani tamanio lake ni kuona kila tawi la CCM lina ofisi kwa ajili ya vijana.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifurahia baada ya kufungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akipandisha Bendera ya CCM baada ya kufungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akipandisha Bendera ya CCM baada ya kufungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akipandisha Bendera ya CCM baada ya kufungua Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akikata utepe wakati akifungua ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 2,2021.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akipiga makofi baada ya kukata utepe akifungua ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahongenaa viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa ndani ya ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahongenaa viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa nje ya ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, viongozi mbalimbali wa CCM na wananchi wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye shin la wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, viongozi mbalimbali wa CCM na wananchi wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye shin la wakereketwa wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa UVCCM, Muhsin Zikatim akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga
Kada wa CCM Edwin Masha Charles aliyetoa jengo la nyumba yake litumike kama ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Kada wa CCM Edwin Masha Charles aliyetoa jengo la nyumba yake litumike kama ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
 Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Raphael Nyandi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza, Suzana Dotto akisoma risala wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
 Katibu wa Hamasa na Chipukizi CCM mkoa wa Shinyanga , Hashim Issa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
 Diwani wa kata ya Mwawaza, Juma Nkwabi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Wananchi na wanaCCM wakiwa kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mwawaza, Dotto Mamboleo akizungumza kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakifurahia jambo kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge (katikati) akiandamana na vijana wa CCM kuelekea kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge (katikati) akicheza muziki na vijana wa CCM kuelekea kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge (katikati) akicheza muziki na vijana wa CCM kuelekea kwenye ufunguzi wa Shina la Wakereketwa wa CCM na ofisi ya CCM tawi la Negezi kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

SERIKALI KUANZISHA SHULE ZA MICHEZO UMISSETA 2021

 


Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akihutubia leo Julai 2,2021 kwenye ufungaji wa UMISSETA mjini mtwara.

Waziri bashungwa akiwa na Katibu Mkuu wake Dkt. Hassan Abbasi, viongozi na wachezaji wa timu za mpira wa miguu kwenye fainali baina ya timu ya Pemba na Mtwara ambapo Pemba wameibuka washindi baada ya kuiadhibu mtwara mabao 2-0.



Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akitoa maneno ya kumkaribisha Bashungwa leo Julai 2,2021 ili atoe hotuba ya ufungaji wa UMISSETA 2021



Msanii Sholo Mwamba akitumbuiza leo Julai 2,2021 kwenye sherehe ya ufungaji wa UMISSETA 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.



Msanii Nandy akitumbuiza leo Julai 2,2021 kwenye sherehe ya ufungaji wa UMISSETA 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.



Msanii Mr Bluu akitumbuiza leo Julai 2,2021 kwenye sherehe ya ufungaji wa UMISSETA 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara



Na John Mapepele, Mtwara

Serikali imesema ipo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha shule maalum za michezo, za msingi na sekondari, katika mikoa yote nchini lengo likiwa ni kuwa na shule na vituo maalum vya kuendelezea vipaji vya michezo (sports academies).

Akizungumza kwenye Sherehe za kufunga mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari(UMISSETA) mjini Mtwara leo Julai 2,2021 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amese Shule hizi zitakuwa zinalea na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali, na Serikali itakuwa inasimamia kwa ukaribu, kuhakiksiha kuwa vituo vya michezo vya shule za msingi na sekondari, vinapatiwa mahitaji muhimu yatakayo saidia katika kuendeleza vipaji hivyo.

Amesema Serikali kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo – Malya, inaanzisha kituo maalum cha michezo cha kuendeleza vipaji (Centre of Sports Excellency), vitakavyokuwa vinapatikana kutokana na mashindano haya, na maeneo mengine mbalimbali nchini.

« Chuo cha maendeleo ya michezo Malya kimeanzisha mafunzo ya astashahada, ili kupanua wigo wa wanufaika wake, pia kimefungua kituo cha mafunzo Dar es salaam na Ruvuma, ili kusogeza huduma kwa wananchi wengi zaidi. Ni matumaini yetu kuwa, kupitia Chuo hiki, tutaweza kupunguza pengo la watalaam, na walimu wa Michezo ambalo tunalo hivi sasa » amesisitiza Mhe. Bashungwa

Katika mashindano ya mwaka huu ya UMISSETA mkoa wa Dar es Salaam umeibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika michezo yote.

Pia amememshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu, kwa maelekezo yake ya kuondoa kodi ya VAT, katika kununua na kuingiza nyasi bandia nchini, ili tuweze kujenga na kukarabati miundombinu yetu ya michezo.

« Wizara yangu imejipanga kuanza kuhamasisha taasisi na wadau mbalimbali, kuchangamikia fursa iliotolewa kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vyao. Nimatumaini yetu kuwa, kwa hatua hii tunakwenda kuimarisha, na kuboresha mioundombinu ya michezo nchini » amefafanua Mhe. Bashungwa.

Ameongeza kuwa, Mhe. Rais kupitia bunge la bajeti lililoisha mwezi Juni, 2021, ameruhusu asilimia 5 kutoka kwenye michezo ya kubashiri (sport betting), kuingia kwenye mfuko wa maendeleo ya michezo, unaosimamiwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ili fedha hizo ziweze kutumika kwa ajili ya maendeleo ya Michezo.

Amesema kutunishwa kwa mfuko huo kutatoa fursa ya kuendeleza michezo mbalimbali nchini, kwa ngazi zote, ikiwemo mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA.

Amemhakikishia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Majaliwa utekelezaji wa maagizo mbalimbali, ya kuhakikisha Wizara yake inaweka mikakati mbalimbali ya kuendeleza michezo nchini ambayo aliyatoa wakati wa ufunguzi wa UMITASHUMTA hivi karibuni ambapo amesema baadhi ya maelekezo tayari yameshafanyiwa kazi.

Baadhi ya maelekezo hayo ni pamoja na, kufanya tahimini ya Vyuo vya Elimu, vilivyokuwa vinafundisha michezo na sasa havifundishi; na uanzishwaji wa shule maalum za michezo mikoani.

. « Kupitia ushirikiano na umoja wa Wizara zetu maagizo haya na mengine tutayashughulikia kwa kasi na weledi, ili kuhakikisha sekta ya michezo inakuwa nchini »

Aidha amesema Serikali kwa, kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo itazindua mpango mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Michezo mwezi Julai, 2021. Mpango mkakati huo umetoa muelekeo wa jinsi ya kuendesha michezo, kwa kuzingatia maelekezo mbalimbali yaliotolewa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, ambapo pamoja na mambo mengine, mpango huo unaweka mkakati wa jinsi ya kuingia kwenye michezo ya kulipwa, ili kuwapatia vijana ajira kwa kutumia vipaji vyao, na kujipatia vipato wao binafsi lakini pia kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya michezo. Kama Waziri mwenye dhamana, nitahakikisha kwamba tunafikia malengo hayo na kazi inaendelea.

Pia ametumia muda huo kuwashukuru wasanii wa kizazi kipya waliokuwa wakitoa burudani katika kipindi chote cha UMITASHUMTA na UMISSETA ambao wameleta hamasa kubwa na burudani kwa wanamichezo na wadau mbalimbali walioshiriki mashindano ya mwaka huu.

Miongoni mwa wasani wa kizazi kipya waliotoa burudani kwenye ufungaji wa UMISSETA leo Julai 2,2021 na kuteka mji wa mtwara na viunga vyake ni pamoja na Maarifa, Kala Jermiah, G-Nako, Mr Blue, Shishi, Nandy na Sholo Mwamba.

“Asanteni sana kwa ushirikiano wenu mkubwa, pamoja na burudani mlioionesha, na mtakayo endelea kuifanya hapa leo, ili kutoa burudani ya kuhitimisha michezo hii. Kwa hakika wana Mtwara wamefurahi na kuburudika sana. Michezo sasa ni ajira, hivyo kwa kuendeleza michezo hii, ni kuaandaa eneo muhimu litakalowapatia vijana wetu ajira kupitia vipaji walivyonavyo” amesisitiza Bashungwa

Naye Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara ya habari itaendelea kusimamia sera na kuweka mikakati madhubuti ili kuinua maendeleo ya wasanii nchini.
Share:

WAZIRI AWESO –WAKANDARASI WANAOSUASUA KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI TUTAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mngandilwa
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa

MKUU wa wilaya ya  Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza jambo ewakati wa kikao hicho
Baadhi ya washiriki wakifiatikia kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga
Baadhi ya washiriki wakifiatikia kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga

 

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa hatashindwa kuendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwapokonya kazi wakandarasi wanaosuasua ikiwemo wanaokwamaisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini

Kauli hiyo alilitoa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga ambapo alisema kuwa katika kutekeleza tayari ameshawafuta kazi jumla ya wakandarasi 118 pamoja na makampuni 69 yaliyokuwa yanaendesha miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inampatia mwananchi huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yake bila ya kulazimika kutembea umbali mrefu lakini uwepo wa huduma ya uhakika.

"Uhandisi wa maji ni pamoja na kufuatilia miradi uliyopewa n a kujiridhisha kama huduma ipo, pale unapo sema Mradi umekamilika basi inamana unatoa maji kwa asilimia 100% na sio ujanja ujanja"Alisema Waziri Aweso.

Aliwataka wataalamu wabadili fikra zao juu ya utekelezaji wa miradi ya maji akitolea mfano miradi ya maji vijijini una sehemu tatu ya kwanza ni chanzo eneo la pili tanki la maji la tatu ni kituo cha usambazaji au kama kuna eneo lenye maji ya mserereko lazima kuwea na eneo la kitibu maji.

“Sasa unajenga chanzo, unajenga tenki la maji, unatandaza vituo vya maji halafu unaangiza pump miezi sita watu wanaona vituo vya maji lakini maji hayatoki unatengeneza malalamiko, manung’uniko na masononeko yalisiyo na ulazima “Alisema Waziri Aweso.

Alisema kumbe wakati unapojenga kwanini usiangize na pampu hata kabla maji hayajaingia kwenye tenki watu wayatumie lakini wanaweza kuyatumia wakati wa ujenzi wa tenki.

“Kwa hiyo hizo ndio fikra ambazo lazima zibadilike kwenye wizara ya maji umejenga intake ya maji agiza pampu ya maji ili twende sambamba watu waweze kuyatumia maji kuhakikisha dhamira ya Rais wetu Samia Suluhu inatimilika”Alisema







Share:

TAKUKURU Dodoma Yaokoa Mamilioni Ya Fedha


Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) imefanikiwa kuokoa na kudhibiti Jumla ya Tsh . Milioni mia mbili kumi na tano ,laki sita na sitini elfu (215,660,000)/= ambazo zingepotea kwa kuchepushwa ,kufujwa  ama kulipwa kwa watu wasiostahili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 2,2021 jijini Dodoma,Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo  ametaja mmoja wa uchepushaji ni gari la Ofisi ya katibu tawala  mkoa wa Dodoma ambalo baada ya kupata ajali  lilipelekwa kwenye gereji moja mkoani Dodoma  na kubainika vifaa 101 vyenye thamani ya Tsh. Milioni themanini na Saba ,laki Saba na themanini na tano elfu(87,785,000/=) vilichepushwa kutoka kwenye gari hilo.

"Tulishirikiana na wakala wa ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Dodoma ikabainika katika gari hilo kuna vifaa 101 vilichepushwa  tuliingilia kati vifaa hivyo vikarejeshwa"amesema .

Bw. Kibwengo amesema kitendo cha uchepushaji ni kosa chini ya Sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2019 ambapo amewataka wamiliki wa gereji  binafsi mkoani Dodoma  kuacha mara Moja tabia ya wizi wa vipuri vya magari ya umma .

Aidha, Kibwengo amesema miradi 20 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi  bilioni Moja ,milioni mia Saba sabini na tano  laki Saba  ,sitini na tatu elfu na mia Saba arobaini na sita (1,775,763,746/=) imekaguliwa katika sekta za elimu,Afya na ujenzi  na kubaini uchepuzi wa vifaa vya ujenzi  vyenye thamani ya Tsh. Milioni arobaini na Moja  laki nane na hamsini elfu( 41,850,000/=) huku miradi 19 ikibainika kutekelezwa kwa kiwango stahiki.

Katika hatua nyingine Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU mkoa wa Dodoma imepokea taarifa 124 za malalamiko zikiwa ni taarika 52 pungufu ya zile zilizopokelewa kwa robo ya mwaka Jana ambapo taarifa zinazohusu rushwa ni 70  na 54 hazihusiani na rushwa .
Sekta zinazoongoza kwa kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa ni serikali za mitaa kwa asilimia 39,ardhi asilimia 19,sekta binafsi asilimia 7,elimu,Afya,na polisi kila Moja asilimia 6.

"Tumepokea taarifa 124 za malalamiko ambapo pia majalada 20 ya uchunguzi yalikamilika na mashauri mapya mawili yalifunguliwa Mahakamani na mashauri mawili yalitolewa maamuzi  ambapo jamhuri ilishinda Moja na kushindwa Moja.

Sanjari na hayo Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema elimu imetolewa kwa makundi mbalimbali ya Kijamii wakiwemo Vijana  na kufanya semina 28 ,mikutano 7 ya hadhara ,vipindi 11 vya redio,maonesho mawili na ufunguzi wa klabu 41 za wapinga rushwa na kusikiliza kero za rushwa Kupitia mpango wa TAKUKURU inayotembea.

Pia katika robo ya Julai,hadi Septemba ,2021 Kibwengo amesema wataweka msisitizo katika uelimishaji wakati wa mbio maalum za mwenge na kwa makundi hasa ya Vijana huku akitoa msisitizo ushiriki wa kila mwananchi katika mapambano dhidi ya rushwa.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger