Thursday, 2 January 2020

Picha : HIACE YAGONGA BAISKELI IKIKWEPA GARI NA KUJERUHI SHINYANGA MJINI


Watu watatu wanaelezwa kujeruhiwa baada ya gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB ikitokea Kishapu kwenda Shinyanga Mjini kumgonga mwendesha baiskeli na kutumbukia mtaroni wakati ikikwepa gari aina ya Toyota Harrier yenye namba za usajili T726 DFM.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 jioni leo Alhamis Januari 2,2019 katika eneo la Pepsi ‘Ushirika’ barabara ya Shinyanga – Mwanza.

Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde 1 blog kuwa dereva wa Hiace akitokea Kishapu alikuwa anajaribu kumkwepa dereva wa gari aina ya Toyota Harrier aliyeingia kwenye njia isiyo yake ndipo Hiace ikamgonga mwendesha baiskeli ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa wakiwemo wale waliokuwa ndani ya Hiace na wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga likiongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga (RTO) Anthony Gwandu wamefika eneo la tukio na tayari gari aina ya Harrier inashikiliwa katika kituo cha polisi.

Taarifa kamili tutawaletea hivi punde.
Gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB ikiwa kwenye mtaro baada ya ajali - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB na baiskeli eneo la ajali








Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blo
Share:

MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA MME WAKE

Na Amiri Kilagalila-Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia ndugu Josphat Mtega (24) mkazi wa Ramadhani mjini Njombe kwa tuhuma za kumsababishia kifo  mkewe kilichotokana na ugomvi.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kugombana na mkewe Angelina Sanga (24)  ambapo inadaiwa alimpiga na hivyo kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake.

Kamanda amesema mara baada ya ugomvi huo, Angelina alisafirishwa hadi hospitali ya Ikonda iliyopo wilayani Makete  ambapo baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo uchunguzi wa kitabibu ulibaini kuwa dada huyo alionekana amevunjika mkono na sehemu mbali mbali za mwili wake zilionekana zimeshambuliwa vibaya.

Amesema mwanaume  huyo anaendelea kushikiliwa  na jeshi la polisi  kwa uchunguzi zaidi huku taratibu za kisheria zikiendelea.


Share:

WATOTO 4 WAFA MAJI NJOMBE

Na Amiri Kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limesema kwa nyakati tofauti watoto wanne mkoani humo wamepoteza maisha  kutokana na maji.


Akizungumza na vyombo vya habari mkoani humo kamanda wa polisi Hamis Issa amesema,mtoto wa kwanza aliyefahamika kwa majina ya Alpha Pilla (6) mkazi wa mtaa wa Kibendange mjini Makambako na mwanafunzi wa shule ya Makoga akiwa akicheza 25-12-2019 alitumbukia  kwenye dimbwi la maji yaliyotuama ambayo hutumika kwa  shughuli za uchimbaji mchanga na kusababisha kifo chake.

Kamanda amesema tukio jingine ni la mtoto Shani Belevete (8) huko kijiji cha Msimbazi kata ya uhambule wilaya ya Wanging’ombe alikutwa ametumbukia ndani ya kisima cha maji na mpaka watu kutafuta ngazi alikutwa amekwishafariki.

Amesema tukio jingine linahusisha vifo vya watoto wawili Joel Kutika (6) na Abromovich Hosea (3) huko kijiji cha Saja wilayani Wanging’ombe mnamo tarehe 1-1-2020 walikufa maji katika mto Bokelo uliopo kijijini hapo huku kiini cha tukio hilo kikiwa ni wazazi kutokuwa makini na watoto wao wanapokuwa wanacheza.

Aidha kamanda wa polisi ametoa wito kwa wazazi kuwa makini na watoto huku jeshi hilo likianza kuchukuwa hatua kwa mzazi yeyote asiyekuwa makini kuhakikisha ulinzi wa watoto na kusababisha vifo vya uzembe.


Share:

Mahakama Yamgomea Kabendera Kuhudhuria Ibada ya mazishi ya mama yake.

Mahakama ya Kisutu imetupilia mbali ombi la Erick Kabendera kwenda kutoa heshima za mwisho kufuatia kifo cha mama yake mzazi. 

Hakimu Janeth Mtega amesema mahakama haina mamlaka ya kutoa ruhusa hiyo, na mtuhumiwa hana fursa ya kukata rufaa  kupinga uamuzi huo. 

Maombi hayo yaliwasilishwa na mawakili wake wakiongozwa na Jebra Kambole.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alitoa pole kwa Erick kufiwa na mama yake ambapo licha ya pole hizo, upande wa mashtaka ulipinga ombi hilo kwa madai ya kuwa hoja za upande wa utetezi hazikuwa na mashiko.


Kesi imeahirishwa hadi Januari 13.

Mwili wa Verdiana Mujwahunzi (80), mama mzazi wa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera aliyefariki dunia Desemba 31, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Amana jijini Dar es Salaam utagwa kesho Ijumaa Januari 3, 2019 Chang’ombe Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa maziko yatakayofanyika Januari 6, 2020.


Share:

Picha : MGOGORO WA MAKINIKIA YA ALMASI MWADUI WAIBUKA KISHAPU, MKUTANO WA WACHIMBAJI WAPIGWA STOP…MADIWANI WAZIMIWA SPIKA


Diwani wa kata ya Maganzo, Lwinzi Mbalu Kidiga ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madiwani wa kata zinazozunguka mgodi wa Mwadui akiwatangazia wananchi kuhusu taarifa za kuzuiwa kwa mkutano wao.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Katika hali isiyotarajiwa mkutano wa wananchi wanaozunguka mgodi wa almasi wa Williamson Diamond LTD ‘Mgodi wa Mwadui’ ulioandaliwa na Madiwani wanaozunguka mgodi huo kujadili hatima ya Masalia ya mchanga wa madini ya almasi ‘Makininikia’umepigwa marufuku dakika chache kabla ya mkutano kuanza ambapo ghafla viti viliondolewa huku spika zikizimwa wakati diwani wa Maganzo Lwinzi Kidiga akizungumza.

Tukio hilo limetokea leo Alhamis Januari 2,2020 majira ya saa sita mchana ambapo madiwani wa kata zinazozunguka mgodi huo pamoja na wananchi waliokusanyika katika soko la kata ya Maganzo ‘Mji wa Maganzo’ wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kutakiwa kutawanyika mara moja kwa madai kuwa ni ‘Order’ Agizo kutoka juu. 

Tukio la kuzuiwa kufanyika mkutano ni kielelezo cha mgogoro uliozuka kati Wachimbaji wadogo wanaozunguka mgodi wa Mwadui na Chama cha Wachimbaji Madini mkoa wa Shinyanga ‘Shinyanga Region Miners Association – SHIREMA’ siku chache baada ya Mgodi wa Williamson Diamond Ltd kuamua kutoa mchanga wa Makinikia ya Almasi bure kwa wachimbaji wa wadogo wa madini.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Madini Dotto Biteko baada ya wachimbaji kuomba wapewe makinikia ili kuondoa mgogoro kati yao na mgodi ambapo SHIREMA walipewa jukumu la kusimamia utaratibu mzuri wa kugawa mchanga huo.

Akitoa taarifa kwa wananchi kuhusu kusitishwa kwa mkutano huo,wakati tayari viti na meza kuu vikiwa vimetolewa,Diwani wa kata ya Maganzo, Lwinzi Mbalu Kidiga ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madiwani wa kata zinazozunguka mgodi wa Mwadui, ghafla spika zilizimwa na watu ambao hawakujulikana mara moja.

Kidiga alisema wameahirisha kufanya mkutano huo kutokana na Amri kutoka juu iliyowataka waahirishe mkutano huo vinginevyo watawekwa ndani.

Alisema chanzo cha kuzuiwa kufanya mkutano ni watu wachache waliojipanga kuhujumu uchumi wa watu wa Maganzo ili wapate asilimia za chini huku akibainisha kuwa yeye kama diwani hakubali. 

“Ndugu wananchi mmeiona sura hapa, sura ya hapa haijakaa vizuri tulikuwa tumetoa viti kwa ajili ya mkutano wa hadhara lengo na madhumuni ilikuwa ni kuzungumza changamoto zilizopo katika hata hii na kata za jirani.Mkutano wetu ulikuwa ni mzuri tu wa kupeana habari haukuwa na ashki yoyote.Lakini cha kushangaza hapa meza zimetolewa,huu mkutano umeahirishwa..kwa Kiswahili kingine Tumezuiwa”,ameeleza Kidiga.

“Nimezuiwa lazima niseme ukweli..Huu mkutano wangu upo ndani ya kisheria na nina mamlaka ya kuitisha mkutano bila kuuliza kwa mtu yeyote,sheria na katiba ya nchi inanilinda. Kwa Order kutoka Juu mkutano huu nimeambiwa nisifanye mara moja..Sasa mara moja maana yake huwezi kuuliza lakini wanasema chelewa chelewa mwishowe ukweli utaonekana.

“Sisi hapa ni wakweli,tunataka tuzungumze ukweli na ukweli wenyewe ni kutetea watu walio chini wapate maslahi siyo waingilie watu wachache,hiyo biashara haipo.”,alisema Kidiga huku akishangiliwa na wananchi.

“Mmetuchagua kwa ajili ya kusimamia haki zenu siyo baadhi ya watu wanufaike,hiyo biashara haipo..Tumezuiwa sawa,sisi tuko chini ya sheria hakuna mtu aliye juu ya sheria lakini ilikuwa halali yetu tufanye mkutano huu na madiwani wa kata jirani, tulikuwa tumepanga tuzungumzie kuhusu Makinikia basi.

Tumeambiwa tukifanya mkutano tutawekwa ndani na tukiendelea ku – force udiwani ndiyo basi tena. Ndani tutakwenda kwani waliomo ndani siyo watu?. Tukiwekwa ndani basi Rais Magufuli atakuja kutuwekea dhamana. Nilitaka niseme hilo ili msisambae kienyeji kwani tuliwaita kwenye mkutano na wengine mmetoka mbali”,alieleza Kidiga.

Kidiga alisema SHIREMA imekuwa ikifanya vikao vyake na kufanya mambo bila kuwashirikisha madiwani wa kata zinazozunguka mgodi wa Mwadui akidai kuwa haina nia nzuri ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini wilayani Kishapu.

Hata hivyo baada ya mkutano huo uliokuwa umezungukwa na askari polisi wakiongozwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Kishapu kuahirishwa,Madiwani wanaozunguka mgodi wa Mwadui,waliamua kufanya mkutano na waandishi wa habari ‘Press Conference’ ili kueleza lengo la mkutano wao.

Katibu wa Jumuiya ya Madiwani wanaozunguka mgodi wa Mwadui Abdul Ngolomole ambaye ni Diwani wa Kata ya Songwa (CCM) alisema hawakubaliani na kitendo cha SHIREMA kumpatia Mkandarasi anayesafirisha mchanga wa madini kutoka Mwadui asilimia 75 ya mauzo ya almasi na wachimbaji wadogo kupewa asilimia 15. 

“Tunataka Mkandarasi wa kusafirisha makinikia atangazwe hadharani kupitia zabuni kwani mkandarasi aliyepo sasa ni Mkandarasi wa mfukoni ambaye ni Junior Construction ya Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi,ni mkandarasi ambaye amebuniwa na SHIREMA ,huyu ni mtu mkubwa sana, mamlaka zipo lakini kwanini hazisemi?. Sisi tunapotaka kufanya mkutano kuwaeleza wananchi ukweli tunaonekana tunataka kuzuia maslahi ya watu flani”,alisema Ngolomole.

“Baada ya kulalamikia hizo asilimia 15 SHIREMA wameongeza asilimia kwamba mchimbaji mdogo apate asilimia 37.5 ambayo haiwasaidii wanyonge.Sisi madiwani tumekubaliana wananchi wapate zaidi ya asilimia 60 ili kuwasaidia wanyonge,ndicho anachokitaka Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwani hajatoa Makinikia haya ili wachache wanufaike nayo”,alifafanua Ngolomole. 

“Sisi madiwani tunawataka wananchi wasikubali kufanya kazi chini ya SHIREMA kwani inanyonya wananchi wamejiwekea fedha kwenye makinikia haya na wamekuwa wakiwatoza wachimbaji wadogo shilingi 200,000/= tena bila risti ili wapewe usajili SHIREMA. Tunataka wananchi wapewe mamlaka ya kuchagua viongozi wa kuwasimamia kutoka kwenye vikundi vyao vya uchimbaji”,alisema Ngolomole.

“Tumezuiwa kufanya mkutano kwani inaonekana tunaingilia maslahi ya watu binafsi.Kwenye mkutano tulitaka tuwaeleze wananchi mapendekezo ya madiwani na kupokea maoni ya wananchi kuhusu makinikia”,alisema.

Ngolomole alimuomba Rais Magufuli wakati anatoka kwenye mapumziko yake Chato mkoani Geita apitie Maganzo kukutana na wachimbaji wadogo wa madini ili kutatua mgogoro huo wa makinikia.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwadui Luhumbo Paul Magembe, William Luhende Jijimya wa kata ya Mondo walisema hawapo tayari kuona wananchi wananyonywa na hawatarudi nyuma huku wakimuomba Rais Magufuli kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini wilayani Kishapu.

Nao wananchi waliozungumza na waandishi wa habari,akiwemo Ramadhani Amani,Bala Masanja na Hamis Sizya walisema zoezi la kupewa makinikia lilitolewa bila asilimia hivyo wanashangaa kuona baadhi ya viongozi wanatumia fursa hiyo kujipatia kipato na kuomba serikali kujali wanyonge.

Kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wananchi pamoja madiwani kuhusu SHIREMA,Viongozi wa Chama cha Wachimbaji Madini mkoa wa Shinyanga (SHIREMA) ambao ni Hamza Tandiko (Mwenyekiti) na Gregory Kibusi (Katibu) walikataa kuzungumza na waandishi wa habari wakidai kuwa watatoa taarifa kuhusu Makinikia kwenye kikao chao na vikundi vya wachimbaji wadogo wa madini Januari 3,2020.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Diwani wa kata ya Maganzo, Lwinzi Mbalu Kidiga ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madiwani wa kata zinazozunguka mgodi wa Mwadui akishangaa baada ya spika kuzimwa wakati akiwatangazia wananchi kuhusu taarifa za kuzuiwa kwa mkutano wao katika Soko la Maganzo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga leo Januari 2,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa Jumuiya ya Madiwani wanaozunguka mgodi wa Mwadui Abdul Ngolomole ambaye ni Diwani wa Kata ya Songwa (CCM) akiwaomba wananchi kuwa watulivu baada spika kuzimwa baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara.
Katibu wa Jumuiya ya Madiwani wanaozunguka mgodi wa Mwadui Abdul Ngolomole ambaye ni Diwani wa Kata ya Songwa (CCM) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari 'Press Conference'  baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara uliolenga kujadili kuhusu Makinikia ya almasi yaliyopo katika Mgodi wa Mwadui.
Katibu wa Jumuiya ya Madiwani wanaozunguka mgodi wa Mwadui Abdul Ngolomole akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.
Diwani wa kata ya Maganzo, Lwinzi Mbalu Kidiga ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madiwani wa kata zinazozunguka mgodi wa Mwadui akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari 'Press Conference'  baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara uliolenga kujadili kuhusu Makinikia ya almasi yaliyopo katika Mgodi wa Mwadui.
Kulia ni William Luhende Jijimya wa kata ya Mondo akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari 'Press Conference'  baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara uliolenga kujadili kuhusu Makinikia ya almasi yaliyopo katika Mgodi wa Mwadui.
Diwani wa kata ya Mwadui Luhumbo Paul Magembe akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari 'Press Conference'  baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara uliolenga kujadili kuhusu Makinikia ya almasi yaliyopo katika Mgodi wa Mwadui.
Mchimbaji mdogo wa madini akizungumza na waandishi wa habari.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Upande wa Jamhuri wakataa Kabendera kumzika Mama yake...Mahakama Kuamua

Upande wa Serikali umempa pole Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi huku ukipinga maombi yake ya kutaka ashiriki Ibada ya mazishi ya mama yake.

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati Kabendera anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha alipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.

“Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba,”amesema Wankyo.

Wankyo amedai kuwa maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na pia Mkurugenzi wa Mashitaka hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.

“Katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka, hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini mahakama isifungwe mikono,” amesema.

Kuhusu mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefika hatua nzuri ya maelewano baina ya mshitakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP).

Kukataliwa kwa Kabendera kushiriki mazishi ya Mama yake, kumeibuka kutokana na maombi aliyoyatoa Kabendera kupitia Mawakili wake akiwemo Jebra Kambole.

Wakili Kambole amedai wanaiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki Ibada ya Mazishi ya Mama yake mzazi katika Kanisa la Roman Katoliki lilipo Changombe majira ya mchana.

Kambole ameieleza mahakama kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya Binadamu, suala la faragha.

“Kushindwa kuudhuria maziko ya Mama yake tutakuwa tumemuadhibu adhabu kubwa tena kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza na ni vizuri akatoa heshima ya mwisho,”ameeleza.

Wakili Jebra amedai kuwa ni muhimu kwa Kabendera kushiriki kwa sababu Mama mzazi ni mmoja, akifa anaagwa mara moja.

“Jamhuri haitaathirika kwa lolote kwa sababu mshitakiwa atakuwa chini ya ulinzi na ibada itakuwa mchana kanisani na Temeke sio mbali na gerezani, tunaomba akatoe heshima ya mwisho,” ameomba.

Baada ya kutoa hoja hizo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi saa 8:45 mchana kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Kabendera ashiriki Ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi ama lah.


Share:

Waandamanaji waondoka eneo la ubalozi wa Marekani, Iraq

Waungaji mkono wa makundi ya kijeshi nchini  Iraq yanayoungwa mkono na Iran ambao waliovamia maeneo ya viunga vya ubalozi wa  Marekani na kurusha mawe katika maandamano ya siku mbili wameondoka jana(01.01.2020).

Hatua  hiyo  imewezekana  baada  ya  Marekani kupeleka  vikosi vya  ziada na  kutishia  kuchukua  hatua  dhidi  ya  Iran. Lakini  wachambuzi wa masuala  ya  kisiasa  wanaonya  kuwa  hali  hiyo  inaweza  kuwa  na athari  za  kudumu  katika  sekta tete  ya  usalama  nchini  Iraq pamoja  na  mahusiano  ya  kidiplomasia.

Waandamanaji , ambao wamekasirishwa  na  mashambulizi  ya anga  ya   vikosi  vya  jeshi  la  Marekani  dhidi  ya  kundi linaloungwa  mkonom na  Iran  la  Hezbollah  ambapo  kiasi  ya  watu 25 waliuwawa, walirusha  mawe katika  jengo  la  ubalozi  wakati wanajeshi wa   jeshi  la  Marekani  waliokuwa  katika  mapaa ya jengo  hilo  wakifyatua  mabomu  ya  kutoa  machozi kuwatawanya.

Ilipofika  mchana , wengi walionekana  kutii wito  wa  kujiondoa kutoka  katika  eneo  hilo, uliotolewa  na  kundi  la  wanamgambo  wa Kishia linaloongoza  vikundi  vya umma  vya  mapambano PMF, ambalo  lilisema  ujumbe  wa  waandamanaji  tayari  umesikika.

Vijana walitumia  matawi  ya miti  ya  mitende kufajia  mtaa  mbele ya  eneo  la  ubalozi  wa  Marekani. Wengine  walikusanya  vifaa hivyo na magari yaliwasili  kuvichukua.

Maandamano  hayo  yameonesha mabadiliko  mapya  katika  kivuli cha  vita  kati  ya  Marekani  na  Iran  vinavyotokea  katika  eneo  la mashariki  ya  kati. Rais Donald Trump  ambaye  anakabiliwa  na kampeni  ya  uchaguzi  mwaka  2020, ameishutumu  Iran kwa kuchochea  ghasia  hizo. 

Ametishia  siku  ya  Jumanne  kuchukua hatua  dhidi  ya  iran lakini  alisema  baadaye  kuwa  hataki  vita. 

Makamu  ya  rais  katika  taasisi  ya  Charles Koch  anayehusika  na utafiti  na  sera Will Ruger  amesema  hatua Marekani  inazochukua kuibinya Iran hazitafanyakazi:

"Moja ya  matatizo  hapa  ni  kwamba  sio tu shambulio la  roketi  la jeshi  la  Marekani ndio lililochochea mzozo  huu, lakini  pia  kile tulichoshuhudia  jana katika  ubalozi wa  Marekani mjini  Baghdad, nafikiri  hii inaonesha  kwamba  kampeni  kubwa  ya  shinikizo ambayo  utawala  wa  Trump  umekuwa  ukitumia dhidi  ya  Iran haifanyikazi kupunguza  wasi  wasi. Na haifanyi Iran kutulia. Badala yake  inaleta  uhasama na  changamoto nyingi kwa  mahusiano."
 
Iran , ikiwa  katika  hali  mbaya  ya  kiuchumi kutokana  na  vikwazo vya  kuumiza  vilivyowekwa  na  Trump, imekana  kuhusika. 

Ghasia hizo  zilitokana  na  mashambulizi  ya  anga  siku  ya  Jumapili dhidi ya  vituo  vya  kundi  la  Kataib Hezbollah kwa  kulipiza  kisasi  kwa mashambulizi  ya  makombora  ambayo  yalisababisha  kifo  cha mkandarasi  wa  Marekani  kaskazini  mwa  Iraq wiki  iliyopita.

Marekani imesema  wanadiplomasia wako salama na inapeleka  mamia  ya  wanajeshi wa ziada  katika  eneo  hilo. 

Wizara ya  mambo ya kigeni ya  Marekani imesema  jana  kuwa  waziri wa  mambo  ya  kigeni Mike Pompeo  ameamua  kuahirisha  ziara  yake  kwenda  Ukraine, Belarus , Kazakhstan, Uzbekistan, na  Cyprus  na  kubakia  mjini  Washington ili  kufuatilia  hali  nchini  Iraq.

-DW


Share:

Polisi adaiwa kukatwa sehemu za siri na mkewe

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Flora Adamu (23), mkazi wa Shinyanga Mjini, kwa tuhuma za kumkata mumewe sehemu za siri, ambaye ni askari Polisi mwenye Namba H, 8980 Pc Kazimiri, kwa madai ya kumtuhumu kutokuwa muaminifu katika ndoa.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alimtuhumu mumewe kuwa ana  nyumba ndogo.

Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Deborah Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea Desemba 28 mwaka jana, majira ya saa 6:30 usiku wakati wanandoa hao wakiwa wamelala.

Alisema wakiwa wamelala, ghafla Flora aliamka na kuanza kumnyatia, huku akiwa ameshika kitu chenye ncha kali kisha kumkata mumewe sehemu za siri na kumjeruhi vibaya.

“Baada ya askari huyu kukatwa uume wake alikimbizwa kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga ili kupatiwa matibabu ya haraka, ambapo alilazwa kwa muda wa siku mbili  kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea kujiuguza kidonda,” alisema  Kamanda Magiligimba.

“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mwanamke alikuwa akimtuhumu mume wake kuwa ana nyumba ndogo, ndipo akaamua kuchukua kitu chenye ncha kali kisha kuanza kuukata uume wa mumewe na kumjeruhi vibaya,” aliongeza.

Aidha, kamanda huyo alisema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke huyo, na kwamba uchunguzi ukikamilika, atafikishwa mahakamani.


Share:

Papa Francis aomba radhi kwa kumchapa kibao muumini Aliyemvuta kwa Nguvu

Papa Francis ameomba radhi kwa kumpiga kibao mkononi mwanamke mmoja aliyemvuta kwa nguvu wakati akisalimiana na waumini katika mkesha wa mwaka mpya. Papa amesema alikosa uvumilivu na kwamba kitendo kimeweka mfano mbaya.

Papa alikuwa akisalimiana na watoto na mahujaji na wakati akigeuka mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye umati wa watu waliokuwa karibu aliuvuta mkono wa Papa kwa nguvu karibu amuangushe.

Hali iliyomfanya Papa kugeuka na kumpiga makofi mawili mkononi mwanamke huyo kwa hasira.


Badaye Papa alikiri kwamba alishindwa kujizuia na yeye pia huwa anakosea kama binadamu wengine.

Hivyo anaomba radhi kwa kitendo hicho kwa muumini huyo na kila mtu.

Kitendo cha Papa cha kumzaba makofi ya mkononi mwanamke huyo, kimezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, hasa Twitter, wengi wakimuunga mkono Papa.


Share:

DC Njombe ataka amani isichezewe

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri,ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa sehemu ya kuilinda amani ya Tanzania ili kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla na kuendelea kuifanya tanzania kuwa ndio sehemu pekee yenye amani ya uhakika Duniani.

Pamoja na hayo amewakaumbusha wananchi wa mkoa wa Njombe kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata fursa ya kushiriki uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani hapo baadaye mwaka huu

Ametoa wito huo wakati akizungumza na waumini wa kanisa la Angricana dayosisi ya Tanganyika magharibi lililopo mtaa wa Mji mwema mjini Njombe wakati wa ibada ya mwaka mpya ambapo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kulinda amani.

“Tusichezee amani watanzania wenzangu,kuna watu wachache ambao hawajui amani kwamba ni pamoja na uhai wako,amani hii ambayo ndio msingi wa taifa letu,tusithubutu kuivuruga kwa wakati wowote wala kwasababu yeyote wala kwa ushawishi wa aina yoyote ile”alisema Ruth Msafiri

Aidha ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kujiandikisha na kuhakiki katika daftari la mpiga kura, zoezi lililo anza hii leo na kumalizika januari 5,2020 mkoani humo.

Mchungaji wa kanisa hilo Ayub Haule amesema uwepo wa amani katika taifa hutoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi hivyo ni vema kila mtanzania kuwa sehemu ya kulinda amani ya Tanzania

“Tunao uchaguzi mkuu wa nchi hii ambao tunategemea kabisa kama amani ilivyoendelea kudumu ndivyo tutakavyofanya,tunapokuwa tunauona mwaka huu tuone ambavyo tunaweza kupambana na adui mkubwa anayetusakama katika mkoa wetu nae ni maambukizi ya VVU”alisema mchungaji Ayub Haule

Nje ya ibada baadhi ya waumini  wamekiri kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuilindi amani iliyopo.

Mwaka 2019 umekamilika hapo jana ambapo watanzania waliungana kwa pamoja kuukaribisha mwaka mpya 2020 ambapo walio wengi wamekuwa wakituma maombi yao kwa Mungu ili mwaka huu 2020 uwe mwaka wa mafanikio makubwa katika maisha yao


Share:

PAPA FRANCIS AOMBA RADHI KWA KUMCHAPA VIBAO MUUMINI

Share:

BITEKO AKAMATA KIWANDA BUBU CHA UCHENJUAJI DHAHABU SHINYANGA


Ndani ya kiwanda bubu kilichokamatwa na kufungiwa na waziri wa Madini Dotto Biteko.
Baadhi ya mifuko zaidi ya 25 ya cabon iliyokamatwa kabla ya kuchenjuliwa katika kiwanda hicho.
Maafisa madini wakifunga kiwanda bubu cha Uchenjuaji dhahabu katika kijiji cha Bunango wilayani Kahama.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumaza na mwenyekiti wa kitongoji cha Mnara wa voda Masoud Bakari kijiji cha Bunango katika kata ya Bugarama.

Na Salvatory Ntandu - Kahama
Licha ya serikali kuboresha sekta ya madini kwa wafanyabiashara wadogo wa madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga imebainika kuwa wapo ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu ikiwemo kuanzisha viwanda bubu na kuikosesha serikali mapato.

Hayo yalibainishwa Januari Mosi mwaka 2020 Waziri wa Madini Dotto Biteko katika ziara yake ya siku mmoja ya kushitukiza katika kijiji cha Bunango katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga baada ya kubaini kiwanda bubu cha kuchenjua dhahabu kilichopo katikati ya makazi ya watu.

“Kiwanda hiki kipo hapa katika nyumba hii tangu mwezi julai mwaka 2019 huku kikiendelea kufanya kazi,serikali imepoteza mabapo mengi tutachukua hatua kali za kisheria kwa miliki wa mtambo huu na nyumba hii”,alisema Biteko.

Sambamba na hilo Biteko aliwataka viongozi wa vijiji na Mitaa wilayani humo kuhakikisha wanawafichua wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara haramu ya madini ambazo zinafanyika katika makazi ya watu ambao hawana vibali wanaoikosesha serikali mapato.

“Niwaagize viongozi wa mkoa wa Shinyanga kuthibiti vitendo vya biashara haramu ya madini ambavyo vinaendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali kwani mpaka sasa tumeshakamata viwanda bubu viwili vya uchenjuaji wa dhahabu ili kutokomeza vitendo hivi", alisema Biteko.

Hata hivyo Biteko aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Bunango Kajanja Kajanja na Mke wa mwenye nyumba iliyobainika kuwa na mtambo wa kuchenjulia dhahabu aliyefahamika kwa jina mmoja la Shule kuhusiana na kuhusishwa na tukioa hilo.

Masoud Bakari Balozi wa kitongoji cha mnara wa voda alisema alishatoa taarifa kwa mamlaka za kisheria kuhusiana na uwepo wa kiwanda hicho katika eneo lake lakini hakuona hatua zozote zikichukuliwa kwa wahusika.

“Kiwanda hiki kipo katika nyumba hii tangu julai mwaka jana kuna vijana wageni wanne ambao walikuwa wakifanyashughuli ya kuchenjua dhahabu hapa viongozi wote wa eneo hili wanajua tumelalamika sana kuhusiana kumwagwa ovyo kwa maji yenye kemikali kwenye makazi yetu”,alisema Bakari.

Katika ziara hiyo mifuko zaidi ya 35 imekamatwa ikiwa na Cabon zinadhaniwa kuwa na madini ya dhahabu katika kiwanda hicho huku mashine hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 500 za Cabon ikiwa tayari imewekewa mzigo kwa ajili ya kuanza kazi.

Share:

Biteko Akamata Kiwanda Bubu Cha Uchenjuaji Dhahabu Shinyanga.

SALVATORY NTANDU
Licha ya serikali kuboresha sekta ya madini kwa wafanyabiashara wadogo wa madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga imebainika kuwa wapo ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu ikiwemo kuanzisha viwanda bubu na kuikosesha  serikali mapato.

Hayo yalibainishwa Januari Mosi mwaka 2020 Waziri wa Madini Dotto Biteko katika ziara yake ya siku mmoja ya kushitukiza katika kijiji cha Bunango katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga baada ya kubaini kiwanda bubu cha kuchenjua dhahabu kilichopo katikati ya makazi ya watu.

“Kiwanda hiki kipo hapa katika nyumba hii tangu mwezi julai mwaka 2019 huku kikiendelea kufanya kazi,serikali imepoteza mapato  mengi tutachukua hatua kali za kisheria kwa miliki wa mtambo huu na nyumba hii”alisema Biteko.

Sambamba na hilo  Biteko aliwaka viongozi wa vijiji na Mitaa wilayani humo kuhakikisha wanawafichua wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara haramu ya madini ambazo zinafanyika katika makazi ya watu ambao hawana vibali wanaoikosesha serikali mapato.

“Niwaagize viongozi wa mkoa wa Shinyanga kuthibiti vitendo vya biashara haramu ya madini ambavyo vinaendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali kwani mpaka sasa tumeshakamata viwanda bubu viwili vya uchenjuaji wa dhahabu ili kutokomeza vitendo hivyi alisema Biteko.

Hata hivyo  Biteko aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Bunango Kajanja Kajanja na Mke wa mwenye nyumba iliyobainika kuwa na mtambo wa kuchenjulia dhahabu aliyefahamika kwa jina mmoja la Shule kuhusiana na kuhusishwa na tukioa hilo.

Masoud Bakari Balozi wa kitongoji cha mnara wa voda alisema alishatoa taarifa kwa mamlaka za kisheria  kuhusiana na uwepo wa kiwanda hicho katika eneo lake lakini hakuona hatua zozote zikichukuliwa kwa wahusika.

“Kiwanda hiki kipo katika nyumba hii tangu julai mwaka jana kuna vijana wageni wanne ambao walikuwa wakifanyashughuli ya kuchenjua dhahabu hapa viongozi wote wa eneo hili wanajua tumelalamika sana kuhusiana kumwagwa ovyo kwa maji yenye kemikali kwenye makazi yetu”alisema Bakari.

Katika ziara hiyo mifuko zaidi ya 35 imekamatwa ikiwa na Cabon zinadhaniwa kuwa na madini ya dhahabu katika kiwanda hicho huku mashine hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 500 za Cabon ikiwa tayari imewekewa mzigo kwaajili ya kuanza kazi.

Mwisho.


Share:

Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya Latoa Ufafanuzi Kuhusu Jeneza Kukutwa Sokoni Soweto.

Ni kwamba mnamo tarehe 21/12/2019 mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MASUOD MUSA MOHAMED [47] mfanyabiashara na mkazi wa makambako mkoani Njombe aliletwa kwa gari ya wagonjwa [Ambulance] katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na mnamo tarehe 23/12/2019 majira ya 05: 00 alfajiri mtu huyo alifariki dunia na ndipo mmoja wa ndugu yake aitwaye HAMIS MUSSA HAMAD [61] mkazi wa Pambogo Iyela Jijini Mbeya aliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika msikiti wa MASJID TAUFIQ uliopo Block Q Soweto kwa ajili ya kuoshwa na kuswaliwa ambapo baada ya shughuli hizo kukamilika mwili wa marehemu ulihifadhiwa kwenye jeneza lililokuwa msikitini hapo na kisha kusafirishwa kuelekea Makambako kwa mazishi ambapo siku hiyo hiyo majira ya saa 18:00 jioni ulizikwa.

Baada ya kumaliza mazishi jeneza hilo lilibaki kwenye msikiti wa Makambako baada ya kukosa usafiri wa kulirudisha Mbeya kwa siku hiyo. 

Mnamo tarehe 31/12/2019 ALLY MOHAMED Mkazi wa Makambako alimkabidhi jeneza dereva wa lori ili aweze kulileta hapa Mbeya na kumpatia namba ya simu ya HAMIS MUSSA HAMAD ili alipokee jeneza hilo.

 Aidha lori hilo lilikuwa limebeba mzigo wa nyanya ambapo baadhi zilikuwa zinashushwa soko la Soweto na zingine zinapelekwa Songwe, hivyo majira ya saa 01:00 usiku wa kuamkia tarehe 01.01.2020 dereva huyo alifika Soweto na kushusha nyanya pamoja na jeneza lakini alipompigia HAMIS MUSA HAMAD mtu ambaye aliyeambiwa kuwa atalipokea jeneza hilo hakuweza kupatikana hewani hivyo ilimlazimu dereva huyo kukaa mpaka saa 04:00 usiku wa tarehe 01.01.2020 bila mafanikio na ndipo aliamua kumuachia mmoja wapo wa walinzi wa sokoni hapa ili ikifika saa 05:00 alfajiri kipindi cha swala aweze kuwakabidhi jeneza msikitini hapo.

Sambamba na hilo alimuachia namba ya simu ya mpokeaji kwa ajili ya mawasiliano na kisha dereva aliondoka kwenda Songwe lakini mlinzi huyo alilitelekeza jeneza hilo pale liliposhushwa na kuondoka zake hali iliyosababisha taharuki kwa wafanyabiashara wa soko hilo pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, limefuatilia kwa karibu suala hili na nitumie nafasi hii kukanusha habari zilizokuwa zimeenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitando ya kijamii kwani uhalisia wa suala hilo ni huu, hivyo niwatake wafanyabiashara na wananchi wa mkoa wa Mbeya kuendelea na kazi/biashara zao kama kawaida.


Share:

ADAIWA KUKUTWA NA MIHURI 56 YA SERIKALI IKITUMIKA KUGHUSHIA NYARAKA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ABRAHAM  OBEDI [55] wakala wa bima ya GTM na Mkazi wa Isanga Jijini Mbeya akiwa na mihuri hamsini na sita [56] ya idara mbalimbali za serikali na ofisi binafsi ambayo imeghushiwa na kuhifadhiwa katika ofisi yake ya Stationaries.

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya Mtaa wa Sokoine uliopo Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.

Baadhi ya mihuri na nyaraka alizokutwa nazo mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-

1.Mhuri wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,

2.Mhuri wa Afisa biashara wa Halmashauri ya Mbeya,

3. Access Bank Tawi la Mbeya,

4.Mamlaka ya Mapato Mbeya [TRA]

5. Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini,

Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na  Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima, Poss Machine na nyaraka mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao vimeghushiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia AGREY MASHAKA @ MBOTO [25] Mkazi wa Kilambo Wilayani Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi kavu kilogramu thelathini [30].

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 14:45 mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanya msako mkali huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bangi hiyo. 

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi January 2



















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger