Wednesday, 2 December 2020

Picha : DC MBONEKO AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA....RPC SHINYANGA AONYA 'WATOTO KULALA NA WAGENI'

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amezindua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yakiongozwa na Kauli mbiu 'Tupinge Ukatili wa kijinsia, Mabadiliko yanaanza na mimi'. 

Akifungua maadhimisho hayo leo Jumatano Disemba 2,2020 katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga,Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mboneko amesema ni wajibu wa kila mtu katika jamii kushiriki kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, wanaume na watoto. 

“Ukatili wa kijinsia ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine, ni lazima kila mmoja ashiriki katika kuutokomeza kwani ukatili unapotokea katika jamii wanaoathirika zaidi ni wanawake na watoto”,amesema Mboneko. 

“Chapa kazi siyo kuchapa mke, mme au mtoto. Lakini pindi matukio ya ukatili ikiwemo ubakaji, mimba na ndoa za utotoni yanapotokea toeni taarifa kwenye vyombo vinavyohusika ili hatua zichukuliwe haraka kwani tunataka watu wote wawe salama”,ameongeza Mboneko. 

Katika hatua nyingine amewataka viongozi wa serikali kuanzia wa serikali za mitaa kusimamia ipasavyo haki za binadamu kwa kutoyafumbia macho matukio ya ukatili bali wachukue hatua haraka.

Mboneko amewashauri wawazi na walezi kutenga muda kwa ajili ya kukaa na watoto ili kubaini changamoto zinazowakabili lakini pia kuwaeleza madhara ya ukatili wa kijinsia. 

Mkuu huyo wa wilaya pia ametumia fursa hiyo kuwataka wanaume wanaofanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kupigwa na wake zao watoe taarifa kwenye mamlaka husika yakiwemo madawati ya Jinsia na Watoto. 

Pia amewataka wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia akisisitiza umuhimu wa kutumia wasanii wa nyimbo za asili kufikisha elimu katika jamii. 

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amesema jeshi la polisi kupitia Mtandao wa Wanawake Polisi na Dawati la Jinsia na Watoto wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia. 

Kamanda Magiligimba amesema hivi sasa kuna mwamko mkubwa wa jamii kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia akitolea mfano kuwa katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2020 kumeripotiwa matukio 231 ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikilinganishwa na kipindi cha Mwezi Juni hadi Agosti mwaka 2019 ambapo kulikuwa na matukio 151 ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

“Tunashukuru wananchi wameanza kuziamini ofisi za madawati ya jinsia takribani matano tuliyonayo katika mkoa wa Shinyanga ambapo wamekuwa wakitoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia. Lakini pia tunazishukuru taasisi na mashirika tunayoshirikiana nayo katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia”,amesema. 

Kamanda Magiligimba ametumia fursa kuwataka wazazi na walezi kuachana na tabia ya kuwalaza watoto kwenye chumba kimoja na wageni wanaofika nyumbani kwani baadhi yao siyo watu wema wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya ukatili watoto. 

“Matukio mengi ya ukatili katika na watu wetu wa karibu,ndugu zetu. Usikubali mgeni alale chumbani na mtoto wako. Usilaze mtoto chumba kimoja na mgeni kwani baadhi yao wanawafanyia ukatili ikiwemo kuwabaka na kuwalawiti watoto”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

“Naomba pia wazazi na walezi waache kumaliza kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia kifamilia. Mzazi usikae na kusuluhisha kesi ya mtoto kufanyiwa ukatili,toa taarifa ili watuhumiwa wachukuliwe hatua za kisheria ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia”,ameongeza. 

Aidha Kamanda huyo amezitaka familia kuacha kuficha matukio ya ukatili wa kijinsia na kulipana fidia watoto wakifanyiwa ukatili ili kumaliza kesi na kuhakikisha wanatoa ushahidi kuhusu matukio hayo sambamba na kuepuka kutoa ushahidi wa uongo hali ambayo inakwamisha kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack leo Jumatano Disemba 2,2020 katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga. Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yameandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakiongozwa na Kauli Mbiu ya 'Tupinge Ukatili wa Kijinsia,Mabadiliko yanaanza na mimi" - Picha zote na Kadama Malunde & Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack leo Jumatano Disemba 2,2020 katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga. Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yameandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mwakilishi wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT) mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga, Magreth Abuor akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, ACP Africanus Sulle akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mkuu wa Dawati la Jinsia la Watoto mkoa wa Shinyanga , Victoria Maro akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Uhuru Edward Kulwa akiimba shairi wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Vijana kutoka kikundi cha burudani cha Kambi ya Nyani wakitoa burudani
Kwaya ya AIC Shinyanga ikitoa burudani.
Burudani ikiendelea 
Burudani ikiendelea
Wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru wakionesha igizo
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Meza kuu wakifuatilia burudani kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wadau wakiwa kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Askari polisi wakiwa wamebeba bango wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Askari polisi na wadau wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Wanafunzi wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Askari polisi wakiwa wamebeba bango wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wanafunzi wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wanafunzi wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Waendesha bodaboda wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Askari polisi wakiwa wamebeba bango kwenye Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

- Picha zote na Kadama Malunde & Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Share:

Wahamiaji haramu 34 wakamatwa Simiyu.

Samirah Yusuph
Busega. Wahamiaji haramu 34 raia wa Ethiopia wamekamatwa katika kitongoji cha Mwalukonge kijiji cha Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu.

Wahamiaji hao wameingia nchini kupitia mpaka wa Sirari Mkoani Mara ambapo afisa uhamiaji mkoa wa simiyu  Mariam Mwanzalima aliviambia vyombo vya habari kuwa wamewakamata watu hao mashambani.

"Kwa mujibu wa maelezo yao walikuwa wanaelekea Malawi  na walikuwa  wenyeji watatu ambao ni wakenya wawili na mtanzania mmoja ambao walikuwa wanawasafirisha kwa kutumia mchomoko (noah).

Wakaingia mtafaruku na wenyeji wao baada ya kuwashusha kwenye gari na kutaka kuwapandisha mtumbwi ndipo walipoanza ugomvi na kundi hili lilikimbia kuelekea mashambani.

Huko tulipata taarifa na askari wetu kwa kishirikiana na askari wa jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuwakamata,"

Mwisho.

Share:

Rais Mwinyi Ateua Wakuu wa Mikoa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi,  jana Desemba Mosi, 2020,  ameteua wakuu wa mikoa, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 61 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, walioteuliwa ni Idrissa Kitwana Mustafa, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi; Ayoub Mohammed Mahmoud (Kaskazini Unguja) na Rashid Hadid Rashid (Kusini Unguja).

Wengine ni Salama Mbarouk Khatib (Kaskazini Pemba) na  Mattar Zahor Masoud (Kusini Pemba).

Share:

DPP Afafanua Alivyomtoa Gerezani Kada CHADEMA Nusrat Hanje

Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga ametoa ufafanuzi kuhusu kumfutia mashitaka kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Nusrat Hanje ambaye alivuliwa uanachama Novemba 27 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Biswalo amesema kesi ameifuta yeye kwa mamlaka aliyonayo kisheria chini ya kifungu cha 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Amesema wanaolalamika kuwa amemfutia kesi kada huyo kinyume na taratibu wanakiuka utaratibu .

Biswalo amesema sheria ipo na inafanyakazi zake na hakuna kufanya kazi kwa upendeleo.

Share:

Waziri Mkuu Awaonya Wataalamu Wa Ununuzi Naugavi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi ambao bado wanaendekeza vitendo viovu kama rushwa, upendeleo, kuingilia michakato ya ununuzi kwamba waache mara moja kwani Serikali haitomhurumia yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumatano, Desemba 2, 2020) alipofungua Kongamano la 11 la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Kongamano hilo la siku tatu linatarajiwa kufungwa Desemba 4, 2020.

“Mjitahidi kuwa mstari wa mbele kuepuka vitendo viovu vinavyohusishwa na fani hii ya ununuzi na ugavi. Mtambue sheria kali zipo na kwamba Serikali haitakuwa na huruma kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa. ”

Pia, Waziri Mkuu amezitaka taasisi zote zitekeleze maagizo ya Serikali ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao kwa kupitia mfumo wa kisasa wa manunuzi unaofahamika kwa jina la TANePS, ambao unasaidia kuongeza kasi ya utekelezaji, uwazi, kupunguza gharama na mianya ya rushwa.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi zinazolenga kupunguza au kuondoa kabisa uzembe na ukiukwaji wa maadili katika fani ya ununuzi na ugavi kwani pesa nyingi za serikali, zinatumika kupitia taaluma hiyo.

Amesema manunuzi katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali ni zaidi ya asilimia 70, hivyo shughuli hiyo isipofanyika kwa kuzingatia weledi ni dhahiri kuwa wananchi hawataweza kupata huduma iliyokusudiwa na miradi haitatekelezwa kwa viwango kusudiwa.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu ameitaka bodi inayosimamia taaluma hiyo ijiridhishe kwamba wataalamu wanaofanya manunuzi wana sifa stahiki na lazima watahiniwe ili kuhakikisha wana viwango na maadili yanayotakiwa.

 “Bodi katika kusimamia weledi wa wataalam wa manunuzi na ugavi ihakikishe inafanya kazi kwa umakini, weledi na uadilifu ili kuhakikisha haki inatendeka bila ya uonevu, pia wakuu wa taasisi wote nchini wawatambue maafisa manunuzi na ugavi kwa kiwango sawa na timu ya menejimenti ili wazishauri taasisi husika ipasavyo.

Waziri Mkuu amewataka wataalamu wa manunuzi na ugavi wahakikishe wanatoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi kwa kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi ya umma ili kupata matokeo yenye uthamani wa fedha iliyotumika.

“Simamieni vizuri uandaaji wa mikataba ya manunuzi ili kuepuka nyongeza ya kazi (Variations) na hivyo kuziepusha taasisi katika gharama zilizo nje ya bajeti kwa kuzingatia uwepo wa uwazi katika utayarishaji na utekelezaji wa zabuni ikiwemo kujiepusha na migongano ya kimaslahi au kufuata maelekezo kutoka kwa watu wenye kutaka kufikia malengo binafsi.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema amefarijika sana na mada kuu ya kongamano hilo ambayo ni “Wajibu wa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Katika Kufikia Ubora wa Juu wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ununuzi na Ugavi” kwa lugha nyingine “Reaching Excellence in Procurement Supply Chain and Management)”.

“Mada hii imejikita katika kutambua wajibu wa wataalam wa ununuzi na ugavi katika kufikia ubora wa juu wa usimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi. Serikali inatambua umuhimu wa taaluma hii kwani ndiyo wasimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi kwa taasisi za umma na sekta binafsi.

Amesema wakati huu ambao Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na kuibua miradi mipya katika sekta mbalimbali za kiuchumi, utekelezaji madhubuti wa miradi hiyo unategemea sana weledi na ujuzi wa wataalam hao.

Waziri Mkuu amesema kuwa uzembe na ukosefu wa weledi katika kusimamia mnyororo wa ununuzi na ugavi unachangia kukwamisha utekelezaji wa miradi au kufanyika chini ya kiwango na aghalabu kutokamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kila mwaka TSPTB imekuwa ikiandaa kongamano kwa ajili ya kutafakari mwenendo halisi wa ununuzi na ugavi nchini ili kubaini kasoro, msfanikio na kushauri namna ya kuboresha.

Amesema kongamano la mwaka huu litajikita kujadili namna ya kufikia umahiri katika kusimamia mnyororo wote wa ununuzi na ugavi ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia, mbinu mpya za kuhakikisha manunuzi yanaendana na thamani ya fedha zilizotumika pamoja na mafanikio na changamoto za kutumia mfumo wa force account.

“Matumaini yangu na Wizara ya Fedha ni kuwa kongamano hili litawatendea haki Watanzania hasa wanyonge, ambao fedha zao zinaibiwa kutokana na udhaifu mkubwa katika manunuzi na ugavi kwenye Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji. Mada ziwasilishwe kwa lugha ya kiswahili ili tuelewane vizuri katika jitihada za kufyeka kichaka cha wizi, ubadhilifu, rushwa na ufisadi kupitia ununuzi na ugavi.”

Waziri Dkt. Mpango amesema Maafisa Ununuzi na Ugavi hawazingatii maadili ya taaluma zao na kwamba uzalendo wao ni wa mashaka, wanatumia utaratibu wa force account kama kichaka cha kuiba, mfano wa bei za vifaa zinazotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zinatumika nchini kote.

“Mlango shilingi 400,000 Uvinza, Dar es Salaam na Mwanza. Bei ya tofali la block shilingi 2,000 inatumika hata pale wanapotumia tofali za udongo za kuchoma, pia bei ya lori la mawe shilingi 180,000 Mwanza, Dodoma, Mbeya, Kisarawe. Hii si sawa kwani hata katika maeneo ambayo vifaa vinapatikana kwa ukaribu bei ilingane na maeneo ambayo vifaa vinapatikana mbali.”

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi, Godfred Mbanyi alisema Bodi imeandaa kongamano hilo kwa lengo la kuwakutanisha na kuwaleta pamoja wataalamu wa ununuzi na ugavi na wadau wengine ili waweze kujifunza, kujadili na kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi kwenye maeneo yao ya kazi.

Pia, katika kongamano hilo mada sita zinazotokana na mada kuu isemayo kufikia ubora wa juu katika usimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi zitajadiliwa. Ambapo, madhaifu na changamoto zinazojitokeza katika michakato ya manunuzi, zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na kuweka maazimio na mikakati ya utatuzi wake ili Serikali iweze kupata thamani ya fedha katika manunuzi yake.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, DESEMBA 2, 2020

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger