Saturday, 16 November 2019

Picha : SHUHUDIA HAPA MAHAFALI YA 11 YA KIDATO CHA NNE 2019 KOM SEKONDARI SHINYANGA


Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi ameongoza sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 189 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.

Mahafali hayo yamefanyika leo Jumamosi Novemba 16,2019 katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na mamia ya wazazi,wageni waalikwa,wanafunzi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.

Akizungumza wakati wa Mahafali,Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalipia ada watoto wao kwa wakati.

“Nimeambiwa kuna baadhi ya wazazi wanachelewa kulipa ada.Niwakumbushe tu kuwa ukimpeleka mtoto katika shule binafsi maana yake una uwezo wa kulipa ada, sasa lipeni. Elimu ni gharama, hata kwenye shule za serikali ‘ Public Schools’ kuna gharama,kuna nguvu za wananchi”,alisema Kahundi.

“Ni muhimu kumpeleka shule mtoto mara tu shule inapofunguliwa,kwani shule ikifunguliwa masomo yanaanza. Usimuweke mtoto nyumbani,anafanya nini nyumbani muda wa shule?,alihoji Kahundi.

Afisa Elimu huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuwakatia bima ya afya watoto wao ili kurahisisha matibabu pindi wanapougua.

“Vijana mnarudi nyumbani mnatakiwa kuwa watii kwa wazazi wenu,nanyi wazazi msijaribu kuwaozesha wanafunzi hawa”,alisema.

Kahundi aliipongeza shule ya Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma na kinidhamu na imeendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali ngazi na mkoa na taifa.

Awali Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi alisema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kitaaluma ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 wanafunzi 179 walihitimu kati yao 167 walijiunga na kidato cha tano.

Aidha kwa kipindi cha miaka 10 kati ya mwaka 2009 hadi 2018,Koyi alisema jumla ya wanafunzi 1420 wamehitimu kidato cha nne kati yao wanafunzi 1093 walichaguliwa kuendelea na kidato cha tano.

Alisema wanafunzi waliobaki 327 wengi wao wamejiunga na vyuo mbalimbali vikiwemo vya uhasibu,biashara,ualimu,uuguzi,sheria n.k huku akibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na kazi nzuri inayofanywa na walimu darasani pamoja na nidhamu ya hali ya juu ya wanafunzi.

Akisoma taarifa ya shule,Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Warioba alisema shule hiyo iliyosajiliwa mwaka 2006 ikiongozwa na kauli mbiu ‘ Elimu bora kwa wote – Quality Education for All’,alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 579 kati yao wavulana ni 314 na wasichana 265 huku walimu wakiwa ni 32 hivyo uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:18.

Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na gharama kubwa za uendeshaji zinazosababishwa na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha,baadhi ya wazazi kutolipa ada kwa wakati hivyo kuwafanya watoto wachelewe kufika shule inapofunguliwa na baadhi ya watoto kutowalipia watoto wao bima ya afya. 

Mbali na shule ya sekondari Kom,pia kuna shule ya awali na shule ya msingi Kom iliyoanzishwa mwaka 2016 ipo nyuma ya ofisi za KASHWASA umbali wa takribani mita 500 kutoka shule ya sekondari Kom.Pia wameanzisha kituo cha watahiniwa wa kujitegemea wa kidato cha nne na wale wa QT ‘Private candidates & Qualifying test”.

 ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA WAKATI WA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE 2019 KOM SEKONDARI
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akivalishwa skafu na vijana wa Skauti baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kom leo Jumamosi Novemba 16,2019 wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akikata utepe kwenye mahafali hayo.Aliyevaa nguo nyeusi nyuma ni Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi.
Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akiwasalimia wazazi na wageni waalikwa kwa kuwapungia mkono
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga. Jumla ya wanafunzi 189 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akizungumza wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom, ambapo alitumia fursa hiyo kuipongeza shule ya Sekondari Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma kwani imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akizungumza wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom na kuwakumbusha wazazi wajibu wa kulipa michango na ada kwa wanafunzi.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akizungumza wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi akitoa neno la salamu wakati wa Mahafali ya 11 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Warioba akisoma historia ya shule ya Sekondari Kom. Warioba aliwaomba wazazi kuwaongoza na kuwaelekeza vizuri vijana waliomaliza elimu ya kidato cha nne wakati wakisubiri matokeo yao yatakayowawezesha kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na vyuo.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Sekondari,Peter Kugulu akizungumza wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne 
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikata keki maalumu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakilishana keki kwa niaba ya wenzao 189 wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakimlisha keki Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi 
wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakimlisha keki Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwaowakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikabidhi zawadi ya keki kwa walimu wa shule ya sekondari Kom.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kom wakitoa burudani wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 Kom Sekondari.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom wakitoa burudani ya wimbo.
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya Sekondari Kom wakisoma risala ambapo walisema walianza kidato cha nne wakiwa 108 lakini wamehitimu wakiwa 189 huku wakiomba wazazi kuwa wanawalipia bima za afya watoto wao ili kupunguza gharama za matibabu watoto wanapougua.
Mahafali yanaendelea.
Mahafali yanaendelea.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali.
Wanafunzi wakitoa burudani ya wimbo.
Kundi cha The Family kikitoa burudani ya wimbo.
Onesho la mitindo ya ubunifu wa mavazi likiendelea.. Pichani ni vijana wakionesha ubunifu wa mavazi ya Mama Afrika.
Onesho la vazi mavazi ya wahudumu wa kwenye Ndege likiendelea.
Vijana wakiwa katika mavazi mbalimbali wakati wa onesho la mavazi kwenye mahafali ya 11 ya kidato cha nne Kom Sekondari mwaka 2019.
Kulia ni Walimu waliofanikisha zoezi la vijana kuonesha mitindo ya mavazi wakizungumza kwenye mahafali ya 11 ya kidato cha nne Kom Sekondari mwaka 2019.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Vijana wa Skauti wakionesha michezo ya ukakamavu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne Kom Sekondari mwaka 2019.
Vijana wakisoma taarifa ya habari ya Vichekesho wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wakiimba shairi.
Mahafali yanaendelea.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akizungumza wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom,ambapo makadirio ya gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo ni milioni 6.
 Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akichangia pesa wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
 Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akiendesha Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom. Pichani ni sehemu ya wanaume wakichangia pesa ili kufanikisha ununuzi wa vifaa hivyo.
 Akina mama wakichangia pesa kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
 Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akimpa Kampani ya kucheza mzee aliyejitokeza kuchangia pesa huku akicheza muziki wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akikabidhi zawadi kwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kom.
Zoezi la utoaji zawadi kwa walimu wa shule ya Kom Sekondari likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi kwa walimu wa shule ya Kom Sekondari likiendelea.
Ukawadia muda wa kugawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne 2019 katika shule ya Sekondari Kom.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akiendelea na zoezi la kukabidhi vyeti mbalimbali kwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2019 katika shule ya sekondari Kom.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea.
Walimu  wa shule ya sekondari Kom wakikabidhi zawadi kwa Mgeni rasmi ,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi.
Mshereheshaji 'MC' wakati wa mahafali akiendelea kutoa utaratibu wakati wa mahafali hayo.
Wazazi wakifurahia na kijana wao.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Walichokizungumza Chama cha ADC kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema licha ya baadhi ya wagombea wake kuenguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kitashiriki uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Katibu mkuu wa chama cha ADC, Hassan Doyo amezungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya chama hicho na kuweka wazi kuwa hawatajitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Wakati ADC wakieleza hayo vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, UPDP, NLD, Chauma, ACT-Wazalendo na CUF vimeshatangaza kutoshiriki uchaguzi huo kwa madai ya kutotendewa haki ikiwa ni pamoja na wagombea wake wengi kuenguliwa.

“Sisi ni mabingwa wa changamoto hatupelekwi na mihemko ya watu, tunapelekwa na misingi ya chama cha siasa kwa sababu hata walipofuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar wengine walisusa lakini sisi hatukufanya hivyo,” amesema Doyo


Share:

Jeshi la Polisi Lamshikilia Halima Mdee....Kufikishwa Mahakamani Jumatatu

Mbunge wa Kawe Halima Mdee anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay, kufuatia agizo la Mahakama ya Kisutu la kukamatwa kwa wabunge wanne wa CHADEMA.

Jeshi la Polisi Kinondoni limesema Mdee ameripoti mwenyewe kituoni hapo leo Novemba 16, 2019 na atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

'Ni kweli yupo hapa kituoni tunamshikilia kama ambavyo Mahakama iliagiza na yeye amekuja mwenyewe kuripoti hapa, hivyo taratibu zote za kipolisi zinafanyika na Jumatatu atafikishwa mahakami', amesema Msaidizi wa RPC Kinondoni.

Amri hiyo ya kukamatwa kwa wabunge hao Halima Mdee, Peter Msigwa, John Heche na Ester Bulaya, ilitolewa jana, Novemba 15, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba, ambapo alisema kuwa kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya upande wa mashtaka kumhoji Mbowe na baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake kutoka upande wa utetezi na ndipo ilipobainika washtakiwa hao wanne kutokuwepo mahakamani.
 


Share:

Mtoto wa miezi mitano atelekezwa nyumba ya kulala wageni Njombe

Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limefanikiwa kumpata mtoto wa miezi mitano aliyetelekezwa nyumba ya kulala wageni na kumuhifadhi chini ya uangalizi wa idara ya ustawi wa jamii.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa ametoa taarifa hiyo kwa wanahabari mkoani humo akibainisha kuwa mtoto huyo amekutwa kwenye nyumba ya kulala wageni inayofahamika kama Shamba Guest House iliyopo mjini Njombe huku akiacha ujumbe wa kuelekea mwanza .

“Shamba Guest amekutwa mtoto ambaye ana umri mdogo zaidi na ametelekezwa na mwanamke ambaye ni mama yake na ameacha ujumbe amesema anaenda eneo la Mwanza na huyu msaidizi amemuachia huyo mtoto,na pindi mambo yatakapo kuwa mazuru atamtumia hela”anasema Hamis Issa

Kwa mujibu wa kamanda mwanamke huyo anafahamika kwa jina la Stella Mtweve na mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miezi mitano na nusu  ametambuliwa kwa jina la Kelvin Mmagoma .


Share:

Chief Internal Auditor Job at Kariakoo Markets

Chief Internal Auditor Employer: KARIAKOO MARKETS Date Published: 2019-11-15 Application Deadline: 2019-11-29 DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i.To provide an independent appraisal of the effectiveness of financial control system and compliance with the Corporation Policies; ii.To review Corporation Accounting procedures to ensure they comply with the financial accounting system; iii.To observe Plans, Policies and Procedures of the Corporation operations and… Read More »

The post Chief Internal Auditor Job at Kariakoo Markets appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Head of Procurement And Supplies at Job at Kariakoo Markets

Head of Procurement And Supplies Unit Employer: KARIAKOO MARKETS Date Published: 2019-11-15 Application Deadline: 2019-11-29 DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i.To Head the Procurement and Supplies Unit; ii.To advise the General Manager on matters related to Procurement and Supplies according to the rules and regulations; iii.To prepare and implement Annual Procurement Plan of the Corporation; iv.To plan, manage, coordinate and… Read More »

The post Head of Procurement And Supplies at Job at Kariakoo Markets appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Human Resources And Administration Manager at Job at Kariakoo Markets,

Human Resources And Administration Manager Employer: KARIAKOO MARKETS Date Published: 2019-11-15 Application Deadline: 2019-11-29 DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i.To manage the Department of Human Resources and Administration; ii.To assist and advise the General Manager on all issues related to Human resources and administration; iii.To coordinate all Corporation Meetings; iv.To prepare budget of the section in liaison with Planning and… Read More »

The post Human Resources And Administration Manager at Job at Kariakoo Markets, appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu: Ukuaji Wa Uchumi Kuendana Na Maendeleo Ya Watu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020/2021 umelenga kutekeleza maeneo ya kipaumbele ikiwa ni pamoja na kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa kuweka mkazo katika upatikanaji wa huduma bora za jamii ikiwemo elimu, maji, afya, umeme na barabara.

Ametaja maeneo mengine ni ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda kwa kuimarisha sekta ya kilimo kwa kujenga viwanda vitakavyotumia malighafi inayopatikana nchini, kuimarisha mashirika ya viwanda na kuanzisha na kuendeleza maeneo ya viwanda.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Ijumaa, Novemba 15, 2019) wakati akiahirisha mkutano wa 17 wa Bunge la 11 jijini Dodoma. Amewasisitiza wananchi kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uzalendo ili kuiwezesha nchi kufikia malengo ya kujenga uchumi imara, unaojitegemea na wenye kuweza kuhimili ushindani.

“Ujenzi wa mazingira wezeshi katika kuendeleza miundombinu itakayosaidia maendeleo ya biashara na uwekezaji nchini; kuhakikisha Watanzania wenye sifa stahiki wanapewa kipaumbele katika kandarasi au ajira zinazotokana na utekelezaji wa miradi ya kimkakati.”

Amesema eneo lingine ni kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa Mpango. Baada ya tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/2017–2020/2021 kwa lengo la kuimarisha usimamizi na kuanza maandalizi ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022–2025/2026).

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kusisitiza Maafisa Masuuli wazingatie maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo na wahakikishe kamati za mipango na bajeti katika mafungu yao zinatekeleza majukumu yake ipasavyo. “Serikali kwa upande wake itaandaa mipango ya kisekta, kitaasisi na kimaeneo ambayo utekelezaji wake utachochea ujenzi wa uchumi wa viwanda, mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.”

“Katika udhibiti wa matumizi, naendelea kuwasisitiza Maafisa Masuuli wahakikishe wanatumia mfumo wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (Tanzania National Electronic Procurement System – TANePS). Hivyo, kila taasisi ya nunuzi ihakikishe inatumia mfumo huo kabla ya tarehe 31 Desemba 2019.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa upande wake itaendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta zinazogusa wananchi moja kwa moja na kuhakikisha kuwa matunda ya kukua kwa uchumi yanawafikia wananchi.

“Watanzania wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika kipindi hiki ambacho amekuwa akichukua hatua za makusudi kuhakikisha anajenga uchumi imara, kuboresha kipato na hali ya maisha ya wananchi.”

Amesema matunda ya maboresho hayo yanayoendelea yanaonekana katika maeneo mengi. “Ndani ya miaka 26 kuanzia 1991/1992 hadi 2017/2018 kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kimeweza kupungua kwa asilimia 13. Kadhalika, umaskini wa chakula nao umepungua kutoka asilimia 10 mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18.”  

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema katika kuelekea msimu wa kilimo wa 2019/2020 hali ya upatikanaji wa chakula nchini imeendelea kuimarika kutokana na uzalishaji mzuri wa mazao ya chakula kwa msimu 2018/2019, ambao ulifikia tani milioni 16.41 ikilinganishwa na mahitaji ya tani milioni 13.84 na kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula kwa asilimia 119.

Amesema pamoja na uzalishaji huo mzuri, kumekuwepo na mahitaji makubwa ya nafaka katika baadhi ya maeneo kutokana na hali ya mvua kutokuwa nzuri na kuwepo kwa dalili za kupanda bei za nafaka, Serikali imetoa maelekezo kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa kuhakikisha inasambaza nafaka kwenye maeneo yenye upungufu ili kukabiliana na changamoto ya kupanda kwa bei.

“Nitumie fursa hii kuwahimiza wakulima kutumia vizuri mvua za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mengi ya nchi yetu kwa kupanda mazao yanayostahimili ukame na ekolojia ya maeneo husika. Aidha, tukumbuke pia kujiwekea akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya matumizi ya kaya baada ya mavuno badala ya kuuza chakula chote.”

Kuhusu upatikanaji wa pembejeo, Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha wakulima wanapata mbolea kwa wakati na bei nafuu, Serikali imetoa bei elekezi kwa mbolea aina ya DAP na UREA ambazo zipo katika Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja. “Hivyo, nitumie fursa hii kuzikumbusha mamlaka husika kuhakikisha kwamba bei elekezi zinafahamika kwa wakulima katika maeneo yote na wauzaji wanauza kwa kuzingatia bei hizo.”

Pia, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu masoko ya mazao ya kilimo ambapo amesema licha ya kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini, kumekuwepo na changamoto kadhaa za upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa baadhi ya mazao ikiwemo la pamba, korosho na tumbaku.

Amesema changamoto hizo zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko na mwenendo wa bei katika soko la dunia pamoja na uwezo mdogo wa kuchakata mazao hayo nchini, hivyo Serikali inaimarisha mifumo ya masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji kwa kuimarisha viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. 

“Hatua hizi zitasaidia kuongeza thamani ya mazao na hivyo, kuimarisha bei. Kwa sasa tunaendelea na msimu wa mauzo wa zao la korosho baada ya mazao ya pamba na kahawa kumaliza. Minada ya korosho inaendelea vizuri. Viongozi wa Mikoa na Wilaya wasimamie malipo kwa wakulima na kuhakikisha wanalipwa kwa wakati.”


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi November 16




Share:

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Daniel Budeba kuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania – GST).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Budeba umeanza tarehe 15 Novemba, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Budeba alikuwa Mhadhiri wa Idara ya Uhandisi wa Kemikali na Madini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).


Share:

Taifa Stars Yaichapa 2-1 Equatorial Guinea michuano ya Kufuzu Afcon 2021.

Taifa stars jana imeanza vema michuano ya Afcon kwa kuibuka kidedea mbele ya timu ya Equatorial Guinea kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Stars iliyo chini ya Etienne Ndayiragije iliyoanza kwa kasi kipindi cha kwanza haikuweza kutumia vema nafasi saba za kipindi cha kwanza na kuruhusu wapinzani wao Equatorial Guinea kuandika bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Pedro Obiang akimtungua kipa mkongwe wa Tanzania, Juma Kaseja kwa shuti la mbali.

Dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili, kocha Mrundi wa Tanzania, Etienne Ndayiragijje alianza na mabadiliko ya kuongeza nguvu katika safu ys ushambuliaji, akimtoa beki wa kulia Hassan Ramadhani Kessy na kumuingiza mshambuliaji, Ditram Nchimbi.
 
Ni mabadiliko hayo yaliyoisaidia Taifa Stars kupata bao la kusawazisha likifungwa na kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Happygod Msuva dakika ya 68 akimalizia mpira uliookolewa na kipa baaada ya yeye mwenyewe kuunganisha kwa kichwa kona ya beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
 
Taifa Stars iliongeza kasi ya mashambulizi baada ya bao hilo na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 90  baada ya kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar Junior ‘Sure Boy’ kufunga bao la ushindi kwa shuti la mbali.
 
Baada ya ushindi huo, Taifa Stars itasafiri kuwafuata Libya Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir Jumanne ya Novemba 19 kwa mchezo wa pili wa kundi hilo.


Share:

Friday, 15 November 2019

Watumishi 44,800 Wa Kada Ya Afya Kuajiriwa Nchini Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/20 Ili Kuboresha Huduma Za Afya

Happiness Shayo-Dodoma
Serikali imepanga kuajiri Watumishi 44,800 wa Kada ya Afya kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi wa kada hiyo na kuboresha huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mhe. Silafu Jumbe Maufi (Viti Maalum) aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuajiri watumishi wa kada ya afya ili kuboresha huduma za afya nchini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele cha ajira kwa kada ya afya na imekuwa ikitoa vibali vya ajira kwa kuzingatia ukomo wa bajeti kuu ya mshahara na vipaumbele vya mwajiri husika.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameweka bayana kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali ilitoa vibali vya ajira 8,000/= kwa kada ya afya, lakini lengo halikufikiwa kwa sababu ya kuwepo kwa wataalamu wachache wa kada hiyo waliojitokeza kuajiriwa Serikalini.

Ili kukabiliana na upungufu wa Watumishi wa kada ya afya, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamasisha wananchi katika majimbo yao kusoma masomo yatakayowawezesha kuajiriwa katika kada ya afya kwa lengo la kuwahudumia Watanzania.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger