Wednesday, 20 January 2021

MKURUGENZI AGPAHI ATEMBELEA KLINIKI YA TIBA NA MATUNZO YA WAVIU HOSPITALI YA MKOA SHINYANGA, ASHIRIKI KIKAO TATHMINI MRADI WA BORESHA

 

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa na Dk. Richard Mhangwa wakati akifanya ziara ya kukagua Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu  wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Na Marco Maduhu, Shinyanga 
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI linalotekeleza Afua za kupambana na VVU na UKIMWI kwa Watoto na familia zao Dk. Sekela Mwakyusa, ametembelea kuona utendaji kazi katika Kliniki ya Tiba na Matunzo (CTC) ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. 

Dk. Sekela amefanya ziara hiyo leo Jumatano Januari 20,2021 akiwa ameambatana na baadhi ya maofisa wa Shirika hilo la AGPAHI, ambapo ameeleza kuridhishwa na utoaji wa huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. 

Alisema baada ya kutembelea Kliniki hiyo na kuuliza maswali na kujionea utendaji kazi, amefarijika kuona ubora wa huduma ambazo zinatolewa kwa WAVIU. 

"Niwapongeze sana watumishi ambao mnatoa huduma kwenye Kliniki hii ya Tiba na Matunzo kwa watu ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kwani mnafanya kazi nzuri sana," alisema Dk. Sekela. 

"Pale ambapo kuna changamoto msisite kutuambia, ili tuitatue hasa katika kipindi hiki ambapo tunaelekea ukingoni mwa kufunga mradi wetu," aliongeza. 

Naye Kiongozi wa Kliniki ya Utoaji wa Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,Dk. Richard Mhangwa amelipongeza Shirika hilo la AGPAHI, kwa mchango wao katika kusaidia utoaji wa huduma kwenye Kliniki hiyo.

Akiwa mkoani Shinyanga, Dk. Sekela pia Januari 19,2021 alishiriki kikao kazi cha kutathmini mradi wa Boresha kwa mwaka wa nne ukishirikisha Shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI linalotekeleza Afua za kupambana na VVU na UKIMWI kwa watoto na familia zao na serikali mkoa wa Shinyanga

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kaimu Katibu Tawala Mkoa ambae ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa,Mganga Mkuu wa Mkoa,Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na Wilaya,Wajumbe wa Timu za Usimamizi na Uendeshaji Huduma za Afya Mkoa na Halmashauri na Watendaji wawakilishi Idara ya Uhasibu ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Dk. Sekela alisema lengo la mradi wa Boresha ni kuimarisha Ufuasi na Ubakizaji wa WAVIU kwenye huduma za Tiba na Matunzo,Kuhakikisha ubora na matumizi sahihi ya takwimu za VVU na UKIMWI katika ngazi mbalimbali za maamuzi, kuendelea kuimarisha utekelezaji wa huduma unganishi zikiwemo za Kifua kikuu, Afya ya Uzazi na Mtoto, Huduma za Maabara na Famasia pamoja na Saratani ya mlango wa kizazi sambamba na Huduma za kuzuia unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto

“AGPAHI kwa kushirikina na Serikali ya mkoa wa Shinyanga, tumeendesha kikao cha kujadili tathmini juu ya mradi wetu wa Boresha kwa mwaka wa nne, ambao tunautekeleza hapa mkoani Shinyanga, wa kutoa huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi ya Ukimwi (VVU), pamoja na kuzuia maambukizi mapya, ili tunapoelekea kwenye mwaka wa tano wa utekelezaji, tuutekeleze vizuri na kusiwepo na changamoto zilizojitokeza huko nyuma,”alisema Dk. Mwakyusa. 

Kwa upande wake ,Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa mkoani Shinyanga Alphonce Kasanyi, akimwakilisha Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, aliwataka watalaamu hao wa afya, washirikiane kikamilifu na maofisa kutoka Shirika la AGPAHI,na kutatua changamoto zilizojitokeza kwa awamu zilizopita, ili mradi huo wa Boresha utekelezwe vizuri na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Sekela Mwakyusa, akizungumza na watumishi wa Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Januari 20,2021.
Meneja mradi kutoka Shirika la AGPAHI Mkoani Shinyanga Dk. Adarick Makome akizungumza kwenye Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu wanaoishi na Maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Dk. Richard Mhangwa kutoka Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, mara baada ya Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa alipotembelea kwenye Kliniki hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa kwenye Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, akifuatilia utoaji wa huduma kwa watu hao.
Baadhi ya watoa huduma wa Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, wakiwa na baadhi ya watumishi wa Shirika la AGPAHI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Sekela Mwakyusa, kulia akiteta jambo na washauri wa huduma ya VVU katika kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kulia, akimsikiliza Mshauri wa VVU Paulo Seleman katika Cliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa na Dk, Richard Mhangwa wa Kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga, wakati wa ziara ya kukagua utoaji wa huduma kwenye Kliniki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa na Dk. Richard Mhangwa wa Kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga, kulia, wakati wa ziara ya kukagua utoaji wa huduma kwenye Kliniki hiyo, katikati ni Meneja mradi wa Shirika la AGPAHI Mkoani Shinyanga Dk. Adarick Makome.
Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, (wa tatu kutoka kushoto), wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukagua Kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufa ya Mkoa wa Shinyanga, ambayo inatoa huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Januari 19,2021 : Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa mkoani Shinyanga Alphonce Kasanyi, akimwakilisha katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela akieleza namna shirika la AGPAHI linavyosaidia katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk, Yudas Ndugile akizungumza kwenye kikao cha kutathimini mradi wa Boresha kwa mwaka wa nne uliohudhuriwa na baadhi ya watumishi wa afya, Waganga wakuu wa wilaya na waratibu wa Ukimwi, ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa mkoani Shinyanga Alphonce Kasanyi, akimwakilisha katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela. 
Meneja miradi wa Shirika la AGPAHI Mkoani Shinyanga Dk. Adarick Makome, akizungumza kwenye kikao hicho wakati akiwasilisha mada.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, wa kwanza kushoto, akiwa na washiriki kwenye kikao hicho wakisikiliza uwasilishwaji wa mada juu ya mradi wa Boresha.
Washiriki wakiwa kwenye kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Elias Masumbuko, Mfamasia kutoka Wilaya ya Kahama, akichangia kwenye kikao hicho.
Dk. Philibert Ng'wenda Mratibu wa kifua kikuu na ukoma Wilayani Kishapu, akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Dk. Henry Sylivester, Mratibu wa kudhibiti Ukimwi kutoka Kahama Mji, akichangia kwenye kikao hicho.

Na Marco Maduhu-Shinyanga.


Share:

Tazama Picha : DONALD TRUMP AONDOKA IKULU BIDEN AKIAPISHWA KUWA RAIS WA MAREKANI


Rais wa Marekani Donald Trump ameondoka Ikulu ya Marekani akiwa sambamba na mkewe, Melania Trump.

Wawili hao walielekea kambi ya jeshi, huko Maryland ambapo sherehe za mwisho kuwaaga zinafanyika.

Baada ya shughuli hiyo Rais Trump atasafiri mpaka Florida kwa ndege ya Air Force One, na ataishi katika makazi yake ya kifahari ya la Mar-a-Lago

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais , Mike Pence, hatakuwepo kwenye sherehe za kumuaga Trump isipokuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Biden na Harris baadae hii leo.

Akitoa maneno mafupi kwa wanahabari kabla ya kuondoka, Rais Trump amesema Ikulu palikuwa makazi mazuri sana.

''Tumekuwa na miaka minne mizuri sana na tumefanikisha mengi,'' alisema Trump.

''Tunawapenda Wamarekani na kimekuwa kitu cha kipekee'', aliongeza.
'Tulipigwa sana'

Rais Trump amegusia kuhusu Janga la corona- ambalo lilishika kasi katika kipindi cha miezi tisa iliyopita ya utawala wake

''Tulifanya jambo ambalo ni muujiza wa kitabibu nalo ni chanjo,'' alisema.

Amesema kirusi ni ''kitu kibaya sana'' na kwa mara nyingine aliita ''kirusi cha China'' lakini ametoa ''salamu za upendo'' kwa familia zilizoathirika kwa kiasi kikubwa.

Vifo vilivyotokana na Covid-19 nchini humo sasa ni zaidi ya 400,000, na idadi ya vifo imeendelea kuongezeka

Trump awatakia 'mafanikio mema' warithi wake

Akihitimisha hotuba yake, Rais Donald Trump amesema imekuwa "heshima kubwa " kuwa rais. Akiwahutubia wafuasi, amesema "atawapigania kila wakati" na atakuwa "akiangalia na kusikiliza" na anaahidi kurudi kwa kiasi fulani.

Ameutakia pia uongozi mpya "mafanikio makubwa" kwa siku zijazo - lakini hakuwataja Joe Biden au Kamala Harris kwa majina.

Ndege ya Marine One katika Ikulu ya Whitehouse ikimsubiri kumsafirisha rais Donald Trump
Ndege ya Marine One ikitua katika Ikulu ya Whitesoue huku rais Trump akisubiri
Akizungumza na wanahabari muda mfupi kabla ya kupanda ndege ya Marine One , rais Trump alisema kwamba Ikulu ya Whitehouse ilikuwa nyumba bora zaidi duniani
Rais Donald Trump na Mkewe Melania Trump wakiondoka katika Ikulu ya Whitehouse
Trump na mkewe Melania Trump akielekea kupanda ndege ya Marine One
Ndege ya Marine One katika ikulu ya Whitehouse
Ndege ya Marine One ilipokuwa ikiondoka katika ikulu ya Whitehouse

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

MAMA AMCHOMA MIGUU KWA JIKO LA MKAA MTOTO WAKE KISA KAUNGUZA MAHARAGE MJINI SHINYANGA..AMFICHA UVUNGUNI


Mfano wa moto

Na Suleiman Abeid,TimesMajira Online,Shinyanga
MTOTO mwenye umri wa miaka 11 (jina limehifadhiwa) mkazi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga amejeruhiwa miguu yake yote miwili baada ya kupigwa na kuchomwa na mama yake mzazi kwa jiko la mkaa wenye moto akituhumiwa kuunguza maharage.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwa waandishi wa habari jana mjini Shinyanga, mtoto huyo ametendewa ukatili huo mwishoni mwa wiki iliyopita na mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina Hanifa Athumani mkazi wa Mtaa wa Majengo Kambarage Shinyanga.

Pamoja na kutendewa ukatili huo mtoto huyo hakupelekwa hospitali huku mama yake akificha kitendo hicho kuwa siri ambapo hata pale viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Majengo walipopata taarifa hizo mtuhumiwa huyo alidiriki kumficha mwanaye huyo kwenye uvungu wa kitanda.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na majirani mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Majengo imedaiwa mama huyo alitenda ukatili huo baada ya kuchukizwa na kitendo cha mtoto kuzembea na kusababisha kuungua kwa maharage yaliyokuwa jikoni na yeye kutoyaangalia yasiungue.

Mmoja wa majirani hao, Mariamu Thomas amesema, siku hiyo ya tukio alimuona mtoto huyo akitembea kwa shida akichechemea na alimuuliza kwa nini anatembea akiwa na hali hiyo ambapo mtoto alimjibu ameungua kidogo miguuni hata hivyo hakuendelea kumuuliza zaidi.

“Mimi siku hiyo nilipofika hapa nyumbani nilimuona huyu mtoto akitembea kwa shida kwa kuchechemea, ilibidi nimuulize kwa nini alikuwa akitembea hivyo, lakini mtoto alinijibu kwa kifupi kwamba ameungua kidogo miguuni.

“Kwa kweli kwa vile mimi siku hiyo sikushinda nyumbani sikuendelea kumuuliza zaidi nikaamini huenda kweli kaumia kidogo japokuwa alikuwa akitembea kwa shida, na niliendelea na shughuli zangu,” ameeleza Mariamu.

Jirani mwingine amesema aliyejitambulisha kwa jina la Asha Nassor amesema wakati tukio hilo lilitokea hakuwepo nyumbani lakini aliporudi jioni nyumbani alimuona mtoto huyo akiwa ameungua miguuni na alimuuliza ni nani aliyemchoma huo moto ambapo alijibu amechomwa na mama yake.

“Siku hiyo asubuhi sikuwepo nyumbani, nilishinda msibani, niliporudi jioni mtoto akaniambia, mama Saidi nimeungua moto, nikamuuliza umeunguzwa na nani? Akajibu mama ameniunguza eti kwa sababu nimeunguza maharagwe.

“Amesema baada ya mama kukuta maharagwe yameungua alinifokea akawa amenichoma, nikamuuliza alichomwa au alirushiwa jiko, akajibu mama yake alimsukumia jiko, asubuhi yake nilimpatia dawa nikampakaa, lakini baadae sikuendeleza, baadae mama yake aliendelea kumwekea manyoa ya sungura,” ameeleza Asha.

Kwa upande wake mama wa mtoto huyo, Hanifa Athumani amesema siku ya tukio alimpatia mwanaye shilingi 600 akanunue maharagwe na akija ayatenge jikoni kwa ajili ya mboga, na yeye aliingia ndani kujipumzisha.

“Siku hiyo mimi nilimpatia shilingi mia sita akanunue maharagwe na aje ayatenge jikoni kwa ajili ya mboga, mimi niliingia ndani kujipumzisha kidogo, muda mfupi nikasikia majirani wanamwita huku wakimuuliza mbona maharagwe yanaungua?”

“Nilishituka nikatoka nje haraka na kukuta kweli maharagwe yote yameungua hadi juu, nilimwambia sasa umefanya nini, yeye akaniangalia kwa jicho baya kama vile amefanya makusudi, ndiyo nikashikwa hasira nikampiga teke, sasa alipamia jiko na kumwagikiwa majivu yenye moto,” ameeleza Hanifa.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo alidai hakuweza kumpeleka hospitali mwanae ili aweze kutibiwa badala yake alimnunulia dawa na kumtibisha akiwa hapo nyumbani huku akidai kuwa amekuwa na tabia ya utundu na udokozi wa vitu vidogo vidogo hali ambayo haimfurahishi.

Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Majengo, Majid Issa ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Kamanda wa Sungusungu, Hamisi Mkondo walithibitisha kutokea kwa kitendo hicho na kwamba tayari wamechukua hatua za kumwita ofisini mtuhumiwa huyo.

“Ni kweli tulipata taarifa za mtoto huyu kufanyiwa ukatili huu kwa kuchomwa moto na mama yake mzazi, ni jambo linalosikitisha, maana vitendo kama hivi watoto hutendewa na mama zao wa kambo, si mama mzazi, lakini huyo amemtendea mwanae wa kuzaa.

“Tayari tumechukua hatua za kumtaka afike ofisini ili tuweze kumsikiliza kwa kina sababu za yeye kuchukua hatua ya kumfanyia ukatili huu mwanae, na baada ya hapo hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa kwa kumfikisha kwenye vyombo vya dola,” ameeleza Mwenyekiti Issa.

Kwa upande wake Kamanda wa Mtaa, Hamisi Mkondo amesema mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani za kuumizwa kwa mtoto huyo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa ili kupata ukweli lakini alisema mwanaye wakati huo hakuwepo pale nyumbani.

“Sisi viongozi tulipoletewa taarifa tulifika kwa mama huyu kwa lengo la kumuona mtoto ili tuweza kubaini ameumia kiasi gani, lakini huyu mama alidai mwanaye hakuwepo pale nyumbani, ilibidi mimi nitumie nguvu na kuingia ndani, nikakuta mtoto kafichwa kwenye uvungu wa kitanda ambako nilimtoa nje,” ameeleza Mkondo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amesema, hakuwa na taarifa juu ya tukio hilo na kwamba atafuatilia na kisha atalitolea taarifa baada ya kupata habari kamili.

CHANZO - TIMES MAJIRA
Share:

ASKARI POLISI AJIUA MIEMBE SABA KIBAHA


NA VICTOR MASANGU, PWANI
ASKARI wa jeshi la Polisi aliyekuwa anafanya kazi katika kituo cha Polisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani namba E 6472 Yusuph Said mwenye umri wa miaka (52) amekutwa amejinyonga hadi kufariki dunia katika nyumba yake anayoijenga katika maeneo ya miembe saba kata ya Kongowe wilaya ya Kibaha.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea katika eneo la Miembe saba B kata ya Kongowe Wilayani Kibaha ambapo alisema tukio hilo lilitokea Januari 18 majira ya saa 12 jioni.

Kamanda Wankyo alisema Yusuph alikuwa akitumikia katika kituo c anaishi Picha ya ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.

Kamanda alibainisha kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kwenda kwao Lindi kwa maziko zikiendelea.

Msaidizi wa balozi kwenye eneo hilo Imelda Kitosi alisema akiwa nyumbani alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mtu kujinyonga ndipo akaenda kushuhudia akiwa na baadhi ya majirani.

Imelda alisema alipofika alielezwa na wazazi wa watoto waliokuwa na karibu ya eneo hilo kuwa kuna watoto waliokuwa wanacheza kombolela nje ya nyumba hiyo ambao walisema walisikia mtu anajipiga ndani ya nyumba na walipochungulia wakamkuta tayari yupo chini akiwa na kamba shingoni na walikimbia kwenda kutoa taarifa.

Wazazi hao walipofika katika nyumba hiyo ambayo bado inajengwa walimkuta askari huyo tayari ameshafariki ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa viongozi na kumpigia msaidizi huyo wa balozi.

"Mimi sasa baada ya kupigiwa simu niliingia hapa pamoja na baadhi ya watu waliokuwa karibu tulimkuta yuko kwenye chumba ambacho kilikua kinajengwa kama bafu au choo kamba kaifunga juu na chini kulikuwa na tofali ambalo baada ya kuhangaika sana mguu mmoja tulikuta kama umepiga goti na mwingine umeegemea tofali huku kamba ikiwa shingoni" alisema

Balozi huyo alieleza kuwa baada ya kushuhudia tukio hilo ndipo walipiga simu Polisi kutoa taarifa na walifika na kuchukua mwili wa marehemu.
Share:

KIJANA APIGWA SHOTI YA UMEME AKIIBA WAYA KWENYE TRANSFOMA

 
Na Florah Temba - Mwananchi
Riziki Mosha (23) mkazi wa mkoani Arusha amekamatwa na Shirika la umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za kuiba waya katika Transfoma iliyopo kijiji cha Mandaka Mnono Wilaya ya Moshi.
Tukio hilo limetokea leo Jumatano Januari 20, 2021 saa 12:00 asubuhi na alikamatwa kutokana na kushindwa kutembea kwa sababu ya majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa shoti ya umeme wakati akiiba waya huo katika njia kuu ya umeme ya msongo wa 33 Old Rombo kwenye Transfoma yenye uwezo wa KVA 100.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mnono Ndekio amesema alipata taarifa kutoka kwa wananchi saa 12:30 asubuhi na kufika eneo la tukio.

Amesema baada ya kufika eneo hilo alimkuta mtuhumiwa akijaribu kukimbia bila mafanikio, “alikuwa na majeraha ya moto na aliishiwa nguvi kabisa. Alikwenda kwenye moja ya duka na kuomba maji, hapo ndipo alipokamatwa.”

“Nikiwa na wananchi tuliona nyaya zimefunguliwa wakati tukiangalia jinsi zilizofunguliwa ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye shamba la mahindi alikuja mtu mmoja na kutuambia kuna kijana amemuona kwenye duka lililopo jirani akiwa amejifunika na shuka la kimasai na ana majeraha ya moto.”

"Tulimfuata na tulipomkuta alikiri yeye ndiye mhusika, tulimzuia na kutoa taarifa polisi na Tanesco na tayari wamefika kumchukua na kuona namna ya kushughulikia tatizo ili tuweze kurudishiwa umeme"

Akizungumza katika kituo cha polisi Mosha alikiri kuhusika na wizi huo na kusema ni tukio lake la tatu.

"Nilikuwa natafuta waya wa shaba ambao tunakwenda kuuza kama chuma chakavu, na nimefanya tukio hili likiwa la tatu na sikuwahi kukamatwa," amesema Riziki.

Via Mwananchi

Share:

MANISPAA YA SHINYANGA YAZUIA UINGIZAJI WA NGURUWE

 

Nguruwe

Na Josephine Charles
Manispaa ya Shinyanga imepiga marufuku kuingiza Nguruwe kutoka maeneo ambayo yameathirika na Homa ya Nguruwe ikiwemo Wilaya ya Kahama kutokana na homa hiyo kuzuka katika wilaya hiyo na kusababisha vifo vya nguruwe zaidi ya 500.

Marufuku hiyo imetolewa na Afisa Mifugo wa Manispaa ya Shinyanga, Chrispacy Kasimbazi wakati akizungumza katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja Fm Stereo kila jumatatu hadi ijumaa saa tatu asubuhi hadi saba kamili mchana.

Amesema wafugaji wote wanatakiwa kufuata utaratibu wa malisho ya nguruwe,kuwa na vitendea kazi maalum wakati wa kuwahudumia wakiwa kwenye banda lao ili kuwaepusha na homa hiyo kwa kuwa inasababishwa na kirusi ambacho hata binadamu anaweza kukibeba kutoka kwa nguruwe ambaye tayari anavyo akaenda kumhudumia nguruwe mwingine na kumsababishia maambukizi ya kirusi hicho kinachosababisha Homa ya nguruwe isiyo na chanjo wala Tiba.

Aidha, Kasimbazi ameeleza kuwa ugonjwa huo unaenezwa kwa njia ya virusi na unaambukizwa kwa njia ya nguruwe wenyewe wakiwemo nguruwe pori kukutana na nguruwe wanaofugwa na binadamu, kwa njia ya kupe, chakula, kinyesi au maji maji ya mwili.

Ameeleza dalili za Homa ya Nguruwe kuwa ni rangi nyekundu kama vile kuvia damu kwenye masikio, kifua, mapajani na maeneo mengine ya mwili wa Nguruwe lakini mbali na dalili hizo homa ya Nguruwe haiwezi muathiri kiumbe mwingine aidha binadamu au wanyama wengine isipokuwa ni nguruwe wenyewe kwa wenyewe.

Afisa Mifugo huyo ameelekeza wafugaji wote wa nguruwe kuwa endapo wataona dalili zozote kama hizo alizotaja na nyinginezo watoe taarifa haraka sana kwa afisa mifugo wa kata yake au aliyekaribu naye ili wapate maelekezo sahihi ya kuwaepusha nguruwe wengine na homa hiyo.

Siku chache zilizopita serikali wilayani Kahama ilipiga marufuku biashara ya uuzaji na ulaji wa nyama ya nguruwe wilayani humo kutokana na kuibuka kwa homa ya nguruwe na kusababisha vifo vya nguruwe zaidi ya 500.
Share:

TAKUKURU SHINYANGA YAREJESHA NYUMBA ZA MIL. 55 ZILIZOPORWA KWA MKOPO WA MIL. 5 KAMPUNI YA MSILIKARE

Mjasiriamali, Josephine Kiyuga (kushoto) akifurahia na kuonyesha hati za nyumba zake mbili zilizorejeshwa na kukabidhiwa kwake leo na Takukuru baada ya kuporwa na mmiliki wa kampuni ya kutoa mikopo ya Msilikare - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Na Damian Masyenene, Shinyanga
Nyumba mbili zenye thamani ya Shilingi Milioni 55 za mjasiriamali aitwaye Josephine Edward Kiyuga mkazi wa Viwanja vya Mwadui Manispaa ya Shinyanga, zimeokolewa na kurejeshwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Shinyanga baada ya kuporwa isivyo halali na Mmiliki wa kampuni ya kutoa mikopo ya Msilikare, Robert Manyanyiho.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Francis Luena akitoa taarifa ya utendaji kazi ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020-2021 (Oktoba-Desemba) mbele ya waandishi wa habari mjini Shinyanga leo, Mjasiriamali huyo ambaye anafuga kuku alikopa kiasi cha Sh Milioni 1.5 mnamo Septemba 19, mwaka jana kwa mmiliki wa kampuni ya Msilikare inayojishughulisha na kutoa mikopo katika Manispaa ya Shinyanga na kukubaliana kurejesha kiasi cha Sh Milioni 2.1 kwa muda wa mwezi mmoja.

Luena amesema, mnamo Septemba 25, mwaka jana mjasiriamali huyo alikopa tena kwa mmiliki huyo Sh Milioni 4 na kutakiwa kurejesha Sh Milioni 5.6 kwa muda wa mwezi mmoja lakini mmiliki wa kampuni hiyo alimuandikisha Mkopeshwaji mkataba wa mauziano ya nyumba na siyo mkataba wa ukopeshaji wa fedha. Hivyo basi, Jumla ya fedha alizokopeshwa ni Sh Milioni 5.5 ambazo alitakiwa kurejesha jumla ya Sh Milioni 7.7.

Hata hivyo, Mkopaji alifanikiwa kurejesha Sh Milioni 8 kama faida ya riba ya kuchelewesha kulipa deni, lakini mkopeshaji alikataa kurejesha hati za nyumba na kudai kuwa muda wa kurejesha deni ulishapita hivyo kama mkopaji anahitaji nyumba hizo inabidi azinunue tena kutoka kwake kwa gharama ya Sh Milioni 19 ili zitimie fedha hizo yaani Sh Milioni 19 mkopaji alitakiwa kuongeza Sh Milioni 11.

"Baada ya Takukuru mkoa wa Shinyanga kupata malalamiko hayo na uchunguzi kufanyika ilibaini kuwa mkopeshaji alikuwa na nia ya kujipatia nyumba hizo kwa njia isiyo sahihi. Hivyo basi, Takukuru mkoa wa Shinyanga iliweza kuziokoa nyumba hizo na zitakabidhiwa leo (Jumatano) kwa mwananchi huyo," alisema.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati za nyumba zake, Josephine Kiyuga ameeleza kuwa alipata matatizo katika biashara yake kwa kukosa chakula cha kuku hivyo akakutana na dalali ambaye alimuunganisha kwa Msilikare ili kupata mkopo, ambapo hatua zilifanyika na mmiliki wa kampuni hiyo akaenda kuziona nyumba na kukubali kumpa mkopo.

"Lakini alinigeuka, alifikia hatua ya kutaka kuuza nyumba zangu bila mimi kuwepo akiziita ni za kwake, akanipigia simu nikaondoe wapangaji. Nilifanya jitihada mbalimbali za kuongea nae na nikamlipa fedha lakini hakutaka kunipa nyumba zangu na nilikuwa nimekata tamaa baada ya jitihada mbalimbali kushindikana, ikabidi niende Takukuru ambao walinipa matumaini na hatimaye leo nimepata haki yangu, hili limenipa funzo kuwa makini na hii mikopo umiza," ameeleza.

Katika hatua nyingine, Takukuru imerejesha na kumkabidhi Mwalimu Mstaafu Sh Milioni 2.45 ikiwa ni sehemu ya Sh Milioni 45 zinazoendelea kurejeshwa zilizochukuliwa isivyo halali na wakopeshaji watatu tofauti ambao aliwalipa Sh Milioni 52, ambapo tayari Mwalimu huyo alikwishakabidhiwa Sh Milioni 26.6 katika kipindi cha Julai na Oktoba, mwaka jana.

Vile vile, Taasisi hiyo imefanikiwa kuzirejesha Jumla ya Sh Milioni 7.6 na kuwakabidhi wananchi mbalimbali waliokuwa wakidaiana wakiwemo wafanyabiashara, mafundi ujenzi na vibarua ambazo walidhulumiwa na mabosi wao.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga, Francis Luena, katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020-2021 (Oktoba - Desemba), imeendelea kufuatilia miradi ya maendeleo inayopewa fedha za serikali na ufadhili wa wadau wa maendeleo, ambapo imefuatilia miradi miwili yenye thamani ya Sh Bilioni 2.7, huku ikipokea taarifa 54 ambazo baadhi uchunguzi umekamilika na nyingine bado unaendelea.

"Katika kipindi hicho Jumla ya wananchi 10,002 wameelimishwa kupitia elimu kwa umma, pia tumeweka utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi siku moja kila mwezi kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao," amesema.
Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga, Francis Luena akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Shinyanga wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi ya taasisi hiyo kwa kipindi cha robo ya pili (Oktoba -Desemba) ya mwaka wa fedha 2020-2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga, Francis Luena akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Shinyanga wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi ya taasisi hiyo kwa kipindi cha robo ya pili (Oktoba -Desemba) ya mwaka wa fedha 2020-2021
Afisa Mchunguzi Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga, Emily Mandia (kulia) akimkabidhi hati za nyumba Mjasiriamali, Josephine Kiyugazilizorejeshwa na kukabidhiwa kwake leo na Takukuru baada ya kuporwa na mmiliki wa kampuni ya kutoa mikopo ya Msilikare
Mjasiriamali, Josephine Kiyuga (kushoto) akipokea hati za nyumba zake mbili zilizorejeshwa na kukabidhiwa kwake leo na Takukuru baada ya kuporwa na mmiliki wa kampuni ya kutoa mikopo ya Msilikare
Afisa Mchunguzi Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga, Emily Mandia (kulia) akiwakabidhi fedha baadhi ya wananchi waliokuwa wamedhulumiwa na watu mbalimbali

Picha zote na Kadama Malunde
Share:

ACHOMWA KISU AKIGOMBANIA BUKU 'SH. ELFU MOJA'


Na Anthony Mayunga - Mwananchi
Mwita Buruna (30), mkazi wa kijiji cha Rung’abure Wilaya ya Serengeti mkoani Mara amelazwa hospitalini baada ya kuchomwa kisu tumboni katika ugomvi wa kugombea Sh1,000.

Akisimulia tukio hilo lililotokea Januari 15, 2021 mwenyekiti wa kijiji cha Rung’abure, Joseph Meng’anyi amesema ugomvi kati ya wawili hao ulitokana na kupotea kwa simu ya kiganjani ya Burana wakati wakinywa pombe za kienyeji katika moja ya vilabu vinavyouza pombe za kienyeji kijijini hapo.

“Ugomvi huo ulitokea baada ya Buruna kugundua kupotea kwa Sh1,000 aliyoificha ndani ya mfuniko wa simu ndipo akamtaka Bisako kumrejeshea fedha yake bila mafanikio,” amesema Meng’anyi

Kutokana na Bisako kugoma kumrejeshea fedha yake, Burana aliamua kuchomoa kadi ya miziki aliyokuwa anatumia Bisako kupigia muziki na hivyo kuibua malalamiko kutoka kwa wateja kutokana na burudani kukatika.

“Baada ya mzozo wa muda mrefu, Bisako alirejesha Sh1,000 aliyoichomoa kutoka kwenye mfuniko wa simu ya Burana huku wawili hao wakianza kutoleana maneno makali kabla ya kusukumana nje walikoendelea na ugomvi,” amesema Meng’anyi

Amebainisha kuwa katika ugomvi huo, Burana alichomoa kisu kidogo alichokuwa nacho bila kujua mwenzake alikuwa na kisu kikubwa zaidi ambacho alikitumia kumjeruhi na kutokomea kusikojulikana hadi sasa.

Mganga Mkuu wa Hospitali teule ya Nyerere, Tanu Warioba amesema majeruhi huyo anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.

Via Mwananchi


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger