Friday, 6 November 2015

Kikwete Aaga Kwa Kusamehe Wafungwa 4,160

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,160 katika kuaga na kukabidhi madaraka ya Serikali kwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Dk Magufuli aliapishwa jana kuwa Rais wa Tano wa Tanzania katika sherehe zilizofana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku Kikwete akimaliza miaka yake 10 ya kuongoza nchi kama ilivyoelekezwa na Katiba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam, kati ya wafungwa hao, wafungwa 867 wataachiwa huru na wafungwa 3,293 watapunguziwa vifungo vyao na kubaki gerezani wakitumikia sehemu ya vifungo vyao vilivyobaki.

“Ni mategemeo ya Serikali kwamba wafungwa watakaoachiwa huru watarejea katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa na watajiepusha na utendaji makosa ili wasirejee tena gerezani,” alisema Chikawe katika taarifa hiyo.

Chikawe aliwataja walionufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wote wapunguziwe moja ya sita ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya Kifungu cha 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika ibara ya 1 (i-xix).

Aliwataja wengine kuwa ni wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama Ukimwi, kifua kikuu, saratani ambao wako kwenye hatua ya mwisho ambao watathibitishwa na waganga chini ya Mganga mkuu wa mkoa au wilaya.

Pia wazee wenye umri zaidi ya miaka 70, wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani na walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya na walemavu wa mwili na akili na ulemavu huo uthibitishwe na jopo la waganga.

Kwa mujibu wa Chikawe, msamaha hautawahusu wafungwa wenye adhabu za kunyongwa, waliohukumiwa kunyongwa na adhabu hiyo baadaye kubadilishwa kuwa kifungo cha maishaau kifungo gerezani.

Wengine ni wafungwa waliotumikia kifungo kwa makosa ya usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya, makosa yanayohusu uombaji, upokeaji na utoaji rushwa, unyang’anyi na kujaribu kutenda makosa hayo, kubaka, kulawiti au kujaribu kutenda makosa hayo.

Aidha, makosa mengine ambayo vifungo vyake haviko kwenye msamaha huo ni makosa ya kuwapa mimba wanafunzi, wizi wa magari, pikipiki au kujaribu kutenda makosa hayo, matumizi mabaya ya madaraka, waliowahi kupunguziwa vifungo na Rais.

“Wengine ni waliopatikana na hatia kwa kuwazuia watoto kupata masomo, utekaji watoto, usafirishaji binadamu, ukatili dhidi ya albino, usafirishaji nyara za Serikali na ujangili,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mengine ni wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi na ubadhirifu wa fedha za Serikali, kutoroka au kujaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi halali na wafungwa wanaotumikia vifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole Sheria Namba 25 ya Mwaka 1994 ya Sheria ya Huduma kwa Jamii Namba 6 ya Mwaka 2002
Share:

Thursday, 5 November 2015

5th Batch of Selected Students to join with Bachelor Degree at SJUT 2015/2016

Share:

ANGALIA ADA KAMILI KWA WANAFUNZI MLIOCHAGULIWA MBEYA UNIVERSITY MUST 2015/2016

Share:

HAYA HAPA MAJINA 3RD BATCH WALIOCHAGULIWA MZUMBE UNIVERSITY 2015/2016

Share:

DOWNLOAD HAPA JOINING INSTRUCTIONS NA NAMES OF DIPLOMA STUDENTS SELECTED KCMC 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
kcmuco banner

Selected Candidates for Diploma

Admission Offer / joining instructions for 2015
Share:

ANGALIA HAPA ADA KWA WANAFUNZI WA DUCE 2015/2016

Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 5 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Jukwaa la Wahariri Walaani Tukio la Kuzomewa Dk Reginald Mengi na Wafuasi wa CCM

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
JUKWAA la Wahariri (TEF), limelaani kitendo cha kuzomewa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari wa ITV, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, Oktoba 30 mwaka huu.

Akizungunza na waandishi wa habari Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena amesema kuwa kitendo hicho si cha kukaliwa kimya kutokana na kukwaza utendaji wa kazi na kudhalilisha utu wa waandishi hao mbele ya jamii.

