Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa (wa pili kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Wilaya ya Manyoni, Robert Chalamaganza (kushoto) moja ya mzinga wa nyuki kati ya 20 yenye zaidi ya sh.milioni 1.2 ililiyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka jana kwa ajili ya kuanzisha mradi waufugaji nyuki katika Shule ya Sekondari ya Mkwese. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Manyoni.
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Manyoni, Leah Gervas (kulia) akimvika skafu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya siku moja wilayani humo mkoani Singida jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mkoa wa Singida, Mwalimu Ephraim Kolimba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Manyoni, Ally Omary.
Mwekezaji wa shule hiyo, Askofu Williams Wilson Yindi, akielezea historia fupi ya shule hiyo. |
Viongozi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Manyoni wakijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mkoa wa Singida, Mwalimu Ephraim Kolimba (wa pili kuli)
Mkutano ukiendelea.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wazazi Taifa, Focus Mushi, akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka, akizungumza.
Katibu wa UVCCM, Mkoa wa Singida, George Silindu akizungumza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni, Dafroza Lucas, akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi, akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa, akizungumza.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mkwese wakiwa shuleni wakimsubiri kumpokeea Dkt. Mndolwa.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Dkt. Denis Nyiraha, akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi, Yahaya Masere, akizungumza.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa, akipokea zawadi.
Zawadi ya asali ikipokelewa.
Zawadi ya asali ikipokelewa.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Manyoni, Igembya Wambura, akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa.
Vijana wa UVCCM Wilaya ya Manyoni wakifanya gwaride kabla ya kuvalishwa Skafu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa.
NA DottoMwaibale, Manyoni
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa amewataka wanachama wa jumuiya hiyo, kuhakikisha wanakipa ushindi CCM, wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.
Mndolwa alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na wanachama wa jumuiya hiyo wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ya siku moja.
“Rais wetu Dkt.John Magufuli amefanya kazi kubwa ya kutuletea maendeleo hivyo zawadi kubwa ya kumpa ni kuhakikisha tunampa kura nyingi za kutosha wakiwemo wabunge na madiwani” alisema Mndolwa.
Alisema kujiandikisha katika daftari la wapiga kura hakutoshi kinachotakiwa ni siku ikiwadia ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kuanzia wakina mama, vijana nawanaume.
Katika ziara hiyo Mndolwa alikabidhi mizinga 20 ya nyuki aliyoitoa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Daniel Mtuka kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki katika Shule ya Sekondari ya Mkwese yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 1.2.
Pamoja na mambo mengine Mndolwa alizindua luninga iliyonunuliwa na mbunge huyo kwa ajili ya kuangalia wanafunzi wa shule hiyo, lengo likiwa ni kujifunza vipindi mbalimbali.
Katika hatua nyingine Dkt. Mndolwa amemhakikishia Mwekezaji wa shule hiyo, Askofu Williams Yindi atapewa mkataba wa kuindesha shule hiyo, inayomilikiwa na jumuiya ya Wazazi.
“Nikuhakikishie kuwa hadi ifikapo Augosti 15 mwaka huu kama hakutakuwa na hatua yoyote iliyofikiwa kuhusu mchakato wa kupata mkataba wa uendeshaji wa shule hii baina yetu na wewe naomba nipigwe risasi ya kichwani” alisema Mndolwa.
Hatua ya Dkt.Mndolwa kutoa agizo hilo ilikuja baada ya mwekezaji wa sekondari hiyo kueleza kuwa ameboresha miundombinu ya shule ambayo ilikuwa imeharika, ikiwa ni pamoja na kuchimba visima vya maji, kuweka umeme, ukarabati wa majengo zikiwemo nyumba za walimu, madarasa, mashine ya kusaga, ununuzi wa vifaa vya kufundishia, kununua vifaa vya maabara na zana zingine.
“Mhe.Mwenyekiti uwekezaji nilioufanya katika shule hii unafika zaidi ya sh.milioni 80 lakini hadi leo hii sina mkataba wowote kati yangu na jumuiya ya wazazi, ambao ndio wamiliki wa shule.” AlisemaYindi.
Yindi aliongeza kuwa waliipokea shule hiyo januari 2019 ikiwanawanafunzi 40 na wafanyakazi 10 hadi kufia Machi, 2019 waliongeza wanafunzi 37 nakufikia 77, huku idadi ya wafanyakazi ikifikia 17, na mwaka huu wameongeza wanafunzi hadi kufikia 103 na wanatarajia kupata wanafunzi wengi zaidi kadri watakavyo zidi kuimarisha miundombinu ya shule na taaluma.
Aidha, Mndolwa aliomba wanachama wa jumuiya hiyo kujenga tabia ya kulipia kadi zao ili fedha zitakazo patikana zisaidie katika shughuliza za uendeshaji wa jumuiya hiyo ambayo haina vyanzo vingi vya mapato.
0 comments:
Post a Comment