





Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo akinawishwa mikono na Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Kamishna Msaidizi Caroline Malundo mara baada ya zoezi la Upandaji wa miti katika eneo la hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hewa ukaa.




(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, KISARAWE PWANI
Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Seleman Jafo amewataka wananchii wanaoishi pembezoni mwa hifadhi za misitu kuendelea na utamaduni wa utuzaji wa mazingira katika maeneo hayo ili kuendana na mabadiliko ya Tabianchi.
Ameyasema hayo leo Waziri Jafo baada ya kutembelea Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, kuona namna ambavyo Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilivyojidhatiti kuendeleza msitu huo kama sehemu ya kuhifadhi mazingira.
Aidha ameelekeza kila halmashauri ianze programu ya kutumia mvua zinazoendelea kunyesha nchini kupanda miti ili kuweza kufikia lengo la miti milioni 276 kwa mwaka mzima hivyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya watasiimamia zoezi hilo.
"Tunafahamu kila halmashauri imepewa muongozo wa uwekaji wa vitalu kwa lengo la kusaidia katika maeneo mbalimbali hasa katika taasisi, tunataka tuone katika shule zetu zote, vituo vya afya, hospitali maeneo hayo yote yanapandwa miti". Amesema
Amesema upandaji wa miti kwa wingi kwenye mazingira ni njia moja wapo itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya mwanadamu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuna umuhimu wa utunzaji wa mazingira hivyo watanzania wanatakiwa kuweka mazingira yao kama yalivyookuwa awali na vilevile watanzania wakiendelea kupanda miti kwa wingi basi nchi itakuwa imejawa na misitu na tutaweza kupunguza athari kubwa tunazozipata kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Nae Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Kamishna Msaidizi Caroline Malundo amesema Pugu Kazimzumbwi moja ya hifadhi ya msitu muhimu uliopo hapo Wilayani Kisarawe ambao umekuwa ukichochea Utalii ndani kutokana na mikakati iliyowekwa na Wakala wa Misitu TFS.
0 comments:
Post a Comment