Meena amesema kuwa waandishi na wafanyakazi wa kituo hicho walikuwa katika ofisi hizo za CCM, wakirusha na kuandika habari za tukio la mapokezi ya Dk. John Magufuli baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi wa urais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika hafla iliyofanyika siku hiyo katika ukumbi wa Diamond Jublee.

“Kuzomewa kwa waandishi hao katika ofisi za CCM ni muendelezo wa kile kilichoanzia Diamond Jubilee ambapo wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM, walionekana wakiwazomea wafanyakazi wa ITV na baadaye kumzonga Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi ambaye ni mmliki wa kituo hicho,” amesema Meena.

Ametoa onyo kwa kuwataka wafuasi hao waache vitendo hivyo, akisema kuwa utafiti mdogo waliofanywa na Jukwaa hilo kuhusu vitendo hivyo vinatokana na wafuasi hao kuchukizwa na jinsi kituo hicho kilivyoripoti, matukio ya kampeni na kuwapa fulsa wagombea wa vyama vingine vya siasa.

Amesema kuwa kituo hicho ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyofanya kazi zake kwa weredi wakati wa kampeni za wagombea wa vyama vyote nchi nzima ambapo Dk. Magufuli na Mgombea Mwenza, Samia Suluhu walikuwa na wandishi wa kituo hicho miongoni mwao ni Emmanuel Buhohera na Halfan Liundi ambapo umma wa watanzania ulipata kufahamu kinachoendelea katika mikutano yao ya kampeni.

Meena ameongeza kuwa hilo sio tukio la kwanza kufanywa na chama hicho kwani wakati wa kampeni za mgombea urais kilimfukuza katika msafara wa Dk. Magufuli mkoani Mbeya, mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Peter Elias kwa madai ya kutofurahishwa na habari aliyoandika kuhusu mgombea wao.

Amesema kuwa matuko hayo siyo ya kiungwana na hayatakubalika katika jamii ya watu wastaarabu. Ikiwa waandishi wa habari au vyombo vya habari vinafanya makosa zipo njia za kisheria za kushughulikia makosa hayo pamoja na kufanya mazungumzo kupitia taasisi za waandishi wa habari.

“Tunachukua fulsa hii kuvitaka vyama vya siasa kama taasisi viongozi, wanachama na wapenzi wake kuacha mara moja vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari kwa sababu zozote zile. Tusingependa ifike hatua kutangaza kwamba matukio ya chama fulani ni hatari kwa waandishi wa habari,” amesema Meena.

Kadhalika tunachukua fursa hii kuvitaka vyama vya siasa na watu binafsi wanaoandaa mikutano inayowahusisha waandishi wa habari kuhakikisha kuwa waandishi wanakuwa salama wanapo hudhuria kwenye mikutano yao na kuchukua hatua ya kukemea.

“Tunasikitika kwa ukimya wa chama hicho ulionyesha kufurahishwa kwa tukio hilo kutokana na kutotoa kauli yoyote,” amesema Meena.
Share:

New AUDIO | Baba Jonii Ft. Dolafosalamitido - AEIOU | Download/Listen

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
https://mkito.com/song/aeiou-ft-dolafosalamitido/17102/bwi-1-33483
Share:

BEN POL AKIMBILIA SAUZ KUPAKUA MZIGO MPYA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mkali wa R&B Bongo, Ben Pol.
KACHAA mkali wa R&B Bongo, Ben Pol muda wowote kuanzia sasa anatarajia kuelekea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ kwenda ku-shoot video zake mbili mpya.Ben ameliambia Championi Jumatano kuwa akiwa ‘bondeni’ atatengeneza video mbili za nyimbo zake hizo mpya.
Moja inaitwa Ningefanyaje, aliyoimba na mwanadada mrembo wa Kenya, Avril na nyingine amempa shavu msanii mahiri wa Kenya, Nameless.Aidha, ameongeza kuwa Kampuni ya Gorilla Films chini ya Director, Justin Campos, aliyetengeneza video kali ya Nusu Nusu ya Joh Makini ndiye atakayefanya naye kazi hiyo kwa muda wa wiki moja na nusu.

“Muda wowote tangu sasa nitaenda Sauz ku-shoot video zangu mbili na kampuni ya Gorilla Films, kila kitu kimekaa sawa na tutatumia muda kama wa wiki na nusu hivi kukamilisha kila kitu. Nameless nishaongea naye na nitakutana naye hukohuko kumaliza kazi,” alisema Ben Pol.
Share:

Maalim Seif akutana na JK

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake Dkt. Jakaya Kikwete. Mazungumzo hayo yaliyochukua muda wa dakika 50 yalifanyika Ikulu ya Rais Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:24 asubuhi na kumaliza saa 5:14. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Share:

Masanja Mkandamizaji Achukua Form za Kugombea Ubunge Ludewa na Ktangaza nia Kuchukua Nafasi ya Marehemu Filikunjombe

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Masanja Mkandamizaji
MSANII maarufu na mwigizaji Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la (Masanja mkandamizaji) ameahidi kuvaa viatu vya Deo H. Filikunjombe kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Ludewa na kusema ana uwezo mkubwa na kasi kama ya marehemu Filikunjombe ambaye alikuwa rafiki yake.

Ameyasema hayo alipokuja kuchukua fomu ya kugombea kupata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi,jumla ya watu tisa akiwemo mdogo wa marehemu Fillipo Filikunjombe ambaye ni mwanasheria wa TCRA wamechukua fomu ili kuweza kuomba ridhaa
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO RUAHA UNIVERSITY-RUCU 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Students Eligible for loan (2015/2016) 
<<Download Here>>
Share:

Wednesday, 4 November 2015

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA UDSM 8TH BATCH 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tokeo la picha la UDSM
The following additional applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2015/2016 academic year. The selected applicants should report at the Mwl. J.K. Nyerere Mlimani Campus for the orientation week which  will end on Saturday 7th November 2015.  Applicants selected for admission into Dar es Salaam University College of Education (DUCE) and Mkwawa University College of Education (MUCE) should report directly to the college's campuses in Chang'ombe and Iringa respectively on the same dates. Joining instructions and admission letters should be collected at the University campuses where one is admitted. Joining instructions  and other important information can also be downloaded from the University website at www.udsm.ac.tz  (go to the Undergraduate Section).
Click Here to View the selected  applicants.
Share:

FIFTH AND FOURTH BATCH -STUDENTS SELECTED MWENGE UNIVERSITY 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Research and Publication image

SELECTED APPLICANT FOR ACADEMIC YEAR 2015/2016 FIFTH BATCH

SELECTED APPLICANT FOR ACADEMIC YEAR 2015/2016 FOURTH BATCH

Share:

Tume ya taifa ya uchaguzi yaombwa kutoa tarehe ya kupiga kura jimbo la Lulindi.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tume ya taifa ya uchaguzi imeombwa kuweka wazi mapema iwezekanavyo tarehe ya kupiga kura ya ubunge jimbo la Lulindi vinginevyo ucheleweshaji huo unaathari kwa wapiga kura na vyama vyenye wagombea.
Tume ya taifa ya uchaguzi ililazimika kusitisha upigaji kura ya ubunge katika jimbo la Lulindi baada ya jina la mgombea wa chama cha wananchi CUF Amina Thomas Msham kukosewa katika karatasi za kupigiwa kura na kusomeka Msham Thomas Mcham.
 
Akizungumzia hilo mdhamini wa chama cha NLD ambaye pia ni mgombea wa jimbo la Lulindi Modesta Makaidi na uongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mtwara wameonyesha wasiwasi wao na kuzungumza haya.
 
Akizungumza kwa njia ya simu msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo Beatres Maiko amesema analitambua hilo na kwa sasa yuko jijini Dar es Salaam kufuatilia suala hilo.
 
Jimbo la Lulindi limefanikiwa kufanya uchaguzi wa rais na madiwani, wagombea ubunge wanaotarajiwa kupigiwa kura ni Jerome Bwanausi wa CCM, Modesta Makaidi wa NLD na Amina Thomas Msham wa CUF, jimbo lingine linalotarajiwa kufanyiwa uchaguzi mkoani Mtwara ni la Masasi mjini kutokana na mgombea wake Emmanuel Makaidi kufariki dunia.
Share:

Marais 8 Kushuhudia Magufuli Akiapishwa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MARAIS wanane wa Afrika ni miongoni mwa viongozi mbalimbali kutoka nje ya nchi, watakaohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli. 

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Magufuli ataapishwa rasmi kuwa Rais wa Awamu ya Tano kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Dk Magufuli (56) alitangazwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, baada ya kupata kura 8,882,935, sawa na asilimia 58.46 ya kura halali zilizopigwa, hivyo kumrithi Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Magogoni, ambayo tayari imeshakaliwa na marais wengine wanne. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyotolewa jana Dar es Salaam, sherehe za uapisho zitahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Kikanda na Wawakilishi mbalimbali kutoka nje ya nchi. Iliwataja miongoni mwa marais watakaohudhuria sherehe hizo ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini. 

Wengine ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji na Rais Edgar Lungu wa Zambia. Taarifa ya Mambo ya Nje ilieleza kuwa Malawi itawakilishwa na Makamu wa Rais, Saulos Chilima wakati Namibia itawakilishwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Netumbo Nandi-Ndaitwah. Aidha, Serikali ya China itawakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala. 

“Vilevile nchi nyingine ambazo zimethibitisha kushiriki na zitawakilishwa na kati ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika au Balozi ni pamoja na Burundi, Comoro, Angola, Botswana, Lesotho, Madagascar na Mauritius. “Nyingine ni Norway, Oman, Sudan Kusini, Sweden, Umoja wa Falme za Kiarabu, Marekani, Uingereza, Shelisheli, Swaziland, Algeria, Misri, Benin, Denmark, Ethiopia, Finland, Ufaransa, Ghana, India, Japan, Kuwait, Uholanzi na Nigeria,” ilifafanua taarifa hiyo. 

Ilieleza kuwa Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Kikanda, waliothibitisha kushiriki au kutuma wawakilishi wao ni Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR). 

Wabunge wapya kuwasili Dar Katika hatua nyingine, wabunge wapya waliochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli zitakazofanyika kesho. 

Akizungumzia kuwasili kwa wabunge hao, Ofisa Habari Mwandamizi wa Bunge, Prosper Minja alisema wabunge hao wanatarajiwa kuwasili leo Dar es Salaam wakiwa na vyeti vyao vya kuteuliwa kuwa wabunge vinavyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa eneo husika. 

“Tunategemea kesho (leo), wabunge wapya watawasili kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule na tunategemea waje na cheti hicho pamoja na kitambulisho kingine kinachomtambulisha,” alisema Minja. 

Alisema mara baada ya wabunge hao kuwasili, wanatakiwa kwenda Ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kutambuliwa na kupewa kitambulisho cha siku ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk Magufuli. 

Tamko la Jeshi la Polisi Wakati huo huo, Jeshi la Polisi nchini limejipanga kuhakikisha usalama na ulinzi unaimarishwa wakati wa kuelekea sherehe za kumwapisha Rais Mteule, Dk John Magufuli. 

Akizungumza jana Dar es Salaam, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, Makao Mkauu ya Polisi, Paul Chagonja alisema jeshi lake kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, litahakikisha kunakuwa na usalama wa raia na mali zao katika kuelekea sherehe za kumuapisha Rais Mteule. 

“Niwaombe wananchi kutupa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi waonapo vishawishi ama vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria,” alisema Kamishna Chagonja. Aidha, Chagonja aliwataka wananchi kuendelea kuheshimu sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao. 

“Jeshi la Polisi linawataka wananchi kote nchini kuendelea kuheshimu sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vya aina yoyote ile ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama wa raia na mali ikiwemo maandamano yanayopangwa bila kufuata taratibu,” alisema Chagonja na kuongeza: “Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa mtu au kikundi chochote kitakachoonesha viashiria vya uvunjifu wa sheria ama kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu.” 

Mbali ya kuwashukuru wananchi na wadau waliotoa ushirikiano kuhakikisha amani ya Watanzania inadumu katika kipindi cha uchaguzi na wakati huu wa kuelekea kuapishwa kwa Rais Mteule, alikiri jeshi hilo kuwashikilia watu kadhaa na baadhi yao kufikishwa mahakamani kutokana na kufanya makosa wakati wa uchaguzi. 

Bila kutaja idadi, Chagonja alisema, “Ni kweli kuna watu kadhaa tumewakamata kwa makosa mbalimbali wakati wa uchaguzi, kuna wengine wamefikishwa mahakamani, na kuna wengine bado wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi na wengine wamewekewa dhamana.” Imeandikwa na Ikunda Eric na Anastazia Anyimike.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger