Monday, 6 April 2020

Tanzia : MWANDISHI WA HABARI ELIYA MBONEA AFARIKI DUNIA

...
Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya 

New Habari 2006 Ltd Eliya Mbonea amefariki dunia leo Jumatatu Aprili 6,2020 wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (Arusha Press Club), Claude Gwandu amethibitisha taarifa za kifo cha Eliya Mbonea alipozungumza na Malunde 1 blog mchana huu.

"Ni kweli ndugu yetu Elia Mbonea ametutoka mchana huu.Alikuwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kumtoa hospitali ya KCMC hivi karibuni. Tutapeana taarifa zaidi baadaye",amesema Gwandu.

Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Elia Mbonea. Amina

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger