Sunday, 12 July 2020

Trump avaa barakoa hadharani kwa mara ya kwanza

...
Rais Donald Trump wa Marekani hapo jana alivaa barakoa hadharani kwa mara ya kwanza ikiwa ni ishara ya kusalimu amri kwa shinikizo la kumtaka kuwa mfano kwa umma katika wakati janga la virusi vya corona linaendelea kuitikisa Marekani. 

Trump alionekana akiwa amefunika pua na mdomo kwa kutumia barakoa yenye nembo ya rais alipotembea hospitali moja ya kijeshi nje kidogo ya mji mkuu Washington alipokwenda kukutana na maveterani waliojeruhiwa. 

Duru zimearifu kuwa mapema wiki hii wasaidizi wake walimuomba kiongozi huyo kuvaa barakoa hadharani katika kipindi ambacho visa vya virusi vya corona vinaongezeka katika baadhi ya majimbo nchini Marekani.

 Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa sharti la kuvaa barakoa, mara kadhaa ametetea jinsi utawala wake unavyolishughulikia suala la corona licha ya kwamba Marekani ndiyo taifa linaloongoza duniani kwa maambukizi pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19. 

Credit:DW


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger