Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza
kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.
Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme
Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama
za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.
Bei mpya kwa
watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni sh.292 toka
298 ya zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka sh. 200 ya
hapo awali.
Bei mpya kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157
toka sh. 159. Wanaonunua kwa wingi (bulk) ni sh. 152 toka sh. 156 ya
hapo awali
Transferred Students from St. Joseph University to The University of Dodoma
IMPORTANT ANNOUNCEMENT TRANSFERRED STUDENTS FROM ST. JOSEPH UNIVERSITY TO THE UNIVERSITY OF DODOMA
This is to inform all students transferred from St. Joseph University
in Tanzania to The University of Dodoma that, they are required to
report to their respective Colleges (College of Education and College of
Natural and Mathematical Sciences) at the University of Dodoma on
Saturday 9th April 2016. effectively from 8.00am to 6.00pm.
All students are required to pay tuition fees and direct costs for
academic year 2015/2016. Students who will fail to comply with this
notice will not be allowed to join the university. Payment must be made
before students reporting to the University as follows:
Kondakta wa daladala, Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala
Ujiji, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli kwa maneno.
Seif
alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana mchana na kusomewa shtaka
hilo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kenneth Sekwao.
Mshtakiwa
huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa alisema kuwa
dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini
wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambaye atasaini hati
ya dhamana ya Sh2 milioni.
Licha ya dhamana yake hiyo kuwa wazi,
mshtakiwa huyo alishindwa kukamilisha masharti hayo kwani baada ya
kusomewa mashtaka alipoulizwa kama alikuwa na wadhamini alishindwa
kuwapata.
Akimsomea shtaka linalomkabili, Wakili Sekwao alisema
kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya
Soweto, Makumbusho wilayani Kinondoni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (a)
na kifungu cha 35 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.
Wakili Sekwao
alisema akiwa katika baa hiyo, mshtakiwa alitishia kumuua Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa maneno kwa njia ya
kujitoa mhanga.
“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli,
mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alisema
Wakili Sekwao akimnukuu mshtakiwa huyo.
Hata hivyo, Wakili
Sekwao alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na akaomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.
HATIMAYE wakuu wa Mikoa yote nchini
wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe ripoti
ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika.
Wakuu hao wa mikoa wapya wamewasilisha
ripoti za watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi,Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Georgy Simbachawene ili
kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi waliohusika katika kashfa
hizo,
Mkoa wa Dar Es Salaam.
Akiwasilisha ripoti ya watumishi
hewa.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mkoa
wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali
wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa
wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.
“Katika mkoa huu tumepata watumioshi
hewa 73,ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwanini unakuwa na watumishi
hewa wachache,nakata kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa
kina”amesema Makonda .
Mkoa wa Arusha.
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Arusha
,Daudi Felix Ntibenda amesema katika mkoa huo umegundurika kuwepo na
watumishi hewa 270 ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya
Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja,
Mkoa wa Dodoma.
Pia Mkuu wa Dodoma Jordan Lugimbana
amesema katika mkoa wake wamegundua kwenye mkoa huo kuna watumishi hewa
101 ambao amedai wameisabishia hasara serikali Milioni 287.3 kwa kipindi
cha miezi sita.
Mkoa wa Iringa.
Mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema
katika mkoa wake wamegundua kuwa kuna watumishi hewa 15 ambapo
amemweleza Waziri Simbachawene kuwa licha hao kuna watumishi 145 ambao
hajaonana nao huku akidai kuwa akimaliza kuonana nao huwenda idadi ya
watumishi hewa ikaongezeka.
Mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenelal
Mstaafu Salum Kijuu amesema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi
hewa 14 ambao wamesababisha upotevu wa pesa za serikali Milioni 49.1
Mkoa wa Katavi,
Pia Mkuu wa mkoa huu, Jeneral Raphael
Muhuga amesema mkuo huo umegundurika kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao
wameitia hasara serikali Milioni 20.7.
Mkoa wa Kigoma.
Pia Mkoa wa Mkuo huyo, Bregedia Jenaral
Mstaafu Emmanuel Maganga amesema katika mkuo huo wamebaini kuwepo
watumishi hewa 171 ambao wameitia hasara serikali milioni 114.6.
Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa huo,Merck Sadick amesema
wamebaini mkuo wake umegundurika kuwepo na watumishi hewa 111 ambao
wamekuisababishia hasara serikali hasara ya milini 281.4.
Mkoa wa Lindi
Kwa Upande wa Mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi amesema mkoa wake unawatumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali milini 36.2.
Mkoa wa Manyara.
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa huo,Joel
Bendera, amesema mkuo umekuwa na watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara
serikali Milioni milioni 313.9.
Mkoa wa Mara.
Kuhusu Mkuoa wa Mara,Mkuu wa mkoa
huo,Magesa Mulongo amesema katika mkoa wake wamebaini kuna watumishi
hewa 94 ambao wameitia hasara serikali milioni 121.
Mkuo wa Mbeya.
Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Mkuo
huo,Amos Makalla amesema katika mkoa wake kumekuwa na watumishi hewa 98
ambao pia wameitia hasara serikali Milioni 459 .6.
Mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo mkuu wa mkoa huo,Dkt Steven
Kebwe,ambapo amesema mkoa wake umegundurika kuwepo na watumishi hewa
122 ambao wameitia hasara serikali milioni 450.7.
Mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa mkoa huo,Halima Dendegu amesema
mkoa wake ubainikika kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku watumishi
wengine 285 uchunguzi ukiendelea,ambapo watumishi hao 17 wameitia hasara
serikali milioni 216.5.
Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa John Mongella amesema mkoa wake umengundurika kuwepo kwa watumishi hewa 334.
Mkoa wa Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa NJombe,Dkt Rehema
Nchimbi amesema mkoa wake umekuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amedai
wamekuwa wakiitia hasara serikali Milioni 20.1.
Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa huyo,Mhandisi Evarist
Ndikilo amesema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku hakishindwa
kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.
Mkua wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa huo,Kamishna Mstaafu Zerote
Steven amesema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa, 18 na wametia
hasara serikali milioni 55.6.
Mkuo wa Ruvuma,
Mkuu wa Mkoa huo,Thabiti Mwambungu amesema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali milioni 58.4.
Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa huo,Antony Mataka amesema mkoa huo umegundurika watumishi hewa 62 wameitia hasara serikali ya Milioni 320.9.
Mkoa wa Singida,
Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew
Mtigumwe amesema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake,231 nakueleza
kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.
Mkoa wa Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
ameanisha kuwa katika mkoa wake watumishi hewa 48 ambapo wanaitia hasara
Serikali Milioni 118.7.
Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela
amesema kuwa watumishi hewa katika mkoa wake ni 104 ambapo amesema kuwa
tathimini ya kuhakiki bado inaendelea.
Hata hivyo katika mkoa wa Shinyanga
imekuwa tofautina mikoa mingine ambapo hadi sasa hakuna watumishi hewa
kutokana na mikakati iliyowekwa na kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 na
mkuu wa mkoa aliyepita.