Saturday, 12 June 2021

RAWAN:MLIMA KILIMANJARO UMENISAIDIA EVEREST

...
Mtanzania mwanamke wa kwanza na binti mdogo kuliko wote Afrika kupanda Mlima Everest, Rawan Dakik amesema kuwa zoezi alilofanya zaidi ya mara tano Mlima Kilimanjaro limechangia kufanikiwa kwake kupanda Mlima mrefu zaidi duniani wa Everest wenye urefu wa mita 8,850 kutoka usawa wa bahari.

Rawan ameyasema hayo jana asubuhi mara baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Nepal kwenye zoezi hilo lilochukua miezi miwili.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii  Mhe. Mary Masanja aliyekuwepo uwanjani kumpokea alieleza kufurahishwa kwake na hatua hii ya mafanikio ya Rawan na kuwa itakuwa njia nzuri zaidi ya kuutangaza Mlima Kilimanjaro kiutalii kama sehemu bora kwa mazoezi kwa wanaopenda kupanda milima mirefu zaidi duniani kama Everest.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela amepongeza uamuzi huu wa kishujaa wa Rawan kuwa utahamasisha Watanzania wengi zaidi kupenda utalii wa kupanda milima hususan Mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo aliahidi kuhamasisha Watanzania wengi zaidi kupanda Mlima Kilimanjaro na kuwa ataongoza zoezi maalum la kupanda Mlima Kilimanjaro kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Dotto Felix


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger