Friday, 28 February 2020

Makamu wa rais wa Iran athibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona

Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia mambo ya wanawake na familia Bibi Masoumeh Ebtekar jana amethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona.

Mapema jana mwenyekiti wa kamati ya usalama wa taifa na sera za kidiplomasia wa Iran Bw. Mojtaba Zonnour, ambaye pia amethibitishwa kuambukizwa virusi, ametoa wito kwa raia wa Iran wawe watulivu na kusema, nchi yao ina uwezo wa kushinda mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Habari zinasema, ibada ya sala ya ijumaa mjini Tehran imefutwa kutokana na mlipuko wa virusi hivyo.


Share:

NATO Kukutana Kwa Dharura Leo Baada ya Wanajeshi 33 wa Uturuki Kuuawa Syria

Baraza la kiutawala la Jumuia ya Kujihami ya NATO linakutana leo katika kikao cha dharura kuhusu mzozo wa Syria, baada ya wanajeshi wapatao 33 wa Uturuki kuuawa katika shambulizi la anga huku wengine wengi wakijeruhiwa vibaya..

Baraza hilo ambalo linawajumuisha mabalozi wa nchi zote 29 za NATO wanakutana baada ya Uturuki kuomba mazungumzo yafanyike chini ya kifungu cha 4 cha Mkataba wa NATO, kuhusu hali ya Syria. 

Kulingana na kifungu hicho, mwanachama yeyote wa NATO anaweza kuomba mazungumzo yafanyike iwapo ataamini kuwa kuna kitisho katika uhuru wake wa kisiasa au usalama. 

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg ametoa wito wa mapigano kusitishwa na amelaani mashambulizi ya anga katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu.


Share:

Kauli Ya Kwanza Ya Benard Membe Baada ya Kufutwa Uanachama wa CCM

Muda mfupi baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt Magufuli  kumfuta uanachama wa CCM Bernard Membe, Waziri huyo wa zaman wa Mambo ya Nje amefunguka na kutoa kauli.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Membe amewataka wafuasi wawe watulivu na kwamba ataliongelea hilo muda si mrefu.


Share:

Breaking News: BENARD MEMBE AFUKUZWA CCM....MAKAMBA ASAMEHEWA, KINANA APEWA KALIPIO


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt Magufuli katika kikao cha kawaida cha Kamati hiyo kilichoketi leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es salaam imeazimia kumfukuza uanachama Bernard Membe.


Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho Yusuf Makamba, amesamehewa kutokana na kuomba kusamehewa makosa aliyokuwa akidaiwa kuyatenda  ya kwenda kinyume na maadili ya chama hicho. 

Aidha, Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana,amepewa adhabu ya kalipio kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho.


Share:

BARABARA ZILIZOHARIBIWA NA MVUA UKEREWE KUANZA KUTENGENEZWA



Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoana serikali za Mitaa Josephat Kandege akiwa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Maendelea pamoja na barabara zinazotengenezwa na Tarura.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoana serikali za Mitaa Josephat Kandege akiwa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Maendelea pamoja na barabara zinazotengenezwa na Tarura.


Na Geofrey A. Kazaula - UKEREWE
Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Mhe, Josephat Kandege ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kufanya ukarabati kwa barabara zilizoharibiwa na mvua Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.


Ameyasema hayo alipotembelea barabara hizo ili kujionea hali halisi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Mwanza.

‘‘TARURA mnafanya kazi nzuri ila nitoe wito kuwa pale mnapo endelea na ujenzi wa barabara hizi mjitahidi kuangalia maeneo korofi yaliyoharibiwa sana ndo mkaanze nayo ili wananchi hawa wapate huduma’’, amesema kiongozi huyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa barabara za Vijijini kutoka TARURA Mhandisi Abdul Digaga amesema kuwa tayari kuna fedha kiasi cha Sh 50 Millioni zilizoletwa Ukerewe kwaajili ya kufanya matengenezo ya barabara hasa kwa maeneo yaliyoharibiwa na mvua ambapo Meneja wa TARURA Katika Halmashauri ya Ukerewe Mhandisi Reuben Muyungi amekiri kupokea fedha hizo na kwamba Mkandarasi tayari amepatikana na kazi itaanza wiki ijayo.

Naye Mbunge wa Ukerewe Mhe, Joseph Mkudi amesema kuwa kazi inayofanwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini - TARURA ni kubwa na kusema kuwa kuna haja ya Serikali kuongeza bajeti ya Wakala huo ili uweze kutekeleza majukumu yake kwa urahisi kwani kazi inayofanyika inaonekana licha ya ufinyu wa bajeti.

‘‘Mimi kama mbunge nitaendelea kujenga hoja kwa Serikali ili iongeze bajeti ya TARURA barabara zetu ziweze kutengenezwa kwa urahisi na kuwapatia wananchi wetu huduma’’ amesema Mkudi.

Mmoja wa wananchi Katika Kata ya Ukerewe Ndg,Nesphory Kangi amesema kuwa TARURA inasaidia sana kuwajengea barabara na miundombinu miingine na na kwamba kuna upungufu wa barabara za lami ambapo ameomba Serikali iwaongezee barabara hizo.

Miradi mingine iliyokaguliwa na Mhe, Kandege ni pamoja na Kituo cha Afya cha Busya -Ukara, Vikundi vya akina mama vinavyokopeshwa na Halmashauri kupitia mgawanyo wa asilimia kumi ya mapato ya ndani pamoja Ujenzi wa Vyumba vya madarasa vine na Ofisi moja ya Walimu Katika shule ya Msingi Murunsuli ambapo pia ameweka jiwe la Msingi.
Share:

PICHA: Rais Magufuli Akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa Ya CCM Dodoma

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti  Rais John Magufuli wakiwa katika kikao cha kawaida cha Kamati Kuu kinachoendelea katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es salaam.


Share:

Waziri Simbachawene Apiga Marufuku Polisi Kukamata Wananchi, Bodaboda Bila Kufuata Utaratibu

Na Mwandishi Wetu, MOHA, Mpwapwa.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amepiga marufuku ukamataji wa wananchi, bodaboda pamoja na kufanya operesheni ya aina yoyote kwa kukurupuka bila kufuata utaratibu, hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani badala ya kujenga amani.

Pia Waziri huyo aliagiza kuwa, kila operesheni itakayopangwa kufanywa na Polisi Nchini, wanapaswa watoe taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ili ajue nini kitafanyika kwa kuwa yeye ni Mwenyikiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, na pia ndio utaratibu unapaswa kuwa hivyo.

Akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma na baadaye kulisisitiza agizo hilo katika Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya, leo, Simbachawene alisema ukamataji usio na mpangilio hauna tija na unaweza kuvunja amani badala ya kujenga amani.

“Wananchi wanawalalamikia askari wetu sana kukamata bodaboda bila sababu, sio bodaboda tu hata kukamata kamata hovyo watu, ukamataji mwingine unakua kama kukomoana, hauna tija, hauleti amani, badala yake unasababisha amani itoweke,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, “Yaani msako fulani unatungwa hauna kichwa wala mguu, hauna maelekezo yoyote ya Mkuu wa Jeshi la Polisi au chombo, ni watu tu wanajitungia wanaondoka na pikipiki yao wamepakiana wanaenda kufanya operesheni ambayo haina utaratibu.”

Alisema vyombo vya ulinzi na usalama ni vya wananchi, na operesheni yoyote haipaswi kufanyika bila Mkuu wa Wilaya kupewa taarifa ambapo ndio utaratibu unapaswa kuwa hivyo.

Pia Waziri Simbachawene aliupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuifanya Wilaya hiyo kuendelea kuwa na amani na utulivu na wananchi kuendelea kuwa na imani na viongozi hao.

“Endeleeni kuwa karibu na wananchi, kwa kusikiliza kero zao na pia kuzitatua, na epukeni malalamiko ya hapa na pale yasiyokuwa ya lazima,” alisema Simbachawene.

Aidha, Simbachawene aliewaomba viongozi wa Wilaya hiyo kujipanga vizuri katika maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

“Mwaka huu ni wa uchaguzi, wananchi kupitia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na taasisi zote za utawala, mnapaswa kuwa na ushirikiano mkubwa ili kujenga msingi wa uchaguzi utakaokuwa wa amani na utulivu,” alisema Simbachawene.

Alisema mwaka wa uchaguzi haupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao unapaswa kuwa na utulivu kwasababu ni jambo zuri la kidemokrasia linafanyika.

“Rai yangu kwa wananchi, kuhakikisha kwamba tunapaswa kujenga utulivu kuanzia sasa kuelekea uchaguzi mkuu, hatupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao amani na utulivu wa nchi unajengwa kuanzia sasa, mshikamano wa vyombo vyetu ndio msingi wa kujenga uchaguzi utakao kuwa wa huru na haki ambao utafanya mwaka huu,” alisema Simbachawene. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jabir Shekimweri alimshukuru Waziri huyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yake aliyoyatoa katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Kikao cha Baraza la Madiwani.

Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa (OCD), ASP Maulidi Manu alisema ujio wa Waziri huyo umewasaidia zaidi kwa kujipanga zaidi, na kufuata maagizo yote aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi Wilayani humo.

“Tumefarijika kwa ujio wa Mheshimiwa Waziri, maagizo yake aliyoyatoa tunaahidi kuyafanyia kazi,” alisema Manu.

Waziri Simbachawene, alifanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Baraza la Madiwani Wilayani humo.


Share:

MALAWI YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI

Nchini Malawi bangi itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Malawi imekua nchi ya hivi karibuni iliyoko Kusini mwa Afrika kuhalalisha kisheria ukulima na uuzaji wa ndani na nje wa bangi.

Wanaotumia bangi kama kiburudisho wanaiona bangi kama , "Malawi Gold", yaani Thahabu ya Malawi kama wanavyoiita wenyewe, kuwa moja ya dawa nzuri.

Lakini maafisa wamezuwia matumizi ya kisheria ya bangi kwa mtu binafsi.

Itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Mauzo ya bangi yanaweza kuchukua nafasi ya biashara ya tumbaku, ambayo inategemewa sana na Malawi.

Nchi nyingine za Afrika zilizolegeza sheria juu ya ukulima wa mmea wa bangi ni pamoja na Afrika Kusini, Zambia, Lesotho na Zimbabwe

Nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa.

Lesotho

Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo. Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.Image captionMaeneo ya nyanda zaa juu ya Lesotho yana udongo wenye rutuba unaofaa kwa kilimo cha bangi

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini

Nchini Afrika Kusini Mahakama ya kikatiba nchini Afrika kusini ilihalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha mwaka 2018.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kuima kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi walisheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''. Hata hivyo ni haramu kutumia bangi katika maeneo ya Umma au kuiuza.Image captionMampho Thulo huvuna bangi bila kibali

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini lilifurahia uhalalishwaji wa matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Ghana

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .

kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.

pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.
Korea Kaskazini

Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.
CHANZO- BBC
Share:

Coordinator – Purchasing Job opportunity at School of St. Jude

Job Summary About us- The School of St Jude is an educational institution, entirely funded by charitable donations, that provides free, high-quality primary and secondary scholarships to 1,800 of the poorest and brightest students in the Tanzanian region of Arusha. Objectives -To be responsible for sourcing equipment, goods and services and managing vendors. -The successful candidate will be… Read More »

The post Coordinator – Purchasing Job opportunity at School of St. Jude appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Halmashauri Zatakiwa Kutenga Ardhi Ya Kilimo Kwa Ajili Ya Vijana

Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga ardhi ya kutosha kwa ajili ya vijana kuzalisha mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi .

Ametoa agizo hilo leo mjini Njombe wakati alipofungua kongamano la vijana wa mikoa ya Njombe,Ruvuma na Iringa kujadili fursa zilizopo katika sekta ya kilimo nchini.

Mgumba amesema kumekupo na malalamiko ya vijana kukosa ardhi kutokana na halmashauri kuwa na mashamba pori mengi yasiyopimwa na kulimwa.

“Halmasahauri zote zihakiki mashamba pori yote au yaliyochukuliwa mikopo na hayalimwi yapimwe na kugawiwa kwa vijana walio tayari kufanya kazi za kilimo nchini”.alisema Naibu Waziri Mgumba.

Ili kufanikisha hilo Mgumba mewataka vijana kujisajili kwenye daftari la wakulima linaroratibiwa na wizara yake ili serikali iwatambue na kujua changamoto zao na kisha kuwaonyesha fursa za ajira kwenye kilimo.

Naibu Waziri Mgumba amesisitiza halmashauri nchini kutoa fedha za mikopo kwa vijana bila urasimu ili vijana wanufaike na kuanzisha kazi za uzalishaji mazao ya kilimo na mifugo.

Mgumba aliwafahamisha kuwa serikali imeelekeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kuendelea kutoa mikopo kwa vijana ili wapate mitaji.

“Wapo vijana wengi wasomi wameamua kujiajili katika kilimo ili kufikia malengo ya kuongeza ajira ikiwa ni malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano kukuza sekta ya kilimo” alisema Mgumba.

Tanzania ina eneo la hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo hivyo vijana wajitokeze kutumia fursa hiyo kuanzisha kazi za kuzalisha mazao ya kilimo .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe aliziagiza halmashauri zote za mkoa wa Njombe kuandaa katiba kwa
ajili vijana kushiriki shughuli za kilimo.

Aliongeza kusema watendaji wote wa halmashauri wapunguze urasimu kwa kukaa muda mrefu bila kupitisha maombi ya vijana wanaostahili mikopo ya fedha za mapato
ya ndani.

“Halmashauri punguzeni urasimu msikae zaidi ya robo mwaka bila kutoa mikopo kwa vijana,akina mama na walemavu” alisema Mkuu huyo wa wilaya ya Njombe.

Naye Mkurugezi wa Shirika la SUGECO Revocatus Kimario linaloratibu mafunzo maalum kwa vijana kwenda Israel na Marekani kujifunza fursa za kilimo kwa vitendo kwa mwaka mmoja amesema wengi wamenufaika.

Kimario amesema hadi sasa zaidi ya vijana 1000 wamepatiwa mafunzo ya kilimo,mifugo na uvuvi nchini Israel na wengine 90 nchini Marekani wamerudi nyumbani
wamefanikiwa kuzalisha ajira nyingi kwa wenzao .

Kimario ameishauri jamii kutotumia kilimo kama adhabu bali kitumike kama fursa ya kukuza ajira na kipato cha kaya na taifa.

Kongamano hilo la siku mbili linawakutanisha vijana wapatao mia mbili toka mikoa ya Njombe,Ruvuma na Iringa chini ya uratibu wa Wizara ya Kilimo na wadau toka wizara za kisekta na taasisi binafsi.


Share:

Shop Manager: Mbeya Job vacancy at Vodacom Tanzania

Shop Manager: Mbeya Posting Country:  TZ Date Posted:  27-Feb-2020 Full Time / Part Time:  Full Time Contract Type:  Permanent Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If you think for a minute about the people you rely on…the likelihood is… Read More »

The post Shop Manager: Mbeya Job vacancy at Vodacom Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Insights and Reporting Dar and Coast Job vacancy at Vodacom Tanzania

Insights and Reporting Dar and Coast Posting Country:  Tanzania, United Republic of Date Posted:  27-Feb-2020 Full Time / Part Time:  Full Time Contract Type:  Permanent Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If you think for a minute about the… Read More »

The post Insights and Reporting Dar and Coast Job vacancy at Vodacom Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wanajeshi 33 wa Uturuki Wauawa Katika Mapigano Makali Huko Syria

Wanajeshi 33, wa Uturuki wameuawa katika mapigano kwenye mkoa wa Idlib nchini Syria, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la serikali ya Uturuki, Anadolu, lililomnukuu gavana wa jimbo la Uturuki la Hatay lililopakana na mkoa wa Idlib, Rahmi Dogan. 

Dogan amesema wanajeshi hao wamekufa katika shambulizi la angani lililofanywa na ndege za jeshi la serikali ya Syria na kuongeza kuwa kulikuwa na wanajeshi waliojeruhiwa vibaya sana na wanaendelea kupatiwa matibabu.

 Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amefanya mikutano miwili ya dharura jana jioni kujadiliana kuhusu hali ilivyo katika mkoa huo wa Idlib. 

Waziri wa mambo ya kigeni, Mevlut Cavusoglu kwa upande wake alijadiliana kwa njia ya simu na katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami barani Ulaya, NATO Jens Stoltenberg, kuhusu hali kwenye mkoa huo hii pia ikiwa ni kulingana na Anadolu.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 28,2020

















Share:

Thursday, 27 February 2020

Mfanyabiashara wa madini ya dhahabu Mwanza akamatwa kwa tuhuma za kuwajeruhi watu wawili kwa risasi Akiwemo Mpenzi Wake

Mfanyabiashara wa madini ya dhahabu jijini Mwanza, Salum Othuman (44) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa tuhuma za kuwajeruhi watu wawili, akiwemo mpenzi wake Happiness Israel (32).

Anadaiwa kumpiga risasi ya mguuni mpenzi wake baada ya kutokea ugomvi wakati wakiwa chumbani kwenye hoteli ya Kilimanjaro mjini Geita.

Leo Alhamisi Februari 27, 2020 Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea jana Februari 26, 2020.

Amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya tukio hilo, alimbeba Happiness aliyekuwa akichuruzika damu kwa lengo la kutoroka lakini meneja wa hoteli hiyo, John Maftar(43) alimuona na alipomtaka asiondoke alitishia kumpiga risasi.

Mwabulambo amesema baada ya meneja kusogea pembeni mtuhumiwa aliingia kwenye gari lake na kumgonga, kisha kugonga geti na kuondoka eneo hilo.

Amebainisha kuwa polisi walimkamata na Happiness alipewa huduma ya kwanza na kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Bugando baada ya kubainika mfupa wake wa paja umepasuka.

Amesema Maftar amepata majeraha maeneo mbalimbali mwilini, anaendelea na matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Geita.

Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Paulo Lyimo amesema mtuhumiwa ni mteja wao wa mara kwa mara.

Amesema siku hiyo asubuhi akiwa na mpenzi wake chumbani, wahudumu wa hoteli walisikia mlio wa risasi na baadaye alitoka chumbani akiwa amembeba Happiness.

“Wahudumu hao walisema alimuweka kwenye gari na alipozuiwa asiondoke alimtishia meneja kwa bastola na alipojihami, mtuhumiwa aligonga geti na kumburuza meneja kisha kukimbia hadi pale alipokamatwa kwa msaada wa polisi na madereva bodaboda waliokuwa wakifukuzia gari yake .


Share:

UOGA WA WANAWAKE WATAJWA KIKWAZO KWA MAENDELEO


Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akizungumza na washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Jijini Dodoma leo tarehe 27/02/2020.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akizindua maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani na Kongamano la kujadili utekelezaji wa maazimio ya Ulingo wa Beijing leo tarehe 27/02/2020 jijini Dodoma
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na aliyekuwa mwenyekiti wa Mkutano wa ulingo wa Beijing Getrude Mongela wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kitaifa la maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani leo tarehe 27/02/2020 jijini Dodoma.
Msanii wa muziki Stara Thomas akitumbuiza na kucheza na wanawake waliohudhuria Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani leo tarehe 27/02/2020 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa neno wakati wa Kongamano la uzinduzi wa siku ya Wanawake Duniani leo tarehe 27/02/2020 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea hatua za utekelezaji wa maazimio ya Ulingo wa Beijing katika Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani leo jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga akizungumza na washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani jijini Dodoma leo taree 27/02/2020.
Waziri Mstaafu na Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Getrude Mongella akizungumza na washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani leo jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani wakimsikiliza mgeni Rasmi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda leo Tarehe 27/02/2020 jijini Dodoma.
***
Na Mwandishi wetu Dodoma

Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amewataka wanawake nchini kuacha uoga katika wakati wa mapambano ya kutafuta fursa mbalimbali za kielimu, uchumi na siasa vinginevyo masuala ya usawa wa kijinsia itabaki kuwa ndoto.

Makinda amesema hayo jijini DODOMA katika Kongamano la uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambalo pamoja na mambo mengine limejadili utekelezaji wa maazimio ya ulingo wa Beijing yaliyowekwa miaka 25 iliyopita.

Amesema wanawake nchini Tanzania ni zaidi ya asilimia 51 ya wananchi wote hivyo kundi hili lina uwezo kufikia maamuzi yenye tija kwa wanawake lakini tatizo kubwa ni woga wa kuthubutu ilhali uwezo wanao.

“Wanawake acheni uoga na unyonge maana wanawake ambao ni wawakilishi wa majimbo wameendelea kuaminika na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa amesema.

Ameongeza kuwa, jitihada zinaonekana ingawa zinasuasua sana hasa kwenye mambo ya siasa. 

Hatuwezi kusema tuna usawa wa kijinsia wakati bado hatujaweza kuchaguliwa na watu. Kama isingekuwa kipengele cha viti maalum, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lingekuwa na wanawake asilimia 6 tu, idadi ambayo ni ndogo sana”

Ameongeza kuwa asilimia 30 ya wabunge wa viti maalum na wale wa kuteuliwa haina mantiki katika kuelekea usawa wa kijinsia. 

Amewahimiza wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi hasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mchango wa viongozi wanawake wakiwemo wastaafu umeleta mabadiliko makubwa katika kuelekea maendeleo jumuishi.

Waziri Mwalimu amemtaja Mama Makinda kuwa kuwa kioo kwake wakati wa kutekeleza majukumu yake katika Wizara huko akiwapongeza wanawake walioshiriki katika harakati za kuelekea ukombozi wa mwanamke maarufu kama Mkutano wa BEIJING.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiwasilisha utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Beijing amesema mambo mengi yamefanyika ikiwemo kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia mifuko ya uwezeshwaji kiuchumi.

Dkt. Jingu amesema kwa kipindi cha miaka minne, zaidi ya shilingi bilioni 39 zimetolewa kwa wanawake zaidi ya laki 8 kupitia asilimia 10 ya fedha za ndani za Halmashauri na shilingi bilioni 2 zimetolewa kwa zaidi ya wanawake elfu 3 kupitia dirisha la wanawake la Benki ya Posta Tanzania mwezi Agosti 2018 hadi Machi 2019.

Ameongeza pia kuwa, umiliki wa ardhi umeongezeka kwa wanawake kutoka asilimia 6 mwaka 2014 hadi 16 mwaka 2017 pamoja na ushiriki wa wanawake katika maonesho ya Biashara ya kimataifa kutoka 1183 mwaka 2017 hadi 13016 mwezi Machi mwaka 2019.

Kongamano hilo la siku moja limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. AUGUSTINE MAHIGA, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. JOYCE NDALICHAKO, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella Manyanya na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, JULIANA SHONZA pamoja na Mawaziri Waziri wastaafu ANNA ABDALLAH, GERTRUDE MONGELLA na MARGRETH SITTA.

Kusanyiko hilo ni ufunguzi rasmi kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya wanawake Duniani yatakayofanyika Mkoani Simiyu kwa Kauli mbiu KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA BAADAYE

Share:

Rais Magufuli Amteua Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Ya Wakala Wa Ndege Za Serikali




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger