Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini kimetangaza majina ya Wanachama 10 wa CCM waliotia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga amesema hadi leo asubuhi Alhamis Julai 9,2020 jumla ya Wanachama wa CCM 10 wamejitokeza kutia nia kugombea kiti cha Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na kueleza kuwa zoezi la kuchukua Fomu kugombea ubunge litafanyika Julai 14,2020 hadi Julai 17,2020.
Bwanga amewataja waliojitokeza kutia nia ya kuwania ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kuwa ni Stephen Julius Masele, Dotto Joshua, Erasto Kwilasa, Bandora Salum Mrambo, Wilbert Masanja, Severine Luhende Kilulya, Jonathan Manyama, Lydia Winga Pius, Mary Izengo na Eunice Jackson.
0 comments:
Post a Comment