Na.Amiri kilagalila Timu za NJOMBE MJI FC na NAMUNGO FC zimegawana pointi moja, baada ya kumaliza dakika tisini za mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe mkoani mkoani humo, matokeo ambayo yamewafanya mashabiki wa soka wa Njombe mji kutoa lawama za wazi kwa waamuzi wanaochezesha michuano hiyo. Penati iliyochezwa dakika tatu kabla mpira haujamalizika ndiyo iliyopoteza matumaini ya timu ya Njombe Mji Fc kutoka uwanjani na alama tatu kufuatia mchezaji wa timu hiyo kumwangusha mchezaji wa Namungo Fc katika eneo la hatari,…
Saturday, 2 February 2019
RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI CHARLES KITWANGA ALIYELAZWA HOSPITALI MUHIMBILI
MCHIMBAJI WA MADINI AFARIKI KWA KUFUKIWA KIFUSI
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Joachimu Kibinda, (48), mchimbaji wa madini na mkazi wa Songambele, wilayani Simanjiro, amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo akiwa anachimba madini.
Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Augustino Senga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya matukio mbalimbali ambayo yametokea mkoani hapa.
Alisema tukio hilo lilitokea Januari 28 majira ya saa 9:00 alasiri katika maeneo ya Machekecho Machimboni, Kata ya Naisinyai.
Katika eneo hilo, alisema watu wa aina tofauti wanafanya shughuli za uchimbaji wa madini kwa ajili ya kujiingizia kipato.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa uchunguzi zaidi wa madaktari na taratibu zikikamilika mwili huo utachukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya maziko.
ABIRIA WANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA BASI BIHARAMULO
Biharamulo, Na mwandishi wetu Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Bukoba kuelekea mikoani wamenusurika kifo huku Watu wanane wakijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kupata ajali wakiwa katika basi la Frester linalofanya safari zake Bukoba kwenda Dar es Salaam kisha kuacha njia na kupinduka katika kata ya Katahoka wilayani Biharamulo mkoani kagera. Gari hilo limetambulika kwa namba za usajili T375 DND ambapo mkuu wa polisi wilaya ya Biharamulo Rashid Mududhwari amekiri kuwepo ajali hiyo na kwamba yuko na mkuu wa wilaya Saada Malunde wanakusanya taarifa kamili na kwamba msemaji wa…
NABII MTATA ANAYEPAA ANGANI AKAMATWA
Nabii mwenye utata raia wa Afrika Kusini Shepherd Bushiri wa kanisa la Enlightened Christian Gathering Church (ECG) ametiwa nguvuni.
Bushiri alikamatwa Ijumaa, Februari 1, jijini Rustenberg, Afrika Kusinia na kulingana na taarifa kutoka kanisa lake nabii huyo na mke wake wanatuhumiwa kwa ulanguzi wa pesa.
Raia kadhaa Afrika Kusini walijitokeza mtandaoni na kusimulia walivyolaghaiwa pesa na Bushiri.
Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba, kukamatwa kwa nabii huyo kunajiri saa chache baada ya kuondolewa lawama kuhusu kisa cha waumini kukanyagana katika kanisa lake.
Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu 3. "Ukikumbuka kutokea mwaka jana tumesumbuka na tuhuma eti baba yetu alihusika na mganyagano uliotokea.
Amekamatwa na anahojiwa na makachero jijini Silverton, Pretoria," taarifa kutoka kanisa hilo ilisema.
Msemaji wa Bushiri kwa jina Maynard Manyowa alisema polisi walifika alfajiri na kumchukua nabii na mke wake na walidai walitaka kusema nao.
“Baadaye tuligundua ni wanachama wa Hawks. Walimchukua nabii watu na mama Mary Bushiri, waliwafunga pingu na kuwapeleka Pretoria," taarifa hiyo ilisema.
Ripoti zaidi zinasema kuwa, mamia ya watu wamekuwa wakilalamika kupitia mtandao kuhusu Bushiri kulaghaiwa pesa.
Reneilwe Mphahlele alidai kuwa, alipeana R21 000 (158,310.96 KES) wakati wa Pasaka 2017 ili kuonana ana kwa ana na mchungaji huyo.
Kulingana naye, anajutia kwa sababu hamna mabadiliko yoyote aliyoyaona baada ya kumwona Bushiri na kwamba sasa anafahamu Mungu ni wa kila mtu na hatolewi pesa.
Haijabainika wazi ikiwa ufichuzi wa punde kutoka kwa watu unahusiana kivyovyote na mashtaka yanayomkabili Bushiri.
Nabii Bushiri si mgeni katika kuhusishwa na kashfa zenye utata lakini inashangaza jinsi anavyoendelea kuwa na ufuasi mkubwa wa watu katika kanisa lake la ECG.
Karibuni alichapisha video mtandaoni akidai kuwa na uwezo wa kupaa angani wakati akihubiri.
Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.
Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
DIWANI WA CHADEMA AWEKWA NDANI KWA AMRI YA RC KISA DHARAU KAKUNJA NNE KWENYE KIKAO
Diwani wa Susuni (Chadema), Abiud Solomon amesimulia jinsi alivyoondolewa kwenye kikao na mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima na kuwekwa ndani kwa saa saba kisha kuachiwa akielezwa kuwa ana dharau kwa kuwa alikunja nne kikaoni.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Februari 2, 2019 amesema Malima alitoa agizo hilo kwa polisi kumweka ndani kwa madai kuwa ameonyesha dharau kwenye kikao cha kumtambulisha mkuu mpya wa wilaya ya Tarime, Charles Kabeho.
Katika tukio hilo lililotokea jana Ijumaa Februari Mosi, 2019, Solomon amesema kabla ya kuondolewa alihojiwa kuhusu wadhifa wake, “lakini nilishangaa kusikia agizo la kuniweka ndani kisa nimekunja nne kwenye kikao cha mkuu wa mkoa.”
“Niliwekwa ndani kuanzia saa saa 9 alasiri hadi saa 3 usiku baada ya viongozi wangu wa chama kufanya taratibu za kuniwekea dhamana wakafanikiwa kunitoa lakini nikatakiwa kurudi siku ya Jumatatu Februari 4.”
Ameongeza, “Tulikuwa na kikao cha kumkaribisha mkuu wa wilaya mpya, nilipata nafasi ya kukaa eneo la waandishi wa habari ili kuwapisha wapite, nililazimika kubebanisha miguu yangu (kukunja nne) ili kutoa nafasi ya wao kupita na kufanya kazi yao vizuri, ila ikachukuliwa kwamba namdharau mkuu wa mkoa.”
Via Mwananchi
Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.
Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
MTOTO MWINGINE AUAWA NJOMBE
Mtoto wa miaka 10, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili, amekutwa ameuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa kichakani eneo la Lupembe, wilayani Njombe.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Renata Mzinga, amesema kuwa maiti hiyo iliokotwa karibu na nyumbani kwao na mtoto huyo, baada ya majirani kuanza kumtafuta mara tu baada ya kupata taarifa kutoka kwa wazazi wake kuwa mtoto wao haonekani.
“Mtoto alipotea tangu saa 12, lakini wazazi wake walianza kumtafuta majira ya saa nne ndo wakakuta ametupwa karibu tu na nyumbani kwao, baada ya mtoto kwenda kucheza kwa jirani ilipofika saa moja hajarudi, walienda kutoa taarifa kwa majirani na polisi, sasa wakaanza kutafuta mpaka wakakuta hiyo maiti, haikupita siku nzima, ni masaa machache sana”, amesema Kamanda Mzinga.
Matukio hayo ya watoto kuuawa yamekuwa yakitokea mara kwa mara mkoani Njombe na taarifa zake kufikishwa Bungeni, jambo ambalo Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema kwamba jeshi la Polisi linafanyia kazi kuweza kuwabaini wauaji.
Chanzo-EATV
ALIYEONDOLEWA JELA KWA MSAMAHA WA RAIS AKAMATWA NA SARE ZA JWTZ
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia aliyekuwa mfungwa katika Gereza la Segerea na kuachiwa kwa msamaha wa Rais mwaka jana, Emmanuel Magoti (18), kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Kamishna wa Polisi, Lazaro Mambosasa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Januari 30, mwaka huu, saa 8 mchana eneo la Mbagala. Alisema Polisi ilimkamata kijana huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba amekuwa akijihusisha na makosa ya uhalifu ndani ya kanda hiyo huku akiwa amevaa sare za JWTZ.
“Lengo la mtuhumiwa huyu ni kujificha baada ya kutenda makosa hayo ili lawama ziwaendee wanajeshi hao. Tulivyopata taarifa hizo tulianza ufuatiliaji mara moja na kwa bahati tulimkamata na tulimkuta akiwa na sare hizo ambazo ni suruali mbili, koti moja na fulana,” alisema. Alieleza kuwa makachero wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari polisi wa JWTZ (MP) walifika katika nyumba ya mtuhumiwa huyo na kukuta sare hizo.
Alifafanua kuwa katika mahojiano na mtuhumiwa huyo alikiri kujihusisha na matukio ya uhalifu akishirikiana na wenzake wawili ambao walifanikiwa kutoroka na kwamba wanaendelea kuwafuatilia. “Mtuhumiwa huyu alikiri kwamba alikuwa mfungwa katika gereza la Segerea kwa kosa la wizi na kwamba aliachiwa kwa msamaha wa Rais mwaka 2018.
Msako mkali unaendelea kuwatafuta wenzake wawili wanaoshirikiana nao katika matukio hayo,” alieleza. Mambosasa alitoa onyo kwa wafungwa wanaotoka magerezani kwa rufaa, msamaha wa rais au kumaliza vifungo, kuacha kujihusisha na matendo hayo kwa sababu wanakuta hali shwari lakini wanachochea mitandao ya uhalifu.
Alisisitiza kuwa lengo la msamaha ni kumfanya mtu aliyejutia arudi kwa jamii kuungana nao kufanya shughuli za jamii na kwamba wanachotegemea ni mabadiliko ya tabia wanapofanya mafunzo jela ili aweze kupata maarifa waweze kuishi kama raia wema wanaofuata sheria. Kwa mujibu wa Mambosasa, wafungwa wanaotoka gerezani na kuanzisha makundi ya uhalifu watambue kwamba jeshi hilo liko macho kwani wataendelea kufuatilia ili kuwalinda raia wema dhidi ya wahalifu.
WANNE WAUAWA TENA NJOMBE
Na Amiri kilagalila Mtoto mwingine anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 7-10 aliyefahamika kwa jina la RECHAEL MALEKELA mkazi wa kijiji cha Matebwe wilayani Njombe amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali mita chache kutoka nyumbani kwao. Akithibitisha tukio hilo mkuu wa wilaya ya Njombe RUTH MSAFIRI alisema kuwa ni kweli mtoto huyo amekutwa amefariki na walizipata taarifa hizo usiku wa kuamkia leo. “Mtoto huyo amechomwa chomwa na vitu vyenye ncha kali nadhani mtoto huyu alikuwa peke yake akitoka kwa mama yake na kuelekea kwa kaka yake…
BABA MZAZI AWAPACHIKA MIMBA MABINTI ZAKE WAWILI
Baba wa mabinti wawili mjini Eldoret nchini Kenya anasakwa na maafisa wa polisi baada ya kuwabaka na kuwapachika mimba watoto hao kwa wakati tofauti.
Baba huyo anasemekana kuanza kuwabaka wanawe mwaka wa 2014 mama yao alipoaga dunia.
Mshukiwa alikuwa amerejea nyumbani kutoka gerezani baada ya kukamatwa kwa kumbaka binti wake kitinda mimba.
Kulingana na taarifa za Citizen TV, jamaa huyo alipofika nyumbani kwake, alimbaka tena bintiye mkubwa ambaye kwa sasa amempachika pia mimba.
Msichana huyo aliwambia wanahabari kuwa dadake mdogo alijitoa uhai mwaka wa 2018 akiwa na ujauzito wa miezi saba.
Msichana huyo ambaye pia ni mjamzito, alisema aliwasilisha malalamishi yake kwa wazee wa kijiji ila hakuna hatua ambayo imechukuliwa dhidi ya baba yao
Aliamua kuranda katika mitaa ya mji wa Eldoret ila wasamaria wema wajitokeza na kumpa makazi.
Wasichana hao wamekuwa wakiteseka mikononi mwa baba yao ambaye anapaswa kuwalinda tangu mama yao alipofariki mwaka wa 2014.
MWALIMU MKUU ATUPWA JELA KWA WIZI WA FEDHA ZA SHULE
Mwalimu Mkuu shule ya sekondari Mikwambe, Paulo Lorry, amehukumiwa kifungo cha miaka sita na kutakiwa kulipa Sh milioni 16 katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke alizoiba kutoka akaunti ya shule.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Taasisiya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Temeke, Pilly Mwakasege, ilieleza kuwa mwamu Lorry amekutwa na hatia na kuhukukiwa kwenda jela.
Ilieleza kuwa mwalimu huyo alishtakiwa na makosa matatu ya matumizi mabaya ya ofisi kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mshitakiwa alikuwa ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikwambe Manispaa ya Temeke mwaka 2010 alipokea Sh milioni 28 kupitia akaunti ya shule namba CA 2011100236 kwa ajili ya ujenzi wa maabara shuleni hapo.
LUGOLA AWATAKA VIJANA KUTUNZA WAZEE WAO..HAKUNA ATAKAYESALIMIKA MAUAJI YA WAZEE
Waziri Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametoa wito kwa vijana wote nchini kuachana na tabia ya mauaji ya vikongwe na Wazee Nchini na kutoa onyo kwamba hakuna muuaji hata mmoja atakaye salimika na kukwepa mkono wa sheria.
Amesema hayo jana jijini Dodoma katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wazee makamanda wa jeshi la polisi na maofisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kujadiliana kwa pamoja kuhusu mbinu mpya za kutokomeza mauaji hayo kwa kutumia Mkakati mpya wa miaka 5 wa Kutokomeza Mauji ya Wazee na Vikongwe Nchini.
Mkakati huo uliozinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania tarehe 29, January 2019 wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Nchini uliofanyika Jijini Dodoma.
Aidha Waziri Lugola amewataka vijana kutambua kuwa kijana wa leo ni Mzee wa Kesho hivyo atambue kuwa machungu ya mauaji ya wazee wanayoyapata leo naye ayatarajie baadae kwa kuwa kila mtu atazeeka.
Kufuatia hali hiyo Waziri Lugola aliwataka Vijana kutunza wazee wao kwasasababu machozi ya wazee wanayolia kila siku kwa kwa kukosa matunzo ya watoto wao yanapelekea wazee wengi kuwa na macho mekundu yanayoplekea watu wenye imani potofu kuwapoteza maisha yao kwa imani za kishirikina.
Aliongea kuhusu Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee Waziri Nchini Lugola alisema lengo la mkakati huu ni kuhakikisha tunashirikiana ili ifikapo mwaka 2023 mauaji ya wazee yawe yamekomeshwa kabisa.
”Hatutakua na sababu yoyote ya kueleza tukishindwa kutekeleza wajibu huu muhimu wa kulinda uhai wa kundi hili tete. Naomba muongeze kasi ili tufikie lengo hili, tena ikiwezekana mapema zaidi kwani tutapimwa kwalo 2023’’. Aliongeza Mhe. Lugola.
Alitoa wito kwa vyombo vya dola hasa Jeshi la polisi kuendelea kufuatilia kwa ukaribu sababu na vichocheo vya mauaji haya ikiwa ni pamoja na kuwabaini wahusika wanaopanga na kutekeleza mauaji haya ili wafikishwe kwenye vyombo vya Sheria, na pale inapothibika wahusika wachukuliwe hatua kali ili tukomesha kabisa vitendo hivi vya kikatili.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu aliwaambia wajumbe wa Mkutano kuwa mahuaji ya vikongwe yalianza tangu miaka ya 1960 na serikali imekuwa ikipambana nayo lakini yamekuwa yakiendelea.
Dkt. Jingu aliongeza kuwa jughudi za serikali kupitia Jeshi la Polisi zimefanikiwa kupunguza mauaji haya lakini hayajakwisha kwasababu bado kuna watu wengi wenye Imani potofu katika Jamii hivyo ni lazima mapambano dhidi yao yaendelee.
Alisema kuwa Mkakati wa Kutokomeza Mauaji dhidi ya Wazee unalenga kuwa na Taifa linaloazingatia haki na ustawi wa wazee kwa kupiga vita imani za kushirikina, ubaguzi, ukatili na mauaji.
Aidha Dkt. Jingu aliongeza kuwa tafiti zilizopo zinaonesha mauaji na ukatili dhidi ya Wazee yanachochewa na Imani za kishirikina pamoja na migogoro ya ardhi hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee Nchini kwa lengo la kutokomeza kabisa mauaji haya.
TPDC YAIMARISHA SEKTA YA ELIMU MKOANI MTWARA
Bi. Marie Msellemu, Meneja Mawasiliano wa TPDC akimkabidhi hundi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Bw. Gelasius Byakanwa kiasi cha Tsh,. 13, 258,042 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa Mkoani Mtwara.
Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akikabidhi hundi kwa mratibu wa tasisi ya TAKUWA Bi. Hadija Malibecha
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Ndg.Omari Kipanga akitoa ufafanuzi wa mahitaji ya elimu mkoani Mtwara.
***
Katika jitihada za kutekeleza dhana ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kutekeleza kwa vitendo dhana hii kwa kushiriki katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo Mkoani Mtwara.
Katika tukio la hivi karibuni, TPDC imeweza kumkabidhi Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mh. Bw. Gelasius Byakanwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni kumi na tatu laki mbili hamsini elfu na arobaini na mbili ili kusaidia ujenzi wa darasa moja katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara.
Akiongea katika tukio hilo, Mh. Byakanwa alisema TPDC imefanya jambo kubwa na kuonyesha uzalendo kwa kurudisha kwa jamii, na aliishukuru TPDC kwa kuendelea kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali mkoani Mtwara, husani zile zinazoikumba sekta ya huduma za jamii ikiwemo elimu.
Vile vile mkuu wa mkoa alitoa rai kwa wadau na wawekezaji waliopo mkoani Mtwara kuiga mfano wa TPDC katika kuwajali wananchi kwa kuchangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Akimkabidhi mfano wa hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Bi. Marie Msellemu ambaye ni Meneja Mawasiliano wa Shirika alisema..
“TPDC ni mdau mkubwa wa Mkoa wa Mtwara, na kwa kupitia mfuko wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), TPDC imekuwa ikiwashika mkono wananchi wa Mkoa wa Mtwara na mikoa ya jirani katika kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji na hivyo kiasi hiki cha fedha kitauwezesha mkoa kuendelea kufikia lengo la kuweka mazingira mazuri ya kusomea kwa watoto wetu”.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Ndg. Omari Kipanga alieleza kuwa..
“Sisi kama halmashauri tumefarijika sana kwa msaada huu uliotolewa na TPDC, kwani fedha hizi zitaelekezwa moja kwa moja katika ujenzi wa madarasa katika halmashauri ya Wilaya yetu kama ilivyokusudiwa. Mchango huu uliotolewa na TPDC unakwenda kukamilisha kazi ya kuezeka madarasa manne katika shule ya msingi Mitambo pamoja na madarasa mawili katika shule ya sekondari ya Madimba’’.
Mkurugenzi Kipanga aliendelea kusisitiza kwamba uhitaji bado ni mkubwa kuweza kukamilisha uhitaji wa madarasa kwa Mkoa wa Mtwara na kuwataka wadau wa elimu na wawekezaji mbalimbali waliopo mkoani Mtwara kuiga mfano wa TPDC katika kurudisha kwa jamii na kuimarisha elimu mkoani hapo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndg. Evod Mmanda naye aliungana na viongozi waliotangulia kwa kuishukuru na kuipongeza TPDC kwa kusaidia kuboresha huduma mbali mbali za kijamii mkoani Mtwara.
Alieleza kuwa...
“Si mara ya kwanza kwa TPDC kuchangia kwani mwaka jana tumepokea kiasi cha 21,151,500 za kumalizia ujenzi wa zahanati ya kijjiji cha Mngoji pamoja na kiasi cha 12,000,000 za ujenzi wa choo cha wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Shangani”.
Katika hatua nyingine TPDC ilikabidhi Taasisi ya Kusaidia Wanawake Mkoani Mtwara (TAKUWA) kiasi cha milioni tatu laki tisa na elfu sabini kwa ajili ya unununuzi wa vitendea kazi vya ofisi ili kurahisisha shuguli za kila siku za taasisi hiyo.
Mratibu wa taasiis hiyo Bi. Hadija Malibecha alishukuru TPDC kwa msaada huo na alieleza kuwa “kabla ya upatikanaji wa vifaa hivyo tulikua tunafanya kazi katika mazingira magumu lakini sasa TPDC imetuboreshea mazingira ya kazi na kazi zinaenda vizuri”. TAKUWA inasaidia vikundi vya wanawake kwa ajili ya kuinua shughuli mbalimbali za kiuchumi na elimu.
Jumla ya vikundi 12 vya wakinamama mkoani mtwara vinasimamiwa na taasisi hii katika kupewa mafunzo ya ujasiriamali kama kutengeneza sabuni, ufugaji wa nyuki na ufugaji wa wa mbuzi lengo ikiwa ni kuboresha maisha ya wanawake.
WASANII WA FILAMU NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI NA UFANISI KWENYE KAZI ZAO
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu wa mkoa wa Tanga
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akizungumza katika mafunzo hayo
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco akizungumza katika mafunzo hayo
Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt. Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.
Msanii nguli wa Filamu mkoani Tanga akizungumza wakati wa mafunzo hayo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala
Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakifuatilia mafunzo hayo
Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo kulia ni KATIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo kushoto ni nKATIBU Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco.
Wasanii wa filamu hapa nchini wametakiwa kuhakikisha wanazingatia waledi na ufanisi mkubwa kwenye kazi zao ili ziweze kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii zinazowazunguka kutokana na tasnia hiyo hivi sasa kuwa mkombozi kwenye jamii.
Hayo yalisemwa na Mwezeshaji wa Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt. Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.
Alisema sanaa inaweza kuwa tija kubwa ya maendeleo kwa wasanii kwa kutengeneza ajira nyingi na kuweza kuwakomboa iwapo wataizingatia na kuithamini kwa kuonyesha walezi kwenye kazi zao.
“Ndugu zangu wasanii labda niwaambie kwamba mkiwa makini kwenye kazi zenu na kuzingatia weledi mkubwa mnaweza kufika mbali kimafanikio kutokana na namna tasnia ya filamu hapa nchini iliyokuwa”,alisema.
Aidha alisema pia wasanii lazima watambue kwamba hawawezi kutengeneza filamu nzuri kama hawatakuwa na muda wa kutazama wenzao wanafanya nini kwani kupitia wenzao wanaweza kujifunza na kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa”,alisema.
“Labda pia niwaambie kwamba waledi kwenye kazi ya sanaa ni kitu muhimu sana inaweza kukupa maendelea makubwa kwa kuhakikisha mnaipenda na kuithamini",alisema.
Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo alisema sekta ya filamu ni ya kiuchumi kutoka Tanzania ni ya pili kwa idadi uzalishaji ukilinganisha na nchi ya Nigeria lakini ukija kwenye pato la taifa kidogo wanahitaji kuongeza nguvu.
Alisema bodi ya filamu imeweka mpango mahususi wa kuwajengea uwezo wadau wa filamu hapa nchini hususani kwenye maeneo ya kuboresha kazi zao ili ziwe kuwa na tija.
Aidha alisema hilo linatokana na baadhi ya wasanii hususani wanaochipukia kutokutambua namna ya kuweza kutengeneza kazi zao na kuweza kuzitangaza ili ziweze kuwa na manufaa makubwa kwao.
KAGAME ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI - EAC
Rais Kagame amechukuwa nafasi ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliyemaliza muda wake.
Akizungumza Ijumaa Februari Mosi, 2019 jioni baada ya kutangazwa kwake katika mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya hiyo unaofanyika jijini Arusha nchini Tanzania, Kagame amesema ataitumikia vyema jumuiya hiyo.
Friday, 1 February 2019
WAWILI WAFARIKI,WATANO HOI BAADA YA KUBUGIA DAWA ZA MITI SHAMBA
Watu wawili wamefariki dunia huku wengine watano wakilazwa hospitalini baada kunywa dawa za miti shamba mtaani Karen jijini Nairobi nchini Kenya.
Watu hao saba wanasemekana kunywa dawa hizo walipokuwa wakifanya kazi ya ujenzi wa jengo eneo la Kazuri kule Marula Alhamisi Januari 31,2019.
Waathiriwa walikimbiziwa hospitalini baada ya kulalamika kuhusu maumivu makali kwenye tumbo na kutapika.
Kulingana na taarifa za polisi, mmoja wa waathiriwa aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Karen na mwingine alifariki akiwa katika zahanati ya St. Odillas.
Waathiriwa wanasemekana kalalama kuhusu maumivu makali kwenye tumbo na kutapika wakati walipofikishwa hospitalini.
Manusura 5 walipelekwa katika hospitali ya St. Mary's ambapo wanapokea matibabu.
"Uchunguzi ulionyesha kuwa walikunywa dawa za miti shamba wakiwa kazini wakifanya ujenzi eneo la Kazuri, maafisa wa polisi walifika eneo la tukio na wakapata jagi iliyokuwa na matawi ya mmea wa Aloe Vera," taarifa ya polisi ilisoma.
Miili ya wawili hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha Umash huku maafisa wa polisi wakiendelea na uchunguzi kubaini aliyewapatia dawa hizo.
Via Tuko