Maajabu hayawezi kuisha duniani, unaambiwa mwanamke mmoja aliyekuwa mmoja wa abiria katika ndege ya Delta inayofanya safari zake kati ya Syracuse, New York na Atlanta, Georgia amekutwa akimnyonyesha maziwa paka wake ambaye hakuwa na manyoya.
Tukio hilo limeibuka upya baada ya kusambaa kwa meseji zinazoonesha mawasiliano kati ya rubani wa ndege hiyo na mamlaka inayojulikana kama Redcoat inayojishughulisha na huduma kwa wateja au abiria wa ndege. Meseji hizo zinaonesha rubani akiripoti tukio hilo na kuiomba Redcoat imshikilie na kuzungumza na abiria huyo pindi tu ndege itakapotua.
Ripoti zinaeleza kuwa mwanamke huyo alikataa agizo la muhudumu wa ndege la kumrudisha paka kwenye kizizi maalumu kilichopo mbele ya siti ya ndege.
Kampuni ya ndege ya Delta inawaruhusu abiria kusafiri na wanyama wadogo kama paka na mbwa katika safari fupi, lakini kwa masharti ya kuwaweka wanyama hao kwenye kizizi maalumu mwanzo hadi mwisho wa safari.
0 comments:
Post a Comment