Saturday, 13 June 2020

Rais Magufuli azungumza kwa simu na Rais Mteule wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye.

...
Rais Magufuli amezugumza kwa simu na Rais Mteule wa Burundi Evariste Ndayishimiye na kumpongeza kufuatia uamuzi wa mahakama ya Katiba kuagiza Rais huyo aapishwe haraka.

Katika taarifa iliyotolewa leo Juni 13 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, imeeleza kuwa, Rais Magufuli amemhakikishia Ndayishimiye kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza ushirikiano na Burundi.

Aidha Rais Magufuli amerudia kumpa pole Rais huyo mteule kwa msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Pierre Kurunziza, aliyefariki Juni 9, 2020.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger