Monday, 18 July 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULY TAREHE 18.7.2016


IMG_20160718_045027
IMG_20160718_045100
IMG_20160718_045124
IMG_20160718_045140
IMG_20160718_045158
IMG_20160718_045222
IMG_20160718_045247
IMG_20160718_045313
IMG_20160718_045329
IMG_20160718_045347
IMG_20160718_045405
IMG_20160718_045437
IMG_20160718_045506
IMG_20160718_045531
IMG_20160718_045553
IMG_20160718_045612
IMG_20160718_045628
IMG_20160718_045655
IMG_20160718_045716
IMG_20160718_045743
IMG_20160718_045759
IMG_20160718_045838
IMG_20160718_045901
IMG_20160718_045921
IMG_20160718_045940
IMG_20160718_050008
IMG_20160718_050058
IMG_20160718_050112
IMG_20160718_050149
Share:

Taarifa kamili kuhusu habari ya Rais Magufuli kumteua Jerry Murro kuwa msaidizi wa mawasiliano ya Rais Ikulu


Baada ya taarifa kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rais John Pombe Magufuli amemteua Jerry Murro ambaye alikuwa afisa habari wa Yanga kuwa msaidizi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, kurugenzi ya mawasiliano imekanusha habari hizo na kusema kuwa sio za kweli.

Barua iliyoandikwa kutoka Ikulu imesema ‘kuna taarifa zimesambazwa zikisema kuwa Rais Magufuli amemthibitisha Gerson Msigwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu huku msaidizi wake akiwa ni aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Murro, taarifa hizo sio za kweli na wananchi wazipuuze'
Share:

Sunday, 17 July 2016

Rais Magufuli kafanya uteuzi mwingine leo


July 17 2016 headline kutoka Ikulu Dar es salaam ni pamoja na hii Rais John Pombe Magufuli kumteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa makamu mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA), Rutasitara anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Nyamajeje Weggoro ambaye muda wake umemalizika.Pia Rais Magufuli amempandisha cheo kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Kedmon Mnubi kuwa kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP)
 
 
WhatsApp-Image-20160717



Share:

DOWNLOAD HAPA JOINING INSTRUCITIONZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MKOA WA SINGIDA

Image result for tamisemi 

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO

17 Jul, 2016
Share:

VIDEO:HILI NDIO JIJI LA PAUL MAKONDA- DAR ES SALAAM


Share:

HII NDIO SIRI YA SHULE YA KISIMIRI SEC KUONGOZA KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA 6 2016





MJADALA kuhusu ubora wa shule binafsi, kuchangia kuongoza katika matokeo ya mtihani wa mw

isho, ambao umekuwa ukijirudia kila mara wakati wa matangazo ya matokeo hayo, umebadilishwa mwelekeo na shule ya sekondari Kisimiri. Shule hiyo kati ya wanafunzi 63 waliohitimu kidato cha sita, wanafunzi 50 wamepata divisheni ya kwanza na wanafunzi 13 ndio waliopata divisheni ya pili.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa shule hiyo iliyoibuka kinara wa matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha sita, Mwalimu Emmanuel Kisongo, kabla ya kuelezea siri ya mafanikio ya shule hiyo, alisema kuwa akili na fedha ni vitu viwili tofauti.

Mwalimu Kisongo alisema pamoja na jamii na wanasiasa kutukana shule za kata, kwa kuzipa majina pamoja na walimu waliokuwa wakiziongoza; walimu na wanafunzi wa shule hiyo, waliazimia kufanya mapinduzi, ambapo alisema sasa yametimia kwa ada ya Sh 70,000 kwa mwaka, kupindua ada ya Sh milioni 10.

“Si mnajua tulipewa kila aina ya jina, mara shule ya kata na wengine wakatuita yeboyebo, sisi tuliamua kuibadilisha yetu kutoka shule ya kata kuwa shule maalumu, yaani walimu wetu ni maalumu na wanafunzi ni maalumu.

“Miundombinu yetu haijakaa sawa, tunakula maharage na hata baadhi ya wazazi wenye fedha, waliondoa watoto wao na kwa kiburi na dharau wakasema huku kuna mavumbi, lakini tukasema japo tunaletewa divisheni ya tatu, wengine wanakaribia divisheni ya nne, sisi tutatoa divisheni ya kwanza,” alisema Mwalimu Kisongo.

Mifumo imara Mwalimu Kisongo ambaye ni msomi wa Shahada ya Uzamili ya Menejimenti ya Elimu na Uongozi, alisema siri ya kwanza ya ufaulu wa shule hiyo, ilianzia katika kuimarisha idara na mifumo ya shule. Idara na mifumo iliyoimarishwa kwa mujibu wa Mwalimu Kisongo, ilihusu uchakataji wa majaribio yanayopaswa kutolewa kwa wanafunzi, mitihani na ukusanyaji wa ada.

“Katika tovuti ya shule ukifungua, kuna akaunti ya kila mwanafunzi ambayo ukiingia, unakuta matokeo na mahitaji ya kila mwanafunzi na hata mzazi anaweza kuingia, akakuta kila kitu na kama anadaiwa ada, inamuonesha...kwa hiyo sisi hatuandiki chochote kwenye makaratasi,” alisema Mwalimu Kisongo.

Mfumo huo pia unawajibisha walimu, ambapo alisema mwalimu asipotoa majaribio, alitoa mfano kama ni majaribio manne kwa muda walivyokubaliana, mfumo huo unamuonesha mwalimu husika.

Kwa mujibu wa Mwalimu Kisongo, walimu wote walipaswa kuwajaribu wanafunzi kwa kufuata viwango vya Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), ili kuhakikisha kuwa mwanafunzi anaiva kwa viwango hivyo.

Mbinu za uongozi Akizungumzia siri ya pili, Mwalimu Kisongo alisema walimu wote na wanafunzi walipandikizwa mbinu za uongozi, kiasi kwamba Mkuu wa Shule na hata walimu wasipokuwepo shuleni, Kaka Mkuu anatosha kuongoza shule.

Mwalimu huyo alitoa mfano wa mmoja wa wanafunzi waliomaliza shuleni hapo, Madaraka Amos ambaye alikuwa Kaka Mkuu, kwamba mara kwa mara aliongoza shule na kuna wakati alifikia hatua ya kuwa Mkuu wa Shule Msaidizi.

“Kuna wakati tulikuwa na walimu tisa, kati ya hao sita wakapewa kibali kwenda kusoma chuo kikuu, wakabaki watatu nao wakapewa kibali kwenda kusoma, Amos (anataja kampuni moja ya simu anakofanya kazi sasa), alikuwa Second Master,” alisema.

Katika kupandikiza mbinu za uongozi, Mwalimu Kisongo alisema aliwafundisha walimu na wanafunzi kwamba hakuna wajibu mdogo na hakuna serikali nyingine, isipokuwa yeye mwalimu na mwanafunzi, hivyo kila mwalimu na mwanafunzi alijiona kuwa ni sehemu ya uongozi na kila mmoja alijiona ana wajibu mkubwa.

“Kwa hiyo kila mmoja wetu alikuwa na kasi na shinikizo la ndani la kufanikiwa,” alisema na kuongeza hata Kaka Mkuu wa sasa, ‘anatumbua majipu’ kama Rais John Magufuli. Uzalendo Mwalimu Kisongo alisema pia alipandikiza uzalendo kwa wanafunzi hao na walimu kwa kuwaeleza hali halisi ya nchi yao, ili wajue kinachowakabili mbele yao.

“Nilipanda mafundisho ya Mwalimu Julius Nyerere (Baba wa Taifa), niliwaambia Mwalimu alisema kuwa hakuna mtu anayeweza kukulazimisha kupenda wengine, kuliko kujipenda wewe mwenyewe.

“Niliwaambia kuwa wewe (walimu na wanafunzi) na mimi tumepata elimu bora, hivyo tunatakiwa kuhudumia jamii ipate hali bora na huko ndio kujipenda,” alifafanua na kusema wanafunzi wanaotoka Kisimiri, wakiwekwa popote watafanikiwa.

Mwalimu Kisongo alisema walimu wa shule hiyo walifikia hatua wakashindwa kutenganisha mali binafsi na za shule, kwa kuwa walihakikisha hata dawati likivunjika, haliachwi liharibike bali linafanyiwa kazi mara moja.

Taaluma Katika mazingira hayo ambayo walimu wote wanasoma, akiwemo yeye Mwalimu Kisongo na hivyo shule katika baadhi ya nyakati kulazimika kuendeshwa na Kaka Mkuu, Mkuu huyo wa Shule alisema waliamua kumuona kila mmoja wao; mwalimu na mwanafunzi wote wanazo akili za kutosha.

“Walimu wote wanasoma, mimi nasoma na wanafunzi wanasoma, huku tuliko ni kijijini na chuo tunachosoma walimu kiko mjini, Kilometa 80 kutoka shuleni ...kila siku tunakimbizana na bodaboda, lakini Mungu akijalia baada ya muda tutakuwa na walimu wenye shahada za uzamili,” alisema.

Kutokana na ukosefu wa walimu na waliopo kuendelea na masomo, Mwalimu Kisongo alisema wanafunzi wa shule hiyo hawakujitenga kwa tofauti zao za dini, wala hawakuyumbishwa na tofauti hizo, ndio maana walifundishwa na walimu wa kukodi siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

“Jumatatu mpaka Alhamisi huwa tunajifunza tulichofundishwa Ijumaa mpaka Jumapili, topiki haisubiri mwalimu, wakati mwingine tunaendelea wenyewe, hivyo walimu wakija Ijumaa mpaka Jumapili, lazima awe amejipanga, maana ataulizwa maswali kwa kuwa wanafunzi wanakuwa wameshapitia kinachofundishwa,” alisema.

Mpaka sasa kwa mujibu wa Mwalimu Kisongo, mbali na changamoto ya miundombinu, shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa hesabu na fizikia, ingawa hali ya walimu kwa sasa ni nzuri kuliko shule ilivyoanza.

Mwalimu Kisongo alimpongeza Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kwa kutembelea shule hiyo na kuona wanafunzi wanavyojifunza, ambapo alisema walianza kufanya vizuri wakati waziri huyo alipokuwa Katibu Mtendaji wa Necta.

Tandahimba Naye Mkuu wa shule ya sekondari Tandahimba, mkoani Mtwara ambayo imekuwa ya kumi kitaifa, Mwalimu Mathew Andilile, alielezea mazingira ya shule hiyo kuwa ni ya kawaida, yenye changamoto nyingi, lakini wanashukuru Mungu ndani ya changamoto hizo, wamefanikiwa. Shule hiyo imetoa wanafunzi 49 waliomaliza kidato cha sita, kati ya hao 19 ni divisheni ya kwanza, na waliobakia divisheni ya pili.

Mwalimu Andilile alisema hata wanafunzi wanaopokea si wa vipaji maalumu, maana tangu wameanza kufundisha wanafunzi wa kidato cha tano na sita, hawajawahi kupokea mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye divisheni ya kwanza na wanafunzi wengi ambao wamekuwa wakiwapokea, ni wenye divisheni ya tatu.

Alisema mazingira ya kuishi ya wanafunzi hao ni ya kawaida, asubuhi wanakunywa chai, mchana ugali wa maharage na jioni ugali wa maharage isipokuwa Jumatato, ambapo hula nyama mchana na jioni na Alhamisi na Jumapili, ambapo hupata wali maharagwe mchana na usiku.

Katika moja ya changamoto za shule hiyo, Mwalimu Andilile alisema ingawa gharama za kumtunza mwanafunzi ni Sh 1,500 kwa siku; kuna wakati halmashauri ilipungukiwa fedha, Julai na Agosti mwaka jana, ambapo wanafunzi hao walilazimika kuamkia uji wa chumvi asubuhi na kushindia na kulalia ugali maharage kila siku.

Aliwataka wazazi kujenga ushirikiano na walimu akisema baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamefaulu, hawakuwahi kufika katika shule hiyo, wala hawafahamu iliko wala mazingira yake, ila watakuwa tu wamesikia watoto wao wamefaulu.

Alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo, kuwa ni pamoja na ukosefu wa madarasa, ambapo kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano, wanasomea katika bwalo la chakula na kusababisha wanafunzi kila mmoja kutafuta eneo la kulia chakula.

Mwalimu Andilile alisema kufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo, ambayo imewahi kuwa na matokeo mabaya katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne, kumetokana na kuzingatia walichofundishwa darasani na kujitafutia wenyewe ya nyongeza nje ya walichopewa darasani. Changamoto zingine alisema ni kutokuwepo kwa maktaba katika shule hiyo na upungufu wa vitabu.
Share:

MPYA:KUNA AJALI IMETOKEA MIKUMI MDA HUU,NIMEKUWEKEA PICHA HAPA

 Bado tunafatilia chanzo kamili,ila angalia picha hapo chini;




Share:

USHAURI KWA WANAFUNZI WOTE WA FORM 6 AMBAO HAWANA CUTT OF POINTS ZA CHUO KIKUU 2016/2017

Ministry of Livestock and Fisheries Development
Habari yako?

Ntumaini u mzima wa afya ,mimi pia ni mzima wa afya na nianendelea kukutafutia kitu roho inahitaji na kuwaza kila wakati.

Kutokana na kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita juzi na kuwa ndivyo sivyo kwa wanafunzi wengi kwa kukosa sifa za kwenda chuo kikuu,kwa kukosa minimum points za kwenda chuo kikuu ambazo ni pts 4 kwenye masomo yako ya combination.

Nimeamua kuwapa ushauri nini cha kufanya kwa mda huu kabla ya JULY 30 MWEZI HUU

 Je,ungependa kuwa afisa uvuvi na samaki?

Basi wizara ya mifugo bado inapokea maombi kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya samaki na uvuvi mbalimbali hapa Tanzania.

Kama umesoma SAYANSI ADVANCE,TAFADHALI OMBA COURSE HIZI KW PIA NI MARKETABLE.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI 

Maombi ya kozi hizi yalikuwa yanapokelewa kwa njia mbili 
1.NACTE
2.KUTUMA FORM CHUONI DIRECT

kwa kuwa nacte kwa sasa wamefunga kupokea maombi nakushauri ,na hawa jamaa bado wanapokea maombi hadi tarehe 30 july 2016.

basi ninakushauri download form then,lipia gharama ya apps ambayo ni tshs 20000 ,then watumie chuo unachotaka kuomba.

Pia ada zao ni nafuu sana,kwani ni vyuo vya serikali.

 KUSOMA TANGAZO LA ADMISSION SOMA HAPO CHINI

>>>>>>>>>BONYEZA HAPA KUONA TANGAZO

KUSOMA KUHUSU JINSI YA KUAPPLY NA VIGEZO

>>>>>>>> BONYEZA HAPA

MASWAYETU BLOG TUNAKUPENDA 


NB:KWA KOZI ZA AFYA NA UALIMU NK,NITAKUTAARIFU NACTE WAKIFUNGUA APPLICATION TENA. 

PIA:  KAMA UMEPATA D &E =3 pts CHUO KIKUU HUENDI,HAUNA SIFA  
Share:

AUDIO | Nillah – Abee | Download

Share:

VIDEO | Darassa – Too Much | Watch/Download


Share:

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016,UALIMU DSEE 2016,UALIMU GATCE 2016

Share:

Basata Wafungia Wimbo Wa ‘Pale Kati Patamu’ Wa Ney Wa Mitego.


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
 
Msanii huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo.
Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. 
Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.

Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo
 
• BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile.
• Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
 
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao.
SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI.
Share:

Magazeti ya Leo Jumapili Julai tarehe 17.7.2016



























































Share:

Saturday, 16 July 2016

TAARIFA KWA WANAFUNZI WOTE WA SUA AMBAO HAWAJAHAKIKIWA NA BODI YA MIKOPO 2016/2017




SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE
OFISI YA MAKAMU WA MAKAMU MKUU WA CHUO TAALUMA (SUA) 14 JULAI,  2016

UHAKIKI KWA WANAFUNZI WA SUA WANAOPATA UFADHILI TOKA
BODI YA MKOPO KWA WANAFUNZI WOTE:
NAPENDA KUWATAARIFU KUWA UHAKIKI ULIOFANYIKA SUA UMEONESHA KUNA WANUFAIKA 388 TOKA SUA KATIKA MWAKA WA MASOMO 2015/16 AMBAO HAWAJAJITOKEZA KUHAKIKIWA KATIKA CHUO CHETU.
HIVYO WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI PAMOJA NA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ZINAWATAKA WANAFUNZI WOTE AMBAO HAWAKUJITOKEZA KUHAKIKIWA WAJITOKEZE KUHAKIKIWA TAREHE 18 JULAI 2016 BILA KUKOSA. UHAKIKI UTAANZA SAA 2:00 ASUBUHI MPAKA SAA 10:00 JIONI. UHAKIKI HUU UTAFANYIKA UKUMBI WA BARAZA LA CHUO ULIOPO  JENGO LA UTAWALA.
WANAFUNZI WATATAKIWA KUJA NA KITAMBULISHO CHA  CHUO NA KITAMBULISHO KINGINE KINACHOTAMBULIKA KITAIFA NA CHENYE PICHA YAKE. KUTOKUTOKEA KATIKA ZOEZI HILI LA UHAKIKI KUTASABABISHA MWANAFUNZI HUSIKA KUFUTIWA UFADHILI WA MKOPO TOKA SERIKALINI.




Prof. P.R. Gillah
NAIBU MAKAMU WA MKUU WA CHUO (TAALUMA)
Nakala kwa:      Mshauri wa Wanafunzi                   Rais wa Wanafunzi, SUA
                         Wawakilishi wa Madarasa Yote
Share:

TAMKO LA KAMATI YA MAWAZIRI WA MIKOPO WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TANZANIA KUHUSU UCHELEWESHWAJI WA MALIPO YA FEDHA ZA KUJIKIMU KATIKA KIPINDI CHA MAFUNZO KWA VITENDO MWAKA 2016/2017

TAMKO LA KAMATI YA MAWAZIRI WA MIKOPO WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TANZANIA KUHUSU UCHELEWESHWAJI WA MALIPO YA FEDHA ZA KUJIKIMU KATIKA KIPINDI CHA MAFUNZO KWA VITENDO MWAKA 2016/2017
Ndugu waandishi wa habari tulio mbele yenu ni kamati ya mawaziri wa mikopo ya serikali za wanafunzi wa Elimu ya juu nchini Tanzania na wajumbe wa kamati hii ni mawaziri wa mikopo kutoka vyuo na Taasisi za Elimu ya juu zote nchini.Kamati hii inaundwa na mawaziri,Manaibu waziri na makatibu wa wizara ya mikopo kutoka vyuo vyote nchini.
Kamati ya mawaziri ya mikopo ilianzishwa Rasmi mnamo tarehe 11/10/2015 kwa madhumuni na malengo ya kulinda na kutetea pia kusimamia haki na maslahi ya wanafunzi wa Taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu nchini Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania wanatarajia kuingia katika kipindi cha mafunzo kwa vitendo kinachotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwenzi huu ambapo wanafunzi wa Elimu ya juu watatakiwa kufika katika vituo vyao vya kazi vilivyo sambaa nchi nzima tarehe 25/07/2016 ili kuendelea kupata mafunzo kwa vitendo huku wakihudumia umma wa watanzania katika kada mbalimbali kama madaktari,waalimu,maafisa ardhi,waandisi na wachumi.

Ndugu waandishi nwa habari kinachosikitisha ni kwamba mpaka sasa hakuna fedha zozote zilizotolewa na BODI YA MIKOPO wala mchakato unaoendelea kupelekea utolewaji wa fedha hizo. licha ya ukweli kwamba Wanafunzi wengi ni wafadhiliwa wa bodi hiyo, hivyo fedha za nauli pamoja na fedha za kujikimu kwa malazi na chakula wawapo katika mafunzo kwa vitendo zinapaswa kutolewa na bodi hiyo ili kufanikisha azma hii njema ya serikali ya kutoa huduma kwa jamii.

Ndugu waandishi wa habari ni ukweli usio kificho kuwa BODI YA MIKOPO kwa kushirikiana na TCU wanazo taarifa kuwa wanafunzi hawa wanapaswa kuondoka vyuoni mapema tarehe 23/07/2016 lakini mpaka hivi sasa hawaoneshi dalili yoyote ama nia ya kutoa fedha hizo kwa muda muafaka huku wakijua fika kuwa mchakato wa utolewaji wa fedha hizo lazima upitie hatua ya wanafunzi kusaini ili kuthibitisha utayali wa kupokea fedha hizo . Mpaka sasa hivi tukiwa tumebakiwa na takribani siku tano kabla ya kufunga chuo hakuna hata karatasi za kusaini zilizotumwa vyuoni ili kukamilisha zoezi hilo.

Ndugu waandishi wa habari licha ya juhudi nzito zilizofanywa na mawaziri wa mikopo kiutoka vyuo mbalimbali tukishirikiana na menejimenti za vyuo kufanya mawasiliano na hata kukutana ana kwa ana na watendaji wa BODI YA MIKOPO, na hata WIZARA YA ELIMU lakini bado mpaka hivi sasa hakuna jibu muafaka linalotolewa ama lililokwisha kutolewa juu ya upatikanaji na utolewaji wa pesa za kujikimu za wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi hiki cha mafunzo kwa vitendo.

Ndugu waandishi wa habari imekuwa ni utamaduni sasa kwa BODI YA MIKOPPO kutotoa fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa Elimu ya juu nchini kwa wakati mpaka pale inapotokea migomo na maandamano ya wanafunzi jambo ambalo ni kinyume cha mkataba tuliosaini baina yetu na BODI YA MIKOPO.

Ndugu waandishi wa habari ikumbukwe wazi kuwa pesa zinazotolewa na BODINYA MIKOPO kwa wanafunzi wa Elimu ya juu si Hisani bali ni mkopo uliochini ya mkataba na mwanafunzi hulazimika kulipa fedha hizo kwa wakati huku kukiwa na riba ya asilimia sita (6%) kwa mwaka ambayo mwnanafunzi hukatwa mara tuu baada ya kuajiriwa.

AZIMA YA KAMATI

Ndugu waandishi wa habari kutokana na hali hii kamati ya mawaziri wa mikopo ya Elimu ya juu nchini Tanzania tunaitaka serikali kupitia wizara ya Elimu,sayansi,tekinolojia na mafunzo ya ufundi iisimamie BODI YA MIKOPO kutekeleza wajibu wake na kutufikishia fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo mapema wiki kesho ili mwanafunzi wanaonufaika na bodi hiyo waweze kusafiri kutoka vyuoni mpaka katika vyuo vyao kutekeleza wajibu wao kwa Taifa hili.

Ndugu waandishi wa habari kamati hii inatoa muda wa masaa sabini na mbili (72) kwa BODI YA MIKOPO kufikisha fedha katika vyuo ambavyo mpaka sasa hawajapata fedha ya kujikimu awamu ya nne na pia kamati hii inaitaka BODI YA MIKOPO kutoa fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo ndani ya muda huo.

Ndugu waandishi wa habari kama BODI YA MIKOPO ikishindwa kutekeleza wajibu wake ndani ya masaa sabini na mbili (72) tuliyoyatoa kamati ya mawaziri wa mikopo tutakuwa tayali kuchukua hatua yeyote dhidi ya BODI YA MIKOPO na tutajitokeza mbele ya vyombo vya habari siku ya Jumatano kutangaza kwa umma hatua tutakayoadhimia kuichukua.
IMETOLEWA; TAREHE 16/07/2016


SHITINDI VENANCE MWENYEKITI KAMATI TAIFA.
0759704444
NTILE JOEL
KATIBU KAMATI TAIFA 0754255744
Share:

TAARIFA :APPLICATION ZA MASOMO VYUO VIKUU 2016/2017 KUANZA RASMI TAREHE 20 JULY 2016


Habari yako kazi yangu ni kukutafutia kila kinapojiri kipya.

KWA WANAFUNZI MNAOSUBIRIA KUOMBA VYUO VIKUU KUPITIA TCU,NI KWAMBA WATAFUNGUA RASMI TAREHE 20 JULY 2016.

TANGAZO LINASOMEKA HIVI;

"CAS will be opened for applicants with form six qualifications on 20th July 2016. Thank you."

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger