Friday, 13 November 2020

HUYU NDIYO MILIONEA GENIUS 'GINIMBI' ATAKAYEZIKWA NA GUNIA LA FEDHA...'WAOMBOLEZAJI KUVAA NGUO NYEUPE TU'


Marafiki wa milionea raia wa Zimbwabwe, Genius Kadungure aliyejulikana kama Ginimbi kwa muktadha wa kijamii, wamesema atazikwa na gunia lilojaa Dola, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Mfanyabiashara huyo aliyeishi maisha ya kifahari aliacha maagizo hayo kwa wanachama wa "all-white funeral", kama ilivyoandikwa na gazeti la Herald.

Ginimbi alifariki kutokana na ajali ya gari Jumapili, jijini Harare pamoja na mlimbwende Mitchelle Amuli aliyejulikana kama Moana.


Familia ya Moana imetaka fedha za mazishi kutoka kwa wanaowafariji.


Familia imeahirisha mazishi kwa wiki mbili ikisubiria majibu ya DNA na kukusanya michango ya kifedha kwa ajili ya kumuaga kwa heshima, imeripotiwa na Zim Morning post.


Matajiri wa Zimbabwe wamekuwa wakiahidi fedha kwa ajili ya mazishi ya Ginimbi.

Naibu Waziri Tino Machakaire ameahidi kununua jeneza kubwa kwa ajili ya Ginimbi, Mbunge Temba Mliswa amechangia wanyama wengi kwa ajili ya kuchinjwa kwenye mazishi hayo.

Wakati mwanasiasa Acie Lumumba ameahidi lita 1000 za mafuta ya dizeli, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani.

Ginimbi na Maona kwa pamoja walikuwa wanatoka kwenye sherere ya "all-white" ambapo gari yao iligongana na gari nyingine iliyokuwa inakuja mbele yao, ilichepuka nje ya barabara na kugonga mti kisha kulipuka moto.

Sherehe ya Ginimbi ya kuvalia mavazi meupe maarufu 'All White Party'

Ginimbi Genius Kadungure alijulikana kama mfalme wa mitindo mbali na kufanya sherehe kubwa .

Mwaka 2010 alifanya sherehe kubwa ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambapo waliohudhuria walivaa mavazi meupe maarufu kama all White party mjini Harare Zimbabwe , sherehe hiyo ilizungumziwa sana mjini humo .

Miaka miwili baadaye mwaka 2012 alisimamia maadhimisho ya siku nyengine ya kuzalia kwake.

Mwaka 2013, Ginimbi aligharamia sherehe ya siku tatu katika kijiji cha kwao huko Domboshava ili kusherehekea nyumba mpya aliyojenga katika eneo hilo
Familia ya milionea maarufu nchini Zimbabwe, Ginimbi Genius Kadungure - aliyefariki na ajali ya gari Novemba 8, inasema watu watakaoudhuria mazishi ya milionea huyo siku ya Jumamosi lazima wavaa nguo nyeupe.

Mavazi hayo meupe yatavaliwa kama sawa na wakati alipokuwa hai, aliandaa sherehe na kutaka kila mmoja apendeze kwa kuvaa nguo nyeupe.

Vilevile alikuwa anawakumbusha mara nyingi kuwa hivyo ndivyo angependa kuzikwa , watu wasiwe na haraka haraka ya kumzika na wavae nguo nyeupe katika mazishi yake.

"Mchukue muda kupanga mazishi yangu. Nitahitaji kila anayehudhuria mazishi yangu avae nguo nyeupe tu, kupendeza ni lazima siku hiyo.

Tafadhali kumbuka kuchukua muda wenu muwezavyo kupanga mazishi yangu. Kumbuka ,nitakuwa nimevalia nyeupe tu. Hicho tu ndio ninakihitaji kwenye mazishi yangu." Juliet ambaye ni dada yake alinukuu maneno ya kaka yake alivyosisitiza kabla ya kifo chake.

Ginimbi Genius Kadungure, alifariki siku ya Jumapili , majira ya asubuhi katika mji wa Borrowdale, Harare, Zimbabwe.

Jina lake halisi ni Genius Kadungure na alikuwa maarufu kwa jina la Ginimbi.

Alizaliwa Oktoba 10,mwaka 1984. Hivyo amefariki akiwa na miaka 36.
Alikuwa mfanyabiashara maarufu , alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya Piko Trading Holdings & Founder of Genius Foundation, na mmiliki wa klabu ya Sankayi (AKA Dreams Nightlife Club).

Alikuwa na 'Master of Business Administration - alipata MBA yake katika chuo kikuu cha at Great Zimbabwe.

Aliishi: Govan Mbeki, Mpumalanga, Afrika Kusini ingawa nyumbani ni Harare, Zimbabwe.
Moana mlimbwende aliyefariki katika ajali pamoja na Genius Kadungure

Mlimbwende huyu alikuwa maarufu Zimbabwe, alifariki akiwa kwenye gari moja na milionea Ginimbi Genius Kadungure.


Jina lake kamili ni Michelle Moana Amuli.

Ripoti zinasema kulikuwa na zaidi ya abiria mmoja na wote walifariki ndani ya gari lililopata ajali baada ya gari hilo kuwaka moto.

Kwa mujib wa ripoti ya polisi, Ginimbi, Moana na abiria wengine wawili walikuwa wametoka kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Moana aliyekuwa anatiiza miaka 26.

Kwa mujibu wa iHarere News, abiria wengine wawili ni Rolls Royce Wraith na Limumba Karim - mmoja akiwa raia wa Malawi na mwingine raia wa Msumbiji alifahamika kama 'Elisha'.

CHANZO - BBC
Share:

IT Digital Channel Officer at KCB Bank

Key Responsibilities Provide technical support for digital channels applications by performing administrative role on the applications. Provide technical support during implementation of tasks related to digital channel projects. Provide monitoring for channels system to increase system availability Ensure all faults of the existing channel services and provide strategic initiative that will improve customer experience and […]

The post IT Digital Channel Officer at KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Account Officer at Tanzania Girl Guides Association (TGGA)

About Us Tanzania Girl Guides Association (TGGA) is a volunteer membership or­ganization aiming at empowering girls and young women socially and economically through informal education. TGGA is a Member Organization of the World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS) with more than 10 million members world­wide. Girl Guides and Girl Scouts is the […]

The post Account Officer at Tanzania Girl Guides Association (TGGA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

LIVE: Rais Magufuli analihutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma

 LIVE: Rais Magufuli analihutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma

Share:

Publicity & Training Coordinator at Tanzania Girl Guides Association (TGGA)

About Us Tanzania Girl Guides Association (TGGA) is a volunteer membership or­ganization aiming at empowering girls and young women socially and economically through informal education. TGGA is a Member Organization of the World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS) with more than 10 million members world­wide. Girl Guides and Girl Scouts is the […]

The post Publicity & Training Coordinator at Tanzania Girl Guides Association (TGGA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

National Secretary at Tanzania Girl Guides Association (TGGA)

About Us Tanzania Girl Guides Association (TGGA) is a volunteer membership or­ganization aiming at empowering girls and young women socially and economically through informal education. TGGA is a Member Organization of the World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS) with more than 10 million members world­wide. Girl Guides and Girl Scouts is the […]

The post National Secretary at Tanzania Girl Guides Association (TGGA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mawaziri Wawili


Rais, Dkt. John Magufuli ameteua mawaziri wawili wa Baraza jipya la mawaziri leo, Novemba 13.

Uteuzi huo ni wa Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, nafasi aliyokuwa nayo katika baraza lililopita.

Pia, Prof. Palamagamba Kabudi ameteuliwa kuendelea kushika nafasi aliyokuwa nayo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


 


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Novemba 13



Share:

Thursday, 12 November 2020

MBUNGE MTATURU AANZA AWAMU YA PILI KWA KISHINDO.... AUZA VITABU VYA SH.MILIONI 28 NA KUTOA PIKIPIKI SITA


Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi Kitabu cha Misemo na Methali za Wanyaturu katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mjini hapa jana. 
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) Singida, Alex Mkumbo, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Mbunge wa Iramba  Mwigulu Nchemba,  akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Ni furaha tupu wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akinunua moja ya kitabu hicho kwa sh.milioni moja.
Burudani ikitolewa kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 ***

Na Dotto Mwaibale, Singida.

MBUNGE wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameanza kazi kwa kishindo  katika kipindi chake cha awamu ya pili  kwa kuzindua kitabu na kufanikisha kununuliwa kwa thamani ya sh.milioni 28.

Kitabu hicho kinachoitwa Misemo na Methali za Wanyaturu kilichoandikwa na Mchungaji Dkt.Syprian Yohana Hilinti (PhD) kilizinduliwa jana katika Kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) Singida mjini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi huku mshereheshaji wa hafla ya  uzinduzi wa kitabu hicho akiwa ni Mbunge wa Iramba,  Mwigulu Nchemba.

Katika uzinduzi huo Mtaturu ambaye alikuwa mgeni rasmi alinunua kitabu kimoja kwa sh.milioni moja jambo lililoongeza ari ya watu waliokuwepo kwenye hafla hiyo kujitokeza na kununua vitabu hivyo kwa fedha taslimu.

Katika hatua nyingine Mtaturu alinunua pikipiki sita kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kanisa hilo mkoani humo ambapo pia Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba alichangia pikipiki tatu jumla zikiwa tisa.

Askofu wa kanisa hilo Mkoa wa Singida, Alex Mkumbo aliwashukuru wabunge hao kwa msaada huo.

Share:

SERIKALI KUTOA ELIMU YA SHERIA KWA VIONGOZI WA MABARAZA YA ARDHI NGAZI ZA KATA

 

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Amir Mruma akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo imeadhimishwa kitaifa mkoani Tanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Amon Mpanju akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo imeadhimishwa kitaifa mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Amir Mruma kulia akifurahia jambo wakati alipofika kutembelea banda la Tawla Mkoa wa Tanga kulia wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella

Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali

 
Serikali inatarajia kutoa elimu ya sheria kwa viongozi wa mabaraza ya ardhi walioko katika ngazi ya kata ili waweze kutatua migogoro kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Amir Mruma wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo imeadhimishwa kitaifa mkoani Tanga.

Alisema Kuwa hapo awali viongozi wa mabaraza hayo yalikuwa hawana elimu ya kisheria katika eneo lao la kazi hivyo walikuwa wanashindwa kuendesha kesi zao kwa sheria na taratibu zilizotungwa na Bunge.

"Kwa utaratibu huu wa sasa uliwekwa na serikali itarahisisha utendaji kazi wa mabaraza hayo lakini hata kesi zinapofika katika ngazi ya Mahakama ,maji wataweza kutuma maamuzi yaliyotolewa katika ngazi ya baraza Kama sehemu ya maelezo ya kesi "alisema Jaji Mruma.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Amon Mpanju alisema kuwa wiki ya msaada wa kisheria imekuja kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanyonge ambao walikuwa wanashindwa kupata haki zao.

Alisema kuwa wiki hiyo wataitumia kwa ajili ya kuwatembelea wananchi ambao wamefungwa katika maeneo mbalimbali ili kuwasaidia kutoa msaada wa kisheria .

"Kutoa elimu kwa viongozi wa vitongoji na mitaa ili kutatua kero zinazowakabili wananchi kwa kujua sheria husika kusimamia majukumu yao vizutina kupunguza malalamiko na kero zinazowakabili wananchi"alisema Naibu Katibu Mpanju.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela alisema katika mkoa huo zipo kero nyingi ambazo zinazogusa maslahi ya wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Alisema kuwa katika jitihada za kutafuta ufumbuzi wa kero ni wamekiwa wakiwashirikisha wanasheria kutoka Chama Cha wanasheria ili kuwasaidia kupata ufunguzi wa migogoro ya ardhi .

"Niwaombe wananchi kutumia wiki hiyo kupata misaada ya kisheria katika kero mbalimbali wanazokabiliana nazo pamoja na kupata elimu ya kisheria ambayo itaweza kuwasaidia kufanya maamuzi mbalimbali"alisema RC Shigela
Share:

RC TANGA NA TAN TRADE KUSHIRIKIANA UHAMASISHAJI WENYE VIWANDA KUSHIRIKI MAONYESHO YA VIWANDA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano wa wadau wa viwanda mkoani Tanga kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Latifa Mohamed Khamisi
NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Latifa Mohamed Khamisi akizungumza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
AFISA wa  Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gibson George  akizungumza wakati wa mkutano huo
MKURUGENZI Mkazi wa Kampuni ya Simba Cement Mhandisi Benedict Lema akichangia jambo kwenye  mkutano huo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu wadau wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali
SEHEMU ya Wadau wa Viwanda mkoani Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali

 

NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Latifa Mohamed Khamisi amesema kwamba watashirikiana kwa ukaribu na wenye viwanda mkoani Tanga kuhakikisha wanafanikiwa na kuendelea kukua kibiashara.

Latifa aliyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na wadau wa viwanda Mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo wamefika mkoani Tanga kuona namna ya kutatua changamoto za wenye viwanda hatimaye viweze kuzalisha na kuuza kwenye masoko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma

Alisema hilo litasaidia kwa asilimia kubwa kurudisha enzi za miaka ya nyuma ambako kulikuwa na masoko mpaka ya ukanda wa afrika masharika pamoja na masoko ya ndani ili kuwawezesha kuweza kunufaika kupitia viwanda hivyo.

“Leo tumefika mkoani Tanga kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella tunatoa shukrani kwa kutupokea na kukubali agizo la Rais la Tanzania ya Viwanda”Alisema

 Alisema kwamba mkoa huo unawaunga mkono kwenye maandalizi ya maonyesho makubwa ya kitaifa ya viwanda vya Tanzania kwa kushirikiana na mkoa kuhamasisha viwanda vya Tanga kuweza kushiriki.

“Kama unavyofahamu Tanga kulikuwa na historia kubwa ya viwanda ambavyo vilikuwa vinauza bidhaa kwenye ukanda wa Afrika vilikuwa vinatoka Tanga lengo la RC ni kuhakikisha viwanda hivyo vinafufuka na ndio maana tupo hapa kwa kushirikiana na mkoa tumefika kuhamasisha ushiriki wa maonyesho ya Tano ya viwanda vya Tanzania”Alisema

Alisema kwamba maonyesho hayo ni fursa adimu kwa viwanda ikiwemo kujifunza na kujua mashine na kuwakutanisha wazalishaji wa mali ghafi na wenye viwanda wenyewe kutatua changamoto za maendeleo ya viwanda.

Awali akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alimshukuru Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade kwa kuandaa mkutano huo wa wamiliki na wazalishaji katika sekta ya viwanda kwenye mkoa wa Tanga.

Alisema kikao hicho ni mahususi kuona changamoto ambazo zinawakabili lakini kuona namna nzuri wanaweza kushiriki kwenye maonyesho ya Tan Trade yatakayoanza Desema 3-9 mwaka huu.

Alisema kwao ni fursa kwa wazalishaji na viwanda ikiwemo wakazi wa mkoa huo kwa sababu kadri viwanda vinavyozidi kupanuka kimasoko ndio uzalishaji unaongeza na unapoongeza unasaidia uhitaji wa malighafi na wafanyakazi ili uweze kuongeza uzalishaji.

“Niwashukuru Tan Trade kuendesha kikao hichi na kuamua kuja Tanga kwa sababu Tanga ni viwanda na viwanda ni Tanga lakini la la pili uwepo wa maonyesho hayo ni fursa kwa wawekezaji watatumia nafasi hiyo kujitangaza na kujifunza na kuona fursa zinazopatikana kwenye maonyesho”Alisema

Hata hivyo alisema wao kama mkoa watahakikisha Tantrade na wenye viwanda kuendelea kuwapa ushirikiano ili dhamira ya Rais ya yenzi wa uchumi wa viwanda iweze kufikiwa kwa kiwango kikubwa na kuwa na tija kubwa.

Share:

Katibu Mkuu Prof. Msanjila Afungua Fursa Kwa Kampuni Ya Aga Bullion Kuwekeza Kwenye Sekta Ya Madini Nchini.


Katibu  Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila leo Novemba 12, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo na kampuni ya AGA Bullion kutoka Nchini Uturuki  ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma ambayo imeonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya madini Nchini.


Katibu Mkuu Msanjila aeleza Tanzania ina masoko mengi makubwa ya Dhahabu  kuanzia mkoani Geita, Mwanza, Kahama na Chunya ambayo AGA Bullion wanaweza kuwekeza, kununua na kusambaza dhahabu kwa wingi hapa nchini.  Msanjila ametaka kampuni ya AGA Bullion kuwafikia wachimbaji wadogo na kati na kutoa mfano wa mgodi wa dhahabu wa Busolwa ambao unafanya kazi vizuri.


Amesisitiza Uwekezaji unaopangwa kufanyika na  kampuni ya AGA Bullion usilenge  kwenye ununuzi na usambazaji wa dhahabu pekee bali kuwekeza pia kwenye madini mengine yanayopatikana nchini yakiwemo  madini ya Tanzanite yanayopatikana mkoani Manyara, vilevile  kupata leseni ili waweze kuchimba  madini  nchini. 


Prof. Msanjila ameitaka Kampuni ya Aga Bullion kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya Madini  wakiwemo  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambao hutoa huduma na ushauri wa kitaalam na kiufundi katika sekta ya madini wakiwemo wachimbaji wadogo kwenye nyanja za kijiolojia, Tume ya Madini na kukutana na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA),  ili waweze kujadili pamoja.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mwanzilishi wa AGA Bullion, Sarp Tarhanaci amemueleza Katibu Mkuu Prof. Msanjila kuwa Kampuni ya Aga Billion inamiliki viwanda viwili vya usafirishaji wa dhahabu (Refineries) katika nchi za Umoja wa Falme za kiarabu (Dubai) na Uturuki, wanauzoefu katika ununuzi wa dhahabu kutoka katika mataifa mbalimbali kama vile Ghana, Burkina Faso, Peru, Malaysia na Uturuki.


Mkurugenzi Mwanzilishi Sarp Tarhananci akijibu hoja ya Katibu Mkuu kuhusu kukutana na wadau wengine wa Sekta ya Madini amesema tayari kampuni hiyo tarehe 10/11/2020 imekutana na kufanya mazungumzo na Tanzania Chambers of Mines (TCME) ambapo imepokea taarifa za uzalishaji na mauzo ya dhahabu, Tarehe 11/11/1010 ilikutana na Mkurugenzi wa Masoko ya Kifedha  wa Benki Kuu ya Tanzania ili kueleza nia yake ya kutaka kutoa huduma ya usafirishaji wa dhahabu, bima na kutafuta masoko ya kimataifa ya dhahabu iliyosafirishwa kwa gharama ya 0.5% hadi 0.8% ya thamani ya madini hayo.


Aidha amesema, kampuni ya AGA Bullion kwa kiasi kikubwa imemueleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini dhamira ya kufanya biashara ya madini ya dhahabu kutoka wa wachimbaji wadodo, pamoja na wachimabji wa kati ikiwemo kuwawezsha mitaji ya fedha ili waweze kuzalisha zaidi. Pia kampuni hiyo imezungumzia namna ya kuanzisha kiwanda cha  uongezaji thamani madini ya dhahabu (jewellery industry) kwa kutengeneza bidhaa zake kama vile pete, herein na mikufu.

Vilevile, kampuni hiyo imeeleza nia yake ya kutoa ushauri kwa Benki Kuu ya Tanzania, kuhusu namna ya kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo na kuwaweesha kifedha pamoja na utunzaji dhahabu kwenye accredited vaults za kimataifa kabla ya kuuza. Hata hivyo, Benki Kuu ya Tanzania ilieleza kampuni hiyo kuipatia taarifa zaidi za huduma zao.


Kikao hicho pia kimehudhuriwa na kamishina wa Madini Muhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Nchasi na wadau kutoka AGA Bullion kwa pamoja wamehaidi kuwekeza katika biashara ya madini hususan dhahabu  nchini.



Share:

Dkt. Tulia Ashinda Unaibu Spika – Video


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mhe.Dkt. Tulia Ackson kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12.

Dkt. Tulia ameshinda kwa kishindo baada ya kupata  kura 350 ambapo  wapiga kura walikuwa 354 .

Uchaguzi huo umefanyika leo tarehe 12 Novemba 2020, jijini Dodoma ambao ulitanguliwa na uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Akiomba kura kwa wabunge Mhe. Dkt. Ackson amesema kuwa atajitahidi kuwatumikia wabunge wote bila kujali tofauti za kisiasa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha amesema kuwa atamshauri  vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumia uzoefu alionao  ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.


Share:

GEMMA ASHAURI WANAUME WAWE NA NIDHAMU KWENYE NDOA ZAO ...."ACHENI KUBAKA WAKE ZENU"

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger