Sunday, 31 October 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 1,2021


Magazetini leo Jumatatu November 1 2021




Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2021 (Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2021


Ili kuwa wa Kwanza kusoma habari na matukio tunakushauri upakue/ download Aplikesheni ya Malunde 1 blog ili tukutumie moja kwa moja kwenye simu yako
Pakua App ya Malunde 1 blog,

 Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Share:

SIMBA YABANWA MBAVU...YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA COASTAL UNION




Na Emmanuel Mbatilo - Dar es salaam
KLABU ya Simba Sc imeshindwa kufurukuta mbele ya wagosi wa kaya Coastal Union kwenye ligi ya NBC.

Simba imelazimishwa sare kwenye mchezo huo ambao ulikuwa mchezo wa aina yake hasa timu zote mbili katika kipindi cha kwanza kucheza kwa kushambuliana japo kwa upande wa Simba walionesha hamu ya kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Kipindi cha pili Simba ilirudi ikiwa imejipanga kwani walitawala mchezo huo licha ya kutokutumia nafasi nyingii za wazi walizozipata.

Timu zote mbili zilipata kadi nyekundu.
Share:

Picha : MAHAFALI YA 23 YA SHULE YA SEKONDARI DON BOSCO DIDIA YAFANYIKA...WAZAZI WAKUMBUSHWA WAJIBU WAO

Wahitimu  wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga wakiwa katika picha pamoja.

Na Josephine Charles - Shinyanga 

Wazazi na Walezi wametakiwa kutekeleza Wajibu wao wa malezi ili kuepusha watoto wasijiingize katika matendo yasiyofaa kwenye jamii.

Hayo yamesemwa Oktoba 30,2021 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga bw. Boniphace Chambi kwenye mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco iliyopo Didia katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.

Katibu Tawala huyo ametolea mfano kipindi cha Corona wanafunzi walipoenda likizo baadhi yao walipata ujauzito,hiyo ikiwa inamaanisha kwamba kipindi walivyokuwa nyumbani wazazi hawakuzingatia nafasi zao katika malezi.

Katika risala aliyoisoma Mkuu wa Shule hiyo Fr. Felix Wagi amesema wanafunzi walioanza kidato cha awali mwaka 2017 Walikuwa ni wanafunzi 250 ambapo wasichana walikuwa 96 na wavulana 154 na waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 164 kati yao wavulana ni 97 na wasichana ni 67 na kueleza kuwa upungufu huo umetokana na changamoto mbalimbali zisizozuilika.

Mkuu huyo wa Shule amesema mbali na mafanikio waliyopata tangu shule hiyo kuanzishwa mwaka 1994 baadhi ya changamoto walizonazo mpaka sasa ni pamoja na uhaba wa maji safi na salama kwa wanafunzi na upungufu wa mabweni.

Tazama picha hapa chini


Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga bw. Boniphace Chambi akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya Shule Sekondari Don Bosco-Didia-Shinyanga
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga bw. Boniphace Chambi akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya Shule Sekondari Don Bosco-Didia-Shinyanga
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga bw. Boniphace Chambia(katikati) akiwa na wageni waalikwa kushoto ni Mkurugenzi wa Gvenwear bi. Grace Mng'ong'o,kushoto mwenye skafu ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Jimbo katoliki Shinyanga pamoja na Mkurugenzi wa Radio Faraja Shinyanga Padre Anatoly Salawa pamoja na Uongozi wa shule ya Shule Sekondari Don Bosco-Didia-Shinyanga wa Kulia asiye na Skafu ni Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Padre Vicent Mokaya,nyuma mwenye shati nyeupe ni Padre Kenneth Omondi na mwenye suti ni Mkuu wa Shule hiyo Padre. Felix Wagi wakiwa tayari kuelekea ukumbuni kunapofanyika mahafali ya 23 ya shule ya sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga Padre Vicent Mokaya akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya kidato cha 4 ya Shule hiyo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga Padre Felix Wagi akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya kidato cha 4 ya Shule hiyo
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la TVMC lenye makao makuu yake Shinyanga bw. Musa Ngangala akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya kidato cha 4 ya Shule hiyo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushonaji na Ubunifu wa Mavazi iitwayo GVENWEAR iliyopo Shinyanga bi. Grace Mng'ong'o akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya kidato cha 4 ya Shule hiyo
Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Radio Faraja 91.3 iliyopo Shinyanga ambaye pia ni balozi wa Don Bosco Sekondari Didia na Balozi wa Gvenwear bi. Josephine Charles akizungumza kwa niaba ya waandishi wenzake alioongozana nao kwenye mahafali ya 23 ya Shule hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Jimbo katoliki Shinyanga pamoja na Mkurugenzi wa Radio Faraja Shinyanga Padre Anatoly Salawa akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Makamu mkuu wa shule ya sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga Sister Mary Magdalene Mativo akizungumza kwenye mahafali ya 23 ya Shule hiyo.
Mtawala wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga Padre Kenneth Omondi akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mgeni Rasmi pamoja na baadhi ya wageni waalikwa wakiwa tayari kwa ajili ya zoezi la ugawaji vyeti kwa wahitimu 164 wa kidato cha 4 Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga ikiwa ni mahafali ya 23 tangu shule hiyo kuanzishwa mwaka 1994.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushonaji na Ubunifu wa Mavazi iitwayo GVENWEAR iliyopo Shinyanga bi. Grace Mng'ong'o na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Jimbo katoliki Shinyanga pamoja na Mkurugenzi wa Radio Faraja Shinyanga Padre Anatoly Salawa wakiwa wamesimama Ukumbini kumsubiri Mgeni Rasmi amalize kusaini kitabu cha Wageni ndipo waketi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushonaji na Ubunifu wa Mavazi iitwayo GVENWEAR iliyopo Shinyanga bi. Grace Mng'ong'o na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga bw. Boniphace Chambi wakiwa wameketi ukumbuni kunapofanyika mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco-Didia.
Wageni waalikwa,Waalimu,Wazazi,Wahitimu na Wanafunzi wakiwa ukumbini kufuatilia matukio yanayoendelea kwenye mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Mgeni Rasmi,Wageni waalikwa,Waalimu,Wazazi,Wahitimu na Wanafunzi wakiwa ukumbini kufuatilia matukio yanayoendelea kwenye mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Mgeni Rasmi,Wageni waalikwa,Waalimu,Wazazi,Wahitimu na Wanafunzi wakiwa ukumbini kufuatilia matukio yanayoendelea kwenye mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Mgeni Rasmi,Wageni waalikwa,Waalimu,Wazazi,Wahitimu na Wanafunzi wakiwa ukumbini kufuatilia matukio yanayoendelea kwenye mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Mgeni Rasmi,Wageni waalikwa,Waalimu,Wazazi,Wahitimu na Wanafunzi wakiwa ukumbini kufuatilia matukio yanayoendelea kwenye mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Wahitimu 164 wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga wakijiandaa kutoa burudani ya wimbo mbele ya Mgeni Rasmi,Wageni waalikwa,Waalimu,Wazazi,Wahitimu na Wanafunzi wasiowahitimu.
Wahitimu 164 wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga wakiwa katika picha pamoja.
Wahitimu 164 wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga wakiwa katika picha pamoja na Mgeni Rasmi pamoja Wageni waalikwa katika mahafali ya 23 ya shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga wakiwa wanafuatilia matukio ya burudani zinazoendelea kwenye mahafali ya 23 ya shule hiyo.

Picha zote na Josepine Charles & Kasisi Kosta
Share:

KUTANA NA MTAALAMU WA TIBA MBADALA BABU MWANASIMBA

 

Share:

VIBOKO WA PABLO KUTAMBULIWA KISHERIA KAMA BINADAMU



Mahakama ya nchini Marekani imepitisha sheria ya kuwatambua Viboko waliokuwa wanamilikiwa na muuzaji hatari wa madawa ya kulevya nchini Kolombia, Pablo Escobar kama watu, kufuatia kesi dhidi ya Serikali ya nchi ya Kolombia juu ya kuwaua na kuwafanya viboko hao wawe tasa ili wasiweze kuzaliana zaidi nchini humo.

Viboko hao walipelekwa nchini Kolombia mwaka 1980 na Pablo Escobar ambaye alifariki mwaka 1993 , tangu hapo viboko hao hawakuwa na muangalizi hivyo kuzagaa ovyo na kuzaliana bila uangalizi. Ripoti zinasema kwa miaka nane viboko hao wameongezeka kutoka 35 hadi 80.

Makundi ya wanasayansi nchini Kolombia yametahadharisha hatari ya viboko hao kwa binadamu, sheria iliyopitishwa nchini Marekani juu ya kuwatambuwa Viboko kama binadamu inaweza isichukuliwe kwa uzito nchini Kolombia.
Share:

MITANDAO YA KIJAMII NA CHANGAMOTO ZA UTOAJI WA CHANJO YA UVIKO-19 TANZANIA



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ugonjwa wa UVIKO-19 umesababisha madhara makubwa kwa watanzania. Athari za ugonjwa huu ni pamoja na vifo, gharama za matibabu, pamoja na kudorora kwa shughuli za kiuchumj. Bahati mbaya, UVIKO-19 hauna dawa mpaka sasa. Njia pekee ya kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa huu ni chanjo zilizogunduliwa na kuthibitishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO). Kwa mujibu wa WHO na Wizara ya Afya ya Tanzania, chanjo hizi zina uwezo wa kuwakinga watu dhidi ya kupata homa kali na kifo.

Katika kuwalinda raia wake dhidi ya ugonjwa huu, Serikali imefanikisha upatikanaji wa dozi zaidi ya milioni moja za chanjo ya UVIKO-19 ya Jensen Jensen ambazo tayari zimetolewa kwa na kutumika. Kwa sasa, dozi Zaidi ya milioni moja za chanjo aina ya Sinopharm zimesambazwa na kutolewa kwa wananchi nchi nzima.

 Hata hivyo, pamoja na faida za chanjo hizi, bado kumekuwepo na upinzani miongoni mwa watanzania unaozorotesha utekelezaji wa chanjo hizi.
Moja ya changamoto kubwa inayochangia mwamko mdogo wa raia kujitokeza kuchanjwa ni kusambaa kwa taarifa, imani na dhana potofu kuhusiana na chanjo ya UVIKO-19 nchini. 

Mitandao ya kijamii imechangia kwa kiasi kikubwa upotoshaji huu. Ingawa kwa upande mwingine mitandao hii imeongeza uhuru wa watu kupata na kutoa taarifa, imekuwa chanzo cha upotoshaji kuhusu chanjo. 

Upotoshaji huu umejenga na/au kuongeza hofu isiyo na mashiko kisayansi katika jamii kuhusu usalama wa chanjo.

 Bahati mbaya, sehemu ya watumiaji wa mitandao hawana weledi wa kutofautisha taarifa sahihi na potofu kuhusu chanjo.

Aidha, takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), zinaonesha kuwa zaidi ya wananchi milioni 16 wanapata taarifa kupitia mtandao wa intaneti.

 Hata hivyo, watumiaji hawa hawana weledi wa kutosha kujua vyanzo sahihi vya taarifa kuhusu chanjo ya UVIKO-19. Aidha, uelewa mdogo wa matumizi ya mitandao umepelekea watumiaji wengi kuamini taarifa zinazopotosha ukweli kuhusu chanjo husika.

 Hii ina maana kwamba, mitandao ya kijamii imekua kikwazo katika kujitokeza kwa wingi kwa wananchi ili kupata chanjo ya UVIKO-19 na hivyo kujikinga dhidi ya madhila ya ugonjwa huu hapa nchini.

Nini kifanyike?
 
👉Elimu na taarifa sahihi ya chanjo ya UVIKO-19 itolewe kwa waandishi wa habari wakiwemo Mabloga ili waweze kutoa taarifa kwa usahihi kuhusu chanjo kwa wananchi wengi.

👉Wizara ya Afya na wataalam wake watumie vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii, radio, televisheni, magazeti, na vipeperushi ili kutoa elimu sahihi na kuwahamasisha wananchi kuhusu chanjo ya UVIKO-19.

👉 Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Tanzania vishirikiane na Serikali, hususan Wizara ya Afya, kutoa taarifa na elimu sahihi kuhusu umuhimu wa kuchanja na hatari ya kutochanja.

👉 Elimu na taarifa sahihi kuhusu chanjo itawaondolea hofu wananchi na hivo kujitokeza kwa wingi kupata chanjo.
Share:

ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA YAENDELEA KUONGEZEKA

Na Dinna Maningo, TARIME.
MABADILIKO ya hali ya hewa yamesababisha athari za Kiuchumi na Kijamii huku Serikali ya Nchi ya Tanzania ikitumia fedha nyingi kugharamia majanga vikiwemo vifo,upotevu wa mali,uharibifu wa mazao,mifigo miundombinu ya barabara,maji na umeme.

Sekta zote za kiuchumi na kijamii zimeendelea kuathirika na zitaendelea kuathirika kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa,sekta ambazo zimeathirika zaidi ni pamoja na Kilimo,Maji,Mifugo,Nishati,Uvuvi,Usafirishaji na Afya.

Hayo yameelezwa katika kijarida Sera cha kusambaza matokeo ya utafiti kilichoandaliwa na watafiti kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwakushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Kwa mujibu wa utafiti Kitengo cha Maafa (Disaster Management) zinaonyesha kuwa katika miaka 20 iliyopita kuanzia 2000 hadi 2019,Serikali imetumia kiasi cha Dolla za Kimarekani Milioni 20.5 kugharamia majanga mbalimbali yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Takwimu za utafiti zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2019 takribani nyumba 35,730 ziliharibiwa na Kaya 25,640 ziliathirika na kusababisha vifo 450 na watu 240 waliumizwa.
Mfano dhahili wa madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa ni mafuriko yaliyotokea mkoa wa Dar es salaam mwaka 2011/2012 ambayo yalisababisha vifo vya watu 43 na uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo  ya maji,barabara na umeme.

 Gharama za uharibifu huo zinakisiwa kufikia shilingi  milioni 7.5 huku serikali ikitumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.8 kuwaokoa watu na kuwahamisha kutoka maeneo ya mabondeni na kuwapeleka maeneo ya Mabwepande.

Thathimini ya kisayansi zinaonyesha kuwa matokeo ya vipindi vya hali mbaya ya hewa yakiwemo matukio ya ukame,mafuriko,na vipindi vifupi vya mvua kubwa na upepo mkali vimeendelea kuongezeka nakusababisha athari za kiuchumi na kijamii.

Athari zingine zinazoendelea kujitokeza ni pamoja kuongezeka kwa kina cha maji ya baharini kwenye ukanda wa pwani kwa wastani wa milimita 3.24 kwa mwaka,kuongezeka kwa magonjwa ya mazao ya kilimo na mifugo.

Tafiti zinaeleza kuwa joto linatarajiwa kuongezeka kwa nyuzi joto 2°C mpaka 4°C katika maeneo mbalimbali nchini,matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo vipindi vya mvua kubwa,mafuriko,upepo mkali na ukame yanatarajiwa kuongezeka katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Imebainika kuwa joto la mchana linatarajiwa kuendelea kuongezeka katika mikoa yote ya Tanzania,joto la usiku linatarajia kuongezeka katika mikoa yote ya Tanzania,kasi ya ongezeko lake linatarajiwa kuwa kubwa zaidi kuliko joto la mchana,maeneo ya magharibi mwa nchi,nyanda za kusini magharibi na upande wa Mashariki mwa Ziwa Nyasa yanatarajiwa kuwa na ongezeko la joto la juu kiasi cha nyuzi 3.5°C.

Tafiti zinaonyesha kuwa maeneo ya Ziwa Victoria,na baadhi ya sehemu ya nyanda za juu kaskazini mashariki yanatarajiwa kuongezeka kwa joto la chini kwa kiasi cha nyuzi joto 4.5°C mpaka 4.8°C,hivyo msimu wa baridi inayoanzia mwezi Julai mpaka Septemba inatarajiwa kuwa na joto la juu kuliko ilivyozoeleka huko nyuma (baridi kidogo).

Upande wa maeneo ya kusini,nyanda za juu kusini na maeneo ya magharibi mwa nchi mvua zinatarajiwa kupungua. Hata hivyo ongezeko la mvua linatarajiwa kuchangiwa zaidi na matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa na sio kwa mtawanyiko mzuri wa mvua.

Kwa mujibu wa watafiti wanasema kuwa kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani kote inaendelea kuongezeka kila mwaka na athari zake katika sekta zote za kiuchumi na kijamii zinaendelea kuwa kubwa hususani kwa nchi zinazoendelea ambazo uwezo wake wa kuhimili na kukabiliana na athari hizo ni ndogo.

Tafiti zinaonyesha kuwa kwa mujibu wa ripoti iliyofanywa na jopo la kiserikali lenye dhamana ya kutoa tathimini ya kisayansi ya mwelekeo wa mabadiliko ya hali ya hewa inaonesha kuwa wastani wa ongezeko la joto duniani unatarajiwa kufikia nyuzi joto 1.5 kati ya mwaka 2030 na 2052,endapo kasi ya mabadiliko itaendelea kwa viwango vya sasa.

Tafiti zinaeleza kuwa kutokana na ongezeko la madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa,serikali kupitia ofisi ya makamu wa Rais kitengo cha Mazingira iliandaa mpango mkakati kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa mwaka 2012.

Mkakati wa mpango huo unaelezwa kuwa umesaidia kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuijengea jamii uelewa na kutekeleza baadhi ya miradi ya kupunguza athari ikiwemo ujenzi wa uzio ufukweni mwa bahari ya Hindi,mradi wa mabasi ya mwendokasi,mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme (Julius Nyerere Hydropower Dam) unaotarajiwa kukamilika 2022, ukikamilika utazalisha umeme wa MW 2115.

Imeelezwa kuwa Serikali imeendelea kuimarisha uangalizi wa hali ya hewa kwa kununua na kusimika rada za hali ya hewa ambazo zimesaidia kuongeza ufanisi wa ufuatiliaji wa vimbunga.

Ili kuongeza uwezo wa Taifa na Jamii yote ya Watanzania wa kuhimili na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa watafiti wamependekeza elimu itolewe kwa jamii kuhusiana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa,kuimarisha mifumo ya uangalizi wa matukio hayo kabla hayajatokea.

Imeelezwa kuwa jitihada ziendelee kufanyika ili kuimarisha usambazaji wa taarifa za hali ya hewa ili ziwafikie walengwa,kuimarisha utafiti wa mifumo ya hali ya hewa na mabadiliko yake,kuwepo wa Sera ya hali ya hewa utaongeza tija na ufanisi katika matumizi ya taarifa na kujenga uelewa na utekelezaji wa sheria ya hali ya hewa Namba 2 ya mwaka 2019.

Watafiti wanapendekeza na kuhitimisha kuwa,kuwepo kwa mkakati wa kitaifa wa kuimarisha kilimo na maendeleo ya viwanda vya ndani,upatikanaji wa mbegu bora zinazostahimili ukame, dawa, pembejeo.

Kuwepo kwa ushirikiano baina ya Taasisi ya Kilimo ( TARI),Taasisi ya Mifugo (TALIRI) Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),Tume ya Tarifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)na Taasisi zingine za utafiti na kuboresha namna ya kusambaza Teknolojia ma matokeo ya tafiti zinazotoa majibu ya changamoto za wakulima,wavuvi na wafugaji nchini.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 31,2021....HABARI KUBWA MATOKEO DARASA LA SABA



Magazetini leo Jumapili October 31 2021..
















Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2021 (Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2021

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger