Thursday, 6 October 2016
Wednesday, 5 October 2016
MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU MUCCOBS(MOCU) USHIRIKA UNIVERSITY-MOCU SECOND ROUND(BATCH 2) 2016/2017
MOCU: Second selection Applicants selected to Join various degree programmes 2016/2017
Second selection Applicants selected to Join various degree programmes 2016/2017
To see all names
MWAMUZI MECHI SIMBA,YANGA AFUNGIWA NA TFF MIAKA MIWILI,KADI NYEKUNDU YA MKUDE YAFUTWA
Dar Es Salaam,Tanzania.
MWAMUZI Martin Saanya aliyechezesha mechi ya watani wa
jadi, Simba na Yanga Oktoba 1, mwaka huu amefungiwa miaka miwili kwa
pamoja na Msaidizi wake, namba moja, Samuel Mpenzu.
Habari za ndani kutoka Bodi ya Ligi ya Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF),zimesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa leo katika
kikao cha Kamati ya Masaa 72 ya shirikisho hilo.
Na pamoja na kuwafungia waamuzi huo kwa makosa ya kutoa
maamuzi ya utata, pia Kamati imefuta Kadi nyekundu ya mchezaji Jonas
Mkude baada ya kubaini hakufanya kosa.
Maamuzi ya utata ya Saanya yalisababisha vurugu Uwanja
wa Taifa Jumamosi baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na
mshambuliaji Mrundi,Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara.