Tuesday, 24 November 2020
Monday, 23 November 2020
TPDC YANG’ARA MASHINDANO YA SHIMUTA TANGA YAILIZA TBS
TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ambao waliigaragaza TBS set 2-0 kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popataly Jijini Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ambao waliigaragaza TBS set 2-0 kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popataly Jijini Tanga walifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza mchezo wao
NA MWANDISHI WETU,TANGA
TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) leo wameibuka na ushindi wa seti 2-0 katika mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya timu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika muendelezo wa michuano ya Shimuta inayoendelea Jijini Tanga.
Kwa upande wa wanaume walivuta kamba na chuo cha DIT jana na kupata seti 2-0 na leo wamevuta na chuo cha IAA na kupata mivuto 2-0 na wanaamini mechi zilizobaki wataendelea kushinda na kutinga hatua ya fainali.
Mchezo huo wa uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Popatlal Jijini Tanga leo ulionekana kuwa na upinzani lakini TPDC ambao walikuwa wamesheheni wachezaji mahiri na wenye viwango waliweza kuwagaragara wapinzani wao.
Akizungumzia ushindi huo na namna walivyojipanga kuelekea kwenye michezo yao mengine,Kocha wa timu hiyo Joram Ndalalwa alisema timu hiyo imejipanga vizuri kunyakua ubingwa kwenye michuano hiyo.
Joram alisema kila wakati mara baada ya kumalizika kwa mchezo mmoja wanarudi kujitafakari na kujipanga upya kuona namna ya kujiandaa vema .
Alisema baada ya kumalizika mchezo huo na kuweza kuibuka na ushindi wanarudi kujipanga kwa ajili ya mchezo wao unaofuata dhidi ya ATC utakaochezwa Novemba 23 mwaka huu asubuhi na jioni watapambana na UDSM.
Akizungumzia mashindano hayo Katibu wa Michezo kutoka TPDC Elinaike Naburi alisema kwamba walishiriki mashindano hayo ya shimuta mwaka huu ikiwa ni mara yao ya tano mpaka sasa wamekwisha kushiriki michezo wa mpira wa miguu,wavu,pete,kikapu pamoja na michezo ya Jadi,Karata,Table na Draft.
Alisema mchezo wa vishale watamaliza kuanzia Novemba 24 na 25 watafanya mbio mpaka sasa wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 katika mpira wa miguu na Pete waliishia kwenye makundi kwa kuwa mshindi wa tatu huku Wavu wakiishia kwenye makundi lakini walionyesha ushindani mkubwa.
Kikapu waliishia kwenye makundi lakini ushindano wao ulikuwa wa hali ya juu katika michezo ya jadi wameshinda kwa kuwa mabingwa karata upande wa wanawake na mshindi wa pili upande wa wanaume.
Katika mchezo wa drafti alisema waliishia hatua ya robo fainali upande wa wanaume huku wanawake wakiishia hatua za makundi na mchezo wa Pooltable wanawake wamefanikiwa kutetea taji lao kwa kuwa mshindi wa pili mwaka jana mshindi wa kwanza na wanaume waliishia nusu fainali.
Alisema kwamba katika mchezo wa bao wachezaji wao wote wameishia hatua ya nusu fainali huku akieleza malengo ya mashindano hayo kwa TPDC ni kuonyesha ushindani wa hali ya juu.
Alisema pia malengo yao ni kuweza kufahamiana na Taasisi nyengine kujenga mshikamano kama wafanyakazi na kuendelea kutoa morali na motisha kwa wafanyakazi kuendelea kushiriki michezo kwa sababu ni afya.
Hata hivyo alisema wamefurahi kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na wanaamini wametoa ushindani wa kutosha na wataendelea kufanya hivyo michezo yao iliyobaki.

SERIKALI YA TANZANIA YASEMA IMEONGEZA UWEZO WA KUGUNDUA WAGONJWA WAPYA WA KIFUA KIKUU
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akigawa cheti cha pongezi kwa Uongozi wa Afya wa Mkoa wa Manyara kupitia Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Damas Kayera mara baada ya kushika nafasi ya kwanza ngazi ya mikoa kwa kufanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa afua za kupambana na kifua kikuu na ukoma.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akisema jambo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akisema jambo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe akisema jambo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Jijini Dodoma.Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma wakisikiliza mada zinazotolewa kwenye mkutano.
Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma wakiwa katika picha ya pamoja.
***
Na Englibert Kayombo WAMJW - Dodoma
Serikali ya Tanzania imeazimia kutokomeza kabisa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuongeza uwezo wa ugunduzi wa wagonjwa wapya wa kifua kikuu na kuwaweka kwenye matibabu.
Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu an Ukoma uliofanyika Jijini Dodoma.
“Uwezo wa nchi kugundua wagonjwa wapya na kuwaweka kwenye matibabu umeongezeka kutoka wagonjwa 62,908 (33%) mwaka 2015 na kwa sasa kufikia wagonjwa 82,166 (59%)” amesema Prof. Makubi
Kufuatia hatua hiyo Prof. Makubi amesema kuwa maisha ya wananchi takribani 300,000 ikiwemo ya watoto 45,000 yameponywa kwa kupatiwa dawa kwa wakati na kufuatiliwa kwa usahihi kuanzia mwaka 2015 hadi sasa.
Juhudi hizo pia zimeweka kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na kifua kikuu kwa 33%. “Mwaka 2015 kulikuwa na vifo 30,000 hivi sasa vimepungua hadi kufikia vifo 20,000” amesema Prof. Makubi.
Prof. Makubi amesema kuwa mafanikio hayo ya ongezeko la kasi ya ugunduzi wa wagonjwa wapya yametokana na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma ikiwemo kuboresha huduma za ugunduzi wa TB na kutoa kipaumbele kwa makundi yaliyoathirika zaidi kama vile kaya zenye wagonjwa, wanaoishi kwenye kaya duni, gerezani, wachimbaji wadogo wadogo na kwa waathirika wa madawa ya kulevya.
“Aidha tumewekeza katika afua bunifu mbalimbali za matumizi ya teknolojia mpya za molekyula za kubaini TB kwa usahihi na kwa haraka” amesisitiza Prof. Makubi.
Awali akizungumza, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi amesema Wizara imefanya vizuri kwenye kwa kufikia malengo waliyoyaweka kwenye Mpango mkakati ambao unamalizika mwaka huu 2020.
“Malengo ambayo tulijiwekea ya kupunguza vifo vitokanavyo na kifua kikuu tumeweza kuyafikia pamoja na kupunguza madhaa yanayotokana na ugonjwa huo” amesema Dkt. Subi
Amesema kuwa Serikali imefanikiwa kuongeza vituo vya upimaji wa kifua kikuu sugu kutoka kituo 1 mwaka 2015 hadi kufika vituo 145 hivyo kuongeza wigo wa huduma za matibabu ya ugonjwa huo
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Dkt. Ntuli Kapologwe amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana Wizara ya Afya katika kipindi cha miaka 5 ijayo imejiwekea mikakati ya kuwawezesha watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wawe na ujuzi na uwezo wa kutambua na kutoa huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu.
TIMU YA WAZIRI MKUU YAKABIDHI MALI ZA SHIRECU ZILIZOPORWA. ..LIMO GHOROFA LA ILALA DAR
Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Shinyanga (SHIRECU) Asangy Bangu, (kulia), akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, Hati Saba za viwanja, pamoja na nyumba na ghala, ambazo ni mali tena za SHIRECU zilizokuwa zimeporwa na kuuzwa kinyume na taratibu.
Na Marco Maduhu - Shinyanga.
Timu ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, iliyoudwa kwa ajili ya kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliporwa na kuuzwa kinyume na utaratibu, imekabidhi baadhi ya mali na kumilikiwa tena na chama hicho.
Akikabidhi Hati za viwanja, pamoja na nyumba na ghala leo, Mwenyekiti wa timu hiyo Asangy Bangu, amesema wamefanikiwa kurudisha viwanja saba vilivyopo mkoani Shinyanga, nyumba ghorofa tatu ambayo ipo Ilala, pamoja na ghala lililopo Kurasini Jijini Dar es salaam, ambazo ni mali za Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU).
Amesema zoezi hilo la kufuatili mali hizo za SHIRECU, walilifanya kwa kupitia nyaraka za chama hicho,pamoja na kuhoji watu ambao walikuwa wameuziwa wakiwamo watumishi wa Serikali na watu binafsi, na kufanikiwa kukomboa viwanja hivyo saba, ghala, pamoja na nyumba na kwamba wanaendelea kufuatilia mali zingine.
"Leo tunakabidhi hati saba za mali za Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na taratibu, kuwa rasmi mali za chama hiki tena, na zoezi hili litakuwa endelevu ili kurudisha mali zote," amesema Bangu.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, ameipongeza timu hiyo kwa kufanya kazi kwa uzalendo, ambayo ilikuwa na mizengwe mingi, huku akiutaka uongozi wa SHIRECU, kuzitunza mali hizo na zisiweze kurudi tena mikononi mwa watu binafsi.
Amesema zoezi hilo la kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), pamoja na vyama vingine ikiwamo Nyanza cha Jijini Mwanza, na KNCU cha Kilimanjaro, lilianza mwaka 2016, ambapo Rais Magufuli aliagiza mali hizo zifuatiliwe, ndipo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akaunda timu ya kufuatilia mali za vyama hivyo.
Ameongeza kuwa Jijini Mwanza tayari jana wameshakabidhi mali za Nyanza, na sasa wanaelekea mkoani Kilimanjaro kukabidhi mali za KNCU.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, ametaka watu ambao waliuza mali hizo za SHIRECU na kuisababishia hasara kubwa wawajibishwe, ili kuwa mfano kwa watumishi wengine ambao siyo waaminifu na kuuza mali za umma.
Pia amekitaka chama hicho baada ya kupata mali hizo, kijiendeshe kibiashara pamoja na kukuza miradi yao kuinuka kiuchumi, ikiwamo na Shule ya Sekondari Buluba, kurudi kwenye hadhi yake ya kufaulisha wanafunzi kwa kuajiri walimu wazuri.
Aidha Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU), mkoani Shinyanga Lenis Jishanga, ameishukuru timu hiyo kuwarudishia mali zao, na kuahidi kuzitunza pamoja na kujiendesha kibiashara zaidi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akizungumza kwenye makabidhiano ya mali za SHIRECU.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, akizungumza kwenye makabidhiano ya mali za SHIRECU.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), Lenis Jishanga, akishukuru kupata mali hizo na kuahidi kuzitunza.
Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Shinyanga (SHIRECU) Asangy Bangu, (kulia), akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, hati saba za viwanja, pamoja na nyumba na ghara, ambazo ni mali tena za SHIRECU zilizokuwa zimeporwa na kuuzwa kinyume na taratibu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wa pili kushoto, akimkabidhi katibu mkuu wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, hati Saba za viwanja, nyumba na ghala, ambazo ni mali rasmi tena za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, meza kuu akimkabidhi Mwenyekiti wa (SHIRECU) Lenis Jishanga, Hati saba za viwanja, nyumba na ghala, ambazo ni mali tena za chama hicho, wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, kushoto, akishikana mkono na mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga Lenis Jishanga, mara baada ya kukabidhiwa mali za SHIRECU, ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Zainab Telack, kushoto, akishikana mkono na mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga Lenis Jishanga, mara baada ya kukabidhiwa mali za SHIRECU, ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.

Picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU).
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
HIACE YAPINDUKA NA KUUA WATU NANE BUKOBA

Watu wapatao nane wamepoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari la abiria lenye namba za usajili T.471 DCG linalofanya safari za kubeba abiria kutoka Kemondo kwenda Bukoba Mjini, baada ya gari hilo kufeli breki na kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea Novemba 22 saa 1:45 usiku na gari hilo aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T. DCG lilikuwa likiendeshwa na Ismail Rashid (37) mkazi wa Kemondo.
Via Mwananchi