Sunday, 5 December 2021

RAIS SAMIA : NJOO UNIAMBIE DADA NIMESHINDWA,NITAANGALIA MWINGINE

...


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, na kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa
***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemtaka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, afanye marekebesho yanayowezekana ndani ya wizara yake ili mambo yaendelee kufuatia uwepo wa ubadhirifu mkubwa katika bandari ya Dar es Salaam.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 4, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa gati 0 hadi 7 ya Bandari ya Dar es Salaam.

"Mh. Waziri nilikuweka kwa kukuamini na ninaomba nenda kasimamie kazi hii kama ninavyotarajia na utakaposhindwa njoo uniambie, Dada nimeshindwa, nitaangalia mwingine labda ataweza kunisaidia, lakini haya hayawezi kuendelea," amesema Rais Samia.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger