Wednesday, 1 September 2021

MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA KUFANYIKA NOVEMBA 26 NCHINI TANZANIA

...

Makamu wa Rais wa Miss East Africa Beauty Pageant Joyli Mutesi (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano wao na wanahabari kutangaza rasmi kufanyika kwa shindano la Miss East Africa 2021 litakalofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwezi Novemba 26 mwaka huu Jijini Dar es salaam. (wa kwanza kulia) ni Rais wa Taasisi hiyo Rena Callist na (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko.
Makamu wa Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika Mashariki( Miss East Africa Beauty Pageant Joyli Mutesi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) kwenye mkutano huo.
Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika Mashariki( Miss East Africa Beauty Pageant ),Rena Callist akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari juu ya mambo mbalimbali yanayohusu mashindano hayo.

Na Mwandishi wetu

JUMLA ya zawadi zenye thamani ya shilingi Milioni Mia moja arobaini na sita 146,000,000/= zitatolewa katika mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa 2021 yanayotarajia kufanyika nchini Tanzania.

Akizungumza jana mkoani Dar es Salaam na waandishi wa habari,Rais wa Mashindano ya Urembo ya mrembo wa Afrika Mashariki( Miss East Africa Beauty Pageant ),Rena Callist amesema katika mashindano hayo Mshindi wa kwanza atazawadiwa gari jipya la kisasa aina ya Nissan x Trail,toleo la Mwaka 2021/21 lenye thamani ya shilingi 110,000,000.

Amesema huku mshindi wa pili atapata pesa taslim shilingi 11,000,000 na mshindi wa tatu atajipatia pesa taslim shilingi 5,000,000.

"Kutakuwa na zawadi zingine mbalimbali kwa washiriki wa mashindano hayo zenye thamani ya shilingi milioni ishirini na jumla ya nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ambayo yatafanyika Tarehe 26- 11-2021 jijini Dar es salaam na yameandaliwa na Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam,"amesema.

"Katika Mashindano hayo Takribani nchi zilizothibisha kushiriki ni Tanzania,Kenya,uganda,Rwanda,Burundi, South Sudan,Ethiopia,Elitrea,Djibouti,Somalia,Malawi,Visiwa vya Seychelles,Comoros,Madagascar,Reunion na Mauritius ", Calist amesema.

Mashindano ya Mwaka huu yanatarajiwa kurushwa moja kwa moja kupitia Television na internet Dunia nzima ambapo Tanzania itafaidika na mashindano hayo moja kwa moja kwa kutangaza vivutio vya utalii fursa za uwekezaji wa Biashara pamoja na utamaduni kwa ujumla.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger