Monday, 10 May 2021

WAZEE KAHAMA WASHTUKA TAARIFA ZA MAUAJI YA MZEE MAYOMBO SONGO


Katibu wa baraza la wazee Manispaa ya Kahama Underson Lyimo, akizungumza kwenye kikao cha kutathimini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee.

Na Marco Maduhu, Kahama
BARAZA la wazee Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wamelaani tukio la mauaji ya mzee Mayombo Songo (75) mkazi wa Wendele Manispaa hiyo, ambaye aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

Wazee walipaza kilio hicho jana kwenye kikao cha kutathmini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee Manispaa hiyo, kilicho andaliwa na Shirika la TAWLAE  ambalo linatekeleza miradi ya kutetea haki za wazee mkoani Shinyanga.

Katibu wa Baraza la wazee Manispaa ya Kahama Underson Lyimo, alisema mauaji ya wazee yalikuwa yamekwisha, lakini mwaka huu yameanza kuibuka upya, na kuitaka Serikali pamoja na vyombo vya usalama kuyadhibiti ili yasiendelee kutokea.

"Baraza la wazee Manispaa ya Kahama, tunalaani mauaji ya mzee mwezetu ambaye aliuawa kwa kukatwa mapanga usiku akiwa amelala nyumbani kwake na watu wasiojulikana, tunaitaka Serikali na vyombo vya usalama kuyadhibiti ili yasitokee tena,"alisema Lyimo.

Naye Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi wilayani Kahama Elias Sikanda, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wilayani humo, alithibitisha kutokea kwa mauaji ya mzee huyo, na kubainisha kuwa bado wanawasaka watu waliohusika na mauaji hayo.

Pia alisema Jeshi la Polisi wamejipanga vyema kudhibiti mauaji ya wazee yasitokee tena, ambapo wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara kutoa elimu kwa wananchi, juu ya kuthamini wazee na kuacha kutekeleza mauaji dhidi yao.

Naye Afisa miradi kutoka Shirika hilo la TAWLAE Winie Hinaya, alisema jamii inapaswa kuwalinda wazee pamoja na kuwatunza, na siyo kuwaona kama mikosi kwao huku wakiwatuhumu ni washirikina, na kuwa uwa kwa mapanga, kitendo ambacho ni ukeukaji wa haki za binadamu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Katibu wa baraza la wazee Manispaa ya Kahama Underson Lyimo, akizungumza kwenye kikao cha kutathimini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee.
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi wilayani Kahama Elias Sikanda, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wilayani humo kwenye kikao hicho.
Afisa miradi kutoka Shirika la Tawlae Winie Hinaya, akizungumza kwenye kikao hicho na kuelezea mradi wao wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee.
Wazee wakiwa kwenye kikao cha kutathimini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee Manispaa ya Kahama.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea cha kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee kikiendelea.
Picha ya pamoja baada ya kikao kumalizika.

Na Marco Maduhu, Kahama.

Share:

RAIS SAMIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI 5 WALIOTEULIWA KUZIWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI

 

Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea hati za utambulisho za Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha kwa nyakati tofauti hati zao za utambulisho kwa Rais Samia Suluhu Hassan wanatoka katika nchi za Namibia, Msumbiji, Uturuki, Italia na Ireland.

Tukio la Rais Samia Suluhu Hassan kupokea hati hizo za utambulisho kutoka kwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini limefanyika Ikulu jijini Dar es salaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.

Baada ya kupokea hati hizo za utambulisho, Rais Samia Suluhu Hassan kwa nyakati tofauti amefanya mazungumzo na Mabalozi hao.


 

Share:

SERIKALI INAHITAJI SHILINGI TRILIONI NANE KUSAMBAZA UMEME KATIKA VITONGOJI VYOTE


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja akifungua Mkutano wa Kwanza wa Mwaka baina ya REA na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati uliofanyika tarehe 7,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Juliusi Kalolo,akizungumza wakati wa mkutano wa Kwanza wa Mwaka baina ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati uliofanyika Mei 7,2021 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, akizungumza wakati wa mkutano wa Kwanza wa Mwaka baina ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati uliofanyika Mei 7,2021 jijini Dodoma.

**********************

Na Jaina Msuya - REA

Serikali inahitaji zaidi ya Shilingi Trilioni Nane kwa ajili ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vitongoji ambavyo havijafikiwa na nishati hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo alisema hayo katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati kilichofanyika tarehe 7 Mei 2021.

Wakili Kalolo alisema kuwa kazi ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vijiji vilivyobaki inaenda sambamba na kupeleka umeme katika vitongoji kupitia miradi ya ujazilizi.

"Vijiji vilivyobaki ni vichache hivyo kwa wakati huu pia tunaendelea na zoezi la kupunguza idadi ya vitongoji ambavyo havina umeme" alisema.

Akizungumzia lengo la kikao hicho, Wakili Kalolo alisema kuwa ni pamoja na REA kuwasilisha Mpango Kazi wa Mwaka ujao wa Fedha pamoja na Mpango wa Miaka Mitano wa REA kwa ajili ya kujadiliwa na Wabia wa Maendeleo kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa mipango hiyo.

"Moja ya mambo tunayotarajia katika kikao hiki ni ahadi kutoka kwa wafadhili kuhusu utayari wao wa kusaidia katika baadhi ya maeneo. Ni muhimu tujenge hoja zinazokidhi vigezo vyao vya kupata ufadhili," alisema Wakili Kalolo.

Awali, akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini umeongeza fursa za uwekezaji katika maeneo ya vijijini. Alitoa wito kwa wananchi kutumia umeme kwa ajili ya shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanzisha biashara ndogo ndogo na za kati pamoja na viwanda.

"Umeme ni nyenzo muhimu kwa ajili ya maendeleo, ukiwa na umeme fursa nyingi za biashara zinafunguka," alisema.

Mhandisi Masanja alitoa wito kwa viongozi wa vijiji na mitaa kuwahamasisha wananchi kutoa maeneo yao kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya kusambaza umeme pamoja na kutoa ushirikiano kwa kutunza na kulinda miundombinu hiyo.

"Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana katika kusambaza umeme vijijini. Mwaka 2015 ni vijiji takribani 2,000 tu vilikuwa na umeme, lakini leo tunazungumzia vijiji 10,400 vyenye umeme kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara," alisema

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Jones Olotu aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuunganishiwa umeme ili waweze kuanzisha miradi mbalimbali itakayowainua kiuchumi.

Mhandisi Olotu alisema katika baadhi ya maeneo mwitikio wa wananchi kuunganisha umeme bado upo chini na kuwataka kuunganisha umeme kwa bei nafuu ya Shilingi elfu 27.

Kwa wale wasioweza kumudu gharama za kutandaza nyaya katika nyumba zao aliwahamasisha kutumia kifaa maalum kijulikanacho kama Umeme Tayari ambacho ni mbadala wa _wiring_.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Wabia hao wa Maendeleo, Børjn Midthun aliipongeza REA kwa kazi nzuri ya kusambaza nishati vijijini na kuongeza kuwa imefungua fursa ya uwekezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Share:

Waziri Mkuu Atoa Maagizo Kwa Wizara Ya Habari Kuhusu Sakata la Mechi ya Simba na Yanga Kuahirishwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa juu ya sakata la mechi ya watani wa jadi timu za Simba na Yanga uliokuwa uchezwe katika Uwanja wa Mpira wa Mkapa jijini Dar es Salaam, juzi Jumamosi, Mei 8, 2021.

Kauli hiyo ameitoa leo May 10, 2021 baada ya kipindi cha kutambulisha wageni waliotembelea Bunge .

Amesema baada ya kuahirishwa wa mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga uliotakiwa kuchezwa Mei 8 mwaka huu kulisababisha manung’uniko katika mitandao ya jamii lakini pia kutojua hatima ya waliolipa kiingilio katika mchezo hu

“Kufuatia kero hiyo, tayari tumeagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha wanatoa taarifa haraka sana kwa Watanzania mchezo wenyewe utachezwa lini lakini kuna viingilio ambavyo walikuwa wametoa hatma yake nini,” amesema.

Amesema wizara hiyo inatakiwa kutoa taarifa hiyo kwa kushirikiana na chombo kinachosimamia mchezo huo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania kuwa  wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo.



Share:

Picha : THRDC YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI...MCT, TEF, UTPC WAMLILIA RAIS SAMIA KUFUTA SHERIA ZINAZOLALAMIKIWA


Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendesha semina kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.


Semina hiyo ya Siku tatu iliyoanza leo Jumatatu Mei 10,2021 katika ukumbi wa Nashera Hoteli mkoani Morogoro imekutanisha pamoja waandishi wa habari mtandaoni kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.


Katika Semina hiyo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) wameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, iondoe sheria zote kandamizi zinazoathiri uhuru wa vyombo vya habari.


Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga ametoa ombi la kufutwa kwa sheria zinazolamikiwa, wakati akizungumzia agizo la Rais Samia, alilolitoa hivi karibuni la kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa kutokana na sababu mbalimbali.


Amesema agizo la Rais Samia sio suluhu ya changamoto ya vyombo vya habari kufungiwa na kuminywa visifanye kazi zake kwa uhuru, bali inatakiwa sheria zibadilishwe ili uhuru wa vyombo vya habari uenziwe na viongozi watakaofuata.


"Rais Samia akiapisha Makatibu Wakuu, aliongelea kidogo suala la uhuru wa habari na aliagiza vyombo vifunguliwe. Hili lina mjadala sababu wengine tulisikia ametamka vyombo vya habari lakini wasaidizi wake wamesema agizo lilihusu vyombo ya habari vya mtandaoni. Kwa sababu ofisi yake haijatoa kauli juu ya tarifa ya wasaidizi wake hao, agizo la kufunguliwa mtandaoni bila shaka hilo ndiyo sahihi," amesema Mukajanga.


"Tunadhani bila kushughulikia sheria zinazoongoza, zinazosimamia na kudhibiti kazi zetu, tatizo halitaweza kuondoka. Kwa nia njema hiyo, anaweza akaamua kama hivyo mfungulieni flani, lakini kama sheria ipo maana yake kesho anaweza pata tatizo mtu mwingine au yuleyule aliyefunguliwa akapata tatizo kutokana na sheria zile zile," amesema Mukajanga.


Naye Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF) Deodatus Balile amesema, mchakato wa mabadiliko ya sheria za mtandaoni umeanza kufanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuwaomba wadau kujitokeza kutoa maoni


Amesema kauli ya Rais Samia haikusema vyombo vya habari vya mtandaoni, "alisema vyombo vya habari vilivyofungiwa, vifunguliwe" na akagusia suala la kanuni ziwe wazi hivyo mkanganyiko ulikuja kwa watendaji wa Rais Samia wamekuwa waking'ang'ana ni vya mtandaoni pekee jambo ambalo linaendeleza mjadala wa agizo hilo la Rais.


"Bila kushughulikia sheria,zinazodhibiti kazi zetu changamoto hazitaondoka. Mchakato wa mabadiliko ya sheria tayari umeanza. Vyombo vya habari mtandaoni tunaomba tushiriki kwani TCRA imeanza, tukatoea mawazo yetu," amesema Balile.


"Hivi sasa kazi zenu zina walaji wengi, mnafikia watu wengi sana hivyo ni muhimu Online Journalism iende vizuri kwa kusimamiwa vizuri, na wanaosimamia online wanatakiwa kuwa watu wazuri. Sisi waandishi wa habari, tuonyeshe weledi kidogo katika kuhabarisha umma",ameongeza.


Naye Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo amesema ni vyema Sheria na kanuni kandamizi katika tasnia ya habari ziondoshwe ili uhuru wa kujieleza uwepo.

Kwa upande wake Mratibu wa THDRC, Onesmo Ole Ngurumwa alisema, semina hiyo ina lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mtandaoni ambao ni eneo linalokuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni na kutokana na uwepo wa sheria mbalimbali kandamizi kwa eneo la usimamizi wa vyombo vya habari, wamefungua kesi mahakamani ya kuzipinga.

Amesema mwisho wa mafunzo hayo ya siku tatu, yatawafanya waandishi wa habari wa mitandoni kuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali ili waweze kutimiza majukumu yao kwa weledi.

"Lengo la semina hii ni kuwajengea uwezo ili wafanye kazi vizuri katika kuhabarisha watanzania kwa sababu watu wengi wamehamia mtandaoni. Kundi hili la waandishi wa habari mtandaoni ni muhimu kulisaidia ambapo mpaka sasa vyombo vya habari mtandaoni vilivyosajiliwa ni zaidi ya 400 hivyo kuna wimbi la ukuaji",amesema.

"Siyo kila mtu anayeendesha mtandao ni mwandishi wa habari. Siyo kila mtumiaji wa Youtube Channel ni mwandishi wa habari,baadhi yao hawana taaluma ya habari, lakini siyo kila mtu mwenye channel anapaswa kusajili TCRA. Vyombo vya habari vya mtandaoni zimetungiwa sheria na kanuni za kujiendesha. Tuendelee kupigia kelele kanuni hizi ili tupate kanuni rafiki”,ameongeza Ole Ngurumwa.

 TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF) Deodatus Balile akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF) Deodatus Balile akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
Mratibu wa THDRC, Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
Mratibu wa THDRC, Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
 
Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
Mwandishi wa Habari Salma Said kutoka Zanzibar akizungumza leo Jumatatu Mei 10,2021 kwenye Semina kwa Waandishi wa habari Mtandaoni iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu.
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini
Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini

Waandishi wa habari Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ukumbini

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Weighbridge Operator at TANROADs

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Tanzania National Roads Agency (TANROADS) is an Executive Agency under the Ministry of Works Transport and Communication, established under section 3 (1) of the Executive Agencies Act (Cap 245) and came into operation in July, 2000. The Agency is responsible for the Maintenance and development of the trunk and Regional road network in Tanzania. The […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA VYAKULA VYA FUTARI KWA WATOTO YATIMA KAHAMA


Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akiwakabidhi watoto yatima futari  katika kituo cha Kahama Peace Ophanage Center
Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akimkabidhi tende mtoto, Abbu Malik (5) kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika  Kituo cha Kahama Peace Ophanage Center
Sheikh Alhaj Omary Damka akimkabidhi mfuko wa unga wa ngano Saada Hamis anayelewa katika kituo hicho ikiwa ni mmoja misaada iliyotolewa na benki ya CRDB.
Bi Mariamu Missana mfadhili wa Kituo cha Kahama Peace Ophanance Center akipokea futari kutoka kwa meneja wa benki ya CRDB kanda ya Magharibi Said Pamui.
Mtoto Abbu Malik (5) akiwaombea dua viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu walioambatana na maafisa wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa ajili ya kutoa futari katika kituo hicho.


***
Na Salvatory Ntandu - Kahama

Benki ya CRBD Kanda ya Magharibi imetoa futari kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Kahama Peace Ophanage Center kilichopo katika mtaa wa Mhungula Manispaa ya Kahama ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya dini ya kiislamu ya kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii hususani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akikabidhi futari hiyo leo Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui amesema kuwa kila mwaka katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani benki ya CRDB imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ya futari kwa watu wenye mahitaji kama vile wazee, wagonjwa, watu wenye ulemavu na watoto yatima.

“Mwenye Mungu ameagiza sisi wanadamu kutenda matendo mema katika mwezi mtukufu wa Ramadhani,hususani kuwakirimia wajane, wagonjwa, wazee na mayatima hivyo watu wengine wenye uwezo wa kuwasaidia wahitaji wanapaswa kuiga mfano wa benki ya CRDB kwa kuwasaidia watoto yatima ambao wanahitaji uangalizi wa karibu,”alisema Pamui.

Pamui ameahidi benki ya CRDB kuendelea kushiriana na uongozi wa kituo hicho ili kuhakikisha kero mbalimbali zinazowakabili zinatatuliwa na zile ambazo zipo nje ya uwezo wao atazipeleka kwa mamlaka husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Awali akipokea msaada huo kwa niaba ya uongozi wa kituo hicho shekhe wa wilaya ya Kahama Alhaj Omary Damka ameishukuru benki ya CRDB kwa kutoa futari hiyo kwa watoto yatima kwani imewapa faraja kwa na kuiona bado jamii inawapenda na kuwathamini.

“Benki ya CRDB Kuwafuturisha watoto yatima katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kujipatia thawabu kutoka kwa mwenyezi Mungu niwaombe msikate tama endeleeni kuwasaidia wahitaji mbalimbali katika jamii,”alisema Shekhe Damka.

Kwa upande wake mfadhili mkuu wa kituo hicho, Bi Maimuna Missana Matembe amesema kuwa watoto hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo chakula mavazi na malazi na kutoa rai kwa wadau wengine kuiga mfano wa benki ya CRDB kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili kuwawezesha kujikimu.

“Kituo chetu kinawatoto yatima wapato 25 wenye umri kuanzia miezi mitatu hadi miaka 12,ambao wanalelewa hapa na akinamam ambao wanajitolea kwa hali na mali,tunaomba kusaidiwa kujengewa uzio wa nyumba wanazolala watoto wetu ili kuongeza usalama hususani nyakati za usiku kutokana na eneo letu kutokuwa na uzio,”alisema Missana.


Share:

Consultancy at HakiElimu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

At HakiElimu, we know that change begins with ourselves. Working at HakiElimu is not just a professional experience; it is a personal journey. We support each other in reflecting on and envisioning the change we seek in our individual lives. We take the time to meaningfully examine why we each do this work, what it […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

ASSOCIATE LEGAL OFFICER, P2 at United Nations

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Org. Setting and Reporting The post is located in the Office of the Registrar, Arusha Branch, Registry. Under the supervision of the Deputy Officer-in-Charge and within limits of delegated authority, the incumbent will provide legal and administrative support to the Registrar, Officer-in-Charge and staff of the Office of the Registrar in support of the operations […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Majaliwa: Viongozi Wa Dini Wekezeni Katika Malezi Ya Vijana,ashuhudia Kusimikwa Kwa Askofu, Lushoto Tanga

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini katika mahubiri yao waweke msisitizo katika masuala ya kuwekeza kwa vijana ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vyote hatarishi visivyozingatia maadili ya Mtanzania.

“Tusisahau pia kwamba ukimwi bado upo. Aidha, vijana wengi wapo katika hatari ya kupata maambukizi. Kwa Msingi huo, tumieni nafasi yenu katika jamii kutoa ushauri nasaha na hatimaye kupunguza kasi ya maambukizi kwa vijana”.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Mei 9, 2021) katika ibada ya kusimikwa kwa Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto. Waziri Mkuu ameshiriki ibada hiyo kwa niaba ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Amesema Serikali inatambua na kuthamini kazi na majukumu makubwa ya Viongozi wa Kanisa ambayo ni pamoja na kuwaongoza watu kiroho na kuwapa mafundisho, ushauri na kuwajenga kiimani.

Mheshimiwa Majaliwa amesema “Hubirini masuala ya vijana kwani kauli yenu inapokelewa vizuri kwenye jamii na watu wa rika zote. Endeleeni kuwasaidia watu katika shida mbalimbali hususan wale wenye uhitaji kama yatima na wajane”.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi hao waendelee kutoa mafundisho yenye kuhimiza wananchi wadumishe amani na utulivu nchini kwa manufaa ya vizazi vya sasa na ya vizazi vijavyo.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali inatambua kwamba maendeleo ya nchi hayawezi kwenda bila ya ushirikiano na sekta binafsi na kwa kuzingatia hayo, imekuwa ikishirikiana na Sekta binafsi zikiwemo Taasisi za dini katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi na kuleta maendeleo ya Taifa.

Amesema Serikali imekuwa ikishirikiana na Dayosisi hiyo katika utoaji wa huduma za afya kwenye hospitali zake zilizopo Bumbuli, Kilindi na Lutindi Mental Hospital kwa kutoa dawa pamoja na kuleta madaktari na watumishi ndani ya hospitali hizo ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma stahiki na kwa wakati.

“Nitumie nafasi hii tena kuwahakikishia kuwa Serikali itaendeleza ushirikiano huu kwa manufaa ya Watanzania wote. Nitoe Rai kwa viongozi mnaowekwa wakfu leo kuwa viongozi wa Dayosisi hii ya Kaskazini Mashariki muendelea kuhubiri amani, upendo na mshikamano kwa wana Dayosisi na kwa Watanzania wote kwa ujumla”.

 Hizo ndizo Tunu alizotuachia Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambazo zilitunzwa na kuheshimiwa na viongozi wote waliopita, na zitaendelea kutunzwa katika awamu hii ya uongozi. Vilevile msichoke kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kwa maendeleo ya jamii ya Watanzania”.

Kwa upande wake, Askofu Dkt. Mbilu amemshukuru Waziri Mkuu kwa kushiriki katika ibada na amemuhakikishia kwamba Dayosisi yao itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kudumisha amani


Share:

Uadilifu Kuwezesha Ukuaji Wa Uchumi Wa Blue


Na. Peter Haule, WFM, Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman, amewataka watakaopewa jukumu la kuendesha Boti iliyotolewa kwa Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Kikwajuni kwa ajili shuguli za uchumi wa blue kuwa waaminifu ili kutimiza lengo lililokusudiwa.

Mhe. Waziri Suleimani ametoa rai hiyo kwa niaba ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa Shindano la Kuhifadhi Quran pamoja na kukabidhi Boti kwa Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya elimu Jimbo la Kikwajuni, yaliyoandaliwa na kutolewa na Naibu Waziri Fedha na Mipango, na Mbunge wa jimbo hilo, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni.

Alisema kuwa bila kuwa na uaminifu katika matumizi ya Boti, hakuta kuwa na tija la boti hiyo, hivyo kudidimiza lengo la Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo la kuwapatia ajira vijana kupitia Boti litakalotumika katika shughuli za uvuvi.

“Nimewahi toa Boti mbili tatu kwa ajili ya uvuvi lakini kila nikihitaji kupata mrejesho naambiwa leo baharini hakuingiliki au Samaki hawapatikani, wakati napata taarifa kwa wengine kuwa Samaki wamepatikana, kama hakutakuwa na vijana waaminifu basi mradi huo hautaendelea”, alieleza Mhe. Waziri Suleiman.

Aidha amewataka vijana kujiepusha na vitendo vya utumiaji dawa za kulevya, uzalilishaji na kukosa uaminifu ili miradi hiyo iliyobuniwa iweze kutekelezeka na kuwanufaisha vijana na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge wa jimbo la kikwajuni, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema kuwa Serikali imekuwa ikiweka miundombunu wezeshi kwa wananchi, lakini kutokana na kukosekana kwa uaminifu miundombinu huharibiwa na miradi kufa, hivyo ameamua kutoa Boti kwa Taasisi Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Kikwajuni ambayo inasimamiwa na watu wenye Imani ya Dini ili kukomesha ubadhirifu na kuleta tija stahiki.

Mheshimiwa Mhandisi Masauni amebainisha kuwa Boti na Mashine inathamani ya ya zaidi ya Shilingi milioni 15 na ameikabidhi  Taasisi hiyo pamoja na Shilingi milioni tano ya mradi wa Majongoo Bahari, ili kutekeleza lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la kuwekeza nguvu kwenye uchumi wa Blue.

“Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Kikwajuni imekuwa na shughuli nyingi za kutatua changamoto za elimu kwa kufadhiliwa na watu binafsi kwa ruzuku,  kwa kuwa Serikali inayonia thabiti ya kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi, tumeamua kuifanya taasisi hiyo iweze kujiendesha kwa kiasi kikubwa kwa kutumia miradi yake yenyewe”, alieleza Mhandisi Masauni.

Kuhusu Mashindano ya Kuhifadhi Quran, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mao Zanzibar, Mheshimiwa Mhandisi Masauni, aliwapongeza wote walioshiriki katika mashindano hayo ambayo lengo lake ni kuleta mshikamano na umoja miongoni mwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni na Wazanzibar kwa ujumla.

Alisema elimu ya Dini ni chachu kubwa katika kudumisha amani na uadilifu, hivyo ni muhimu mashindano haya yakaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ili vijana waweze kukabiliana na changamoto ya utandawazi na mambo yasiyo na tija katika jamii

Amewapongeza vijana kwa kuonesha umahiri katika kuhifadhi Quran na kuwataka waendelee na juhudi hizo ili kuwa na kizazi chenye uaminifu si tu katika masuala ya Dini lakini pia katika shughuli za maendeleo ya nchi .


Share:

MASHINDANO MISS DODOMA 2021 YAZINDULIWA



Na Faustine Gimu,Dodoma

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma Mlezi wa Mashindano hayo ya Miss  Dodoma na Morogoro  ambaye pia ni Mbunge wa viti  Maalumu Mkoa wa Morogoro Norah Waziri Mzeru  amesema kuwa jamii itambue Tasnia ya Urembo na Mitindo imekuwa chachu katika kujengewa mabinti uwezo wa kijasiriamali,kijamii na kiutamaduni.

Aidha,Mhe.Mzeru amewaomba viongozi mbalimbali na Taasisi binafsi na za kiserikali hususan  wabunge na wafanyabiashara kuwasaidia mabinti katika tasnia ya urembo na mitindo kuwapatia michango mbalimbali ili kuweza kuendeleza Tasnia ya urembo Nchini.

"Nikiwa kama mbunge wa viti maalumu mkoa wa morogoro katika Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania nawaomba wabunge wenzangu kuchangia Tasnia  ya urembo na Mitindo kwani inatoa Ajira kwa mabinti zetu pamoja na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji nchini",amesema .

Kwa upande wake  mkurugenzi wa NIKALEX LTD Alexander Nikitas ambae pia ni mwandaaji wa mashindano hayo amesema kuwa hii ni fursa kwa mabinti wa mkoa wa dodoma kujitokeza kwa wingi ili kushiriki mashindano haya ambayo yatawapa nafasi za kushiriki Miss Tanzania na  mshindi wa kwanza mpaka wa tatu ndiye atakayepata nafasi  ya kushiriki Miss Tanzania.

"Kabla ya Mashindano haya kufanyika ,Tarehe 21 mwezi wa 6 mwaka huu tutawakutanisha washiriki na  yatahusisha wilaya zote saba za Dodoma hivyo mabinti wote mnakaribishwa kushiriki mashindano haya"amesema Nikitas

Pia  Nikitas amesema jamii itambue kuwa tasnia ya urembo na mitindo  imekuwa chachu katika kuwajengea mabinti kuwa wana jamii wenye kutegemewa wawapo  katika mashindano haya.

Afisa Habari wa Mashindano hayo Ezekiel  Kwakwa amewahakikishia Wanadodoma na watanzania kwa ujumla kuwa mashindano hayo yatakuwa ya haki  na vigezo vyote vitazingatiwa na hakutakuwa na upendeleo wowote.
" Katika mashindano haya haki itatendeka hakuna upendeleo wowote utakaojitokeza"amesemaKwakwa.

Mashindano hayo yameshirikisha Warembo kutoka vyuo mbalimbali mkoani Dodoma na usaili unaendelea katika wilaya zote za Dodoma.

Mashindano ya Miss Dodoma yatahitimishwa Rasmi mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.
Share:

English Language Teacher at Baobab Secondary School

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Baobab Secondary School Management invites applications from suitably qualified teachers to fill in the vacancies available in the following subjects for Advanced level: Position Title: English Language Teacher  General qualifications: A minimum of Bachelor Degree in Education in the relevant area of specialization Teaching experience of at least three (03) years in a reputable Institution. […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

DEREVA WA MASHUA/VIVUKO DARAJA LA II at Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST DEREVA WA MASHUA/VIVUKO DARAJA LA II – 1 POST POST CATEGORY(S) TRANSPORT AND LOGISTICS EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe APPLICATION TIMELINE: 2021-05-07 2021-05-19 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Kufunga na kufungua kamba za mashua/kivuko; ii.Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya mashua/vivuko; iii.Kupanga abiria au magari kwenye mashua/vivuko; iv.Kuendesha na […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Tanzia : MC DICKSON MITUNDWA AFARIKI DUNIA

 

Mshereheshaji (MC) Dickson Mitundwa mkazi wa Shinyanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo

***

TANZIA TANZIA

Kwa masikitiko makubwa kabisa Uongozi wa KISIMA CHA MAFANIKIO unawatangazia kifo cha Mc Dickson Mitundwa kilichotokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Mei 10,2021.

Ikumbukwe Marehemu alisafiri kutoka Shinyanga tarehe 07 na kufika Dsm tarehe 08 mchana kwa ajili ya kuja kumzika baba yake mzazi.

Alifanikiwa kumzika tarehe hiyo hiyo jioni akisindikizwa na baadhi yetu wana KCM huko makaburi ya Kisarawe.

Kesho yake asubuhi tarehe 09.05.2021 alifanikiwa  kushiriki kisomo na dua kwa marehemu baba yake na kumalizia na kikao cha familia akiwa na nduguze wa baba pamoja na mama yao mjane hukohuko Kisarawe.

Marehemu alipanga kurejea mkoani  Shinyanga siku ya leo Jumatatu lakini ghafla saa 5 Usiku jana hali ilibadilika na ndani ya sekunde chache akajisikia kukosa nguvu, na kukimbizwa haraka sana Hospitali, lakini pamoja na juhudi za madaktari ilishindikana kuokoa maisha yake na kufariki dunia.

Mwili wa marehemu Mc Dickson Mitundwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kusubiri mipango ya mazishi.

Tutaendelea kuwapa taarifa za msiba baada ya kikao asubuhi hii kitakachofanyika ukweni Mombasa ila kwa sasa tunaomba utulivu utawale na kama ilivyo ada mwanachama anapofariki , tunatoa rambirambi kwa familia yake kuanzia sh 10,000 na kuendelea.

Mtunza Hazina Christina Matai ndiye mpokea rambirambi na aina yoyote ya mchango na atatuongoza kwa hilo.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA

JINA LAKE LIHIMIDIWE

MC TEN

KATIBU  MKUU - KCM.



Share:

EWURA YABAINI UKIUKWAJI WA SHERIA KATIKA MAMLAKA ZA MAJI

 

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu Mwenendo wa Mamlaka za Maji Katika Utoaji wa Bili za Maji.

......................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji hapa nchini  EWURA imesema imebaini baadhi ya mamlaka za maji kukiuka sheria zinazosimamia mamlaka hizo katika kutoa huduma kwa wananchi ikiwamo kutoza bei ambazo hazijapitishwa na EWURA na ubambikiziwaji wa bili za maji.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati akizungumza na wanahabari amesema baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja waliamua kufanya ukaguzi katika mamlaka 24 kati ya 94 zilizopo.

Amesema katika ukaguzi huo wamebaini mamlaka zote 24 zinamapungufu makubwa katika utoaji huduma kwa wananchi ikiwamo ubora wa mita za maji, taratibu za usomaji wa mita, ukokotoaji wa bili za wateja na utaratibu wa kutatua kero za wateja.

“mnamo January 7, 2021 EWURA ilisimamisha matumizi ya bei zote mpya zilizokuwa zianze kutumika mwaka 2021 kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa maji ikiwamo ubambikiziaji wa bili na usomaji wa mita usiokuwa shirikishi tukaamua kufanya uchunguzi,

“katika uchunguzi huo tumebaini udhaifu katika usomaji wa mita, baadhi ya wasomaji wanakosa umakini na tatizo hili limeonekana kwa mamlaka zote 24 zilizochunguzwa, pia baadhi ya mamlaka kutoza bili za maji kwa kukadiria kutokana na kuharibika kwa mita” amesema Mhandisi Chibulunje.

Amezitaja Mamlaka za maji 24 ambazo wamezifanyia ukaguzi wa kina kuwa ni Kigoma, Bukoba, Babati, Moshi, Arusha, Tanga, Geita, Shinyanga, Kahama, Dodoma, Iringa, Musoma, Mbeya, Njombe, Songea, Vwawa-Mlowo, Mugango-Kiabakari, Bunda, Makambako, Sengerema, Muleba, Mwanhunzi, Gairo na Ngara.

Amesema baadhi ya Mamlaka za maji zimekuwa na uzembe katika usimamizi wa bei za maji zinazotozwa kwa wateja kwenye magati ambapo mamlaka hizo zilibainika bei za juu ya zile zilizoidhinishwa na EWURA mamlaka hizo zikiwa ni Mbeya, Makambako, Songea Tanga, Iringa, Shinyanga, Kahama, Geita Arusha, Moshi, Babati, Ngara na Kigoma.

Pia amesema wamebaini kuwa baadhi ya mamlaka hazitoi taarifa kwa wateja inapotokea kuwepo kwa mgao wa maji na hivyo kuleta usumbufu kwa wateja wao, mamlaka nyingi zimeacha jukumu la kutoa elimu kwa wateja juu ya huduma za maji ikiwamo haki ya mteja.

Ametaja baadhi ya hatua ambazo zimechukuliwa na EWURA katika mamlaka zenye mapungufu kuwa imezipiga faini mamlaka za maji Tanga na Babati kwa kuwauzia wananchi maji kwa bei ambayo haijaidhinishwa na EWURA na kuagiza mamlaka hizo kurudisha fedha za ziada zilizotozwa kwa wateja.

EWURA imezipelekea maagizo mamlaka za maji Mbeya, Songea, Makambako, Mwanhunzi na Gairo na kutaka zijieleze kwanini zisichukuliwe hatua kwa kukiuka maagizo ya EWURA, pia katika mwezi May imeziandikia baadhi ya mamlaka kwa kutoza bei kubwa katika magati.

EWURA imezitaka mamlaka zote kuhakikisha wanafanyia marekebisho katika dosari zote huku akibainisha kuwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Babati, Kigoma na Tanga taarifa zao zitawasilishwa katika mamlaka zao za uteuzi kutokana na kujirudia kwa makosa mara kwa mara.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger