Thursday, 31 March 2016

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MARCH TAREHE 31/3/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Magazeti Ya Leo Alhamisi ya March 31, 2016
























Share:

Wednesday, 30 March 2016

DOWNLOAD YAMOTO BAND - NIGANDE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

New AUDIO | YAMOTO BAND - NIGANDE | Download

DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/bhwtk4ve0kjk/YAMOTO_BAND_-_NIGANDE.mp3?d=1
Share:

HAYA HAPA MAJINA NA IDADI KAMILI YA WATUMISHI HEWA MIKOA YOTE TANZANIA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

HATIMAYE wakuu wa Mikoa yote nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika.

Wakuu hao wa mikoa wapya wamewasilisha ripoti za watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Georgy Simbachawene ili kuchukuliwa hatua za kisheria  kwa watumishi waliohusika katika kashfa hizo,

 Mkoa wa Dar Es Salaam.

Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mkoa wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.

“Katika mkoa huu tumepata watumioshi hewa 73,ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwanini unakuwa na watumishi hewa wachache,nakata kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa kina”amesema Makonda .

Mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda amesema katika mkoa huo umegundurika kuwepo na watumishi hewa 270 ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja,

Mkoa wa  Dodoma.

Pia Mkuu wa Dodoma Jordan Lugimbana amesema katika mkoa wake wamegundua kwenye mkoa huo kuna watumishi hewa 101 ambao amedai wameisabishia hasara serikali Milioni 287.3 kwa kipindi cha miezi sita.

Mkoa wa Iringa.

Mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema katika mkoa wake wamegundua kuwa kuna watumishi hewa 15 ambapo amemweleza Waziri Simbachawene kuwa licha hao kuna watumishi  145 ambao hajaonana nao huku akidai kuwa akimaliza kuonana nao huwenda idadi ya watumishi hewa ikaongezeka.

Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenelal Mstaafu Salum Kijuu amesema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa  14 ambao wamesababisha upotevu wa pesa za serikali Milioni 49.1

Mkoa wa Katavi,

Pia Mkuu wa mkoa huu, Jeneral Raphael Muhuga amesema mkuo huo umegundurika kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao wameitia hasara serikali Milioni 20.7.

Mkoa wa Kigoma.

 Pia Mkoa wa Mkuo huyo, Bregedia Jenaral Mstaafu Emmanuel Maganga amesema katika mkuo huo wamebaini kuwepo watumishi hewa 171 ambao wameitia hasara serikali milioni 114.6.

Mkoa wa Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa huo,Merck Sadick amesema wamebaini mkuo wake umegundurika kuwepo na watumishi hewa 111 ambao wamekuisababishia hasara serikali hasara  ya milini 281.4.

Mkoa  wa Lindi

Kwa Upande wa Mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi amesema mkoa wake unawatumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali milini 36.2.

Mkoa wa Manyara.

Kwa Upande wake  mkuu wa mkoa huo,Joel Bendera, amesema mkuo umekuwa na watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara serikali Milioni milioni 313.9.

Mkoa wa  Mara.

Kuhusu Mkuoa wa Mara,Mkuu wa mkoa huo,Magesa Mulongo amesema katika mkoa wake wamebaini kuna watumishi hewa 94 ambao wameitia hasara serikali  milioni 121.

Mkuo wa Mbeya.

Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Mkuo huo,Amos Makalla amesema katika mkoa wake kumekuwa na watumishi hewa 98 ambao pia wameitia hasara serikali Milioni 459 .6.

Mkoa wa Morogoro.

Hata hivyo mkuu wa mkoa huo,Dkt Steven Kebwe,ambapo amesema mkoa wake umegundurika kuwepo na watumishi  hewa 122 ambao wameitia hasara serikali milioni 450.7.

Mkoa wa Mtwara.

Mkuu wa mkoa huo,Halima Dendegu amesema mkoa wake ubainikika kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea,ambapo watumishi hao 17 wameitia hasara serikali  milioni 216.5.

Mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa John Mongella amesema mkoa wake umengundurika kuwepo kwa watumishi hewa 334.

Mkoa wa Njombe.

Mkuu wa Mkoa wa NJombe,Dkt Rehema Nchimbi amesema mkoa wake umekuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amedai wamekuwa wakiitia hasara serikali Milioni 20.1.

Mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Mkoa huyo,Mhandisi Evarist Ndikilo amesema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku hakishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.

Mkua wa Rukwa.

Mkuu wa mkoa huo,Kamishna Mstaafu Zerote Steven amesema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa, 18 na wametia hasara serikali milioni 55.6.

Mkuo wa Ruvuma,

Mkuu wa Mkoa huo,Thabiti Mwambungu amesema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali milioni 58.4.

Mkoa wa Simiyu.

Mkuu wa Mkoa huo,Antony Mataka amesema mkoa huo umegundurika watumishi hewa  62 wameitia hasara serikali ya Milioni 320.9.

Mkoa wa Singida,

Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew Mtigumwe amesema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake,231 nakueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.

Mkoa wa Tabora

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameanisha kuwa katika mkoa wake watumishi hewa 48 ambapo wanaitia hasara Serikali Milioni 118.7.

Mkoa wa Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela amesema kuwa watumishi hewa katika mkoa wake ni 104 ambapo amesema kuwa tathimini ya kuhakiki bado inaendelea.

Hata hivyo katika mkoa wa Shinyanga imekuwa tofautina mikoa mingine ambapo hadi sasa hakuna watumishi hewa kutokana na mikakati iliyowekwa na kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 na mkuu wa mkoa aliyepita.

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MARCH 30 2016


Share:

Tuesday, 29 March 2016

Mpya Kuhusu Ajira za Walimu na Nyinginezo...Wenye Vyeti Zaidi ya Kimoja Kutopangiwa Kituo cha Kazi Serikalini.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

KUNA TAARIFA ZINAENEA KWA KASI MITANDAONI KUHUSU SERIKALI KUTO KUWAPOKEA WASOMI WENYE CHETI ZAIDI YA KIMOJA KATIKA AJIRA..UJUMBE WENYEWE UNAMUHUSISHA WAZIRI SIMBACHAWENE NA UKISOMEKA HIVI:-

Waziri Simbachawene ametoa tamko la serikali kuwa , Serikali ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania haiko tayari kuajiri wasomi wenye vyeti vya baraza la mitihani kuanzia vyeti viwili na kuendelea,watakaopata ajira yoyote ile ya moja kwa moja serikalini ni wasomi wenye cheti kimoja tu. Wale waliosoma kwa kuunga unga, mara kutafuta credit, mara kurudia mitihani watafute ajira kwa mashirika binafsi.Serikali inataka kuwaajiri wasomi wenye cheti kimoja tu waliosoma moja kwa moja. System hii itaanza kwenye ajira za walimu za mwaka huu 2016 zinazoenda kutangazwa mda si mrefu mwezi wa nne mwanzoni. Simbachawene ameyasema hayo akiwa na waandishi wa habari jijini Dar leo majira ya asubuhi ili kuwajuza watanzania kuwa ni tamko la serikali.
Rai kwa wenye vyeti vingi, mtakua mnaomba ajira kivyenu serikalini au kwa mashirika binafsi na si kuajiliwa moja kwa moja kutoka serikali kama ilivyokua awali.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.
Imetolewa na Afsa mawasiliano, wa Tamisemi.

Ndg.Elnest kimash
Dar es salaam.
Share:

Rais Magufuli Akabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais John Magufuli, ambaye amejipa kazi ya “kutumbua majipu”, sasa anaweza kufanya kazi yake vizuri zaidi baada ya kukabidhiwa ripoti tano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambazo anaweza kuzitumia kama kitendea kazi.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli na Serikali yake amekuwa akifanya kazi ya kuibua uozo kwenye taasisi za Serikali, kusimamisha na kutengua uteuzi wa watumishi wa umma wanaojihusisha na ufisadi na wakati fulani amekuwa akiitaja ripoti iliyopita ya CAG kuwa ndiyo iliyoanika uozo anaofanyia kazi.

Jana, “mtumbua majipu” huyo alikabidhiwa ripoti ya kwanza ya CAG tangu aapishwe kuwa Rais Novemba 5 mwaka jana na sasa ana kitendea kazi rasmi cha kufanyia kazi.

CAG Mussa Assad alimkabidhi Rais Magufuli taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba inayomtaka akabidhi ripoti hizo kwa Rais kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, kaimu mkurugenzi wa mawasiliano – Ikulu, Rais Magufuli, ambaye aliwaomba wabunge kumpa ushirikiano katika kutekeleza kazi za wananchi wakati akizindua Bunge Novemba 20, atazikabidhi ripoti hizo kwenye chombo hicho ndani ya siku saba za mwanzo za Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja utakaofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 19.

“Rais Magufuli amempongeza CAG na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi. Ameahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake,” inasema taarifa hiyo. 
Share:

Vigogo Wawili Maliasili Waliotoa Vibali vya Kusafirisha Tumbili Watiwa Mbaroni

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kikosi kazi maalumu cha kuchunguza makosa makubwa ya kihalifu kimewatia mbaroni vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wakihusishwa na utoaji wa kibali cha kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Idara ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Dk Charles Mulokozi na ofisa mfawidhi wa kituo cha uwindaji wa kitalii, utalii wa picha na Sites cha jijini Arusha, Nyangabo Musika.

Kikosi hicho kinaundwa na wachunguzi kutoka Polisi, Idara ya Uhamiaji, Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kikosi cha kupambana na ujangili nchini na Takukuru.

Wakati Dk Mulokozi anakamatwa, tayari alikuwa amesimamishwa kazi kwa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa kutoa kibali wakati Serikali ilishazuia.

Vyanzo mbalimbali vimesema jana kuwa Dk Mulokozi alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana alisafirishwa chini ya ulinzi kwenda kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

“Hivi tunavyozungumza, Dk Mulokozi yuko njiani anapelekwa Kia chini ya ulinzi mkali wa polisi.Nyangabo yeye tayari yuko mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama pale Kia,” kilidokeza chanzo chetu cha uhakika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alipoulizwa jana hakukanusha wala kukiri kuwa na taarifa za kukamatwa vigogo hao, lakini alisema atakuwa na mamlaka ya kuliongelea wakiingia mkoani kwake.

“Bado sijapewa hizo taarifa, lakini hata kama ningezijua nisingeweza kuzungumzia tukio la kukamatwa kwao lililofanyika mkoa mwingine. Nikikabidhiwa ndiyo naweza kusema chochote,” alisema Kamanda huyo. 
Hata hivyo, Waziri Maghembe alithibitisha kukamatwa kwa vigogo hao, akisema katika tukio hilo yeyote aliyetia mkono wake lazima akamatwe na kushitakiwa.

“Ni kweli Dk Mulokozi amekamatwa na siyo yeye tu kuna ofisa mwingine pale ofisi yetu ya Arusha naye tumemkamata. Hatuna mchezo katika suala hili,” alisisitiza.

Profesa Maghembe alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa raia wa Uholanzi waliokamatwa na polisi hawakuwa na vibali halali vya kufanya biashara ya kusafirisha wanyama hai kwenda nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hawa Waholanzi walikuwa na tourist visa (waliingia kama watalii). Halafu Watanzania waelewe mtu hawezi kupata kibali cha kusafirisha mnyama hai kabla ya kumkamata, kuhesabiwa, akakaguliwa na kupata vibali stahiki,” alisisitiza.

Raia hao wa kigeni ambao ni ndugu wa familia moja, Artem Alik Vardanyian (52) ni mkurugenzi wa mgahawa huko Uholanzi na Eduard Alik Vardanyian (44), meneja wa hoteli huko huko Uholanzi.

Hata hivyo, vyanzo vingine vimedai  kuwa pamoja na kuwapo kwa vibali hivyo, lakini hapakuwapo na “release order” inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kama sheria inavyoelekeza.

Chanzo hicho kilidai wanyama hao walikuwa wasafirishwe kwa kutumia ndege ya mizigo ya kukodi ambayo ilitokea Afrika Kusini na ilikuwa iwapeleke wanyama hao Albania kupitia Nairobi nchini Kenya na Nigeria.

“Hao marubani wa hiyo ndege waliitwa pale Polisi (Kia), wakaandikisha maelezo yao kuwa walikuja kuchukua wanyama hao na wakaambiwa wao waondoke tu hakuna mnyama anaondoka,” alidokeza ofisa mmoja katika uwanja wa Kia.
Share:

Dk Shein amteua Balozi Seif Ali Idd Kuwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa visiwa hivyo.

Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein amemteua Balozi Idd ambaye alikuwa na wadhifa huo hata kipindi kilichopita.

Uteuzi wa Balozi Idd aliyezaliwa Februari 23, mwaka 1942, ulianza jana ikiwa ni siku nne tangu kuapishwa kwa Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Balozi Idd anakuwa mtu wa pili kuteuliwa na Dk Shein baada ya kuteuliwa kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said mwishoni mwa wiki.

Dk Shein sasa atakuwa na wakati mgumu wa ama kumteua au kutomteua Makamu wa Kwanza wa Rais ili kukidhi matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani hakuna chama cha upinzani kilichokidhi vigezo vya kushirikishwa katika kuunda Serikali.
Share:

Picha na WEMA SEPETU akiwa katika Instagram Party Mwanza

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Usiku wa tarehe 27, ulipambwa na Show ya Instagram Party kwa upande wa Mwanza 88.1, mastaa kadhaa wa Tanzania walikuwepo kunogesha Party kutoka Bongo movie Wema Sepetu, alikuwepo na kundi la Weusi liliwakilishwa na Joh Makini pamoja G nako.Party imefanyika Rock City Shopping mall Mwanza.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger