Monday, 17 May 2021

IGP Sirro Amvalisha Cheo Cha Ukamishna, Salum Hamduni kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemtaka kamishna Salum Hamdun kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa kiapo chake na kuhakikisha anasimamia sheria na taratibu za nchi ikiwa pamoja na kuwatendea haki wananchi atakaowahudumia.

IGP Sirro amesema hayo wakati akimvalisha Cheo cha Ukamishna wa Polisi CP Salum Hamdun kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya Mhe. Rais kumpandisha cheo hicho.

Hata hivyo, IGP Sirro wakati akimvalisha cheo cha Ukamishna pia alimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kitabu cha muongozo kinachoongoza Jeshi hilo.

Naye Kamishna mteule CP Salum Hamduni amesema kuwa, ataendelea kutenda kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo na kwamba atahakikisha anawatendea haki Watanzania kwa kulinda usalama wao na mali zao.

Kwa upande wake Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa uaminifu ili kuhakikisha Jeshi linaendelea kujijengea heshima kwa wananchi.

Awali kabla ya kupandishwa cheo hicho na Mhe. Rais, Kamishna Salum Hamdun alikuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam akiwa na Cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi.

Share:

FAMILIA YATAKA KUJUA ALIPO MUUZAJI WA COMPUTER DENNIS ALIYEPOTEA KWA SIKU 48

Fundi Computer & CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo)
Dada wa Dennis Richard Katangwa Bi. Winfrida Kalubale (kulia) na Baba Mzazi wa Dennis Bwana Richard Katangwa wakizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Mei 17,2021 katika ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC)

Ofisi ya Fundi Computer & CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo)
Fundi Computer & CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo) akiwa ofisini kwake

Fundi Computer &CCTV Camera na Muuzaji wa  Computer Dennis Richard Katangwa (aliyepotea/hajulikani alipo) akiwa kwenye gari lake aina ya Vitiz lenye namba za usajili DFY 863

Na Shinyanga Press Club Blog

FAMILIA ya kijana Dennis Richard Katambwa (31) mkazi wa Bushushu wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga imeiomba Serikali kuingilia kati ili kujua hatma ya mtoto wao  huyo aliyepotea tangu Machi 31, mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha.

Kijana huyo ambaye ni fundi maarufu wa Kompyuta mjini Shinyanga lakini pia anajihusisha na kufunga kamera za CCTV pamoja na kuuza kompyuta na vifaa vyake, alipotea Machi 31, mwaka huu akiwa na gari lake na hajaonekana hadi sasa licha ya jitihada za familia hiyo kumtafuta kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

Hata hivyo, Mapema mwezi huu inaelezwa kuwa Gari la kijana huyo lenye namba za usajili DFI 863 VITZ rangi ya blue bahari lilipatikana  katika kijiji cha Natta wilayani Nzega likiwa limetelekezwa ambapo ndugu wa kijana huyo walipigiwa simu Mei 5,2021 kuhusu kuonekana kwa gari hilo.

Akizungumza leo Mei 17,2021 na Waandishi wa Habari katika ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Dada wa Dennis, Winfrida Kalubale akiwa ameambatana na baba mzazi wa kijana huyo, Richard Katangwa amesema kuwa siku ya Machi 31, 2021 ndugu yao akiwa kwenye mazingira yake ya kazi asubuhi alienda kupokea mzigo wa Computer eneo la washusha mizigo mbalimbali kutoka Dar es Salaam (Shy elimu) mtaa wa Makongoro mjini Shinyanga na kuufikisha ofisini na kumwambia kijana anayemsaidia kuuza dukani aupange mzigo huo, kisha yeye akaondoka na flash akasema anarudi.

Lakini baada ya takribani dakika 45 gari lake lilirudi na watu wawili mwanamke na mwanaume ambao hawakushuka kutoka kwenye gari, wakafika karibu na ofisi kisha Dennis akampigia kijana wake awapatie laptop na Sh. 10,000.

“Kijana akawapelekea kwenye gari wakashusha kioo wakachukua. Kazi zikaendelea lakini baadae wateja wakiwa wanakuja wanalalamika hawampati Dennis na simu hapokei, ilipofika jioni kijana akawa na mashaka kwamba kwanini boss wake hapokei simu, ikabidi aende nyumbani kuangalia akakuta Jirani nae analalamika kwamba wanampigia simu hawampati maana kaacha bomba chumbani linamwaga maji.

“Asubuhi simu ikawa inapigwa inaita tu lakini haipokelewi na sms hazijibiwi. Rafiki yake mmoja akaona simu yake iko mtandaoni (online) akamtumia sms kwamba mbona unatafutwa hupatikani baadae ile simu ikapotea hewani,” ameeleza Winfrida.

Akisimulia kwa masikitiko, Winfrida aliendelea kwa kueleza kuwa jitihada za kumtafuta ziliendelea na baadhi ya ndugu walikuja ndipo wakapata wazo la kwenda kuvunja mlango wa nyumbani kwake, ambako waliingia ndani lakini wakakuta kila kitu kiko sawa ndani ya nyumba.

"Tukaendelea na juhudi za kumtafuta, simu ikawa hewani mara inapotea, baada ya masaa 24 tukaenda polisi ambao mpaka leo wanaendelea kufuatilia. Leo ni siku ya 48 hajaonekana na hatujui alipo, tunaomba serikali iingilie kati ili tujue kijana wetu yuko wapi", amesimulia.

Wakiwa bado wako njia panda na huzuni kubwa, Jumatano ya Aprili 4, mwaka huu walipokea simu na kuelezwa kuwa gari la ndugu yao aliyepotea limeonekana wilayani Nzega mkoa wa Tabora  ndipo walipofanya juhudi za kufuatilia kujiridhisha na kubaini kuwa ndilo gari lenyewe wakawasiliana na Jeshi la Polisi Nzega ambapo ulipofanyika utaratibu wa kulirudisha Shinyanga na mpaka sasa lipo katika kituo cha Polisi Shinyanga.

Amesema tayari familia hiyo imetoa polisi taarifa ya kupotelewa ndugu yao na kuandikiwa RB namba SHY/RB/1385/2021 ambayo walipewa Aprili Mosi, mwaka huu.

Share:

Tanzania Yaendelea Kufanya Vyema Utawala Bora, Haki Za Binadamu

Na Mwandishi wetu, Dar
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika viwango vya Utawala Bora na Haki za Binadamu hususani katika maeneo ya haki za kijamii pamoja na haki za kisiasa.

Mwenyekiti wa Tume hiyo (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) na kuongeza kuwa licha ya uwepo wa baadhi ya maeneo ya maboresho kwa sasa Tanzania iko katika daraja “A” miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika masuala ya Utawala Bora na Haki za Binadamu.

“Licha ya uwepo wa baadhi ya maeneo ya maboresho kwa sasa Tanzania iko katika daraja “A” miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika masuala ya Utawala Bora na Haki za Binadamu,” amesema Jaji Mwaimu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuishauri Serikali katika kuzingatia na kutekeleza masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama ilivyoridhia katika majukwaa ya kimataifa.

“Naipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kutekeleza majukumu yake vizuri ikiwemo kuishauri Serikali katika kuzingatia na kutekeleza masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama ilivyoridhia katika majukwaa ya kimataifa,” amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya Tanzania ni mwanachama katika tume nyingine za kikanda na kimataifa ambazo hupima viwango vya utekelezaji wa Haki za binadamu na Utawala Bora ambapo kwa sasa Tanzania ina kiwango “A”.

Share:

TECHNICIAN II at TATC/ Nyumbu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), synonymously known as “Shirika la Nyumbu”, was formally established on the 14th December 1985, through a Presidential Order, made under the Public Corporations Act 1969. TATC’s mission is to develop a reputable capacity for automotive engineering by conducting research and innovation, technology transfer and quality assurance services. TATC is wholly […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Engineer II at TATC/ Nyumbu

Prof.makubi Awataka Maafisa Afya Kuwafanyia Vipimo Vya Covid 19 Abiria Uwanja Wa Ndege Wa Julius Kambarage Nyerere

Na.WAMJW-Dsm
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi amewataka maafisa Afya katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na makampuni ya kifedha yanayotoa huduma za kupokea malipo kwa Abiria wanaowasili nchini na kufanyiwa vipimo vya Covid 19, kufanya kazi kwa ushirikiano na ufanisi, ili kuweza kutoa huduma yenye ubora na kutowachelewesha Abiria wanaopatiwa huduma katika Uwanja huo.

Prof Makubi amesema hayo katika ziara yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,yenye lengo la kukagua huduma za upimaji wa Covid 19 kwa abiria wa wanaowasili nchini zinazotolewa na maafisa Afya wa uwanja huo na kuangalia changamoto zinazopelekea kuwepo kwa ucheleweshaji wa huduma kwa abiria hao kama zimefanyiwa kazi.

Katibu Mkuu amesema kitendo cha kuchelewesha kutoa baadhi ya huduma kwa baadhi ya abiria wanaowasili nchini kamwe hakivumiliki, hivyo watendaji wanaohusika wajaribu kuondoa vikwazo vinasababisha kuchelewesha huduma hizo, ambazo zimekuwa kero kwa baadhi ya abiria wanaowasili nchini na kutakiwa kufanyiwa vipimo vya Covid 19 uwanjani hapo.

“Kweli kuna ucheleweshaji unaoweza kufanyika na mtu akakuvumilia wala asikereke lakini ikishafika masaa mawili hiyo haikubaliki, hebu tuondoe hivi vikwazo vinavyosababisha huduma kuchelewa ili wananchi waweze kupata huduma na tusionekane kero kwao” Alisema Prof Makubi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale amemuondoa hofu katibu Mkuu katika kusimamia huduma zinazotolewa katika Uwanja huo, ambapo amesema atahakikisha anasimamia maafisa Afya uwanjani hapo na kuhakikisha wanatoa huduma sahihi na watashirikiana na wadau wengi katika kuhakikisha wageni wanaoingia nchini wanapata huduma zenye kiwango cha ubora wa juu.

Share:

Assistant Lecturers 02 Posts at Mbeya University

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES – RE-ADVERTISED Mbeya University of Science and Technology (MUST) is a result of the transformation of the Mbeya Institute of Science and Technology (MIST) through the Universities Act No.7 (2005) and Charter of Mbeya University of Science and Technology, 2013 with the aim of becoming the leading centre of excellence for knowledge, skills […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Art/Drama/Music Teachers at The Latham School

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

WE ARE HIRING! positions for august 21. Position Title: Art/Drama/Music Teachers Minimum Teaching Requirements: Bachelor’s degree in Education 3-5 years teaching experience International curriculum experience HOW TO APPLY Email us your CV and cover letter only recruitment@thelathamschool.com Deadline: May 30,2021 Preference will be given to qualified Tanzanian candidates, and those already in country Only shortlisted candidates will […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

CCM WASHINDA UBUNGE JIMBO LA BUHIGWE NA MUHAMBWE

Mshindi wa uchaguzi mdogo wa ubunge, jimbo la Muhambwe kupitia CCM, Dkt. Florence Samizi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe, Bi. Marycelina Mbehoma (kulia), akimkabidhi Cheti cha ushindi mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Buhigwe, Felix Kavejuru.
***
Uchaguzi mdogo katika majimbo mawili ya Muhambwe na Buhigwe yote ya mkoani Kigoma, ambao ulifanya Mei 16, 2021 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi kuibuka na ushindi katika majimbo yote.

Msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Muhambwe, Bw. Diocles Rutema amemtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Florence Samizi kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 23,441.

Aliyefuatia ni mgombea wa ACT Wazalendo Bw. Masabo Julius aliyepata kura 10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP), Bw. Philipo Fumbo aliyepata kura 368.

Aidha msimamizi wa Uchaguzi wa ubunge Jimbo la Buhigwe, Bi. Marycelina Mbehoma amemtangaza Felix Kavejuru wa Chama Cha Mapinduzi, kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 25,274 kati ya kura 30320 halali zilizopigwa.

Felix Kavejuru amewashinda wapinzani wake 12 alioshiriki nao katika Uchaguzi mdogo uliofanyika Mei 16,2021.

Uchaguzi katika jimbo la Muhambwe umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM marehemu Atashasta Justus Nditiye aliyefariki mwezi Februari.

Kwa upande wa Jimbo la Buhigwe uchaguzi umefanyika baada ya aliyekuwa mbunge Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Share:

DKT FLORENCE SAMIZI (CCM) ASHINDA UBUNGE JIMBO LA MUHAMBWE

Mgombea wa CCM, Dkt. Florence Samizi ameibuka mshindi uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe. Awali, jimbo hili lilikuwa likiwakilishwa na marehemu Mhandisi Atashasta Nditiye.

Dkt. Samizi ameshinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 23,441 kati ya kura 35,339 sawa na asilimia 68 akifuatiwa na Mgombea wa Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Bw. Masabo Julius aliyepata kura 10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP), Bw. Philipo Fumbo aliyepata kura 368.

Share:

KAVEJURU FELIX (CCM) ASHINDA UBUNGE JIMBO LA BUHIGWE

 Felix Kavejuru (CCM) ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Buhigwe uliofanyika jana Jumapili Mei 16, 2021.

Akitangaza matokeo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 17, 2021 msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Marrycelina Mbehoma amesema Kavejuru amepata kura 25,274 akifuatiwa na mgombea wa ACT-Wazalendo, Garula Tanditse aliyepata kura 4,749.

Amebainisha wapiga kura walioandikishwa ni 112,333 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 30,713. Amesema kura halali zilikuwa 30,320 na zilizoharibika 593.

Share:

Primary Teachers at The Latham School

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

WE ARE HIRING! positions for august 21. Position Title: Primary Teachers Minimum Teaching Requirements: Bachelor’s degree in Education 3-5 years teaching experience International curriculum experience HOW TO APPLY Email us your CV and cover letter only recruitment@thelathamschool.com Deadline: May 30,2021 Preference will be given to qualified Tanzanian candidates, and those already in country Only shortlisted candidates will […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Deputy Head (Bahari & Masaki) at The Latham School

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

WE ARE HIRING! positions for august 21. Position Title: Deputy Head (Bahari & Masaki) Minimum Teaching Requirements: Bachelor’s degree in Education 3-5 years teaching experience International curriculum experience HOW TO APPLY Email us your CV and cover letter only recruitment@thelathamschool.com Deadline: May 30,2021 Preference will be given to qualified Tanzanian candidates, and those already in country Only […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Head of Schools at The Latham School

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

WE ARE HIRING! positions for august 21. Position Title: Head of Schools Head of Schools Minimum Requirements: Masters degree in Education 5-10 years school leadership experience 3-5 years international experience HOW TO APPLY Email us your CV and cover letter only recruitment@thelathamschool.com Deadline: May 30,2021 Preference will be given to qualified Tanzanian candidates, and those already in […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

5 Job Opportunities At Makambako Town Council

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Makambako Town Council is a medium-sized town and ward in the Njombe Region of the Tanzanian Southern Highlands, located roughly 40 miles north of Njombe city by road. It is located at junction of the A104 and B4 roads between Njombe, Iringa, and Mbeya. Its population according to the 2002 Tanzanian census is 51,049. Makambako […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Head of Sales and Marketing at Marie Stopes Tanzania (MST)

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

CAREER OPPORTUNITIES Marie Stopes Tanzania (MST), a Non-Governmental Organization, is a social enterprise and a leading provider of family planning, sexual and reproductive health care and allied services. MST is a partner of the Government of Tanzania and a member of the Marie Stopes International (MSI) Global Partnership, which operates in over 37 countries worldwide. […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Corporation Secretary at TAZARA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Overview The Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA) is a Statutory Institution owned by the two Governments of the United Republic of Tanzania and the Republic of Zambia on a 50/50 share holding basis. With the registered Head Office being in Dar es Salaam, Tanzania, TAZARAhastwo Regional Administrative Centres —one in Mpika, Zambia and the other in […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger