Na Dotto Kwilasa - Malunde 1 blog, Dodoma
KUTOKANA na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutaka wamiliki wa silaha kinyume na Sheria kuzisalimisha, jumla ya silaha 228 zimesalimishwa kwa Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema hayo leo Desemba 6,2021,wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa tangazo la msamaha kwa usalimishaji wa silaha haramu tarehe 1/11/2021 hadi tarehe 30/11/2021.
Waziri Simbachawene amesema Jumla ya silaha zilizosalimishwa ni 228 huku akilitaka Jeshi hilo kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015.
"Kwa mchanganuo wa Pistol 05 sawa na 2.2% ya silaha zote zilizosamilishwa, magobore 174 sawa na 76.3% ya silaha zote zilizosalimishwa, S/gun 38 sawa na 16.7% ya silaha zote zilizosalimishwa, Rifle 10 sawa na 4.4% ya silaha zilizosalimishwa na SMG 01 sawa na 0.4% ya silaha zote zilizosalimishwa,”amesema.
Amesema kufanya hivyo ni ili kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobore kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za ulinzi katika jamii.
Pia imesalimishwa jumla ya mitutu 12 ambapo mitutu 11 imesalimishwa Mkoa wa Tanga na Mtutu 01 umesalimishwa Mkoa wa Mbeya.
“Kati ya silaha zilizosalimishwa imeonekana kuwa magobore ni asilimia 76.3 jambo linaloonesha kuwa tatizo la utengenezaji wa silaha za kienyeji yakiwemo magobore ni kubwa hapa nchini,”amesema.
Amesema kufuatia matokeo haya ya usalimishaji wa silaha haramu,Waziri Simbachawene amelielekeza Jeshi la Polisi kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 ili kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobole kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za Ulinzi katika jamii.
Pia,kufanya misako kwa kutumia taarifa za kiintelelijensia ili kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume na Sheria na kisha kuwachukulia hatua za kisheria.
0 comments:
Post a Comment