Monday, 11 October 2021

TAIFA STARS YAICHAPA 1-0 BENIN UGENINI

...

Timu ya Taifa Stars imefufua ndoto za kutinga hatua ya mwisho ya mtoano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Qatar mwakani baada ya kuwachapa wwenyeji Benin bao 1-0 Mchezo uliopigwa uwanja wa Stade de l’Amitie nchini Benin.

Shujaa wa Taifa Stars ni winga hatari wa klabu ya Wydad Casablanca Saimon Msuva dakika ya 6 baada ya kuachia shuti kali lililotinga moja kwa moja.

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 nyumbani, juzi Alhamisi, Stars imefanikiwa kulipa kisasi hicho cha bao moja.

Kwa ushindi huo Tanzania inafikisha pointi 7 ikilingana na Benin wenye Point 7 ila Tanzania inaongoza kundi J nafasi ya tatu inashikwa na DR Congo watakaoshuka uwanjani kucheza na vibonde Madagascar.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger