Thursday, 8 April 2021

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo April 8



Share:

Wednesday, 7 April 2021

Serikali Yasema Televisheni za mtandaoni tu ndizo zitakazofunguliwa

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amefafanua taarifa ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa hivi karibuni kuhusu kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyofungiwa.

Msigwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online Tv) tu ndio zifunguliwe na sio vyombo vya habari vingine yakiwemo Magazeti yaliyofungwa kwa mujibu wa Sheria.


 

 


Share:

Tanzania Kubeba Ajenda Ya Masoko Uenyekiti Umoja Wa Nchi Wazalishaji Wa Almasi Afrika


 Asteria Muhozya na Steven Nyamiti, Dodoma
Tanzania inatarajia kubeba Ajenda ya Kuanzishwa kwa Masoko ya Madini kwa Nchi Zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika mara baada ya kupokea Uenyekiti wa Jumuiya hiyo lengo likiwa ni kuziwezesha nchi hizo kuuza madini yao kwenye masoko ya ndani ikiwemo kuyaongezea thamani .

Hayo yamebainishwa Aprili 7 jijini Dodoma na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Saba (7) wa Mawaziri wa nchi Zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika ( African Diamonds Producers Association- ADPA) ambao unatanguliwa na mkutano wa Wataalam kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Ameeleza kuwa, faida ya Tanzania kuwa Mwenyekiti ya Jumuiya hiyo kutaipa nafasi ya kusukuma agenda muhimu zinazohusu sekta ya madini ikiwemo kuziita nchi hizo kutumia masoko ya madini yaliyoanzishwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Ameongeza kuwa, katika kipindi chake cha Uenyekiti kama nchi, itazishawishi nchi wanachama kuwa na mfumo wa Kisheria unaofanana ili kuziwesha kunufaika na rasilimali madini ikiwemo kuzilinda.


‘’ Faida ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hii ni kuingiza mawazo yetu kwenye jamii kubwa. Tutatumia uzoefu wetu kutangaza fursa za kibiashara kwenye sekta ya madini na lengo letu likiwa ni kuifanya Tanzania kuwa Hub ya biashara ya madini kwa sababu tuna kila sababu ya kufanya hivyo,’’ amesema Waziri Biteko.

Akizungumzia hali ya sasa ya uzalishaji wa madini ya almasi nchini, amesema kuwa, kama nchi inao Mgodi mmoja mkubwa wa Almasi wa Williamson Diamond Limited (WDL) uliopo eneo la Mwadui Mkoani Shinyanga ambapo uzalishaji wake kwa mwaka umefikia Carat Laki 497 ukiwa ni uzalishaji mkubwa ukilinganishwa na uzalishaji mkubwa wa mwisho uliofanyika mwaka 1977 ambapo zilizalishwa Carat Laki 370.

‘’Kipindi cha janga la ugonjwa wa Corona bei ya almasi ilishuka na sehemu ya mgodi ilifanyiwa matengenezo. Hapa nchini, soko la almasi lipo mkoani Shinyanga na Dar es Salaam lakini soko la dunia liko Antwerp nchini Ubelgiji. Ukizungumzia mapato ya madini yanayoongoza ni dhahabu, inafuata almasi na madini ya ujenzi,’’ ameeleza Waziri Biteko.

Mgodi wa Almasi wa WDL ni mgodi wa ubia ambapo Serikali inamiliki hisa asilimia 25 na Kampuni ya Wilcroft inamiliki asilimia 75.

Aidha, akizungumzia mkutano huo amesema kuwa, mbali na majadiliano, nchi wanachama watapata fursa ya kubadilishana uzoefu kuhusiana na usimamizi wa sekta ya madini, kuimarisha utendaji katika wizara ikiwemo kuhakikisha mifumo ya ADPA inaboreshwa ili kuwa na manufaa ya nchi wanachama.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya amesema kwa kuwa nchi ya Tanzania ni sehemu ya nchi wazalishaji wa madini ya almasi Afrika wanayo fursa ya kushiriki mikutano hiyo.

Tanzania ndiye Mwenyeji wa Mkutano wa mwaka huu wa Siku Mbili unaofanyika tarehe 7 na 8 Aprili, 2021, kwa njia ya Video Conference. Jumuiya hiyo inajumuisha jumla ya nchi wanachama 19 kati yao 12 zikiwa nchi wanachama na 7 nchi waangalizi. Nchi wanachama ni pamoja na Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini, Namibia, Tanzania, Zimbabwe, Cameroon, Afrika ya Kati, Ghana, Togo, Guinea na Sierra Leone. Nchi waangalizi ni pamoja na Algeria, Jamhuri ya Congo, Cote D’ivore, Gabon, Liberia, Mali na Mauritania.

Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2006 kwa mujibu wa Azimio la Luanda Angola na Sheria za ADPA, lengo ilikuwa ni kuzipatia nchi zinazozalisha madini ya almasi Afrika jukwaa la kuzikutanisha katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali madini zinanuifaisha nchi wanachama. Aidha, kupitia jukwaa hilo nchi zinapata fursa za kubadilishana taarifa za uzoefu katika sekta ya madini na kujenga uwezo wa wataalam kuhusiana na masuala ya almasi. Vilevile, kupitia jukwaa hilo, nchi zinaweza kuleta masilahi ya nchi wanachama kuhusiana na biashara ya almasi duniani.

Tanzania inatarajia kupokea kijiti cha Uanachama wa Jumuiya hiyo kutoka nchi ya Jamhuri ya Namibia ambapo Balozi wa Namibia nchini ataikabidhi Tanzania uenyekiti huo, jijini Dodoma.



Share:

Majaliwa: Asanteni Watanzania Kwa Uzalendo Na Mshikamano


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewashukuru Watanzania wote kwa kuonesha mshikamano na uzalendo wa hali ya juu wakati wa kutangazwa na kipindi chote cha maombolezo ya msiba hadi mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 7, 2021) alipozungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Visiwani Zanzibar katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Aman Karume.

Machi 17, 2021 aliyekuwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan majira ya saa 5.15 usiku aliwatangania wananchi kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. Magufuli kilichotokea saa 12.00 jioni katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam.

Baada ya kutangaza taarifa za kifo hicho pia alitangaza siku 21 za maombolezo pamoja na taratibu za kuuaga mwili na mazishi, ambapo Machi 20 na 21, 2021 viongozi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani walipata fursa ya kuaga katika uwanja wa Uhuru.

Machi 22 yalifanyika mazishi ya Kitaifa Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma ambayo yaliongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Marais tisa, Machi 23 zoezi la kuaga lilifanyika kwa wananchi wa Zanzibar.

Machi 24 wananchi wa mkoa wa Mwanza walipata fursa ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli, Machi 25 wananchi wa mkoa wa Geita walimuaga katika Uwanja wa Magufuli wilayani Chato na Machi 26, 2021 alizikwa nyumbani kwake Chato, Geita

Waziri Mkuu amesema anawashukuru Watanzania wote kwa namna walivyoshiriki katika zoezi hilo, hivyo amewaomba waendeleze utulivu na mshikamano mkubwa waliounesha katika kipindi chote cha majonzi. ”Wakati wote tangu msiba ulipotangazwa Watanzania walikuwa watulivu hadi leo tunapomaliza siku 21 za maombolezo, tunawashukuru sana.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa miongozo yake aliyoitoa ambayo iliiwezesha kamati ya mazishi ya kitaifa kuratibu vizuri zoezi hilo na kufanikisha mazishi ya Hayati Dkt. Magufuli. ”Kauli yake iliwasaidia Watanzania kuendelea kuwa watulivu huku wakimuombea Hayati Dkt. Magufuli.”

Pia, Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano mkubwa alioutoa kupitia kwa Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya mazishi ya kitaifa ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi wengine.

”...Nawashukuru wajumbe wa kamati ya mazishi ya kitaifa, mikoa na wilaya. Pia navishukuru vyombo vya habari kwa ushiriki wao ambao umewawezesha Watanzania wote kupata taarifa za tukio zima kuanzia siku ya kutangazwa kwa kifo hadi mazishi. Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata taarifa za matukio mbalimbali.”

”Pia navishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha zoezi zima linafanyika kwa amani na utulivu katika maeneo yote nchini. Nawashukuru wanachama wa Chama Cha Mapinduzi chama ambacho Hayati Dkt. Magufuli alikuwa Mwenyeti wake wa Taifa, kwani nao walishiriki kikamilifu.”

Waziri Mkuu amesema baada ya kumaliza siku 21 za maombolezo ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli Watanzania wanatakiwa waendelee kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili Taifa lizidi kupata maendeleo. ”Tuendelee kuwa watulivu, tushikamane na tushirikiane katika kufanya kazi.”

Akizungumzia kuhusu watumishi, amesema kila mwenye dhamana ndani ya Serikali anajukumu la kuhakikisha kuwa anawapokea, anawasikiliza na kuwahudumia ipasavyo wananchi wote wanaohitaji kuhudumiwa ili malengo yaliyowekwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025  yafikiwe.

 (Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Rais Samia Suluhu Ashiriki Dua Maalum Ya Kumuombea Hayati Rais Amani Abeid Karume Katika Siku Ya Kumbukumbu Yake


Rais Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki Hitima ya kumbukumbu ya miaka 49 ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume, iliyofanyika katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mkoa wa mjini Magharibi.

Hitma ya Hayati Karume imesomwa na Sheikh Mohamed Abbas ambapo viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla.

Katika mawaidha yake baada ya Kisomo hicho, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Zanzibar Sheikh Shabaan Salum Bapashi amemuelezea Hayati Karume kuwa alikuwa ni kiongozi aliyewapenda watu wake na ndio maana aliwafanyia maendeleo makubwa.

Sheikh Bapashi amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuwaenzi viongozi wote waliotangulia mbele ya haki na kuyaenzi yale yote waliyoyafanya.

Aidha ametoa Pole kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa misiba iliyolipata Taifa katika kipindi kifupi



Share:

PETER MSECHU AWACHANA WANAOMDHIHAKI MUONEKANO WAKE....ASISITIZA HIYO NI 'BRAND YAKE'


Picha ya msanii Peter Msechu akiwa na mkewe aliyembeba mtoto wao
***
Msanii wa BongoFleva Peter Msechu amenyoosha maelezo kwa baadhi ya watu wanaomshambulia mitandaoni kuhusu muonekano wake kwa kusema hawezi kubadilika na hiyo ndiyo brand yake pia haimuathiri kwa chochote.

Kupitia EATV & EA Radio Digital Peter Msechu amesema "Hakuna kitu kinachoniathiri nitabakia kuwa Msechu na brand yangu itabaki hivi hivi na nitaendelea kuishi maisha yangu na kuzingatia kula vizuri, kuishi vizuri, kufanya mazoezi na sina magonjwa nyemelezi"

"Kuishi kama shabiki yangu anavyotaka yeye ili afurahi sitaweza ila shabiki ndiyo apende maisha yangu, kitakachoniuma ni watoto wangu wakishinda njaa, kukosa ada au familia yangu kutokuwa vizuri, napenda na nafurahi watu wafanye hivyo kwa sababu inafanya nizidi kuzungumziwa wala hainiumi" ameongeza Peter Msechu

Aidha msanii huyo amesema Mungu amemuumba kila mtu kwa mfano wake na aina yake ambayo anataka ayaishi hapa duniani.

Chanzo - EATV

Share:

DIWANI AFARIKI DUNIA GESTI AKIWA NA MCHEPUKO


Diwani Kata ya Mbagala Kuu, Shabani Othman Abubakari enzi za uhai wake.

Na Dotto Mwaibale - Dar es salaam

DIWANI wa Kata ya Mbagala Kuu Shabani Othman Abubakari (CCM) amefariki dunia katika moja ya nyumba ya kulala wageni iliyopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam alipokuwa na mwanamke anayedaiwa ni mchepuko wake.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtimika na kuwa mazishi yake yatafanyika leo katika makaburi ya Tanita yaliyopo eneo la Kibonde Maji.

Mmoja wa wahudumu nyumba hiyo ya kulala wageni (jina lake linahifadhiwa) alisema diwani huyo alifika akiwa na gari lake wakiwa na msichana huyo usiku wa kuamkia juzi na kuchukua moja ya chumba katika nyumba hiyo.

Alisema asubuhi baada ya kuamka wakati akifanya usafi ndipo alipoukuta ufunguo wa chumba alichokuwa amekichukua diwani huyo na msichana huyo ukiwa umetupwa chini ambapo alishituka na kwenda katika chumba hicho na kukuta kikiwa kimefungwa na kilipofunguliwa walimkuta diwani huyo akiwa amefariki lakini yule msichana waliyekuwa naye hayupo.

Mhudumu huyo alisema baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao walifika na baada ya kuwahoji waliuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Share:

Picha : RAIS SAMIA ASHIRIKI DUA MAALUM YA KUMUOMBEA HAYATI RAIS ABEID AMANI KARUME LEO ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day)..PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiomba Dua mbele ya Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Karume Day.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya Dua Maalumu ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika siku ya Kumbukumbu ya Karume (Karume Day) iliyofanyika leo tarehe 07 April 2021 katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.
Mhe Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa Hayati Rais Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar , ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea katika siku ya kumbukumbu yake.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Mhe Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea katika siku ya kumbukumbu yake.

Mhe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Dua maalumu ya kumuombea Hayati rais Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .
Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjane wa Hayati Rais Abeid Aman Karume Mama Fatuma Karume , wakati alipowasili kwenye Dua maalumu ya kumuombea Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Mke wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanziba Dkt. Hussein Ali Mwinyi , Mama Mariam Mwinyi, na Katibu mkuu Kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said wakishiriki Dua maalumu ya kumuombea Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa, leo April 7, 2021 .

PICHA NA IKULU
Share:

Team leader internal audit Tanzania at GFA Consulting Group

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Team leader internal audit Tanzania   Job description Team Leader and Head of the Field of Action 2 on internal audit of the programme   Overall responsibility for the advisory package of the contractor, that is the implementation of the Field of Action 2 on internal audit of the programme Ensuring the coherence and complementarity […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

National internal audit expert, based in Dar es Salaam at GFA Consulting Group

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

National internal audit expert, based in Dar es Salaam    Job description Tasks of national expert 2 Provision of on-the-job trainings for Internal Audit Unit IAUs of pilot Ministries, Departments and Agencies MDAs and Local Government Authorities LGAs Lead advisor for delivery of Work package B: Strengthening MDAs/LGAs pilot internal audit unit to reach international […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Team Leader – Water & Sanitation, Investment Financing Facility Project at GFA Consulting Group

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Team Leader – Water & Sanitation, Investment Financing Facility Project    Project description Started in April 2016, GFA Consulting Group, on behalf of the KfW, has been implementing the IFF-OBA Programme: “Provision of Consulting Services for the Implementation of the Investment Financing Facility – Output Based Approach” Background: Traditionally, capital investment projects in the water […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

National internal audit expert, based in Dodoma/Tanzania at GFA Consulting Group

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

National internal audit expert, based in Dodoma/Tanzania     Job description Tasks of national expert 1   Lead advisor for delivery of work packages C, D and E:   C: development or revision of guidance documents based on MoFP’s internal audit strategy D: improving knowledge management practices in the public sector internal audit system E: improving […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Vibali Vya Ukusanyaji, Usafirishaji Na Uhifadhi Wa Chuma Chakavu Vitolewe Kwa Miaka Mitatu- Waziri Jafo


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Suleiman Jafo ametoa agizo kuwa vibali vyote vya ukusanyaji, usafirishaji na uhifadhi wa vyuma chakavu vitolewe kwa muda wa miaka mitatu na sio kwa mwaka mmoja kama ilivyokua awali ili kuepusha usumbufu kwa Wawekezaji. Ametoa agizo hilo alipokuwa katika ukaguzi kwenye  kiwanda cha Metro  steel Ltd kinachozalisha nondo kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Aidha akiwa katika kiwanda hicho pia Mh. Jafo ametoa onyo kwa wenye viwanda kwa kutokufuata sheria, taratibu na kanuni za mazingira. Pia alitoa rai kwa wenye viwanda kwa kulinda miundombinu ya Nchi na  kutokufanya uharibifu katika kupata vyuma chakavu.

Ameendelea kusema kiwanda hicho cha Metro Steel Ltd  kinalalamikiwa na wananchi kuwa muda wa usiku kinatoa moshi na kupelekea kero kwa wakazi walio karibu na kiwanda.

“Natoa onyo kali kwa kiwanda hiki leo sijaja kupiga faini ningeweza kumwambia Mkurugenzi Mkuu wa NEMC awapige faini ila ninawapa onyo  mjirekebishe katika hili”. Alisema Waziri Jafo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.  Samuel Gwamaka amesema kiwanda cha Metro steel kina kibali cha usafirishaji lakini kibali hakina tarehe wala kiasi cha chuma chakavu kilichosafirishwa na kushushwa kiwandani. “Utaratibu uliopo lazima kibali kiandikwe tarehe na kiasi cha chuma chakavu kinachosafirishwa na vinginevyo kutoandikwa tarehe kibali kimoja kinaweza kutumika bila kikomo hivyo kuwa na kibali kisichoandikwa tarehe ni makosa”. Dkt. Gwamaka

Katika ziara hiyo pia Waziri Jafo alifanya ziara alitembelea kiwanda cha Steel Masters kukagua uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kutoka katika chuma  chakavu. Akiwa katika kiwanda hicho pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa laHifadhi na  Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dkt. Samwel Gwamaka, walikagua lori lenye usajili T620 AQW likiwa na bidhaa mbalimbali za chuma likingojea kushusha mzigo ambapo walijiridhisha kuwa lori hilo linakidhi mahitaji yote ya kisheria yanayotakiwa.

Waziri Jafo amefanya ziara katika viwanda viwili katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kukagua masuala ya mazingira katika viwanda hivyo.


Share:

Project Accountant at MDH

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Project Accountant    Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH); Nutrition; Non-Communicable […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Health Manager at MDH

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Health Manager    Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH); Nutrition; Non-Communicable […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Regional TB/HIV Officer at MDH

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Regional TB/HIV Officer  Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH); Nutrition; Non-Communicable […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

CTC-2/3 Officer at MDH

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

CTC-2/3 Officer     Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH); Nutrition; Non-Communicable […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger