Tuesday, 7 July 2020

Ni Marufuku Taasisi Zilizosajiliwa Kutoa Huduma Za Msaada Kisheeria Kujiingiza Katika Kampeni Za Uchaguzi Mkuu Ujao -Mpanju

...
NA TIGANYA VINCENT
TAASISI zinazotoa  huduma za  msaada wa kisheria na Wasaidizi wa Msaada wa kisheria zimetakiwa kuhakikisha hazijiingizi katika masuala ya kisiasa ikiwemo kuwapiga kampeni wagombea katika uchaguzi mkuu ujao.

Kauli hiyo imetolewa jana Mkoani Tabora na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba Amon Anastizi Mpanju wakati akizindua Kamati ya Uratibu wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kwa ngazi ya Mkoa.

Alisema Watoa huduma wa Msaada wa Kisheria na Wasaidizi wa Msaada wa Kisheria  waliosajiliwa hawapaswi kutumia mlango wa huduma ya msaada wa kisheria kufanya kampeni za kisiasa.

“Tupo katika majira ambayo tunaelekea katika kampeni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani …Taasisi zilizosajiliwa kama watoa huduma wa msaada wa Kisheria zile 11 na Wasaidizi wa Msaada wa kisheria wasitumie mlango wa huduma za kisheria kufanya siasa” alisema.

Aliwataka Viongozi wa Kamati hiyo ya Mkoa wa Tabora kuhakikisha inazichukulia hatua Taasisi zote ambazo zitabainika kufanya kampeni ya kisasa kwa kuwa zitakuwa zinakiuka masharti na taratibu za usajili wao.

Aidha aliwataka Wajumbe Kamati hiyo ya Mkoa wa Tabora kuhakikisha kuwa hakuna masuala ya ushoga na usagaji yatakayoruhusiwa kuingia mkoani Tabora kwa  sababu ni kinyume cha utamaduni wa kitanzania na Sheria za Nchi.

“Nawaombeni msiruhusu masuala ya ushoga na usagaji yakiingia Mkoani Tabora kwa sababu yakwenda kinyume na Sheria zetu na Utamaduni wa Mtanzania”alisisitiza

MWISHO


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger