KATIBU TAWALA MKOA WA SHINYANGA ZUWENA OMARY AUDHURIA MAULID I AHAIDI USHIRIKIANO
Zaidi ya Shilingi milioni moja zimechangwa na Waumini wa dini ya Kiislam kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Galamba uliopo katika kata ya Ibadakuli wakati wa Harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina uliopo katika kata ya Ndembezi halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Harambee hiyo imefanyika leo Jumamosi Desemba 4,2021 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura pamoja na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Ester Makune.
Fedha hizo zimekusanywa katika harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina Ndembezi ikiwa ni Maadhimisho ya Mazazi ya Mtume Muhammad (Maulid) yaliyoandaliwa na akina mama wa dini ya Kiislamu wilaya ya Shinyanga mjini kata ya Abubakari Swidiq iliyopo katika kata ya Ndembezi.
Katibu wa JUWAKITA Bakwata mkoa wa Shinyanga Mwadawa Hassan ameeleza kuwa wao kama akina mama wa dini ya Kiislamu wilaya ya Shinyanga mjini wameamua kumsifu Mtume Muhammad kwa kuadhimisha na kuzitaja sifa za Mtume Muhammad kwa kuadhimisha Mazazi ya Mtume Muhammad S.A.W (Maulid)
Naye Sheikh Majaliwa Masoud kutoka Ofisi ya BAKWATA mkoa wa Shinyanga ameushukuru uongozi wa akina mama hao na kuwaomba akina mama wengine wa dini ya Kiislamu kuiga mfano uliofanywa na akina mama wa Msikiti wa Safina Ndembezi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa waumini na viongozi wa msikiti huo huku akishauri viongozi kubuni vyanzo vya mapato pamoja na kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri za wilaya.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati wa Harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina uliopo katika kata ya Ndembezi halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga leo Jumamosi Desemba 4,2021. Picha na Amos John
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati wa Harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina uliopo katika kata ya Ndembezi halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
0 comments:
Post a Comment