Friday, 21 May 2021

Mhandishi Masauni: Serikali Ilitoa Msamaha Kwa Wadaiwa Wa Kodi


Na, Saidina Msangi na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa katika Mwaka wa Fedha 2018/19 ilitoa msamaha kwa wadaiwa wa Kodi (Tax Amnesty) uliohusisha riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma ili kuongeza makusanyo.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Henry Maganga Nicodemus, Mbunge wa Mbogwe aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kufuta madeni ya muda mrefu kwa wafanyabiashara wa ndani yatokanayo na ukosefu wa elimu juu ya matumizi sahihi ya mashine za EFD wanayodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Mhe. Masauni alisema kuwa msamaha huo ulilenga kusamehe malimbikizo ya nyuma ya riba na adhabu (Interest and Penalties) kwa kiwango cha asilimia 100 kwa wafanyabiashara wote hapa nchini ambao walikuwa na malimbikizo ya madeni hayo ya kodi.

“Msamaha huo ulitolewa kwa kipindi cha miezi sita (6) kilichoanzia tarehe 1 Julai 2018 mpaka tarehe 31 Desemba 2018, kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wake, Serikali iliongeza muda wa msamaha huo kwa miezi sita ili wafanyabiashara waliokuwa na madeni hayo wakamilishe malipo husika”alieleza Mhe. Masauni.

Aidha Mhe. Masauni alisema kuwa hatua hiyo ya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi SURA 438 ilitarajiwa kuongeza mapato ya Serikali na kukusanya malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi (Principal Tax) pamoja na kuinua kiwango cha ulipaji kodi kwa hiyari kwa zaidi ya asilimia 10.

Mhe. Masauni aliongeza kuwa licha ya nia nzuri ya Serikali ya kufuta riba na adhabu ili kuwawezesha walipakodi wenye madeni sugu ya kodi kuyalipa kwa awamu ili kurahisisha mwendelezo wa biashara zao wengi wao hawakulipa kodi hizo hata baada ya kuingia mikataba na TRA na hata baada ya Serikali kuongeza muda wa ziada wa kufanya malipo ya kodi husika yaliyotokana na msamaha huo.

Mwisho.


Share:

Waziri Wa Kilimo Afungua Warsha Ya Kitaifa Juu Ya “kutumia Uwekezaji Mkubwa Katika Kilimo Kuleta Maendeleo Shirikishi Tanzania”


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Tanzania inatambua umuhimu wa wakulima wote nchini – yaani wakulima wadogo, wa saizi ya kati na wakubwa - katika mageuzi ya kilimo na kuendeleza mbinu za kisasa na kilimo cha kibiashara chenye tija zaidi na faida kubwa  kwao.

Mkakati wa Sekta ya Kilimo (ASDS I na ASDS II) na Programu ya kuendeleza Kilimo (ASDP I na ASDP II) imelenga kukuza kilimo kwa ushirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi ili kuleta matumizi endelevu ya ardhi na maji, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, huduma za utafiti na ughani, upatikanaji wa mbegu bora na pembejeo, masoko na uchakataji wa mazao ili kuongeza thamani za mauzo ya nje (value addition).

Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma tarehe 21 Mei 2021 wakati akifungua warsha ya kitaifa juu ya “kutumia uwekezaji mkubwa katika kilimo kuleta maendeleo shirikishi tanzania” iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kulingana na sera zetu za kilimo wawekezaji wakubwa wanategemewa sio tu kuzingatia haya katika kilimo chao wenyewe bali pia kusaidia wakulima wadogo – outgrowers na wakulima wengine - kwa kuwakopesha mbegu bora na pembejeo, kutoa elimu, ushauri na huduma za ughani kwa ujumla na kuingia mikataba mizuri ya kununua mazao yao” Amekaririwa Mhe Mkenda

Amesema kuwa Wakulima wakubwa wanategemewa pia kuchangia katika kuongeza thamani ya mazao na uboreshaji wa mnyororo wa thamani, na hivyo kuongeza bei za bidhaa za kilimo tunazouza nje ya nchi.

Amesema kuwa kunapokuwa na wawekezaji wakubwa na wa saizi ya kati ambao wengi wao huchukua maeneo makubwa ya ardhi, mojawapo ya majukumu ya serikali ni kulinda haki za raia na kuhakikisha ardhi yao na maji haviporwi, na pia wanalipwa fidia stahiki na bei nzuri kwa mazao yao.

Waziri Mkenda amesema kuwa Zaidi ya asilimia sabini (70%) ya watanzania wanaishi vijijini ambako wanajishughulisha na kilimo, kilimo huchangia 26%  hivi ya pato la taifa na asili mia thelathini (30%) ya mauzo ya nje (exports). “Lakini kwa miaka mingi tumejitahidi kuinua ubora wa kilimo kwa mafanikio japo si makubwa sana, kutokana na ujuzi mdogo wa wakulima wetu na matumizi hafifu ya sayansi na teknolojia ya kilimo, na hivyo tumeendelea kuwa na tija ndogo sana (low agricultural productivity) na upotevu wa mavuno” Amesema

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam/Taaluma Prof Bonaventure Rutinwa amesema kuwa Warsha hiyo ni kilele cha Utafiti wa mwaka mmoja uliofanywa na taasisi ya taaluma za maendeleo ya Chuo Kikuu cha dar es salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya  Bill&Melinda Gates ikiwa na lengo la namna ya kutumia fursa za uwekezaji mkubwa katika kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo Dkt Ronald Ndesanjo amesema kuwa radi huo wa utafiti ni sehemu ya majukumu ya taasisi hiyo ambapo ulikuwa na malengo makubwa mawili ikiwa ni pamoja na kufahamu kiwango cha ujumuishi katika ngazi ya miradi ya Uwekezaji wa kilimo chini ya Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Pia amesema lengo la pili ilikuwa ni kubuni namna bora ya kubadilisha mabadiliko jumuishi ya kilimo katika ngazi za uwekezaji pamoja na ngazi ya sera.

MWISHO


Share:

Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Burundi



Share:

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AITAKA SERIKALI KUANZISHA MAHAKAMA YA FAMILIA “FAMILY COURT”

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira amesema ipo haja ya Serikali kuanzisha Mahakama ya Familia yaani Family Court kama ilivyofanya kwenye Mahakama za Ardhi ili kusaidia kuondosha changamoto zinazojitokeza ikiwemo Masuala ya Matunzo ya Watoto.

Amesema ili Matunzo ya Watoto yaweze kubebwa kwa uzito unaostahili na kupanua wigo mpana wa haki ili kuhakikisha changamoto za namna hiyo zinaondoka kwenye jamii badala ya kuendelea kuwepo kila wakati.

Aliyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati alipouliza Maswali Mawili ya Nyongeza baada ya Serikali kuwasilisha Majibu ua Swali lake la Msingi lililouliza "Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwakomboa Wanawake wanaobebeshwa mzigo mkubwa wa kugharamia matunzo ya Watoto bila msaada wa Baba?" 

Mbunge Neema alisema pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini hata kwa Sheria zilizopo bado kuna changamoto kubwa kwenye eneo hilo.

Mbunge Neema Lugangira alisema ndio maana hata Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ilani yake ya Uchaguzi 2020/2025 imeliona hilo na imeahidi kuielekeza Serikali kwenye Ukarasa wake wa 145 unaosema "CCM itaelekeza Serikali kuimarisha huduma za usuluhuhi wa migogoro ya ndoa na matunzo kwa watoto" na kwa msingi huo aliuliza maswali yake  mawili ya nyongeza.

Katika maswali yake ya nyongeza Mbunge Lugangira aliishauri Serikali iboreshe Sheria zilizopo ili gharama za matunzo ya watoto iendani na hali ya uchumi wa sasa na maisha ya sasa kutokana na maisha kuwa juu kuliko ilivyokuwa awali.

Akijibu Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Mhe Mwanaidi Khamisi amesema "Serikali imetoa maelekezo wazazi kuhakikisha mtoto anapata matunzo yote stahiki, na kama wazazi wa mtoto hawaishi pamoja na mtoto anaishi na Mama yake basi Baba atawajibika kugharamia malezi ya mtoto kulingana na kipato alichonacho". Swali hili pia lilimnyanyua Mhe Waziri Dkt Dorothy Gwajima ambae alisema "Nakiri tatizo Watoto kutelekezwa ni kubwa na ipo haja ya Serikali kufanya harakati za ziada ili kulidhibiti. 

Kwa upande mwingine Mbunge Neema Lugangira aliishauri Serikali ianzishe Mahakama ya Familia yaani Family Court na kwa upande wa Serikali, Mhe Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis alisema Serikali imekubaliana na ushauri wa Mbunge Neema Lugangira na ipo haja ya kuwa na chombo maalumu ambacho kitakuwa kinashughulikia masuala la familia hivyo wameupokea ushauri wa Mbunge Lugangira na wataufanyia kazi  kulingana na Sheria zilizopo.
Share:

TCU 2020/2021 Undergraduate Admission Guide Book for Ordinary Diploma/Equivalent Applicants

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

TCU 2021/2022 Undergraduate Admission Guide Book for Ordinary Diploma/Equivalent Applicants The Tanzania Commission for Universities (TCU) through its mandate as spelt out in Section (12) (2) (a) (b) (c) of the Universities Act Cap 346 of the laws of Tanzania, read together with Regulation 31 (2) (3) (4), coordinates the admission of students into Higher […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Kwa Sasa Tanzania Imeweza Kudhiti Vizuri Corona Na Wananchi Waendelee Kutekeleza Mbinu Zote Za Kinga


Na.WAMJW-Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi amewaondoa hofu Watanzania,wageni pamoja na watalii juu ya ugonjwa wa corona(COVID-19) kwa sababu Serikali na Wananchi wameendelea kuudhibiti vizuri mpaka sasa.

Prof.Makubi ameyasema hayo wakati alipo tembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou -Toure ambapo alipata fursa ya kukagua idara mbalimbali ikiwemo chumba cha CT-Scan pamoja na kuzungumza na wagonjwa walikuwa wakipata matibabu katika hospitali hiyo.

Wasafiri pamoja na watalii waendelee kuja nchini bila wasiwasi lakini kuna utaratibu wanapewa huku Watanzania wakiendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga ili udhibiti uliopo sasa uendele zaidi na ndio suala la msingi ambalo anawaomba wananchi waendelee kukaza na wasilegeze kamba katika kutii maelekezo ya kuchukua tahadhari zote dhidi ya corona.

Amesema Serikali imeendelea kudhibiti tatizo la COVID-19 mpaka sasa hivyo amewathiibitishia wananchi kuwa taifa lipo katika hali nzuri ya udhibiti wa ugonjwa huu.

Pia amesema Rais Samia Suluhu Hassan,ameweka mfumo mzuri wa kushughulikia suala hili na mpaka sasa hivi wanaweza kuona udhibiti zaidi kutoka kwa Wananchi.

“Sisi kama Wizara tunaona tupo kwenye hali nzuri,sasa hivi tumeidhibiti sana COVID-19 pengine kuliko nchi yoyote ile,na jitihada hizi zilianza kuanzia mwaka jana kwenye Serikali ya awamu ya tano na zimepokelewa na kuendelezwa vizuri na Serikali hii ya awamu ya sita,” amesema Prof.Makubi.

Hata hivyo amesema,kinachopaswa kufanywa na wananchi kwa sasa ni kuhakikisha wanatii na kuyafuata maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu kwani amepita katika hospitali hiyo ya Sekou- Tou’re amekuta miundombinu mizuri imewekwa ya kujikinga na COVID-19 ikiwemo sehemu za kunawia mikono na watoa huduma wanavaa barakoa kwani ni eneo ambalo lina hatari kubwa hivyo lazima wajikinge na kuchukua tahadhari zote.

“Niwaambie Watanzania wote na wasafiri muendelee kuwa na amani na wananchi muendelee kuchukua tahadhari kwani awali mmeweza kuchukua tahadhari vizuri sana na ndio maana tumeweza kudhibiti ,niendelee kuwapongeza Watanzania kwa sababu haya ni matunda ya wao kuwa wasikuvu,”amesema Prof.Makubi.

Aidha, Prof. Makubi amesema,tofauti na kunawa mikono na kuvaa barakoa pia kuna njia nyingine ya kujikinga na COVID-19 ambazo ni pamoja na kupunguza misongamano isiyokuwa ya lazima.

Pia kufanya mazoezi kwani ugonjwa huu unaathiri sana watu ambao wanamagonjwa ambayo siyo ya kuambukiza kama kisukari,shinikizo la damu na moyo.

Pamoja na kuzingatia lishe bora ambayo inasaidia kinga za mwili kama matunda pia kumekuwa na tiba za asili ambazo nazo zinapaswa kuendelea kuhamasishwa na wakiendelea kuzingatia hayo yote ugonjwa huo wataendelea kuudhibiti na pengine kuudhibiti zaidi hivyo hakuna haja ya watu kuwa na hofu.

“Tunapo fanya mazoezi inasaidia,tumeona wana michezo wengi wameweza kupata ugonjwa huu katika nchi zilizoendelea lakini sijasikia kifo, wengi wameweza kuudhibiti kwa kutumia kinga ya mwili wao na baadae ugonjwa unaisha,hivyo mazoezi tuendelee kuyafanya angalau mara tatu au nne kwa wiki angakau nusu saa hadi mwili utoe jasho pia tuzingatie lishe,”amesema Prof.Makubi.


Share:

Monitoring and Evaluation Specialist – NSA M&E Framework development at FAO

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

FAO seeks gender, geographical and linguistic diversity in its staff and international consultants in order to best serve FAO Members in all regions. FAO is committed to achieving workforce diversity in terms of gender, nationality, background, and culture Qualified female applicants, qualified nationals of non-and under-represented member nations, and person with disabilities are encouraged to apply Everyone […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

National Project Personnel – Project Team Leader at FAO

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

IMPORTANT NOTICE: Please note that Closure Date and Time displayed above are based on date and time settings of your personal device FAO is committed to achieving workforce diversity in terms of gender, nationality, background and culture Qualified female applicants, qualified nationals of non-and under-represented member nations and person with disabilities are encouraged to apply […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA TAASISI YA UHANDISI NA UBUNIFU MITAMBO TANZANIA TEMDO



Share:

Regional Sales Manager – FMCG at kazini kwetu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

REGIONAL SALES MANAGER Our client; a Group of Companies based in Dar es Salaam is looking for Regional Sales Manager to begin to work the soonest possible. The successful candidate is expected to own the responsibility of effectively appointing distributors, developing them and managing the sales activities within an assigned area, ensuring that sales growth […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Credit Controller at kazini kwetu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

CREDIT CONTROLLER We are looking for Credit Controller to work for our client in Dar es Salaam. As part of a team, and as a Credit Controller, you will be given a debt portfolio and it’s your duty to take every initiative to ensure optimum debt recovery and to consistently meet the monthly collection target […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

RC Makalla amaliza ugomvi wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni


Mvutano baina ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Sipora Liana na Meya wake Songoro Mnyonge, umemalizika baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kuingilia kati.

Liana na Mnyonge walitoleana maneno makali kwenye moja ya kikao cha Baraza la Madiwani kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za makusanyo mbalimbali.

Mapema leo Ijumaa, Makalla aliwaita kwenye kikao maalumu viongozi hao na kuzungumza kwa lengo la kumaliza mvutano huo, ambapo muafaka ulipatikana. Pia, aliwataka kwenda kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kinondoni waliyotumwa.

Kwa upande wa Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya Wananchi.



Share:

MBUNGE MTENGA AWAPA POLE WANANCHI WA JIMBO LA KONDE


MBUNGE wa Jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Mtenga amewapa pole wanafamilia, wananchi wa Jimbo la Konde kisiwani Pemba,wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Chama cha ACT Wazalendo kutokana na kifo cha Mbunge wao, Khatib Said Haji (ACT Wazalendo) kilichotokea jana na maziko yake kufanyika siku hiyo hiyo kisiwani humo.

Ameyasema hayo muda mfupi baada ya taarifa ya kifo cha mheshimiwa Haji kutangazwa bungeni jijini Dodoma Mei 20, 2021 na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Tulia Ackson.

Kifo cha mbunge huyo kilitokea jana alfajiri katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ambapo hivi karibuni hakuweza hakuhudhuria vikao vya Bunge kutokana na kuumwa.

Mheshimiwa Mtenga amesema kuwa, kifo hicho kimekuwa cha huzuni kubwa kwani alikuwa mtu wa watu na alikuwa mcheshi mwenye utani mwingi hali ambayo ilimfanya kuwa na marafiki wengi kwa muda mfupi waliokutana nae bungeni.

‘’Namfahamu vyema ni mbunge ambaye alikuwa na mahusiano mazuri na watu ndani na nje ya Bunge, alikuwa mcheshi mwenye utani na ndani ya bunge alikuwa ni mtetezi mzuri wa chama na mtu wa msimamo,’’amesema Mbunge Mtenga.

Amesema kuwa,amesikitika sana kutokana na kifo hicho na imekuwa ni kilio kwa wabunge wote kwani pia alikuwa kati ya wabunge ambao hajafungamana na chama chochote.

"Marehemu wakati wa uhai wake alikuwa ni kiongozi kwenye jamii kwani alikuwa haegemei upande wowote huku akitoa hoja za mashiko kwa maslahi ya nchi yetu na kuwatetea watu mbalimbali katika jamii,"ameongeza Mtenga.
Share:

Tanzia: JENERALI TUMAINIEL KIWELU (MST) AFARIKI DUNIA



Share:

WAKULIMA WATAKIWA KUBADILI FIKRA NA KUANZA KULIMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI


Mhandisi Christpher Mashalla 

Ili kuhakikisha wakulima mkoani Shinyanga wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini wakulima wametakiwa kubadili fikra na kuanza kulima kilimo cha umwagiliaji.

Wito huo umetolewa  leo Mei 20, 2021 na Mhandisi wa kilimo na
umwagiliaji mkoa wa Shinyanga,mhandisi Christopher Mashalla wakati akizungumza na Malunde 1 Blog ofisini kwake.

Ameeleza kuwa zaidi ya Sh. Bilioni 4 zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji katika kata ya Nyida halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa mradi wa Skimu ya umwagiliaji Mwamalili katika halimashauri ya manispaa ya Shinyanga.

Mashalla amsema kuwa baada ya kuanzisha ofisi ya kilimo na
 umwagiliaji mkoa wa Shinyanga wameweka mkakati madhubuti wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa wananchi kulima kilimo cha umwagiliaji pamoja na kuainisha maeneo maalumu watakayojenga Skimu za umwagiliaji katika mkoa wa shinyanga

Aidha  amesema kuwa iwapo watapata fedha hizo wataweza kujenga na kukarabati miradi hiyo hali itakayo wapa fursa wananchi wengi kuchangamkia.
Share:

Media Buyer at kazini kwetu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

MEDIA BUYER We are seeking a highly motivated Media Buyer with 2-4 years of experience to join our team. You will work closely with cross-discipline client account teams in meeting and exceeding client goals. Responsibilities: Actively manage paid social campaigns to the clients’ goals – which may vary from engagement, acquisitions, direct response, reach and […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Country Manager at AfDB

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

THE BANK: Established in 1964, the African Development Bank is the premier pan-African development institution, promoting economic growth and social progress across the continent. There are 81 member states, including 54 in Africa (Regional Member Countries). The Bank’s development agenda is to deliver the financial and technical support for transformative interventions that will significantly reduce […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger