Tuesday, 3 September 2019
Monday, 2 September 2019
Mahakama Kuu Yakataa Maombi ya Kusimamisha Kuapishwa Mrithi wa Tundu Lissu Jimbo la Singida Mashariki
Mahakama Kuu ya Tanzania imeridhia Mbunge mteule wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CCM, Mhe. Miraji Mtaturu kuapishwa bungeni kesho Septemba 3, 2019 na imedai kuwa maombi rasmi ya Mhe. Tundu Lissu kupinga baadhi ya mambo yatatolewa Septemba 9, 2019.
ZAIDI YA WANANCHI 800 WA WILAYA YA KISARAWE WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA YA AFYA BURE
Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza ambaye ni madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani ambapo amesema kuwa zoezi lao limekuwa la mafanikio makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi wengi zaidi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wananchi wakiojitokeza kupatiwa huduma ya huduma ya afya bure iliyofanyika iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani
Mkurugenzi wa Miradi wa DCAT, Linas Kahisha (mwenye miwani) akigawia wananchi maji wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza (mwenye miwani) ambaye ni madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) akisimamia utoaji wa huduma ya afya bure.
Wananchi wakiwa katika dirisha la kupata dawa wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe Musa Gama (wa tatu toka kulia msitari wa mbele) akiwa na Timu ya Madaktari na wauguzi wa Wilaya ya Kisarawe na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT).
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Zaidi ya wananchi 800 wa wilaya ya Kisarawe, Pwani wamejitokeza katika zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyoandaliwa na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT).
Akizungumza wakati wa zoezi la hitimisho la zoezi la utoaji wa huduma ya afya bure iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza amesema kuwa zoezi lao limekuwa la mafanikio makubwa kwa vile wameweza kupata wananchi wengi zaidi.
"Kikubwa tunamshukuru Mungu kwa kuweza kufanikisha zoezi hili na limekuwa la mafanikio zaidi maana tulitarajia watu 400 ila tumepata watu mara mbili ya namba tuliyoiweka, yani tumepata watu zaidi ya 800 na wote tumeweza kuwahudumia japo sisi hatukuwa wengi," amesema.
Amesema kuwa ushirikiano na umoja walionao ndiyo nguzo pekee iliyoweza kufanikisha zoezi walilopanga kulifanya.
"Kiukweli timu yetu imekuwa na ushirikiano zaidi kuanzia Viongozi wa Wilaya ya Kisarawe wakiwemo wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya, waandishi wa habari na wote tuliokuwa nao kipindi hicho," amesema Dkt Tungaraza.
Ameongeza kuwa magonjwa waliyokuwa wakichunguza ni yale ambayo si ya kuambukiza kama vile Shinikizo la damu, presha na idadi kubwa imeonyesha watu wengi wanaugua shinikizo la damu hasa akina mama.
"Tunashukuru waliojitokeza idadi kubwa ni akina mama kwa asilimia 60, akina baba asilimia 30 na watoto asilimia 10% na magonjwa yaliyoongoza baada ya uchunguzi ni Saratani ya Shingo ya Kizazi na Shinikizo la damu na kidogo Kisukari,' amesema.
Ametoa ushauri kwa jamii kuendelea kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kuweza kujiimalisha kuliko kusubiri mpaka waugue ndiyo waweze kukimbilia kutibiwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Miradi wa DCAT, Linas Kahisha amesema wameshukuru kwa ushirikiano walioweza kuupata kutoka katika serikali ya wilaya ya Kisarawe na pia ubalozi wa China nchini Tanzania ambao ndiyo waliowawezesha kufanikisha zoezi la utoaji huduma ya Afya Bure na pia amewaomba jamii na wadau wengine kuweza kuwaunga mkono ili kufanikisha waweze kufika maeneo mengi zaidi.
"Tumefurahi jinsi uongozi mzima ulivyoweza kutupa ushirikiano kuwezesha wakazi wa Kisarawe kupatiwa matibabu ya afya bure ila japo idadi iliyojitokeza imekuwa ni kubwa nje ya malengo yao waliyokuwa wamepanga," amesema.
Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe, Stanford John amewashukuru madaktari wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT) kwa moyo wao wa kujitoa kuhudumia wananchi wa Kisarawe.
MAHAMUDU AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUHIMIZA AMANI
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera Hamimu Mahamudu
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuhimiza amani kwa waumini wao ili kuwa na ustaarabu wa kumjua Mungu ikiwemo kuishi na watu vizuri na kuwaombea viongozi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 2, 2019 na Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera Hamimu Mahamudu katika hafla ya kuMpongeza Mzee Twail Ismail Tabilane aliyerejea kutoka Makka Saudi Arabia kuhiji iliyofanyika wilayani Misenyi Mkoani Kagera .
Mahamudu amesema nchi ya Tanzania licha ya kuendelea kuwapokea wageni kutoka sehemu tofauti lakini bado ni kisiwa cha amani hivyo amani ili iendelee kuwepo, lazima viongozi wa dini waelekeze kwa waumini wao ili kusisitiza amani hiyo izidi kutawala.
Amesema amani ni tunu kubwa hivyo ni vyema itunzwe na kuenziwa huku akiwaomba viongozi wa dini ,waumini wamuombee sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya na kutaja kufurahishwa na uamzi wake wa kuwaita watendaji wa kata nchi nzima Ikulu kwa ajili ya mazungumzo ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mahamudu amewataka viongozi wa dini na waumini wao kuwa na ustaarabu wa kumjua Mungu ikiwemo ustaarabu wa kuishi na watu vizuri lakini na kuifanya dunia iwe mahali bora pa kuishi.
"Nimeguswa sana na umoja huu wa waumini wa dini ya kiislamu na wasiokuwa waumini wa dini hii katika matukio mbalimbali hasa ya kidin, hakuna ubaguzi wala hamchagui, umoja huu na ushirikiano huu naomba uendelee amesema’’,amesema.
Katika hatua nyingine Katibu huyo amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
SHEIKH TWAHILI ISMAIL TABILANE AREJEA KUTOKA MAKKA KUHIJI...AFANYIWA HAFLA YA MAPOKEZI MISENYI
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Sheikh Twahili Ismail Tabilane (70) mkazi wa kijiji cha Burembo kata ya Mushasha wilayani Misenyi mkoani Kagera amerejea salama hapa nchini akitokea Mji wa Makka Saudi Arabia katika kutekeleza ibada ya Hija ya dini ya kiislamu.
Akizungumza kwenye hafla ya kupongezwa kutoka katika ibada ya Hijja iliyofanyika Septemba 2, 2019, nyumbani kwake Burembo, Sheikh Ismail ambaye kwa sasa ni Khaji amesema kutokana na Umoja uliopo Makka ikiwemo ushirikiano na upendo ni ishara kuwa kila Muislamu aige na kujifunza.
Ameitaja safari hiyo kuwa ni ya neema kubwa iliyosababisha yeye kurudi hapa nchini akiwa salama hivyo ametamani tena kurudi nchini makka.
Shekhe huyo amesema kila Muislamu aione habari ya kwenda hija kama ya kawaida na kuwa kila muumini wa dini hiyo atekeleze suala la kufika makka
"Namshukuru Mungu hali niliyoikuta kule Makka ni nzuri natamani kurudi mwaka ujao, hii ni neema kule hakuna cha tajiri wala maskini kule ni haki sawa kwa wote", amesema.
Amesema safari ya kwenda Hija haina ubaguzi kwani hija hiyo inawapa Waislamu wote haki sawa, ikiwemo chakula cha bure, malazi na mahitaji mengineyo muhimu pamoja na kupewa mafunzo ikiwemo kusoma vitabu vya Quran Tukufu vyenye maudhui ya kuiheshimu dini hiyo.
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta amewahimiza waislamu mkoani Kagera kuendelea kuwa wamoja na kumuomba Mungu ili kila muumini wa dini hiyo aweze kufikia Makka
Hata hivyo Sheikh Kichwabuta ameyashukuru madhehebu tofauti mkoani Kagera yaliyoshiriki kwa kumpokea Sheikh Twail aliyekwenda kuwakilisha dhehebu hilo katika ibada hiyo.
Amewataka Waislamu kujitokeza kwa wingi mwaka ujao 2020 kuudhuria ibada ya Hija.
Naye Sheikh Mkuu Wilaya ya Misenyi mkoani, Abduzaydi Kyagulani ametoa pongezi kwa shekhe huyo kurejea salama hapa nchini na kuhimiza umoja kwa waumini hao na madhehebu tofauti ikiwemo kuiombea nchi amani
Amesema Masheikh kutoka Kanyigo,Buyango, Kilimilile, Mtukula,Bugandika , Burembo wote wamerejea kwa usalama bila matatizo ambapo ameongeza kuwa madhumuni mazito ni kujenga nguzo tano za kiislamu sambamba na umoja.
Shekhe wa mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta akimpongeza Shekhe Ismail kwa kurejea kutoka Makka. Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Kushoto ni Sheikh Twahili Ismail Tabilane (70) mkazi wa kijiji cha Burembo kata ya Mushasha wilayani Misenyi mkoani Kagera akizungumza baada ya kurejea kutoka Makka.
Shekhe wa mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta akizungumza wakati wa kumpokea Sheikh Twahili Ismail Tabilane akitokea Makka.
Shekhe wa wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Abduzayid Kyagulani akizungumza wakati wa kumpokea Sheikh Twahili Ismail Tabilane akitokea Makka.
Shekhe wa mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta akimpongeza Shekhe Ismail kwa kurejea kutoka Makka. Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Kushoto ni Sheikh Twahili Ismail Tabilane (70) mkazi wa kijiji cha Burembo kata ya Mushasha wilayani Misenyi mkoani Kagera akizungumza baada ya kurejea kutoka Makka.
Shekhe wa mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta akizungumza wakati wa kumpokea Sheikh Twahili Ismail Tabilane akitokea Makka.
Shekhe wa wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Abduzayid Kyagulani akizungumza wakati wa kumpokea Sheikh Twahili Ismail Tabilane akitokea Makka.
Picha 12 : RAIS MAGUFULI AKIWA NA MAAFISA WATENDAJI WA KATA NCHI NZIMA LEO IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019. Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata chakula cha mchana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima wakati wa chakula cha mchana baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata wa Mkoa wa Lindi baada ya mkutano wao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019.
Picha na Ikulu
AMSHAMBULIA EX BAADA YA KUMNASA AKIPANGA MIPANGO YA KUOLEWA NA BWANA MWINGINE
Mkulima wa Kijiji cha Nangaru, mkoani wa Lindi Abdallah Shaibu Nyuki (30), amehukumiwa na Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara, kwenda jela miaka 8, baada ya kupatikana na makosa 2 ya kutaka kuuwa bila kukusudia.
Akitoa hukumu hiyo Jaji Mfawidhi Mkuu wa Mahakama hiyo Joel Paul Ngwembe, amesema anamhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 4 kwa kosa la kwanza la kujaribu kuua na miaka 4 tena kwa kosa la kujeruhi.
Awali Mwanasheria wa Serikali, Emmanuel John amesema kuwa mshtakiwa akiwa na panga mkononi Disemba 08, 2018, aliwashambulia Hashimu Bakari Mnocho na Zakia Salum Kindumba, ambaye ni mwanamke aliyeachana naye, baada ya kuwakuta wako pamoja wakizungumzia mipango ya ndoa.
Mwanasheria huyo amesema kuwa baada ya kuwakuta wakiwa wanazungumza mshtakiwa akiwa na panga mkononi aliwajeruhi kwa kuwashambulia mwilini, ambapo baada ya kufanya tukio hilo alikimbia Kijiji cha jirani.
Chanzo- EATV
ROGATHE AENDELEA KUOMBA MSAADA WA MATIBABU AMALIZIE DOZI...AWASHUKURU WALIOJITOKEZA MWANZO
Muonekano wa ngozi ya Rogathe Kabla ya kuanza kupatiwa huduma ya matibabu
Muonekano wa ngozi ya Rogathe Kabla ya kuanza kupatiwa huduma ya matibabu
Rogathe Cycprian Makala akionesha namna matibabu yalivyomsaidia kutibu ugonjwa wake wa ngozi kwa fedha za wasamaria wema na sasa hawashwi tena kama hapo awali na anaendelea na masomo yake ya Kidato cha Tano.
Rogathe Cycprian Makala (kushoto) akiwa na mama yake Happines Stephen Makala wakitoka kupatiwa matibabu leo Septemba 2,2019, na kuomba msaada wa fedha ili amalizie matibabu kwa miezi sita iliyosalia na kutoa shukrani wa wasamaria ambao walimsaidia awali na kupata matibabu kwa miezi mitatu.
*****
Happiness Stephen ambaye ni mkazi wa mtaa wa Busulwa kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga anaendelea kuomba msaada fedha za matibabu kwa binti yake aitwaye Rogathe Cycprian Makala (18), ambaye anasumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka 16 sasa.
Anatoa shukrani kwa wadau ambao awali waliojitokeza kumsaidia fedha za matibabu kwa binti yake ambazo zimetumika kumtibu kwa miezi mitatu na kusalia miezi sita kwani anatakiwa atibiwe kwa muda wa miezi tisa hivyo anaomba wasamaria wema waendelee kumsaidia ili apate kupona.
Anasema kwa matibau ambayo ameyapata binti yake sasa hivi hali yake inaendelea vizuri hajikuni tena usiku kucha kama hapo awali na anaendelea na masomo yake ya kidato cha Tano kama Kawaida.
Awali kabla ya kupatiwa matibabu binti huyo alikuwa halali usiku kucha anashinda anajikuna tu na hata wakati wa jua kali, huku vipele vikimtoka mwili mzima.
Amesema binti yake huyo kwa sasa anapatiwa matibabu na daktari bingwa kutoka apolo india ambaye hua anakuja mkoani shinyanga kila baada ya mwezi, na matibabu yake yatachukua miezi tisa kwa gharama ya shilingi milioni 4,536,000.
Anasema dozi ya dawa ambayo anatumia kila mwezi ni shilingi 504,000/=, ambapo kwa miezi hiyo tisa ni sawa na shilingi 4,536,000/=.
Kwa yeyote atakaye guswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo:
Vodacom : 0764206669 ukitaka kutuma kwa m-pesa jina litasoma Happines Makala
Tigo: 0676368559, jina litasoma Happines Makala (Tigopesa)
Halotel: 0626845953, jina litasoma Eliud Makala (Halopesa)