Friday 27 October 2023

RC SIMIYU ATEMBELEA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI 'VIJANA WAPAMBANAJI' BARIADI,...... AHIMIZA MAREJESHO KWA WAKATI KUJENGA UAMINIFU

...



Bariadi,

Vijana wajasiriamali  Mkoani Simiyu wamehimizwa  kufanya  marejesho ya mikopo inayotolewa na Serikali kwa wakati ili kujenga uaminifu jambo litakalowawezesha kuaminika na kukopeshwa fedha nyingi zaidi jambo  litakayosaidia kukuza mitaji yao na hivyo kujikwamua na umaskini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Nawanda alipotembelea kikundi Cha Vijana Wajasiriamali almaarufu "Vijana wapambanaji" kilichopo eneo la Stendi kuu ya Mabasi Somanda Wilayani Bariadi wanaojihusisha na shughuli za uchapaji mabango kwa lengo la kutatua Kero zao.

"Kwa uzoefu nilionao nikiwa DC  kwa miaka zaidi ya saba ni kuwa  vikundi vingi vya Vijana vina changamoto ya kutofanya marejesho kwa wakati tofauti na vikundi vya walemavu na wakina mama."Alisema mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda. 

Aidha Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda amewapongeza Vijana wapambanaji kwa kuwa mfano mzuri katika kufanya marejesho ya mikopo waliyowezeshwa na Serikali kwa wakati na kuwataka Vijana wengine kuiga mfano.

Kikundi cha Wajasiriamali cha vijana wapambanaji ni moja kati ya Vikundi vya Wajasiriamali Wilayani Bariadi  vilivyonufaika na Mkopo wa Asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha Vijana,akina Mama na wenye ulemavu.

www.simiyu.go.tz



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger