Saturday, 1 May 2021
Picha : MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2021 JIJINI MWANZA
WATUMISHI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WASHIRIKI MAANDAMANO YA MEI MOSI JIJINI DODOMA
BRELA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI
Driver/Messenger at African Union
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
VACANCY ANNOUNCEMENT: DRIVER/MESSENGER (AU ABC) The African Union, established as a unique Pan African continental body, is charged with spearheading Africa’s rapid integration and sustainable development by promoting unity, solidarity, cohesion and cooperation among the peoples of Africa and African States as well as developing a new partnership worldwide. Its Headquarters is located in Addis […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
MUIGIZAJI MAARUFU WA FILAMU MZEE MSIRI AFARIKI DUNIA
Gillie Owino kwa majina yake halisi alifariki dunia Ijumaa Aprili 30,2021 saa chache baada ya kukimbizwa hospitalini.
Kulingana na taarifa kutoka kwa familia yake, Mzee Msiri aliangamizwa na ugonjwa wa saratani.
Mzee Msiri hakuonyesha dalili za kuwa mdhaifu hadi siku zake za mwisho ambazo pia alionekana akiwa studioni akiigiza.
Familia ilisema kwamba marehemu amekuwa akipokea matibabu kwa miaka kadhaa lakini hali yake ilidorora ghafla Alhamisi Aprili 29 ambapo alikimbizwa hospitalini.
Madaktari walijaribu kadri ya uwezo wao kuyaokoa maisha yake lakini Maulana alikuwa ashapanga mpango wake wa kumchukua.
Mzee Msiri alikuwa mwandishi na mkurugenzi wa filamu hasa katika maeneo ya mkoa wa Pwani.
Mashabiki wake watamkosa sana hasa katika kipindi cha Pete ambacho hupeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic.
Kando na kuwa muigizaji, Mzee Msiri pia alikuwa mhasibu mstaafu. Mzee Msiri alijinyakulia tuzo kadhaa katika tasnia ya uigizaji moja ikiwemo ya Sanaa Awards aliyotuzwa mwaka wa 2018.
Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wametuma rambi rambi zao kwa familia, jamaa na marafiki.
Head, Finance and Administration Division at African Court on Human and Peoples’ Rights
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
ADVERTISEMENT OF VACANCY N° AFCHPR/2021/04 HEAD, FINANCE AND ADMINISTRATION DIVISION, P5 AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS The African Court was established by virtue of Article 1 of the Protocol to the African Charter on Human and Peoples’ Rights on the establishment of an African Court on Human and Peoples’ Rights, adopted on 9 June […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Program Coordinator at Pathfinder
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Pathfinder Overview Pathfinder International is driven by the conviction that all people, regardless of where they live, have the right to decide whether and when to have children, to exist free from fear and stigma, and to lead the lives they choose. Since 1957, we have partnered with local governments, communities, and health systems in […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
ITF GHS Project Lab Officer at MDH
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH); Nutrition; Non-Communicable Diseases of public […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
ITF GHS Project Manager at MDH

General Services Driver at MDH

Serikali Yafunga mtambo wa kisasa JKCI wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6
Serikali imefunga mtambo wa kisasa wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 wa uchunguzi na matibabu ya moyo (Catheterization Laboratory – Cathlab) uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System ambao unauwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.
Fedha za kununuliwa kwa mtambo huo ambao umefungwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zilitolewa na Serikali mwanzoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema mtambo huo umeshaanza kutumika, licha ya kutibu mfumo wa umeme wa moyo pia utafanya uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo, kuweka vifaa visaidizi vya moyo pamoja na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba.
“Tunaishukuru Serikali kwa kuiwezesha JKCI na kufunga mtambo huu wa kisasa ambao unauwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.Kufungwa kwa mashine hii yenye teknlologia ya hali ya juu kutaweza kuokoa maisha ya watu wengi wenye matatizo ya moyo ikiwemo mfumo wa umeme wa moyo hapa nchini ”,.
“Tuna wagonjwa wengi ambao mfumo wa umeme wa moyo umekuwa haufanyi kazi vizuri hii ikiwa ni pamoja na hitilamu ya mfumo wa umeme wa moyo ambao mapigo yake ya moyo yanakwenda haraka kuliko kawaida ambao tulikuwa tunawasafirisha kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutibiwa huku wengine wachache wakipatiwa matibabu hapahapa nchini”, alisema Prof. Janabi.
Prof. Janabi alisema mtu akiwa na tatizo katika mfumo wa umeme wa moyo ambalo anaweza kulipata kwa kuzaliwa nalo au athali ya ugonjwa linapelekea mfumo wa umeme wa moyo kubadili mapigo yake inaweza kuwa chini ya 60 kwa dakika na hivyo kusababisha mapigo kuwa chini sana au kuwa juu ya 100 kwa dakika na hivyo kuufanya moyo udunde kwa haraka. Kwa kawaida mapigo ya moyo huwa ni 60 hadi 100 kwa dakika.
Mkurugenzi huyo Mtendaji ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kupitia utaalam wanaoendelea kuupata kutoka kwa wenzao wa nchi za nje ambao wamewatangulia katika matibabu ya moyo pamoja na kusimikwa kwa mtambo huo wataweza kuwatibu wagonjwa hao hapa nchini
“Kwa upande wa wataalamu tunao wa kutosha kwani kuna ambao tumewasomesha nchini China na Afrika ya Kusini pia kupitia kambi mbalimbali za matibabu ya moyo ambazo tunazifanya kwa kushirikiana na wenzetu wa nje ya nchi ambao wanautaalamu mkubwa zaidi yetu kutatusaidia kupata utaalamu wa kutosha na wa kisasa”, alisema Prof. Janabi.
Kwa upande wake Hassan Ally kutoka kampuni ya Biosense webser ambao ndiyo wafungaji wa mtambo huo alisema katika nchi za Afrika ya Mashariki mtambo huo ni wa pili kufungwa hapa nchini ambapo mtambo wa kwanza ulifungwa katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Mombasa nchini Kenya.
Alisema mtambo huo una teknolojia mpya na ya kisasa ambayo hivi sasa inafanyika katika matibabu ya moyo Duniani na kuzitaja nchi zingine ambazo zimefunga mtambo huo katika bara la Afrika kuwa ni pamoja na Afrika ya Kusini na Misri.
“Tumeshatoa na tutaendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Taasisi hii ili wajue jinsi ya kuutumia mtambo huu na tutaendelea kutoa mafunzo hayo kwa nchi zote za Afrika ambazo zimefunga mtambo huu wa kisasa ambao unateknolojia mpya hapa Duniani”, alisema Ally .
Naye daktari mwanamke pekee hapa nchini ambaye ni mtaalamu mbobezi wa moyo na mzibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Honoratha Maucky alisema kufungwa kwa mtambo huo kutawasaidia kutoa huduma nyingi zaidi kwa wagonjwa na kuweza kuokoa maisha yao.
Dkt. Maucky alisema tatizo la mfumo wa umeme wa moyo ni moja ya magonjwa wanayokutana nayo kila siku hivyo basi kuwepo kwa mtambo huo kutawasaidia kutoa huduma kwa wakati kwa wagonjwa wenye matatizo hayo.
“Teknolojia ya matibabu ya moyo inakuwa kila siku kama mnavyoona tumefungiwa mtambo ambao unateknolojia mpya na ya kisasa hivyo basi ni muhimu kwa daktari kutenga muda wako ili uweze kujifunza kwa njia ya mtandao au kupitia kwa wenzetu ambao wameendelea kimatibabu kuliko sisi kwa kufanya hivyo hautakuwa nyuma ya teknolojia ya matibabu”, alisisitiza Dkt. Maucky.
Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo aanza kazi, aongoza kikao cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM
Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, jana jioni ameripoti ofisini na kuendesha kikao maalum cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.
Kikao hiko kimehudhuriwa na Wajumbe wapya akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), -Christina Mndeme na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Viongozi wastaafu wa CCM wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), – Rodrick Mpogolo na aliyekuwa Katibu wa NEC, Oganaizesheni Pereira Silima.
Chongolo amechaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Bashiru Ally.
Kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, Chongolo alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.