Tuesday, 26 January 2021

DK.AKWILAPO AIPONGEZA CSSC KWA KUTOA ELIMU BORA NCHINI,ASEMA SERIKALI ITAYAFANYIA KAZI MAONI YENU

 

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Wakuu wa Shule wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Bw.Peter Maduki,akielezea jinsi wanavyotoa elimu katika shule zao wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa huduma za Elimu wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Mwl.Petro Pamba,akitoa taarifa kwenye Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Mwalimu Deogratius Renatus kutoka Sekondari ya St.Galgan kutoka Arusha akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia Hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC)

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.


Na Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo, ameipongeza Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii(CSSC),kwa mchango wake katika sekta ya elimu nchini huku akiahidi serikali kufanyia kazi maoni yanayotolewa ikiwamo kupunguza kwa mitihani ya majaribio.

Akifungua leo Mkutano wa mwaka cha Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi za makanisa, Dk.Akwilapo, amesema suala la mitihani ya majaribio lina utata na kudai kuwa ni mingi na wakati mwingine inaipa Wizara wakati mgumu kuiratibu.

“Kuna wengine wanadhani elimu inapatikana kwa kuuliza wanafunzi maswali mara kwa mara, ili ng’ombe anenepe ni kuhakikisha amekula na si kumpima uzito asubuhi, mchana na jioni, kitu kizuri ni kuimarisha ufundishaji,”amesema.

Ameongeza kuwa “Kuna dhana nyingine imeongezeka hadi kuweka kambi kufanyishwa mitihani kila siku hadi jumamosi,kuna mambo tumekemea na si sahihi kwamba ili mwanafunzi afaulu ni kupigwa mitihani, majaribio hatuyakatai bali kila mara inamchosha mtoto.”

Aidha, amesema nia ya serikali ni kutoleta mgongano na wanaendelea na majadiliano na kutaka kuimarisha ufundishaji na si kupewa mitihani kila siku.

Pia amezitaka shule kuzingatia maelekezo ya serikali katika kumkaririsha mwanafunzi darasa kwa kuwa suala hilo linalalamikiwa.

“Tunatambua mchango wenu mnaoutoa nchini katika sekta ya elimu, hata hivyo baadhi ya shule zisizo za serikali kama nyingine zipo kwenu au hazipo, ambazo zinaenda kinyume na maelekezo ya serikali, niwakumbushe myazingatie kukaririsha wanafunzi bila kuzingatia taratibu ni tatizo tunalokutana nalo sana,”amesema.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hiyo, Peter Maduki, amesema la mkutano huo ni kuweka mikakati ya utoaji huduma bora ya elimu na kuangalia kero zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

“Pia tutajadili namna ya kuboresha huduma ya TEHAMA itatusaidia sana katika kuboresha elimu na kupunguza gharama ya utoaji wa elimu na kuwapunguzia mzigo wazazi,”amesema.

Ameomba Wizara kuangalia namna ya kupunguza mitihani ya majaribio ambayo imeonekana kuendelea kuibuka mbali na inayopaswa kufanyika kitaifa.

“Kunaendelea kuibuka mitihani ya majaribio mara ya kikata, kiwilaya hali inayosababisha mwingiliano wa mitihani na hii hata inashusha ubora wa mitihani tunaomba umakini zaidi uwepo katika kuendesha mitihani,”amesema.


Share:

AJIKATA UUME AKIJIUA BAADA YA KUGOMBANA NA MKE WAKE



Na  Mussa Juma - Mwananchi
Mkazi Kijenge Mwanama jijini Arusha, John Tarimo amelazwa katika hospitali ya mkoa Arusha ya Mount Meru baada ya kujikata uume na kutaka kujiua kutokana na ugomvi wa mapenzi.

Akizungumza, Januari 25,2021, Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Salum Hamduni amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kijana huyo yupo chini ya ulinzi wa Polisi.

"Ingawa anapata matibabu lakini yupo chini ya uangalizi wa Polisi na anatuhumiwa kwa kutaka kujiua," amesema Kamanda Hamduni.

Taarifa za awali zinadai kuwa mtuhumiwa huyo aliacha ujumbe kuwa anajiua kutokana na ugomvi kati ya mke wake na ndugu zake bila ya kufafanua.

Baadhi ya majirani walioshuhudia tukio hilo wamesema walimkuta Tarimo akiwa hajitambui.

Onesmo Mjema amesema Tarimo alikuwa amejifungia ndani ya chumba alichokiwa amepanga akiwa ameukata uume na kubaki sehemu ndogo na amejikata mkono huku akitoka mapovu mdomoni.

"Mke wake alikuwa ametoka amemuacha ndani lakini aliporudi akiwa mtoto wao mmoja alikuta mlango umefungwa ndipo baada ya kuchungulia dirishani alikuona mumewe akiwa ametapakaa damu na anatoka mapovu," amesema Mjema.

Ameendelea kusema akiwa na jirani mwingine walivunja mlango na kuingia ndani kumtoa nje akiwa hawezi kuzungumza huku damu zikimtoka.

"Baada ya hapo tulimwita mwenyekiti wa mtaa ambaye alitupa maelekezo tumpeleke hospitali kuokoa maisha," amesema.

Hata hivyo, mmoja wa majirani aliyeomba kuhifadhiwa jina lake amesema kwa muda mrefu kulikuwa na ugomvi wa wivu wa mapenzi baina ya Tarimo na mkewe ambaye wamezaa nae mtoto mmoja.

 CHANZO - MWANANCHI
Share:

Monday, 25 January 2021

TBS YAFANYA UKAGUZI WA BIDHAA NA KUBAINI BIDHAA AMBAZO HAZITAKIWI KUINGIA SOKONI KANDA YA ZIWA


 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza 
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kufanya ukaguzi ukiendana na kutoa elimu kuhusiana na makundi 13 ya bidhaa za vipodozi kutokana na watu wengi kukumbana na changamoto ya kutambua nini maana ya bidhaa za vipodozi. 

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo wa kufanya ukaguzi unaoendana na kutoa elimu kuhusiana na vipodozi kwa wananchi katika wilaya zote za mikoa ya kanda ya ziwa na tayari ukaguzi na elimu imetolewa kwenye Wilaya za Nyamagana na Ilemela, jijini Mwanza. 

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa bidhaa za vipodozi uliofanywa na Ofisi ya TBS Kanda ya Ziwa, Kaimu Mkuu wa Kanda hiyo, Evarist Mrema, alisema ukaguzi huo ukiendana na kutoa elimu unafanyika kwenye maduka ya rejareja, jumla, kwa wasambazaji, supermarkets, migahawa na kwingineko. 

Akifafanua zaidi, Mrema alisema; " Tunafanya ukaguzi na kutoa elimu kwa upande wa vipodozi, kwani watu wamepata changamoto ya kujua ni nini maana ya bidhaa za vipodozi, tunaliona hilo nalo ni changamoto kwenye ukaguzi huu na tunahitajika kutoa elimu na tunatoa elimu na tunaendelea kutoa elimu wakati wa ukaguzi." 

Alisema aina za vipodozi zipo katika makundi 13 na kundi la kwanza ni za bidhaa za watoto kama vile poda, shampuu na kundi la pili ni la bidhaa zinazotumika bafuni. 

"Huko nako kuna bidhaa tofauti zinazotumika bafuni kama sabuni za kuogea pamoja na zile ambazo watu wanaziandaa katika maeneo yao ya kuogelea na vitu kama hivyo," alisema Mrema. 

Alitaja kundi lingine kuwa bidhaa za nywele ambako kuna makundi yake kama mawili au matatu. Kwa mujibu wa Mrema kuna rangi za nywele ambazo zinatumika kwenye nywele, lakini pia kuna nywele zinazoongezwa ndani ya nywele asili kama rasta na wigi na kwamba hizo zote ni aina za bidhaa za vipodozi. 

Bidhaa nyingine kwa mujibu wa Mrema ni zile ambazo zinapakwa juu ya ngozi kama mafuta ya kupaka, losheni na bidhaa nyingine zinatumika kwa upande vidole vya akina mama mfano kucha bandia na midomo ambazo nazo ni sehemu ya bidhaa za vipodozi. 

Alitaja aina nyingine za bidhaa za vipodozi kwa upande wa urembo zinazotumika kwenye macho akisema zote hizo ni aina za vipodozi na wananchi wataendelea kufamua kaguzi zinazoendana na kutoa elimu kuhusiana na bidhaa hizo. 

Wakizungumzia kuhusiana na ukaguzi huo, wananchi wengi walielezea kufurahishwa na hatua hiyo kwani wamekuwa wakibambikwa bidhaa za chakula na vipodozi zilizokwisha muda na vilevile kuuziwa vipodozi zenye viambata sumu. 

"Kwa hiyo shirika linatusaidia kuwadhibiti na waendelee kwa nguvu hiyo hiyo hadi maduka ya vijijini," alisema mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Machibya Samuel. Wauzaji madukani wameomba shirika liwafikirie katika malipo ili walipe kwa mikupuo miwili au zaidi kama wanavyofanya TRA, kwani biashara ni ngumu.
Mkaguzi wa TBS akitoa bidhaa ambazo hazina muda wa matumizi
Bidhaa zilizoisha muda wake
Bidhaa zenye viambata sumu ambazo zimepigwa marufuku. 


Share:

ASILIMIA 85 YA TAMASHA LA KAN KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO


Na Woinde Shizza- Arusha
Asilimia 85 ya tamasha la maarifa, sanaa na kujenga mtandao wa kufahamiana (KAN) linatarajiwa kufanyika mtandaoni lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi zaidi na kuweza kukabiliana na changamoto ya virusi vya Corona vinayoendelea kuzikabili nchi nyingi duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Tamasha hilo Khalila Mbowe linaloandaliwa na Chuo Cha Maendeleo na ushirikiano wa Kimataifa(MS- TCDC) alisema kuwa kwa miaka miwili ambayo tamasha hilo lilifanyika, kwa asilimia kubwa ilifanyika chuoni hapo lakini kutokana na changamoto inayoikabili dunia hivi sasa asilimia 15 tu ndiyo itakayofanyika katika chuo hicho na asilimia nyingine kufanyika mtandaoni huku washiriki wakitoka katika nchi mbalimbali za bara la Afrika na baadhi kutoka katika mabara mengine.

Bi. Khalila alieleza kuwa pamoja na changamoto hiyo lengo lao la kujimuisha bara zima la Afrika bado lipo pale pale na ndiyo maana yeyote ambaye ni rafiki wa maendeleo na ni rafiki wa Afrika anapaswa kushiriki KAN Festival kupitia mijadala itayoendeshwa katika mitandao ya kijamii na kuona ni hindi gani wanaweza kukuza maendeleo ya bara la Afrika hasa kwa kuangalia ag pplenda ya 2063 ya umoja wa mataifa.

Alisema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo “Maendeleo ya Afrika, mimi nahusika” pia itambatana na mambo mbali mbali ikiwemo mafunzo, mashindano ya ujasiriamali na ubunifu pamoja na mbio zijulikanazo kwa jina la Kan Run ambapo kila mshiriki atashiriki mahali alipo chini ya tamasha hilo.

“Katika hii Kan Run tumeona ni muhimu tunapoongelea maendeleo ya Afrika tushiriki kwa vitendo kwani bila afya nzuri hatuwezi kufanya jambo popote kwa hiyo watakaokuwa eneo hilo mbio hizo zitaanzia hapa lakin kwa walio nje ya hapa watafanya mahali walipo lakin chini ya uwangalizi wetu”, alisema Bi. Khalila.

Aidha alisema kuwa tamasha hilo litaanza Januari 28 hadi 30,2021 ambapo baada ya tamasha hilo watafuatilia kama wote walioshiriki wamehusika mwenye maendeleo ya bara la Afrika kwa namna moja au nyingine.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa chuo hicho Sara Teri alisema kuwa katika kuifikia agenda 2063 wanaangalia wanakujaje kwa pamoja kwenye mambo mbalimbali yakiwemo afya, demokrasia, haki, utawala bora na masuala ya vijana ambapo wameamua wakae kea kwa pamoja na kujadili maendeleo ya Afrika.

“Hili ndio kusudi la KAN Festival na huu ni mwaka wa tatu na inaendelea kukua na kuonekana ulimwenguni na kwa mwaka huu kutakuwa na mijadala tofauti tofauti hapa na kwenya Mitandao pia na lengo ni moja kuhakikisha tunapotoka hapa tunasemaje au tunatokaje Kama washiriki wa mjadala,” alisema Sara Teri.

Alifafanua kuwa mara nyingi watu wa kawaida wanakosa fursa ya kujadili maendeleo ya bara lao na badala yake Kuna kuwa na watu wanaojadili bila sauti za watu wa kawaida kusikika zikionyesa jinsi wanavyoshiriki au kuhusika hivyo lengo ni wewe na yeye mnasemaje juu ya maendeleo ya bara.

Naye mmoja wa wasanii Editha Leonard alisema kuwa kila mtu akisema yeye anahusika utaongeza chachu ya maendeleo kwani kea sasa Afrika ipo sehemu nzuri na ni kivituo cha dunia katika kila nyanja na hii itawafanya Waafrika wazidi kulipenda bara lao.

“Katika tamasha hili mimi binafsi nitaeleze jinsi afya ya akili inavyochangia vifo vya watu kujinyonga Kutokana na kuwa na msongo wa mawazo na kwa kupitia sanaa yangu watu wataona afya ya akili ni jambo la kawaida na kuanza kutafuta ufumbuzi wa kuondoka changamoto hii,” alisema Editha.
Share:

RAIS MAGUFULI AMPA RAIS WA ETHIOPIA KINYAGO CHA KIMAKONDE




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia kinyago cha Kimakonde cha "UJAMAA" mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Sahle-Work Zewde walipowasili Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumatatu Januari 25, 2021.

Share:

BABA ATUHUMIWA KUBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 11....ANASWA AKIWA NAYE 'LIVE' UCHI WA MNYAMA



Na Anthony Mayunga - Mwananchi
 Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Chamoto, Ikwabe Gibogo (58) kwa tuhuma za kumwingilia kimwili mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka (11).

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Chacha Nyambuche amekiri mtuhumiwa kukamatwa  Januari 23,2021 usiku baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na kumkuta nyumbani kwake amelala chini pamoja na mtoto huyo wote wakiwa hawajavaa nguo.

Mmoja wa majirani amesema mtoto huyo ameingiliwa kwa muda mrefu na baada ya kujiridhisha waliamua kutoa taarifa kwa kiongozi wa kitongoji na polisi walipofika waliwapa ushirikiano.

“Huyo mtoto hajaanza shule mpaka sasa, mama yao aliachana na baba yao baada ya kubaini anamuingilia mtoto wake mkubwa. Aliondoka na watoto wadogo kwenda Simiyu, hata hivyo, alifariki dunia ndipo mtuhumiwa akafuata watoto na kuja kuishi nao,” amesema jirani huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

Via Mwananchi


Share:

CHELSEA YAMTIMUA KOCHA WAKE FRANK LAMPARD





Frank Lampard ameshinda michezo 28 kati ya 57 aliyoiongoza Chelsea katika Ligi ya Primia.

Chelsea imemfuta kazi kocha wake Frank Lampard baada ya kuingoza klabu hiyo kwa miezi 18.

Lampard (42), ambaye ni kuingo wa zamani wa klabu hiyo, anaiacha Chelsea katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi ya Primia huku wakishinda mechi moja tu ya ligi kati ya tano zilizopita. Mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu wiki iliyopita walifungwa na Leicester City.

Mechi yake ya mwisho kama kocha wa miamba hiyo ya London ulikuwa Jumapili wakishinda 3-1 dhidi ya Luton kwenye michuano ya FA.

Kocha wa zamani wa Paris St-Germain na Borussia Dortmund Thomas Tuchel anatarajiwa kutua katika dimba la Stamford Bridge kurithi nafasi ya Lampard.

Lampard amekuwa kocha wa 10 kuajiriwa na Roman Abramovich tangu tajiri huyo alipoinunua Chelzea mwaka 2003. Aliajiriwa mwaka 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri.

Inakadiriwa kuwa Abramovich ameshatumia pauni milioni 110 kuwalipa makocha aliowatimua kazi kabla ya Lampard.

Katika kipindi chote cha umiliki wa Abramovich, Lampard ni kocha wa pili kuwa na uwiano mbovu wa matokeo wa asilimia 52.4, ni Andre Villas-Boas (47.5%) ambaye mwenye uwiano mbovu zaidi.

Uwiano wa wa ushindi wa Jose Mourinho alipoinoa klabu hiyo mara ya kwanza ulikuwa 67.03%, wakati while Antonio Conte, Maurizio Sarri, Avram Grant, Carlo Ancelotti na Claudio Ranieri wote wakiwa na zaidi ya 60%.

CHANZO - BBC SWAHILI 

Share:

Picha : RAIS WA ETHIOPIA AFANYA ZIARA GEITA TANZANIA...APOKELEWA KWA HESHIMA NA JPM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa Ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa Ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.
Mmoja wa Msanii wa kikundi cha Ngoma za asili cha Chato akionesha uhodari wake wa kucheza na nyoka aina ya Chatu wakati wa sherehe za kumpokea Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 25 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 25 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari wa mkoa wa Geita mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari wa mkoa wa Geita mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akizungumza na Wanahabari wa Geita baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita. 
Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akizungumza na Wanahabari wa Geita baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita. 
Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akizungumza na Wanahabari wa Geita baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita. 
Ndege iliyombeba Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.
Ndege iliyombeba Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.
Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.

Picha na Ikulu
Share:

Waziri Bashungwa: Sekta za Wizara ya Habari ni mihimili Muhimu Nchini.


Na Shamimu Nyaki - WHUSM
Sekta za Wizara ya Habari ni sekta muhimu  zenye  mchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi na kuleta  maendeleo.

 Hayo yamesemwa  leo Jijini Dodoma na Waziri  wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa wakati akiwasilisha Muundo pamoja na Majukumu ya Wizara hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Mhe. Bashungwa amesema kwamba Sekta ya Sanaa na Michezo zimechangia katika Ongezeko la pato la Taifa ambapo kwa mwaka 2018, shughuli za burudani zimechangia pato la Taifa kwa asilimia 13.7 na kushika nafasi ya kwanza  na  mwaka 2019 shughuli hizo zilichangia asilimia 11.2 na kushika nafasi ya tatu.

"Tunashukuru Kamati kwa kutupa mawazo chanya ambayo yatasaidia kuboresha na kuendeleza sekta hizi, naahidi mimi pamoja na timu yangu tutayafanyia kazi mawazo mliyotupa na tayari tumeanza kufanya hivyo katika sekta zote" alisema Mhe. Bashungwa.

Akiendelea kuzungumza Mhe. Bashungwa ameeleza kuwa Wizara tayari imeanza kutengeneza Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Michezo pamoja na ujenzi wa Ukumbi wa Michezo na Sanaa (Sports and Arts Arena) ambayo itaanza kujengwa Jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Bashungwa ameeleza kuwa TCRA pamoja na TRA wameanza kushirikiana namna ya  kukusanya mapato ya kazi za Sanaa kupitia njia za Kidijiti (Digital Taxation).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stasilaus Nyongo Mbunge wa  Jimbo la Maswa Mashariki ameipongeza Wizara hiyo kwa Mikakati mizuri ya kusaidia Sekta inazozisimia, huku akishauri Wizara hiyo kuongeza ubunifu katika kukusanya mapato ya Serikali kupitia Sanaa na Michezo.   

"Nashauri Wizara hii, Wizara ya Elimu pamoja na TAMISEMI  kuwa na utaratibu unaotambulika wa kuendesha na kusimamia shughuli za michezo shuleni" Mhe. Nyongo.

Naye Mhe. Jumanne  Sagini Mbunge wa Jimbo la Butiama ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo amepongeza juhudi za Wizara hiyo katika kutekeleza majukumu yake ambapo ameeleza kuwa ipo haja ya kufanya mapitio ya Sera zote zilizochini ya Wizara hiyo ili kama kuna ambazo zinahitaji marekebisho zifanyiwe maboresho ili kuendana na mahitaji ya wakati huu.

Kamati hiyo imepokea taarifa ya Muundo na Majukumu ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo kesho Januari 26, 2021 itapokea Taarifa ya Majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.

Mwishoo....


Share:

KAIMU AFISA VIJANA MKOA WA SINGIDA FREDERICK NDAHANI AISHAURI SERIKALI KUFUFUA SHULE ZA UFUNDI

 

Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (wa pili kushoto) akizungumza na Walimu wa Ufundi  wa Shule ya Msingi Makiungua iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida alipoitembelea juzi kwa lengo la kukagua uwezeshwaji mafunzo na ujuzi kwa vijana.

Madawati yakitengenezwa. na Shule ya Msingi Makiungu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Madawati yaliyotengenezwa.
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (kulia) akikagua utengenezaji wa madawati.
Madawati yaliyotengenezwa.

Na Dotto Mwaibale, Singida.

KAIMU Afisa Vijana mkoani hapa,  Frederick Ndahani ameishauri Serikali kufufua Shule za Msingi za ufundi Nchini. 

Ndahani alitoa ushauri huo juzi alipotembelea  Shule ya Msingi Makiungu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa lengo la kukagua uwezeshwaji mafunzo na ujuzi kwa vijana.

Ndahani alisema Shule ya Msingi Makiungu ni moja ya shule zilizofanya  vizuri katika mradi waliopewa wa kutengeneza madawati 1000  ya shule za msingi zilizopo wilayani humo.

Ndahani alisema shule hiyo ya mchepuo wa ufundi   ni moja ya shule inayoifanya vizuri na kusababisha ofisi ya mkurugenzi wa wilaya ya  Ikungi kuwapa kazi ya kutengeneza madawati hayo.

" Shule hizi za mchepuo wa ufundi hapa nchini zikiboreshwa zinaweza kusawaidia vijana wa kitanzania kupata ujuzi wa ufundi mbalimbali." alisema Ndahani.

Alisema  wanafunzi wanaojiunga katika shule hiyo hapa ni wale ambao wamekosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari na vyuo na kuwa faida wanayoipata ni kupata mafunzo hayo ya ufundi bure  kama ilivyo elimu ya msingi.

Alisema  kuboreshwa kwa shule  hizo kutasaidia kupata mafundi ambao watatumika kukarabati samani mbalimbali zilizopo mashuleni badala ya kuwapa mafundi kutoka nje ambao watahitaji kulipwa fedha nyingi.

Kwa upande wao  Walimu wa Ufundi katika shule hiyo Cosmas Uhiku na  Haji Kidabu Wameiomba Serikali kuwapatia vifaa vya kutosha kwani wanao uwezo wa kuwapatia vijana mafunzo ya kisasa  sanjari na vyeti baada ya kumaliza mafunzo kwa muda wa miaka miwili.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo  Hashimu Ntandu amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi kwa kuwapatia mradi huo mkubwa wa kutengeneza madawati ambapo wanatengeneza kwa gharama nafuu.


Share:

NAIBU WAZIRI SILINDE AAGIZA TSC IPEWE OFISI ZENYE HADHI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), mjini Morogoro, Januari 25, 2021. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TSC Profesa Willy Komba, Kaimu Katibu wa TSC Moses Chitama na Katibu wa Baraza husika,Lawrence Chankani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Profesa Willy Komba, muda mfupi baada ya Naibu Waziri kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TSC, mjini Morogoro, Januari 25, 2021. Katikati ni Kaimu Katibu wa TSC, Moses Chitama. 
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Profesa Willy Komba (kulia), akitoa hotuba ya ukaribisho wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde (katikati), wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo, Januari 25, 2021 mjini Morogoro. Kushoto ni Kaimu Katibu wa TSC, Moses Chitama. 
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo, uliofanyika Jaunuari 25, 2021 mjini Morogoro. Katikati ni Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Profesa Willy Komba. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde (wa tatu - kulia), akiungana na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kuimba wimbo maarufu wa ‘Solidarity Forever’. Naibu Waziri alifungua Mkutano huo mjini Morogoro, Januari 25, 2021. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa TSC, Profesa Willy Komba na kulia kwake ni Kaimu Katibu wa TSC, Moses Chitama. 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano huo mjini Morogoro, Januari 25, 2021. 
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Abihudi Hemba akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Baraza hilo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde (hayupo pichani) baada ya kufungua Mkutano huo mjini Morogoro, Januari 25, 2021. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde (katikati-waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), muda mfupi baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakzi wa Tume hiyo Januari 25, 2021 mjini Morogoro. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mwenyekiti wa TSC, Profesa Willy Komba na kushoto kwake ni Kaimu Katibu wa TSC, Moses Chitama.

*************************

Na Veronica Simba - TSC

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde amewaagiza Wakurugenzi wa Wilaya kote nchini, kuhakikisha wanawapatia ofisi zenye hadhi, watumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) katika maeneo yao.

Ametoa maagizo hayo leo, Januari 25, 2021 mjini Morogoro wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume.

Naibu Waziri ametoa maagizo hayo baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali zinazoikabili Tume husika, ambapo mojawapo ni ya ukosefu wa ofisi zenye hadhi kwa watumishi wa TSC hususani zilizoko katika baadhi ya Wilaya nchini.

“Nitumie fursa hii kuagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanawapatia Makatibu Wasaidizi wa Tume, ofisi ambazo zinaendana na hadhi ya utumishi wa umma.”

Aidha, ameitaka Tume kuhakikisha inawawezesha Walimu kujitambua na kuelewa sheria, kanuni, taratibu, haki na wajibu wao.

Vilevile, ameipongeza Tume kwa kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa moyo wa uzalendo, pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili. Pamoja na kutoa pongezi, ameitaka Tume kuendelea kutoa huduma bora kwa Walimu.

"Sote tunafahamu kuwa tunapotoa huduma bora kwa Mwalimu inamwezesha kutekeleza majukumu yake shuleni kwa ufanisi hatimaye kuinua kiwango cha elimu nchini.”

Naibu Waziri ameihakikishia Tume kuwa ushirikiano uliopo katika utendaji kazi kati ya Tume na Ofisi ya Rais – TAMISEMI ni endelevu. Aidha, ameongeza kuwa Ofisi yake itaendelea kusisitiza kila Wilaya kuhakikisha kazi za kushughulikia masuala ya kiutumishi ya Walimu zinatekelezwa kwa ushirikiano ili kuleta tija na ufanisi katika suala zima la kuwahudumia walimu.

Awali, akiwasilisha hotuba ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Tume, Profesa Willy Komba alibainisha changamoto kadhaa zinazoikabili, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na jengo la Ofisi za Tume Makao Makuu na Wilaya.

Alisema changamoto nyingine ni baadhi ya waajiri kutokuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kushughulikia masuala ya kinidhamu ya Walimu.

“Mfano kuchelewa kuwasilisha mashtaka kwa Mamlaka ya Nidhamu, kuchukua jukumu la kutoa adhabu kinyume cha utaratibu na kuwaondoa Walimu kwenye mfumo wa malipo kabla ya mchakato wa mashauri kuanza na kukamilika,” amefafanua Profesa Komba.

Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa pia na Kaimu Katibu wa Tume, Moses Chitama, Menejimenti ya Tume pamoja na wawakilishi mbalimbali kutoka wilaya zote nchini.

Tume ya Utumishi wa Walimu ni Mamlaka ya Ajira na Nidhamu kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali, Tanzania Bara. Naibu Waziri David Silinde ndiye amepewa wajibu wa kusimamia Taasisi hii pamoja na nyingine zilizo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Share:

Database Administrator at CRDB Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Database Administrator   Background CRDB Bank Plc is an African bank and a leading Financial Services Provider in Tanzania with current presence in Tanzania and Burundi, East Africa. The Bank was established in 1996 and was listed on The Dar Es Salaam Stock exchange (DSE) in June 2009. Over the years, CRDB Bank has grown […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Digital Channels Systems at CRDB Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Senior Specialist, Digital Channels Systems     CRDB Bank PLC is looking for a suitable candidate to fill 2 vacant positions of Senior Specialist, Digital Channels Systems existing in the Department of Information & Communication Technology (ICT) at Head Office, Dar es Salaam. Job Purpose: To effectively lead a team of ICT Specialist, Systems administrators, responsible […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Senior Manager ICT Strategy & Governance at CRDB Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Senior Manager ICT Strategy & Governance     CRDB Bank PLC is looking for a suitable candidate to fill 1 vacant position of Senior Manager ICT Strategy & Governance existing in the Department of Information & Communication Technology (ICT) at Head Office, Dar es Salaam. Job Purpose: The Senior Manager ICT Strategy & Governance is responsible […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

ICT Risk & Compliance specialist at CRDB Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

ICT Risk & Compliance specialists    CRDB Bank PLC is looking for a suitable candidate to fill 2 vacant position of ICT Risk & Compliance specialist existing in the Department of Information & Communication Technology (ICT) at Head Office, Dar es Salaam Job Purpose:   Responsible for managing and maintaining the IT risk assurance program […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Specialist ICT Security solutions at CRDB Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Specialist ICT Security solutions     CRDB Bank PLC is looking for a suitable candidate to fill 2 vacant positions of Specialist ICT Security solution existing in the Department of Information & Communication Technology (ICT) at Head Office, Dar es Salaam. Job Purpose Daily monitoring of the IT Infrastructure using security technical expertise and looking for […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger