Tuesday, 7 April 2020

Kenya yapiga marufuku usafiri katika miji iliyoathirika na virusi vya corona

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jana ametangaza kusitishwa kwa safari zote katika maeneo yaliyoathirika na virusi vya corona nchini humo. 

Katika hotuba aliyoitoa , Kenyatta ametaka kusitishwa kwa usafiri wote wa umma kwa njia ya barabara, reli na hata ndege katika kaunti ya Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale kwa siku ishirini na moja ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona. 

Marufuku hayo yameanza kutekelezwa jana saa moja jioni  huko Nairobi na kuanzia siku ya Jumatano huko Mombasa, Kilifi na Kwale. 

Hapo awali rais Uhuru alitangaza marufuku ya nchi nzima ya kutotoka nje usiku ila maambukizi yanaonekana kuongezeka huku visa vya maambukizi vikifikia 158 baada ya kuripotiwa visa vyengine sita jana. 

Idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo imeongezeka pia na kufikia watu sita.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo 7 April 2020




















Share:

Monday, 6 April 2020

Tanzia : MWANDISHI WA HABARI ELIYA MBONEA AFARIKI DUNIA

Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya 

New Habari 2006 Ltd Eliya Mbonea amefariki dunia leo Jumatatu Aprili 6,2020 wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (Arusha Press Club), Claude Gwandu amethibitisha taarifa za kifo cha Eliya Mbonea alipozungumza na Malunde 1 blog mchana huu.

"Ni kweli ndugu yetu Elia Mbonea ametutoka mchana huu.Alikuwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kumtoa hospitali ya KCMC hivi karibuni. Tutapeana taarifa zaidi baadaye",amesema Gwandu.

Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Elia Mbonea. Amina

Share:

Health Workforce Specialist Job opportunity at ICAP Tanzania

Health Workforce Specialist Job Opportunity at ICAP Tanzania Deadline Date: Monday, 20 April 2020 Position Summary: ICAP at Columbia University seeks experienced and qualified experts to serve as a Health Workforce Specialist for several proposed CDC-funded projects related to improving and protecting global health security (GHS) through developing capacities of government health ministries, institutions, and local partners; strengthening health… Read More »

The post Health Workforce Specialist Job opportunity at ICAP Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Employment Opportunities at The Tanzania Civil Aviation Authority, (TCAA)

3.0 THE TANZANIA CIVIL AVIATION AUTHORITY- (TCAA)  The Tanzania Civil Aviation Authority, (TCAA) was established by the enactment of the  Tanzania Civil Aviation Authority Act 2003 Cap 80 (R.E 2006) to regulate the civil aviation  industry in the United Republic of Tanzania in order to ensure effective implementation of  Standards and Recommended Practices (SARPs) as provided in the… Read More »

The post Employment Opportunities at The Tanzania Civil Aviation Authority, (TCAA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Surveillance Lead Job Opportunity at ICAP Tanzania

Position Summary: Organization: ICAP Country: United Republic of Tanzania Deadline Date: Monday, 20 April 2020 ICAP at Columbia University seeks experienced and qualified experts to serve as Surveillance Lead for several proposed CDC-funded projects related to improving and protecting global health security (GHS) through developing capacities of government health ministries, institutions, and local partners; strengthening health information and surveillance… Read More »

The post Surveillance Lead Job Opportunity at ICAP Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Environment Officer, P3, Kibondo at UN High Commissioner for Refugees

Organizational Setting and Work Relationships Deadline Date: Thursday, 16 April 2020 Organization: UN High Commissioner for Refugees Country: United Republic of Tanzania City: Kibondo The Environment Officer will work closely with colleagues responsible for protection, site planning, water and sanitation, shelter, nutrition, education, health, community services and livelihoods. The incumbent will support the UNHCR Office on all issues related to environment and… Read More »

The post Environment Officer, P3, Kibondo at UN High Commissioner for Refugees appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

New Jobs The Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS)

2.0 MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES (MUHAS) The Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) started as the Dar-es-  Salaam Medical School in 1963. The School transformed into the Faculty of Medicine of  the University of Dar-es-Salaam in 1968. The Faculty was merged with the Muhimbili hospital, to create the Muhimbili Medical Centre (MMC) in… Read More »

The post New Jobs The Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Grants Manager Job at Tetra Tech International Development Services- The USAID Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA)

Grants Manager Job at Tetra Tech International Development Services- The USAID Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA) Tetra Tech International Development Services (https://ift.tt/2xle9Na) headquartered in Arlington, VA is currently accepting expressions of interest from qualified candidates for a potential Grants Manager position on the USAID funded Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA). Deadline Date: Thursday, 30 April 2020 The USAID Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA) is… Read More »

The post Grants Manager Job at Tetra Tech International Development Services- The USAID Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Picha : RC TELACK AKABIDHI VIFAA VYA MILIONI 10.7 KUJIKINGA NA CORONA SHINYANGA WAKATI WA MATIBABU......WASIONAWA KUCHUKULIWA HATUA



Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile Methylated Sprit 'Sanitizer' ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation leo Jumatatu Aprili 6,2020 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile Methylated Sprit 'Sanitizer' ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, Sriex Premium Latex ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (katikati) akiwa ameshikilia Barakoa ' Mask' akiangalia pamba aliyokabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rose Malisa.
Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) akimwelezea Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack kuhusu vidonge vya Chlorine vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rose Malisa.
Sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation. 
Sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiangalia vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mganga Mkuu Mkoa w Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akiwashukuru wadau wa sekta ya afya waliochangia upatikanaji wa vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwashukuru wadau wa sekta ya afya waliochangia upatikanaji wa vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwashukuru wadau wa sekta ya afya waliochangia upatikanaji wa vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza umuhimu wa kunawa muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakati akikabidhi vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza umuhimu wa kunawa muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga. “Kunawa ni jukumu letu sote. Uwe mtoa huduma wa afya uwe mwananchi. Naweni mikono kwa sababu mikono haipungui nguvu kwa kunawa".

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amekabidhi vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile kwa ajili ya kuzigawa katika halmashauri za wilaya ili kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation. 

Hafla fupi ya Makabidhiano ya vifaa hivyo imefanyika leo Jumatatu Aprili 6,2020 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu huyo wa mkoa amewashukuru wadau wote wa afya waliochangia kupatikana kwa vifaa hivyo wakiongozwa na Touch Foundation iliyotoa shilingi milioni 10.4 na wadau wengine walichangia shilingi 300,000/= na kufanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu.

“Tunawashukuru wadau wanaoshughulika na afua za afya katika mkoa wetu,nakumbuka siku ya Ijumaa wili iliyopita tulikaa kikao cha pamoja nao na waliahidi,na mmoja kati ya walioahidi moja kwa moja ni Touch Foundation kwamba wangetoa shilingi milioni 10 na tunashukuru kuwa ahadi yao leo imetekelezeka”,amesema Telack.

“Tunawashukuru sana Touch Foundation na wadau wengine naamini huko waliko wanaendelea kujikusanya kutusaidia ili kama mkoa tuweze kuhakikisha kuwa kama kutatokea mgonjwa yeyote basi tunaweza kumhudumia kwani lengo ni kumhudumia mgonjwa na tunamkinga mtoa huduma wetu kwenye vituo tulivyovitenga ili aweze kumhudumia mgonjwa lakini na yeye abaki salama”,amesema Telack.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono huku akibainisha kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaokaidi kufuata maelekezo ya kunawa mikono.

“Tumeshatoa elimu ya kutosha,hakuna mahali ambapo hatujapita,sasa ni wakati wa kuchukua hatua wale ambao kwa maksudi kabisa wanakataa kunawa tuchukue hatua,tupige faini na wale wanaokaidi kabisa tupeleke kituo cha polisi ili hatua nyingine zichukuliwe ili tuiache Shinyanga ikiwa salama na nchi kwa ujumla kutokana na Corona”,amesema Telack.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kunawa mikono ni jukumu la kila mtu . “Kunawa ni jukumu letu sote. Uwe mtoa huduma wa afya uwe mwananchi. Naweni mikono kwa sababu mikono haipungui nguvu kwa kunawa. Na nyinyi watoa huduma naomba muwe mstari wa kwanza kuhakikisha kuwa mnapoingia pale mlangoni mnanawa mikono yenu muoneshe mifano ili wananchi waige kutoka kwenu”,amesema Telack.

“Kazi kubwa tuliyonayo ni kuhakikisha kwamba tunachukua tahadhari,tujikinge na tuwakinge wengine kwa kunawa mikono. Kwa Maafisa afya muda huu siyo wa kukaa maofisini,ni muda wa kupita kwenye maeneo ya kazi,kwenye ofisi zote,kwa wafanyabiashara kuhakikisha kuwa watu wote wananawa mikono” ,amesema Telack.

“Niwaombe sana watoa huduma kaeni tayari kwa chochote kitakachojitokeza kwa sasa tunamshukuru Mungu kwamba mkoa wetu bado upo salama lakini sisi siyo Kisiwa,pamoja na kuomba Mungu kaeni tayari,jiandaeni kwa ajili ya chochote kile kitatokea,muwe tayari kwenda kutoa huduma na sisi tutaendelea kutafuta kila njia kupata Protective Gears ili muweze kuwa salama wa mnapokwenda kutoa huduma”,ameongeza Telack.

Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amevitaja miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na wadau wa sekta ya afya mkoani Shinyanga kuwa ni Surgical gloves, Non Sterile gloves,Barakoa ‘Mask’,Methylated Spirit, vidonge vya Chlorine na pamba.

“Wiki iliyopita tulikaa na wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga na kwa pamoja wakakubaliana kwamba watachangia na kusaidia mkoa wa Shinyanga katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona. Siku hiyo tulipata mchango wa mtu mmoja mmoja ukiachilia mbali mashirika yao waliweza kuchangia kiasi cha shilingi 300,000/= na kiasi hicho tumeweza kununua vifaa na tunaye mdau Touch Foundation ambaye ametoa pia vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 10.4”, amesema Dkt. Ndungile.

Amesema vifaa vilivyopatikana vitagawiwa katika halmashauri zote za wilaya mkoani Shinyanga.
Share:

Jobs at Kibaha Education Centre

1.0 KIBAHA EDUCATION CENTRE  Kibaha Education Centre is a multi-purpose educational institution situated in Pwani  Region 40 kilometers (24 miles) West of Dar es Salaam along Morogoro Road. The Centre was started in 1963, sponsored by five countries – The then Tanganyika  Government on one hand and the Government of the four Nordic Countries which are Denmark, Finland, Norway and… Read More »

The post Jobs at Kibaha Education Centre appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob atangaza kutogombea tena udiwani

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob ametangaza kutogombea tena nafasi ya udiwani wa kata ya Ubungo katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020 nchini Tanzania.
 
Boniface Jacob ametangaza uamuzi huo kupitia mtandao wake wa Twitter 

 “Nimetangaza kung'atuka ktk udiwani kata ya Ubungo muda wa madiwani utakapo isha, sitogombea tena udiwani uchaguzi ujao..! Miaka 10 utumishi wangu ni kwa sababu Wana-Ubungo mlinikopesha imani. Tumekuwa wote wakati wa shida na raha, mabonde na milima.” Ameandika


Share:

Watumishi wa Wizara ya Habari wapewa Mafunzo ya Kujikinga na COVID-19

Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamepata mafunzo kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19) katika mazingira yao ya kazini pamoja na maeneo mengine wanayokuepo. 
 
Akizungumza na watumishi hao leo katika ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma, Afisa Afya kutoka Idara ya Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Yusuph Seif amesema kuwa Serikali ipo mstari wa mbele kuhakikisha watumishi na wananchi wanapata elimu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo ili kuliweka taifa na watu wake katika hali ya usalama dhidi ya ugojnwa huo.
 
“Virusi hivi ni kabila jipya la virusi vya Corona ambavyo vimegunduliwa mwaka 2019 ambavyo vinasababisha homa kali ya mapafu, kila mtu aendelee kuchukua tahadhari kwa kujikinga na ugonjwa huu” alisema Bw. Yusuph.
 
Bw. Yusuph ametaja baadhi ya dalili ambazo zinapelekea mtu kushukiwa kuwa ameambukizwa ugonjwa huo ni pamoja na kuwa na homa kali zaidi ya nyuzi joto 38, kukohoa kikohozi kikavu pamoja na mwili kuuma na kuishiwa nguvu.
 
Ameongeza kuwa ili  kujikinga na ugonjwa huo mtaalamu ni vyema kila mtu awe umbali wa zaidi ya mita moja, kutokusalimiana kwa kushikana mikono, kunawa mikono ipasavyo kwa maji tiririka kwa sabuni ya kutosha yenye kutoa povu jingi angalau kwa zaidi ya sekunde 20 sehemu zote za kiganja cha mkono.
 
Aidha, amesema kuwa matumizi ya vitakasa mikono (sanitizer) ni njia mojawapo ambayo mtu anaweza kuitumia ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni njia sawa na mtu aliyenawa vizuri kwa kutumia maji tiririka na sabuni.
 
Kuhusu matumizi ya barakoa, Bw. Yusuph amesema kuwa barakoa zinatumiwa na watu wenye dalili za Covid-19, watoa huduma za afya wanapowahudumia wagonjwa ama mtu yeyote anapokuwa kwenye eneo la hatari ya kuwepo au kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
 
Akimkaribisha mtoa mada, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Bw.Bernard Marceline amewataka watumishi hao kutumia fursa hiyo kujifunza namna ya kujikinga na ugonjwa huo ili waweze kutunza afya zao na wawe wajumbe wa kutunza afya za wengine  pamoja na familia zao ili kuwa salama na hatimaye nchi nzima iwe salama na kujikinga na ugonjwa huo. 
 
Akishukuru kwa niaba ya watumishi Bw.Johanssen Kaimukirwa ameishukuru Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kazi nzuri wanayoifanya ili watu wote waelewe hatua ambayo itasaidia kujikinga zaidi.
…MWISHO..


Share:

Takukuru Dodoma Yaokoa Tsh.297,115,474 Na Kushikilia Magari Matatu




Share:

Sekta mbalimbali zinavyoshirikiana katika kupambana na Coronavirus

Wote kote duniani hivi sasa wanapambana na tatizo la ugonjwa wa Coronavirus. Serikali zote barani Afrika kwa namna mbalimbali zinapambana kuhakikisha maambukizi hayasambai.

Tanzania nako hali ni hiyo hiyo. Hatua mbalimbali zimechukuliwa kupunguza mikusanyiko mfano kufunga mashule na kuzuia mikutano ya hadhara na michezo. Hata watu binafsi nao wanabadili mwenendo wao wa maisha kuwa kupunguza idadi ya watu wanaokutana nao.

Sekta ya biashara nayo vivyo hivyo. Baadhi ya hoteli zimesimamisha huduma kwa muda kupunguza uwezekano wa maambukizi huku sekta ya kilimo ikizidisha nguvu kuhakikisha chakula kinapatikana. Ama kwa hakika, ugonjwa huu umeonyesha namna sekta mbalimbali zimejiunga pamoja kukabiliana na adui na uzoefu huu utasaidia sana ziku zijazo hasa katika kufanya maamuzi ya kijamii na kibiashara.

Kwa mfano inafahamika wazi kwamba kampuni ya Tigo nchini Tanzania iko katika hatua za kuorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam baadaye mwaka huu jambo ambalo lingewezesha umma kununua hisa hizo, swali linabaki kwamba, mlipuko huu wa ugonjwa huu utalazimu kuchelewa kwa hatua hiyo chanya kwa sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania?

Wataalamu wa uchumi na biashara wanaeleza kuwa zoezi hilo huleta pamoja wadau katika mikutano mingi kulijadili kabla ya kukamilisha na kuongeza iwapo litacheleweshwa kutokana na janga hili vikao vya wadau kukutana uso kwa uso havitakuwepo msimu huu.

Nyakati hizi za sintofahamu tunapata faraja kwa habari chanya kuhusu tunapoelekea kama nchi na dunia nzima. Hata hivyo ni wakati sahihi pia wa kutofanya yale ambayo yanaweza kusubiri mpaka wakati sahihi lakini lengo iwe ni kusaidia umma.


Share:

Applications For admission into higher degrees academic year-2020/2021

Applications For admission into higher degrees academic year-2020/2021 Applications are hereby invited for admission into Higher Degrees at Sokoine University of Agriculture (SUA) for the academic year 2020/2021. Candidates for Postgraduate Diploma, Master and PhD Degree programmes with course work are admitted and registered  once every year for an academic year that starts in October of each year. Candidates for Master… Read More »

The post Applications For admission into higher degrees academic year-2020/2021 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Vacancies at Tanzania Shipping Agencies Corporation (TASAC) and Marine Services  Company Limited (MSCL)

Job Vacancies at Tanzania Shipping Agencies Corporation (TASAC) and Marine Services  Company Limited (MSCL)   PRESIDENT’S OFFICE  PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT  Ref.No.EA.7/96/01/K/180 31st March, 2020  VACANCIES ANNOUNCEMENT- RE-ADVERTISED On behalf of Tanzania Shipping Agencies Corporation (TASAC) and Marine Services Company Limited (MSCL), Public Service Recruitment Secretariat invites dynamic and  suitably qualified Tanzanians to fill 3 vacant posts.    1.0… Read More »

The post Job Vacancies at Tanzania Shipping Agencies Corporation (TASAC) and Marine Services  Company Limited (MSCL) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger