Kulingana na taarifa kutoka wizara hiyo, Jamhuri ya kiislamu ya Iran imelaani vikali matamshi ya kichochezi yanayoweza kusababisha vita yanayotolewa na maafisa wa Marekani ambayo ni ukiukwaji wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa.
Rais wa Marekani na maafisa wengine wa taifa hilo wameilaumu Iran kwa shambulio la roketi lililisababisha kifo cha mkandarasi mmoja wa Marekani Kaskazini mwa Iraq Ijumaa iliyopita.
Pia wameishutumu Iran kuhusika na uvamizi uliofanywa katika Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na waandamanaji waliojawa na hasira kufuatia shambulio la kulipiza kisasi la Marekani, Magharibi mwa Iraq lililowauwa wanamgambo 25.
Wizara ya kigeni ya Iran hata hivyo imeitaka Uswisi iikumbushe Marekani kwamba Iran ni nchi huru.