Tuesday, 2 August 2016
Monday, 1 August 2016
Rais Magufuli akamilisha ziara yake, atoa onyo kwa walimu
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe amekamilisha ziara ya
siku nne Singida, Tabora, Shinyanga na Geita ambapo amefanya mkutano wa
hadhara katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na
Buseresere mkoani Geita.
akizungumza
katika mkutano huo Rais Magufuli amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi
ya Mkoa hadi Kitongoji hapa nchini kufuatilia matumizi ya fedha
zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo
la kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Katika
agizo hilo Dkt. Magufuli amewaonya walimu ambao wameanza kufanya
udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi halisi
kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema Serikali
itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya hivyo.
>>>’Ninafahamu
mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo,
wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika
shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi
waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii ina
wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki tano, za
wanafunzi laki moja wagawane’
>>>’Napenda nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali’
Video: James Lembeli akizungumza kuhusu hatma yake kurudi CCM
Wakati jana Rais Magufuli akiwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga alimpa nafasi aliyekuwa Mbunge wa Kahama kwa tiketi ya CCM na baadae kuhamia CHADEMA, James Lembeli ili azungumze.
Lembeli
aliongea mambo kadhaa ikiwemo hatma yake kurudi CCM ambapo alisema yupo
tayari kurudi iwapo Rais Magufuli atakisafisha chama kwa
kuwashughulikia wanafiki na wala rushwa
Rais Magufuli Asema Hatagawa Chakula cha Bure Kwa Watakaopatwa na Janga la Njaa Bila Sababu za Msingi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema
serikali yake haitagawa chakula cha bure kwa wananchi wanaopatwa na
tatizo la njaa pasipo kuwa na sababu za msingi na badala yake amewataka
watanzania wajikite kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ikiwa ni pamoja
na kuzalisha chakula cha kutosha.
Rais
Magufuli amesema hayo jana tarehe 31 Julai, 2016 wakati akihutubia
mikutano ya hadhara na kuzungumza na wananchi waliosimamisha msafara
wake akiwa njiani kutoka Mkoani Tabora kuelekea Shinyanga na baadaye
Geita anakoendelea na ziara yake.
Pamoja
na kuwahimiza wananchi kuzalisha chakula cha kutosha ili kuondokana na
njaa Rais Magufuli alisema serikali yake itajikita kuhakikisha
inashughulikia tatizo la uhaba wa maji, ujenzi wa miundombinu hususani
barabara na reli, kuimarisha huduma za matibabu, elimu na kutengeneza
ajira.
Akiwa
Isaka Mkoani Shinyanga Rais Magufuli alisema serikali haitalipa fidia
kwa wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyobomoa nyumba zao
mwezi Machi mwaka 2015 na badala yake itajielekeza kutatua tatizo kubwa
la uhaba wa maji katika mji huo ambao una makutano ya reli ya kati ya
kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Rwanda.
Katika
Mji wa Kagongwa Rais Magufuli alipokea kilio cha wananchi dhidi ya
vitendo vya ujambazi na ametoa siku tano kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Shinyanga kuhakikisha watu wanaojihusisha na ujambazi wanakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mjini
Kahama, Dkt. Magufuli aliiagiza Wizara ya Nishati na Madini
kushirikiana na Mbunge wa Kahama Mhe. Jumanne Kishimba kukokotoa
mahesabu vizuri na kubaini kodi ambayo Serikali inastahili kulipwa baada
ya Mbunge huyo kudai kuna kiasi kikubwa cha kodi hakijakusanywa kama
ambavyo sheria inaelekeza.
Aidha,
Rais Magufuli alisema serikali itahakikisha wawekezaji wanaochimba
madini wanaacha kusafirisha mchanga wenye madini kwa lengo la kwenda
kuchakata nje ya nchi na badala yake ametaka uchakataji huo ufanyike
hapa hapa nchini.
Dkt.
Magufuli alizungumza na wananchi vijiji vya Segese na Bukoli na
kuwahakikishia kuwa Barabara ya Kahama, Segese, Kakola hadi Geita yenye
urefu wa kilometa 146 itajengwa kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi.
Mjini
Geita, Rais Magufuli alipokea kilio cha wananchi wanaodai kuwekewa zuio
la kutumia mawe yenye mabaki ya madini ya dhahabu (Magwangala) kwa
lengo la kusaga na kuchenjua ili kupata dhahabu, na ametoa wiki tatu kwa
Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathimini na kuwaruhusu
wachimbaji wadogo kutumia Magwangala.
Rais
Magufuli pia ameiagiza Bodi ya Pamba hapa nchini kuhamisha ofisi zake
zilizopo Jijini Dar es salaam na kuzileta katika Mikoa ya kanda ya ziwa
ambako uzalishaji wa zao la pamba unafanyika.
Dkt.
Magufuli amewaonya viongozi na watendaji wa bodi hiyo dhidi ya vitendo
vya usambazaji wa mbegu za pamba zisizoota na amesema ikitokea tena
watachukuliwa hatua.
Tarehe
01 Agosti, 2016 Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth
Magufuli anatarajia kukamilisha ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya
Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Geita
31 Julai, 2016
Sunday, 31 July 2016
Mkutano wa Rais Magufuli, Kahama: James Lembeli Atangaza kurejea CCM
Katika hali inayoshangaza wapenzi na mashabiki wengi wa CHADEMA ni pale
aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia CHADEMA ameonekana katika mkutano wa
CCM unaoendelea hapa mjini Kahama.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa hapa Kahama wanadai kiongozi huyo aliyejizolea umashuhuri mkubwa enzi za uongozi wake kwa sasa mambo yake yamekwenda mrama hivyo njia nyepesi ni yeye kutubu na kurejea nyumbani kwao waliko mababu zake
Wadadisi wa masuala ya kisiasa hapa Kahama wanadai kiongozi huyo aliyejizolea umashuhuri mkubwa enzi za uongozi wake kwa sasa mambo yake yamekwenda mrama hivyo njia nyepesi ni yeye kutubu na kurejea nyumbani kwao waliko mababu zake